Maswali ya Biblia Danieli



S: Kwenye Danieli, kitabu hiki kiliandikwa nini?

J: Kitabu cha Danieli kinaelekea kuandikwa muda mfupi baada ya matukio kutokea, kwenye karne ya 6KK, kwa mujibu wa The Bible Knowledge Commentary: Old Testament, uk.1324. Vijana wengi wa Kiyahudi walipelekwa uhamishoni Babeli mwaka 605 KK, na wafafanuzi wengine wa vitabu vya Biblia wanakadiria kuwa Danieli alikuwa na miaka kama 16 hivi. Makadirio haya yanamfanya Danieli awe na umri wa miaka 85 wakati Waajemi walipoiteka Babeli.
Kitabu chenye kutia shaka kiitwacho Asimov's Guide to the Bible, uk.596 kinadai kuwa Danieli inaweza kuwa iliandikwa mwishoni mwa mwaka 165 KK. Hata hivyo, mwana historia wa Kiyahudi Josephus kwenye Antiquities of the Jews 11.8.5 (karibu mwaka 93-94 BK) anarekodi kuwa wakati Alexanda Mkuu alipoikaribia Yerusalemu (karibu mwaka 333 KK), Kuhani Mkuu Jaddua alikutana naye na alimwonyesha sehemu ya kitabu cha Danieli isemayo kuwa Wagiriki watawashinda Waajemi. Alexanda anaelekea kuwa alipendezwa na maneno haya, na aliachana na Wayahudi.
Origen (mwaka 225-254 BK) alisema kuwa wakati Alexanda wa Macedon alipokwenda Yerusalemu, kuhani mkuu wa Kiyahudi, alikutana naye akiwa amevaa joho lake takatifu. Alexanda aliinama mbele zake, akisema kuwa alimwona mtu mwenye joho kama hilo kwenye ndoto aliyoota, akimfahamisha kuwa anapaswa kuishinda Asia yote. Origen Against Celsus, kitabu cha 4, sura ya 50, uk.565.

S: Je Kitabu cha Danieli kiliandikwa kwenye karne ya pili (baada ya ushindi wa Alexanda), kwa sababu ya maneno ya Kigiriki yaliyopo kwenye Danieli?

J: Hapana. Ingawa kitabu cha mwenye kushuku kiitwacho Asimov's Guide to the Bible, uk.597 kinadai, "sehemu nyingine za lugha zisizoeleweka kwa urahisi zilizotumiwa zinaonyesha kipindi cha Kigiriki tofauti na kile cha uhamisho wa Babeli", kuna maneno matatu tu ya Kigiriki kwenye Kitabu cha Daniel, ambayo ni kidogo kuliko maneno saba ya Kiajemi yaliyomo. Yafuatazo ni maelezo zaidi ya mambo haya mawili.
Maneno matatu tu ya Kigiriki
yapo kwenye Kitabu cha Danieli (Dan 3:5, 10, 15), na yote hayo matatu ni majina ya vifaa vya muziki. Hata hivyo, jambo hili halionyeshi kuwa kitabu hiki kiliandikwa kwenye karne ya pili (2 KK), kama maandishi ya Kiashuri yanavyosema kuwa mateka wa Kigiriki walikuwa Mesopotamia kwenye karne ya 8 KK. Isitoshe, kwenye karne ya 7 KK, mshairi wa Kigiriki, Alcaeus wa Lebos, anasema kuwa kaka yake alikuwa kwenye jeshi la Babeli. Vivyo hivyo, The Expositor's Bible Commentary, juzuu ya 1, uk.247 pia inasema, "Hakuna shaka kuwa majina ya vifaa (vya muziki) kwenye Kitabu cha Danieli yalikuwa na sifa za Kiajemi, na yalifanya na Wagiriki kuwa sehemu ya utamaduni wao na kufanyiwa mabadiliko machache ya kitahajia (herufi). Kwa hiyo, hoja hii ni ya muhimu tena katika kutathmini uandishi wa Danieli."
Maneno sita na nusu ya Kiajemi
yaliyomo kwenye Kitabu cha Danieli yanaongelea utawala (Dan 6:1-4, 6-7), na yaliacha kutumika karne moja baada ya Himaya ya Kiajemi kuchukuliwa na Alexanda Mkuu. Kama 735 Baffling Bible Questions Answered, uk.193 inavyosema, ". . . Utumiaji sahihi wa Danieli wa maneno haya hauwezi kuelezwa endapo mwandishi alikuwa hafahamiki kwenye karne ya pili na hakufahamu undani wa serikali ya Kiajemi miaka mia tatu kabla ya muda alioishi." (Neno satrap [maliwali] linahesabiwa kuwa nusu, kwa sababu lilikuwa neno la Kimidiani, ambalo baadaye lilichukuliwa na Waajemi pia.

S: Je Kitabu cha Danieli kiliandikwa baada ya Kitabu cha Sirach, kwani Sirach 47-49 ina orodha ndefu kiasi ya Agano la Kale, isipokuwa Danieli, kama Asimov's Guide to the Bible, uk.623 inavyosema?

J: Utawala wa Wamakabia haukuanza hadi mwaka 165 KK. Hata hivyo, kuna mambo manne yenye kutoa ushahidi unaotofautiana na nadharia hii ya karne ya pili.
1.
Kwenye Apokrifa (vitabu vya kubuniwa vya dini ya Kiyahudi), 1 Maccabees 2:49-60 inawataja Danieli na vijana wengine watatu kwa namna ambayo inaashiria kuwa Kitabu cha Danieli kilikuwa tayari kimeishaandikwa. Vinginevyo, wasomaji wa 1 Maccabees wangewezaje kumwelewa Danieli na vijana wengine watatu?
2.
Wataalamu wa elimukale wamekadiria muda hati ya kale yenye maandiko ya Kitabu cha Danieli ilipoandikwa kuwa ni mwaka 120 KK. Wycliffe Bible Dictionary, uk.436-438 inalitaja jambo hili, ikisema kuwa "linaibua swali kuhusu muda unaodaiwa kitabu cha Maccabean kuandikwa."
3.
Uchimbuaji ulifanyika Babeli unaonyesha kuwa maelezo ya Danieli ni sahihi. M. Lenormant anasema, "Kwa kadri maandishi ya kikabari yanavyozidi kufahamika ndivyo haja ya kurekebisha shutuma zilizofanywa kwa haraka na shule ya ufafanuzi wa maandiko ya Ujerumani dhidi ya Kitabu cha Danieli inavyoongezeka" (La Magie, uk.14; nukuu ya 1001 Bible Questions Answered, uk.367).
4.
Pia marejeo ya Josephus yaliyokwishatolewa kwenye swali lililotangulia.

S: Kwenye Kitabu cha Danieli, kuna vitu gani vinavyofanana na sehemu nyingine za Biblia?

J: Danieli inaweza kuchukuliwa kuwa Ufunuo ya Agano la Kale. Yafuatayo ni baadhi ya mambo yanayofanana na sehemu nyingine za Biblia.
Dhana au msemo Danieli Sehemu nyingine za Biblia
Mnyama mwenye pembe kumi Dan 7:4-7 Ufu 13:1-3; 17:3
Magurudumu ya moto kwenye kiti cha enzi cha mbinguni Dan 7:9 Eze 1:15-28; 10:1-22
Ten thousand times ten thousand and the river of fire in heaven Dan 7:10 Ufu 19:14. Angalia pia Mat 16:27; Jud 14
Yesu anakuja na mawingu; kila jicho litamwona Yesu akirudi Dan 7:13 Ufu 1:7; Mat 24:30; Mak 13:26; Luk 21:27; Mdo 1:11
Joka akiangusha nyota Dan 8:10 Ufu 12:4
Gabrieli Dan 8:16; 9:21 Luk 1:19
Maombi ya toba ya pamoja Dan 9:4-19 Neh 1:5-11
Mafuriko, au mto wenye maji Dan 9:26 Ufu 12:15; Nah 1:8
Miaka 3 ˝ Dan 9:26-27; 12:7,11 Ufu 11:1-3; 12:6; 13:5
Chukizo la uharibifu Dan 9:27; 11:31; 12:11 Mat 24:15
Mikaeli Dan 12:1 Ufu 12:7; Jud 9
Kitabu cha uzima Dan 12:1 Ufu 3:5; 13:8; 17:8; 20:12,15; 21:27; Luk 10:20; Kut 2:32-33; Zab 69:28
Kufufuka Dan 12:2 Ufu 20:4-5
Tia/usiyatie mhuri maneno ya unabii Dan 12:4 Ufu 22:10
Sehemu ya ufunuo wa Mungu ilitiwa mhuri Dan 12:9 Ufu 10:4; Isa 29:11-12
Mema na mabaya yaongezeka Dan 12:10 Ufu 22:11


S: Je muhtasari wa kitabu cha Danieli ni upi?

J: Wanazuoni wanatofautiana katika namna nzuri zaidi ya kuunda muhtasari wa Kitabu cha Danieli. Kuna mihtasari mikuu miwili ya Kitabu cha Danieli. Kwa upande mmoja, sura za 1-6 zinahusu maisha ya Danieli (na maono ya Nebukadneza) ziliandikwa katika nafsi ya tatu, na sura za 7-12 zina maono ya Danieli, zimeandikwa katika nafsi ya kwanza. Njia nyingine ya kuunda muhtasari wa kitabu hiki ni kuwa sura ya 1 inaelezea maisha ya awali ya Danieli iliyonadikwa kwa Kiebrania, sura za 2-7 zimeandikwa kwa Kiarami zikiwa ni maisha ya Danieli akitoa unabii juu ya hali ya baadaye ya watu wa mataifa, na sura za 8-12 zimeandikwa kwa Kiebrania zikiwani ni historia ya kinabii ya Israeli. Kama tuna michezo ya maneno, Mungu angeweza kuwa ana "michezo ya mihtasari?" Kwa vyovyote vile, hapa ni muhtasari rahisi wa kitabu cha Danieli.
Danieli 1-6
Maisha ya Danieli
Danieli 1
Hali ya Danieli
Danieli 2
Ndoto ya Nebukadneza ya sanamu
Danieli 3
Nebukadneza anatengeneza sanamu
yake mwenyewe
Danieli 4
Ndoto ya Nebukadneza ya kuwa
kwake kichaa
Danieli 5
Karamu ya Belshaza na maandishi
ukutani
Danieli 6
Amri ya Dario ya siku thelathini
Danieli 7-12
Maono ya Danieli
Danieli 7
Maono ya wanyama wanne
Danieli 8
Maono ya kondoo mume na mbuzi
Danieli 9
Maono ya sabini saba
Danieli 10-12
Maono ya Wagiriki

S: Kwenye Dan 1:1, tunajua nini kuhusu Nebukadneza II zaidi ya mambo yaliyomo kwenye Biblia?

J: Jina lake limeandikwa kwa Kiingereza kama Nebukadneza na Nebukadreza, lakini la pili linafanana zaidi na jinsi Wababeli walivyolitamka. Linamaanisha Nabo [mungu] linda mpaka wangu.
Kwa mujibu wa Encyclopedia Britannica (1972) Nebukadneza II alikuwa mtoto wa kiume mkubwa zaidi wa Nabopolasa. Aliwashinda Wamisri huko Carchemish mwaka 605 KK. Nabopolasa alipokufa, Nebukadneza II alirudi Babeli na alitawala toka mwaka 605 KK hadi Agosti/Septemba 562 KK. Kumbukumbu ya matukio ya Babeli inatoa maelezo ya mapigano yake huko Misri, kuiteka Tiro, na kuishinda Yuda mwaka 597 KK. Alipigana na Elam mwaka 596 KK na alizimisha maasi mwaka 595 KK. Baada ya hapo, kumbukumbu ya Babeli haipo hapa.
New International Dictionary of the Bible, uk.696 ina picha ya amri ya Kibabeli ikiorodhesha matukio tokea mwaka wa mwisho wa Nabopolasa hadi mwaka wa 11 wa Nebukadneza II. Inataja kutekwa kwa Yerusalemu na Babeli.
Nebukadneza aliijenga bustani ya kunyongea ya Babeli, ambayo imeitwa moja ya maajabu saba ya ulimwengu wa kale. Alizijenga kwa ajili ya mke wake Amytis, na binti wa mfalme Astyages (kwa Kimidiani Ištumegu) wa Midiani.

S: Kwenye Dan 1:1, je Nebukadneza aliivamia Yuda kwenye mwaka wa tatu wa Yehoyakimu, au mwaka wa nne kama Yer 46:2 inavyosema?

J: Vyote, na huu ulikuwa ni uvamizi mmoja tu, kwa sababu mfumo wa tarehe uliotumika Uyahudi kwenye karne ya tano KK ulikuwa tofauti na ule uliotumika Babeli.
Kuna maelezo ya ziada yenye kufurahisha sana hapa. Kama 735 Baffling Bible Questions Answered, uk.192 inavyoonyesha, hakuna Myahudi aliyeandika karne za baadaye ambaye angetumia kalenda ya Kibabeli iliyoonyesha mwaka tofauti na jinsi Yeremia alivyoandika. Badala ya kuwa kosa kwenye Kitabu cha Danieli, jambo hili linathibitisha kuwa Danieli iliandikwa karne ya tano siyo baada ya hapo.
When Critics Ask, uk.291-293 inaeleza undani wa mifumo hii miwili ya kalenda. Kalenda ya mfumo wa "Nisani" ambayo Yeremia (na Waashuri) walitumia ilianza na mwezi wa Nisani (Aprili). Yehoyakimu kwa sababu ya Yuda siku chache baada ya mwaka mpya, hivyo mwaka [mzima] wa kwanza ulianza siku ya kwanza ya mwaka uliokuwa unafuata. Danieli alitumia kalenda ya "Tishri" ambayo mwaka mpya ulianza mwezi wa "Tishri" karibu na Oktoba. Mwaka [mzima] wa kwanza wa kutawala kwa Yehoyakimu ulianza kwenye siku ya kwanza ya Tishri. Uvamizi wa Babeli ulitokea wakati wa majira ya joto ya mwaka 605 KK. Pia, The Bible Knowledge Commentary: Old Testament, uk.1328-1329 inaongeza kuwa Wababeli hawakuhesabu sehemu ya muda wa kutawala wa mfalme mpya kabla ya kuanza kwa mwaka mpya kama mwaka wake wa kwanza, wakati Wayahudi hawakufanya hivyo.

S: Kwenye Dan 1:2, je Shinari iko wapi?

J: Shinari ni jina lenye maana karibu sawa na Babeli. Kitabu cha mwenye kushuku kiitwacho Asimov's Guide to the Bible, uk.599 kinadai kuwa hili ni kosa la kikronolojia. Hata hivyo, waandishi wa riwaya mara nyingi hutumia neno lolote kati yale yenye maana karibu sawa, na Danieli anafanya hivi hapa.

S: Kwenye Dan 1:3-6, wanne hawa hawakuwa vijana pekee toka Yuda waliokuwa wakimhudumia mfalme. Kwa nini unadhani vijana wengine hawajatajwa sehemu yeyote ile kwenye Kitabu cha Danieli?

J: Huenda vijana wengine walifikiri kuwa hawakuwa na uhuru wa kukataa kula chakula cha walichopewa kwa hiyo walikula. Mara baada ya kukubaliana na jambo hilo, waliweza kuafiki mambo mengine zaidi. Lakini kumbuka, unao uhuru wa kuchagua mambo wakati wowote ule.

S: Kwenye Dan 1:7, jina Belteshaza linatamkwaje?

J: Wycliffe Bible Dictionary, uk.216 inalitamka (kwa Kiingereza) bel-te-SHAZ-er. Silabi za kwanza na tatu zina voweli fupi, "te" ina voweli ndefu "e" yenye nukta juu yake, na "er" ina "e" yenye kiwimbi juu yake.

S: Kwenye Dan 1:6, je majina haya yalimaanisha nini?

J: Hivi ndivyo yalivyomanisha kwa mujibu wa The Bible Knowledge Commentary: Old Testament, uk.1330.
Belteshaza
lilikuwa neno la Kiakadi Belet-sar-usur lililomaanisha "Mwanamke, mlinde Mfalme."
Shadraka
yaelekea kilikuwa kitenzi cha Kiakadi Saduraku, kilichomaanisha "Ninamwogopa [mungu]". Kwa upande mwingine, huenda kilitoka Aku, mungu mwezi wa Kisumeria.
Meshaki
huenda kilikuwa kitenzi cha Kiakadi mesaku, kilichomaanisha "Nimedharau, enye kudharauliwa, nyenyekevu [mbele za mungu]."
Abednego
ilimaanisha mtumwa wa [mungu aliyeitwa] Nebo. Nebo alikuwa ni mungu wa Kibabeli wa kuandika na mimea. Alikuwa mtoto wa kiume wa Bel.
Majina haya yaelekea yalikuwa na lengo la kuwakumbusha kuwa walikuwa mateka, na kuitukuza miungu ya Babeli.
Kitabu cha mwenye kushuku kiitwacho Asimov's Guide to the Bible, uk.600 kinatoa maana tofauti kabisa. Kinasema Belteshaza linamaanisha "Bel analinda maisha yake", Shadraki linamaanisha "Aku anaamuru", Meshaki lilikuwa neno lenye maana isiyokuwa na uhakika. Mtunzi anakubali kuwa Abednego linamaanisha "mtumwa wa Nebo."

S: Kwenye Dan 1:7; 4:8, kwa nini Danieli na vijana wengine watatu wa Kiyahudi waliafiki majina yao kubadilishwa kuwa majina yaliyohusisha miungu ya kipagani?

J: Huenda hawakuwa na uhuru wa kuamua kuhusu jambo hili. Biblia haikatazi mtu kupewa jina la mungu sanamu, ingawa kwa kawaida muamini hatapenda kufanya hivyo.

S: Kwenye Dan 1:8-20, Danieli na vijana wengine watatu wangeweza kusema, "kwa kuwa hatuna uhuru wa kuchagua" ni lazima tule chakula hiki. Upande mwingine, wangeweza kusema, "tuko radhi kufa kuliko kula chakula hiki." Je unadhani kitendo cha Danieli kilikuwa kizuri zaidi?

J: Kitendo cha Danieli kilihitaji kumtumaini Mungu. Aliamini kuwa Mungu atawafanya wawe na afya njema, ingawa hawakuwa wanakula nyama, au kunywa mvinyo (ambayo inaweza kupunguza madhara mabaya ya vyakula vilivyoathiriwa na bakteria).

S: Kwenye Dan 1:10, kwa nini Danieli na rafiki zake hawakula chakula hiki?

J: Kwa kuwa vijana hawa wa Kiyahudi walizingatia amri za Agano la Kale zihusuzo chakula, kulikuwa na sababu zisizopungua tatu.
1.
Moja ya sababu hizi hapana shaka ilihusu nyama ya nguruwe, samakigamba, huenda hata nyama ya ngamia, na wanyama wengine waliozuiliwa kuliwa. Isitoshe, hata wanyama wasafi huenda walipikwa kwenye vyombo vilevile vilivyopikia wanyama najisi.
2.
Kwani hata wanyama safi, Wayahudi hawakuwa wanakula damu yake. Hatujasikia jamii za zamani zikitoa damu kabla ya kuwapika wanyama.
3.
Huenda nyama ilitolewa kwa sanamu kwanza, na huenda hawakupenda kula nyama hiyo.
4.
Kulikuwa na sheria nyingine, kama vile kutokumtokosa ndama katika maziwa ya mama yake.
John Chrysostom (kabla ya mwaka 407 BK) anaelezea kwa ushawishi mkubwa taabu yao kwenye makala yenye somo moja iitwayo None Can Harm Him Who Dot Not Injure Himself ch.15 (NPNF, juzuu ya 9), uk.281-282.

S: Kwenye Dan 1:10-15, kwa nini vijana hawa wa Kiyahudi walionekana kuwa na afya bora kuliko wale wengine?

J: Ingawa Maandiko hayasemi, inaweza kuwa ni mchanganyiko wa sababu zisizopungua tano.
1.
Huenda ulikuwa ni muujiza, mbali na hali ya kawaida.
2.
Huenda chakula rahisi, kisichokuwa na nyama ya nguruwe na mapochopocho mengine, walichokula vijana wa Kiyahudi hakikuwa na vijidudu ambavyo vyakula vingine vilikuwa navyo.
3.
Hapakuwa na viu vya kuhifadhi vyakula visioze, majokofu, na palikuwa na karafuu chache wakati ule. (Maradhi yanayosababishwa na bakteria na sumu nyingine zinazokuwa kwenye chakula huenda yalikuwa mengi sana wakati ule).
4.
Huenda watu wengi kwenye jumba la mfalme walikunywa mvinyo kupita kiasi. Mbali ya kutokuwa nzuri kwa ini, mvinyo iliyozidi kiasi inaweza kumfanya mtu mwenye rangi nyeupe awe mwekundu usoni. Hii ni kwa sababu kapilari hupasuka na kuwa na rangi nyekundu.
5.
Uwezekano mdogo sana ni kuwa kupungunguza kula vyakula vyenye mafuta na sukari nyingi kunaweza kuounguza vipele usoni.

S: Kwenye Dan 1:12-16, je Danieli hakuwa anakula nyama na kunywa mvinyo maisha yake yote?

J: Hapana, kwa sababu kwenye Dan 10:2-4 wakati Danieli alikuwa anaomboleza kwa majuma kamili matatu, alibadilisha milo yake na hakula nyama wala kunywa mvinyo. Jambo hili linaonyesha kuwa hakuwa anakula vitu hivyo.

S: Kwenye Dan 1:20, je waganga na wachawi walikuwa watu mashuhuri Babeli?

J: Ndiyo. Kuwa bayana, chimbuko la unajimu wa magharibi ni Babeli. Chanzo kingine cha unajimu kilikuwa Pergamumu, Asia Ndogo, lakini hii ilikuwa miaka 400 baadaye, na huu pia ulitokea Babeli.

S: Kwenye Dan 1:21, je Danieli aliishi hadi mwaka wa kwanza wa Mfalme Koreshi, au mwaka wa tatu kama Dan 10:1 inavyosema?

J: Yote, kwa kuwa Danieli aliendelea hata baada ya mwaka wa tatu. Dan 1:21 inasistiza kuwa Danieli alikuwa kiongozi si tu hadi mwisho wa Himaya ya Babeli, bali hata wakati wa Himaya ya Uajemi. Biblia haisemi kuwa Danieli alikufa au alistaafu mwaka wa kwanza wa Koreshi. Dan 10:1, ambayo inaweza kuwa iliandikwa baadaye kidogo, inasema hata mwaka wa tatu.

S: Kwenye Danieli 2, ndoto hii ilitokea lini?

J: Kwenye Danieli 1, Danieli alichukuliwa mwezi wa sita hadi nane mwaka 605 KK. Tarehe 7 Septemba 605 KK, Mfalme Nebopolasa, baba yake Nebukadneza, alikufa, na Nebukadneza akawa mtawala mkuu wa Babeli. Danieli 2 ilikuwa kwenye mwaka wa pili wa utawala wa Nebukadneza.
Mwaka 604 KK
kwa mujibu wa maelezo kwenye NIV Study Bible, uk.1301 na Evangelical Bible Commentary, uk.592.
Mwaka 603 KK
kwa mujibu wa New International Bible Commentary, uk.854 na Daniel: Key to Prophetic Understanding, uk.45-46 cha Walvoord.
Kati ya Aprili 603 na Machi 602 KK
The Expositor's Bible Commentary, juzuu ya 7, uk.39.
Karibu miaka minne baada ya mwaka 605 KK
na matukio ya Danieli 1 kwa mujibu wa Lange's Commentary on Daniel, uk.66 ya zamani (iliyochapishwa mwaka 1901). Aliamini kuwa Nebukadneza hakuwa mtawala pekee hadi miaka kadhaa baada ya kifo cha baba yake.

S: Kwenye Dan 2:1, kwa nini aliwasiliana moja kwa moja na Nebukadneza, mtu asiyekuwa anamcha, kwenye ndoto badala ya kuongea na Danieli?

J: Uovu wa mtu haumzuii Mungu kuwasiliana naye au kumtumia kwa makusudi yake.

S: Kwenye Dan 2:2-10; 4:7; 5:7,11, je Wakaldayo walikuwa ni watu gani?

J: Ingawa Waamori wa Babeli waliitwa Wakaldayo, hivi sivyo inavyomaanisha hapa. Katika jamii ya Kibabeli, Wakaldayo walikuwa ni tabaka la makuhani. Waamori walitokea kaskazini magharibi. Wakaldayo hawakutokea jangwa la Arabuni, licha ya jinsi Asimov's Guide to the Bible, uk.387 inavyosema.

S: Kwenye Dan 2:2-10; 4:7; 5:7, 11, je kuwaita makuhani Wakaldayo kunaonyesha kuwa Kitabu cha Danieli kiliandikwa maiaka ya baadaye kama kitabu cha mwenye kushuku kiitwacho Asimov's Guide to the Bible, uk.601 kinavyodai?

J: Hapana. Gleason Archer anayo makala ya kina kwenye Encyclopedia of Bible Difficulties, uk.285-286 inayoongelea jambo hili.
1.
Danieli anatumia neno la Kiebrania, Kasdim, si tu kwa makuhani, bali pia kwa Wakaldayo (Wababeli) kwenye Dan 5:30. Kama kutumika kwa neno hili kulionyesha kuwa kitabu hiki kiliandikwa baadaye, basi Dan 5:30 ingeonyesha kuwa kitabu hiki kiliandikwa miaka ya awali.
2.
Hata hivyo, kutumika kwake kwa namna mbili kunaonyesha kuwa kitabu hiki kiliandikwa wakati wa uhai wa Danieli. Lugha ya Kiakadi, ambayo Wababeli wa wakati wa Danieli waliiongea, walitumia neno hilohilo Kal-du (litokanalo na neno la Kisumeri Gal-du) kwa makuhani na taifa. Mbao yenye maandiko iliyoandikwa kwenye mwaka wa 14 wa Shamash-shumukin (mwaka 668-648 KK) unatumia neno Gal-du kwa makuhani. Archer anasema Wababeli kabla wa miaka iliyotangulia kuanguka kwa Ashuri walitumia neno Gas'du kwa Wakaldayo. Baada ya kuangukwa kwa Ashuri, walibadilisha konsonanti "s" kwenye maneno mengi kuwa konsonanti "l."
3.
Wagiriki, waliokuwa wanawafahamu Wababeli muda mrefu kabla Daniele hajazaliwa, waliliita taifa hili Chaldaioi.

S: Kwenye Dan 2:3-7, je Mfalme Nebukadneza alikosa busara kuliko wafalme wengine kwa kuwaambia wanajimu na wabashiri kuwa watauawa endapo hawatato tafsiri ya ndoto?

J: Si lazima iwe hivyo. Kwa mujibu wa Herodotus kwenye History, kitabu cha 14, uk.134, wakati mfalme wa Sinthia alipougua, aliomba watabiri watatu wamwambie mtu aliyemfanya aumwe kwa kuapa kwa uongo kutumia meko ya mfalme. Endapo mtuhumiwa angekiri kufanya hivyo angeuawa. Endapo mtuhumiwa angekana kufanya hivyo, watabiri wengine sita wangeitwa, na endapo wasingemtaja mtu yule yule basi wabashiri watatu wa kwanza wangefungwa na kutupwa kwenye mkokoteni na kichaka kilichowashwa moto.
Hivyi ndivyo inavyoelekea kuwa wakati kazi ilipokuwa na malipo mazuri, lakini bado kukawa na sababu nzuri za kutoifanya. Nafikiri nisingekubali kufanya kazi ya utabiri wa mfalme! Baadhi ya kazi siku hizi, kama kutumikia taasisi za kihalifu, haziwezi kurekebishika na usingetaka kuzifanya. Lakini kazi nyingine zinaweza kuwa zinashinikiza sana, na unaweza kuchoka, lakini Mungu anataka uwepo hapo kumshuhudia. Kwa mfano, tuchukulie kuwa umechaguliwa kuwa kiongozi wa kisiasa ambapo unatakiwa uchague kati ya kuwiwa shukrani na moja ya makundi yenye maslahi maalumu. Unaweza kuchagua kutokuwiwa na kundi lolote lile, ingawa wakatti wa uchaguzi hautapata kiasi kizuri cha hela za kufanyia kampeni, utashindwa vibaya sana kwenye uchaguzi, na utapaswa kutafuta kazi nyingine. Danieli alikuwa anafanya kazi yenye kushinikiza sana. Lakini badala ya kuikimbia kazi hiyo, Danieli alisimama mahali ambapo Mungu alitaka awepo.

S: Je Dan 2:4-16 inaeleza nini kuhusu tabia ya Nebukadneza?

J: Yafuatayo ni mambo matano.
1. Nebukadneza alikuwa na kigeugeu. Aliagiza vijana hawa wanne wa Kiyahudi wafunzwe, na baada ya kufunzwa alikuwa anaenda kuwaua pamoja na watu wengine wenye hekima kwa jambo ambalo mtu yeyote asingeweza kulifanya? Nebukadneza alifurahishwa na Danieli na rafiki zakekwenye Dan 1:18-20, lakini walikuwa wanakwenda kuuawa pamoja na watu wengine kwenye Dan 2:17!
2. Alikuwa mtu katili na mkali. Katika sehemu hii ya dunia, kwenye Dan 2:5 walipokuwa wanabomoa nyumba walivuta mihimili ya mbao hadi vitu vyote vilipoanguka. Wakati wanafanya hivi, familia ilikuwa bado imo ndani ya nyumba.
3. Nebukadneza alikuwa na hasira mbaya.
4. Nebukadneza alikuwa mwenye kiburi na majivuno.
5. Nebukadneza alishangazwa kusikia wanajimu wakimjibu kuwa hakuna mtu aliyeweza kufanya jambo hili kwenye Dan 2:10-11. Anaelekea kutokuwa na fununu yeyote jinsi maneno yake yanavyoweza kuwafanya watu wengine wajisikie au wafikiri. Au huenda hakujali jambo hili.

S: Kwa nini Dan 2:4b-7:28 iliandikwa Kiarami wakati Dan 8:1-12:13 iliandikwa Kiebrania?

J: Danieli au katibu wake mmoja au zaidi aliweza kuandika kwa lugha yeyote aliyoona nzuri zaidi; hakuna kitu chochote kitakatifu zaidi katika lugha ya Kiebrania. Hatufahami sababu ya waandishi wanadamu kuchagua kuandika namna hii. Sababu mojawapo inaweza kuwa kwamba sura za kwanza zilihusu mataifa yaliyopo Mashariki ya Kati, wakati sura za mwisho ziliwahusu Wayahudi.
Ezr 4:8-6:18 na 7:12-26 pia zimeandikwa Kiarami. Pia zingatia kuwa Danieli sura za 1-6 zimeandikwa kwa kutumia nafsi ya tatu, wakati Dan 7:2 inaanza na nafsi ya kwanza.
Sehemu iliyoandikwa Kiarami inaanza mara moja baada ya "kumjibu mfalme kwa Kiarami." Kitabu hakirudi kwenye Kiebrania hadi Dan 8:1.

S: Kwenye Dan 2:4b-7:28, kitu gani zaidi tunachokijua kuhusu Kiarami?

J: Kiarami ilikuwa ni lugha iliyodumu kwa muda mrefu sana, iliyofanana sana na Kiebrania. Ilitumiwa na Labani na watu wa Shamu wakati wa uhai wa Abraham (Mwa 31:47); ilitumiwa hapa, na wakati wa Yesu, na ilitumiwa kwa karne chache zaidi na Wanestori na Wakristo wengine Shamu na upande wa mashariki. The Expositor's Bible Commentary, juzuu ya 1, uk.247 inasema uchunguzi huu wa isimu (sayansi ya lugha) umeonyesha kuwa kulikuwa na makundi makubwa manne ya Kiarami: Kiarami cha zamani, Kiarami rasmi, Kiarami cha Levanti (sehemu ya mashariki ya Bahari ya Mediteramia pamoja na visiwa na nchi jirani), Kiarami cha mashariki. Waashuri kutoka karibu mwaka 1100-605 KK waliongea Kiarami rasmi.
Nje ya Biblia, "Waarami", wakiwemo wale waliome kwenye Kitabu cha Danieli, wameonekana kwenye maandiko ya Ugariti wakati wa kipindi cha Amarna, karibu mwaka 1400 KK. The Expositor's Bible Commentary pia inasema Kiarami cha kwenye Danieli kilitumika kutoka karne ya 7 na kuendelea, na kilitumiwa kwenye karne ya 5 na Wayahudi kwenye makaratasi ya mafunjo huko Yebu (Elephantine), Misri na kwenye Kitabu cha Ezra. The Expositor's Bible Commentary, juzuu ya 1, uk.403 inasema kuwa Kiarami hiki kinachukuliwa kuwa tofauti na Kiarami kilichoandikwa Qumran karibu na wakati wa Yesu.
Tazama The New International Dictionary of the Bible, uk.74-75 kuona picha ya Kiarami kilichoandikwa kwenye chombo cha ufinyanzi kilichomwongelea Eliashibu, mtu ambaye anawekuwa alikuwa kamanda wa ngome ya Aradi. Wycliffe Bible Dictionary, uk.123 inasema kuwa mifano mingi imeonekana ya Wababeli (mwaka 605-538 KK) na Waajemi walikuwa wakitumia Kiarami rasmi katika barua zao za kikazi. Mkusanyiko wa Borchardt una barua 13 za Kiajemi, zilizoandikwa Kiarami, kutoka Misri.


S: Kwenye Dan 2:6, je neno hili "heshima" linadokeza nini?

J: "Thawabu" ni neno la umoja (siyo wingi), na linamaanisha zaidi zawadi kuliko malipo.

S: Kwenye Dan 2:18, Danieli aliwezaje kuwekwa pamoja na "wenye hekima", kwani walikuwa wanafunzwa uchawi?

J: Vijana wa Kiyahudi walifunzwa lugha na maandiko ya Wababeli. Haimaanishi kuwa walifunzwa mambo ya dini au uchawi, na hata kama ilikuwa kinyume cha nia yao, hapakuwa na ushahidi wowote kuwa walifanya mambo hayo. Tazama kwenye Dan 2:2 kuwa Nebukadneza alipowaita wachawi, wafanya mazingaombwe na wanajimu, Danieli hakuwa miongoni mwao. Danieli alikuja kusikia kuhusu jambo hili baadaye.

S: Kwenye Dan 2:20-23 kuna sababu gani zisizopungua nne za Danieli kuchukua muda mrefu kiasi hicho kumsifu Mungu baada ya Mungu kumfunulia maana?

J: Hii ni sara nzuri sana, ambayo imeundwa vizuri sana. Huenda kukawa na sababu hizi nne.
1. Kama Nebukadneza angewaua watu wote wenye hekima, Dan 2:18 inaonyesha kuwa Danieli naye pia angeuawa. Danieli alijawa na shukrani kwa sababu ya usalama wake, rafiki zake, na watu wengine.
2. Hata bila ya hatari iliyopita, Danieli alishukuru bayana kuwa Mungu alimfunulia mafumbo yake kwake. Tunapaswa kuwa na shukrani Mungu anapotufunulia vitu mbalimbali kupitia neno lake.
3. Kwa ujumla, Danieli alikuwa mtu wa shukurani na mwenye mazoea ya kumwomba Mungu, mara tatu kwa siku kwenye Dan 6:10. Danieli alikuwa na mazoea ya kushukuru na kuomba kwa Mungu.
4. Ombi hili huenda lilikuwa "ulinzi" kwa Danieli. Ilikuwa dhahiri kuwa hakuna binadamu ambaye angeweza kulifanya jambo hili, bila msaada wa Mungu. Danieli anaweza kuwa alifikiria kukusanya vitu alivyokuwa navyo kukabiliana na hali iliyokuwepo wakati huo, au kuwa alistahili kwa ajili ya uhusiano wake wa karibu na Mungu. Ombi hili lilikuwa ni ukiri wa Danieli kuwa ni Mungu tu, na hakufanya kitu chochote zaidi ya kile ambacho Mungu alimfunulia.

S: Kwenye 2:24, kwa nini Danieli hakuwaacha watu wenye hekima wa Babeli waliokuwa wapagani wauawe?

J: Danieli hakuwa na chuki au nia mbaya dhidi yao. Yeyote miongoni mwa watu waliochaguliwa na Mungu aliyeshiriki kwenye vitendo vya uchawi alipata adhabu ya kifo kwenye Agano la Kale. Hata hivyo, si watu wenye hekima wa Babeli waliokuwa wachawi, na hata wale waliokuwa wachawi hawakujua kuwa Biblia ilikataza.

S: Kwenye Dan 2:24-25, kwa nini Arioko alisema kuwa amempata Danieli, badala ya kusema Danieli alikuja kwake?

J: Huenda Arioko alitaka kupata sifa njema kwa kitu ambacho hakukifanya. Kwa bahati mbaya, wakati mwingine wafanya biashara siku hizi nao hupenda kupata sifa njema kwa vitu ambavyo hawajavifanya.

S: Kwenye Dan 2:28-3:1, je Nebukadneza alimwamini Mungu baada ya hapo?

J: Nebukadneza walau alimini kuwa Mungu wa Danieli alistahili kuheshimiwa, hasa kwa kuwa alikuwaa na uwezo wa kusimamisha na kuondoa falme. Hata hivyo, baada ya hapo, kwenye Dan 3:1 Nebukadneza alisimamisha sanamu ambayo watu wote walitakiwa kuinama mbele yake na kuisujudia.

S: Kwenye Dan 2:30, kwa nini Danielie alikuwa makini kuhakikisha watu wanafahamu kuwa hekima haikutoka kwake, bali kwa Mungu?

J: Kwenye jamii ambayo watu na sanamu zisizokuwa na uhai ziliabudiwa kwa sababu yeyote ile, Danieli alitaka kuhakikisha kuwa anawafahamisha watu kuwa ni Mungu tu aliyetakiwa kuabudiwa hapa, na si Danieli.
Leo hii, hata panapokuwa hakuna nafasi kwa sisi kuabudiwa, ni muhimu kumpa Mungu utukufu, kuliko kuwafanya watu wengine watupe utukufu wakati walipaswa kumwangalia Mungu.

S: Kwenye Dan 2:31-35, je metali hizi zina sifa gani?

J: Dhahabu ni ya thamani zaidi, nzito zaidi, na laini zaidi. Fedha ni ya pili, na chuma ni ya mwisho. Bila kuangalia uwezekano kuwa sanamu za dhahabu zilikuwa zinafunikwa kwa dhahabu, hazikuwa za dhahabu halisi, jambo hili lilionyesha kuwa Himaya ya Babeli ingeweza kuonekana kuwa bora zaidi, yenye utulivu zaidi, na isiyoweza kutikiswa. Himaya ya Uajemi ilikuwa na maasi kutoka kwa Wagiriki, Wamisri, na maasi ya toka ndani ya nchi. Himaya ya Kigiriki (Makedonia) iligawanyika sehemu nne mara baada ya kifo cha Alexanda Mkuu. Himaya ya Rumi ilikuwa na changamoto nyingi zaidi kuliko himaya nyingine, na ilionekana kuwa yenye usalama kidogo zaidi (miongoni mwa maasi ya Wagaulu, Wakaarthaginia, Wajerumani, Wahuna, nk.) lakini ilikuwa ndio yenye nguvu zaidi. Kulikuwa na metali nyingine ambazo hazikuelezwa kwenye ndoto hii. Vile vile, kuna himaya nyingine ambazo hazijatajwa hapa, lakini hazikuwatawala Wayahudi.

S: Kwenye Dan 2:35a, je upepo uliowapeperusha unaweza kuwa unawakilisha kitu gani?

J: Upepo hapa si muda uliopangwa tu, bali huenda ilikuwa ni utendaji wa Mungu katika historia kutimiza kusudi alilolipanga.

S: Kwenye Dan 2:35b, je mlima ulioijaza dunia nzima ulikuwa ni kitu gani?

J: Huu unaweza kuwa ni ufalme wa Mungu, ulioanzishwa na Yesu Kristo. Huyu ni Yesu anayeyaangamiza mataifa. Jambo hili linatimizwa katika vita vya kThis is fulfilled at the Battle of Har-Magedoni kwa mujibu wa 1001 Bible Questions Answered, uk.291-292.

S: Kwenye Dan 2:37-44, je hizi falme nne zilikuwa zipi kwenye "sanamu kubwa sana kuliko binadamu" na mlima?

J: Hizi ni himaya za Babeli (karibu mwaka 605-538 KK), Uajemi ya Kigiriki (karibu mwaka 538 KK), Ugiriki/Makedonia (karibu mwaka 333 KK), na Rumi. Vifuatavyo ni vidokezo vitatu vitakavyotusaidia kupata jibu.
1.
Hizi hazikuwa himaya zozote zile nne, lakini himaya zilizohusiana na Wayahudi na zilichukua madaraka ya moja toka kwa nyingine. Hivyo, himaya za India, China, Mongoli, na himaya za ulimwengu mpya hazihusiki hapa.
2.
Dan 2:36-39 inaonyesha kuwa himaya ya Babeli ya wakati wa Nebukadneza ni ya kwanza. Hivyo, Himaya ya Misri haiwezi kuwa moja ya hizo nne, kwani ilikuwepo kabla ya Babeli, ingawa iliendelea kuwepo kwa namna fulani hadi wakati wa Waajemi. Vivyo hivyo, Himaya ya Waashuri si moja ya hizo nne kwani iliangamizwa kabisa kabla ya wakati wa Nebukadneza.
3.
Yesu Kristo, kama mfalme wa wafalme, atasimamisha ufalme wake wakati wa himaya ya nne.
Kitabu cha mwenye kushuku kiitwacho Asimov's Guide to the Bible, uk.603 kinasai kuwa himaya za Umedi na Uajemi zilichukuliwa kuwa himaya mbili, na himaya ya nne ilikuwa ya Makedonia ya Alexanda. Asimov huenda akawa anasema hivi kwa sababu anaamini kuwa Kitabu cha Danieli kiliandikwa baada ya Alexanda kutwaa madaraka (huenda ilikuwa baadaye sana hadi mwaka 165 KK. Asimov anadai). Hata hivyo, Himaya ya Umedi haikuwahi kuwa tofauti na Waajemi, kama ambavyo Himaya ya Rumi ilikuwa tofauti, kabla, wakati wa Julias Kaisari, na hata baada ya hapo.

S: Kwenye Dan 2:37-44, je Himaya ya Umedi na Uajemi zilikuwa mbili tofauti badala ya moja?

J: Hapana, kwani kama Encyclopedia of Bible Difficulties, uk.293 inavyotukumbusha, Dan 5:28 iko wazi kabisa. Mwandishi alijua kuwa uthibiti wa ufalme ulihama kutoka Himaya ya Babeli kwenda Himaya ya Ugiriki ya Kigiriki, si kutoka kwa Wamedi kwanza (ambao Waajemi waliwashinda kabla ya wakati huu) na baadaye kwenda kwa Waajemi.

S: Kwenye Dan 2:38, nini inaweza kuwa ni sababu ya Danieli kusema kuwa Nebukadneza alitawala wanadamu, wanyama wa kondeni na ndege wa angani?

J: Ingawa Nebukadneza alitawala kanda wote wa mwezi mwandamo wenye rutuba [eneo linaloanzia pwani ya Mashariki ya Bahari ya Mediterania, kupita kwenye bonde la mito ya Hidekeli (Tigris) na Frati (Euphrates) na kwenda hadi Ghuba ya Uajemi], huenda palikuwa na sababu kubwa zaidi. Wakati wa sherehe ya mwaka mpya wa Babeli, inawezekana walisoma mbele ya watu Shairi la Uumbaji, na mfalme alikuwa mwakilishi wa mungu Marduku, ambaye aliumba vitu vyote. Daniel: Key to Prophetic Understanding, uk.65.
Kihistoria, kila mtu anakubali kuwa Nebukadneza alikuwa ni mfalme mwenye nguvu sana Mashariki ya Kati, lakini hata kila mtu kwenye himaya ya Nebukadneza aliwafahamu wafalme wengine ambao hawakuwa chini yake. Je watu wa kwenye Biblia walijuaje jambo hili?
Neno la Kiarami kwenye Dan 2:38, 39; 4:22 ni ‘ara (Strong's 772) linalotokana na neno la Kiebrania ‘erets (Strong's 776). Lina maana nyingi sana. Kwa mujbu wa Strong's Concordance neno la Kiebrania ‘erets linamaanisha "-a kawaida, nchi, dunia, shamba, ardhi, mataifa, njia, nyika, ulimwengi." Hivyo mbali ya kumaanisha dunia, neno hili linaweza likamaanisha pia nchi (yaani Mesopotamia). Msemo kama huu ulikuwa ni nahau na kichwa cha habari, kama miaka iliyotangulia Mfalme Amar-Enzu wa Utawala wa Tatu wa Kinasaba wa Uru alivyosema kuwa yeye ni lugal dubdalimmubak, au "mfalme wa Pande Nne za dunia" kwenye maandishi yake yaliyo kwenye majengo. Habari hii ni kwa mujibu wa The Expositor's Bible Commentary, juzuu ya 7, uk.63. Inafaa ieleweke na wasikilizaji wote kuwa maneno haya hayaongelei sayari nzima, kama wakati wa Nebukadneza na wakati wa Amar-Enzu, Waelamu, Uajemi, Lydia, Misri, na Ugiriki zilikuwa nchi huru zilizofahamika sana nao. Hata hivyo, Nebukadneza, alikuwa mfalme mwenye nguvu sana Mashariki ya Kati, na kwa kadri alivyozidi kutawala ndivyo alivyozidi kuwa na nguvu zaidi.
Kwa hiyo kuna vitu viwili vinavyo wezekana: ‘ara (‘erets) ilimaanisha sayari yote ya dunia au ilimaanisha nchi ya Mesopotamia. Angalia kuwa Dan 2:38, 39 na 4:22 SI nabii; mwishoni mwa utawala wa Nebukadneza wanamwambia jambo ambalo tayari analo. Inaelekea kuwa ni uwezekano wa pili, kwani hakuna mtu wakati ule ambaye angeelewa kuwa Wababeli walitawala Ugiriki, Umedi, Lidia, nk.
Kama wazo la nyongeza, Nebukadneza alitawala kutoka mwaka 605 hadi 562 KK, na mashambulizi ya kijeshi wakati wa utawala wake:
Mei/Juni 604 KK Wababeli walimshinda Wamisri huko Karkemishi.
11-12/605 au 604 KK Wababeli waliiangamiza Ashkeloni huko Foinike.
Mwaka 603 KK Wababeli waliiangamiza Ekroni huko Foenike.
Mwaka 601 KK Wababeli na Wamisri walipigana bila kupatikana mshindi; hasara kubwa.
Mwaka 600 KK Watu wa Lidia waliiangamiza Smyrna kwenye Asia Ndogo.
Mwaka 599-598 KK Wababeli walipgana na Waarabu.
16 Machi 597 KK Wababeli waliiteka Yerusalem, lakini hawakuiangamiza
Mwaka 596 KK Mfalme wa Babeli Nebukadneza II apigana na Waelami.
Mwaka 595-594 KK Nebukadneza II anazimisha maasi.
Mwaka 593/591 KK Mmisri Psamtik II pamoja na askari wa kukodiwa wa Kigiriki, Kifoenike na Kiyahudi waliishinda Nubia.
Mwaka 589-587 KK Wayahudi wanaiasi Babeli. Yerusalemu inazingirwa kwa miezi muda wa 30.
Mwaka 585-573 KK Wababeli wamzingira Mfalme Ethbaal II wa Tiro.
Mwaka 585 KK Vita kati ya Wamedi na Waaliate wa Lidia imeisha baada ya kupatwa kwa jua kwa tarehe 28 Mei 585 KK.
Mwaka 584-584 KK Nebukadneza II anaizingira Tiro.
Mwaka 581 KK Wababeli wanawarejesha makwao watu zaidi kutoka Yuda.
Mwaka 570 KK Wagiriki na Wakirene wanapigana kwenye jimbo la Kirene.
Mwaka 570 KK Wagiriki huko Kirene walimshinda Apries wa Misri.
Mwaka 568-567 KK Apries na Wababeli walijaribu kuivamia Misri.
Mwaka 560 KK Mfalme wa Lidia Croesus aitwaa miji ya Ionia (sehemu kuu ya pwani ya magharibi ya Asia Ndogo) kuanzia karibu karne ya 8 KK).
Mwaka 560-547/546 Waajemi walimtiisha Mfalme Croesus wa Lidia.

S: Kwenye Dan 2:44, ufalme wa Kristo utazivunjaje na kuziharibu falme nyingine?

J: Utazivunja falme nyingine kwa njia zisizopungua nne.
Kiroho,
mapepo yana uwezo wa kuathiri falme, kama Dan 10:13 inavyoonyesha.
Kisiasa,
falme zilizowahi kudai kuwa za Kikristo, au angalau ziliwahi kujifanya kuwa za Kikristo, zitatawala sehemu kubwa ya ulimwengu, kuanzia na Himaya ya Rumi wakati wa Mfalme Constantine (mwaka 324 BK).
Kitamaduni
, mtazamo wa Kikristo utatawala fikra za kimagharibi kwa zaidi ya miaka elfu moja mia tano.
Hatimaye,
(na jambo hili ni la muhimu zaidi) Mungu Mwana atakuja duniani, ataanzisha utawala wake, kila goti litapigwa kwa Yesu (Fil 2:9-11), na watu wote watakuwa chini ya mamlaka yake (1 Kor 15:24-25).

S: Kwenye Dan 2:48-49, je hatima ya ukatili wa Nebukadneza ilikuwa nini? Je jambo hili linaonyesha kitu gani kuhusu tabia ya Nebukadneza?

J: Nebukadneza alimpa Daniel cheo kikubwa na zawadi nyingi. Huenda Nebukadneza alifanya hivi si kwa ajili ya upendo wake kwa Danieli, lakini kumfanya awe mfano ili watu wengine pia wapende kumtumikia Nebukadneza kwa uaminifu.

S: Kwenye Danieli 3, ni njia zipi ambazo watu wanajaribu kuigiza hali wanayodhani ni hatima yao kwa njia zao wenyewe?

J: Watu wanaweza kuona kitu kuwa jaala au hatima yao, au chaguo la Mungu kwa maisha yao lenye kutokana na vipawa au karama zao, mazingira yao, mambo ambayo watu wengine wanawaambia, au fursa wanazoziona. Watu wazima hufanya hivi, lakini wanafunzi wa shule za sekondari na vyuo vikuu huwa wanaambiwa kuwa wanapaswa kufanya hivi ili waweze kusaidia kufanikisha malengo yao ya kazi, au wakati mwingine mwenzi wa maisha wanayemtaka. Mara wanapofikiria kuwa kuna jambo linalowakabili, huwa wanafanya mambo haya yafuatayo.
Fahamu jinsi matokeo yenye mafanikio yatakavyo kuwa.
Huwa wanataka kupata sura ya kitu kichwani na kuiamini
Kisha watu wengine waamini mwisho walioukusudia
Chukua hatua ndogo kuufikia huku ukiepuka kuweka ahadi au "kutunza kazi yao ya siku"
Tafuta kujua hisia za watu kabla ya kuchukua hatua yeyote na tazama mambo yatakavyo kuwa hadi sasa
Wakati mwingine wanaweza "kuhesabu gharama" na fanya uamuzi kama jambo unalolikusudia kulifanya linastahili rasilimali za muda, fedha na nyinginezo ulizoandaa kuziwekeza
Wakati mwingine huthubutu kufanya vitu ambavyo matokeo yake hayatabiriki, na huweka juhudi zao zote katika malengo hayo, wakitambua kuwa wanaondoa mambo mengine ambayo wangeweza kuyafanya.
Kisha wanafanya ama jambo hilo, au jambo mbadala, au wanapatwa na msongo wa mawazo kwa sababu wameshindwa kabisa na wanafikiri hawawezi kupata nafasi nyingine ya kujaribu kitu kingine. Au, wanatambua kuwa kutakuwa na siku nyingine na fursa nyingine na wanaendelea kujaribu, kitu hicho hicho, au kitu kingine.
Mambo haya hapo juu yanaweza kuwa ni njia ya kawaida na ya busara ya kutimiza lengo lako, lakini kumbuka kuwa Mungu hahusiki na mambo hayo. Badala yake, kwa nini usianze na maombi, na uombe maongozi wa Mungu ili uweze kufanikiwa katika katika jambo ambalo anataka uwe, pia kuwa tayari kwa hali zitakazokujia ili kukuangusha.
Kisha omba maongozi ya Mungu, na kisha unaweza kuendelea na hatua hizo hapo juu, ukiomba uongozi wa Mungu na msaada wake katika kila hatua unayopitia.

S: Kwenye Dan 3:1, kwa nini Nebukadneza alitengeneza sanamu ya dhahabu, kwani alimkiri Mungu wa kweli kwenye Dan 2:46-47?

J: Ingawa Kitabu cha Danieli hakidokezei ama kipindi kirefu au kifupi cha muda kati ya maono na sanamu, mambo haya mawili yana uwezekano mkubwa wa kuhusiana. Wycliffe Bible Dictionary, uk.831-832, inaonyesha kuwa Nebukadneza huenda alikuwa anajaribu kupinga ujumbe wa Mungu uliotolewa kwenye ndoto ya mfalme, kuwa ufalme wake utaangushwa.

S: Kwenye Dan 3:1, kwa nini Nebukadneza alifanya sanamu nyembamba namna hii ya mtu mwenye urefu wa mita 27 (futi 90) na upana wa mita 3 (futi 9)?

J: Hivi si lazima view vipimo vya umbo bali vya sanamu. Sanamu hii huenda iliwekwa kwenye kiegemezo kirefu.

S: Kwenye Dan 3:12, kwa kuwa ni wavulana watatu tu wa Kiyahudi waliokataa kuinama mbele ya sanamu hii, je jambo hili linamaanisha kuwa Danieli nay eye pia aliinama?

J: Hapana, kwa sababu kwenye Dan 1:8 na Dan 6:10, Danieli anaonyesha kuwa hangefanya vitu visivyofuata maagizo ya Mungu. Danieli na Wayahudi wengine wacha Mungu hawakushikwa kwa sababu hawakuwepo pale. When Critics Ask, uk.294 pia inasema kuwa kwa kuwa Danieli alikuwa kiongozi wa serikali, anaweza kuwa alikuwa kwenye safari ya kikazi nje ya mji wakati huo.

S: Kwenye Dan 3:17-18, je Shedraka, Meshaki na Abednego waliamini kuwa Mungu atawaokoa, au hawakuwa na uhakika kiasi? Je tunapaswa kuwa na uhakika kuwa Mungu atauokoa?

J: Hawakuwa na uhakika wa kiasi fulani, kama ilivyoonyeshwa kwenye mstaru wa 18. Lakini hata kama Mungu asingewaokoa, walikuwa radhi kufa kwenye moto uliokuwa unawake kuliko kuafiki kuinama mbele ya sanamu.

S: Kwenye Dan 3:19, mtazamo wa Nebukadneza uliwezaje kubadilika hata hakuwa mwema tena?

J: Mwanzoni alifikiri alikuwa mpole kwa kuwatishia kuwatupa kwenye tanuru la moto, lakini aliwapa nafasi moja zaidi ya mwisho. Baada ya hapo hakutaka kuongea nao tena, lakini alilifanya tanuru kuwa la moto zaidi ili kutoa mfano kupitia kwao. Kwenye aya ya 22, lilikuwa moto sana hata askari waliokuwa wanawatupa ndani waliungua, lakini hakuna kielelezo chochote kuwa jambo hili lilimkera kwa namna yeyote ile. Mara nyingi wafalme na viongozi wakubwa huwa hawajali watu bali madaraka yao, na mamlaka yatokanayo na watu wa chini yao wanaowafuata. Wakati mwingine hata viongozi wanaojali watu wanaweza kuwatelekeza wanaposhambuliwa.

S: Kwenye Dan 3:19, je moto uliwezaje kuwa mkali mara saba?

J: Hawakuwa na uwezo wa kupima joto la moto. Lakini, hakuna shaka kuwa palikuwa na viriba vya kuchochelea moto vilivyotumika kuongezea hewa ya Oksijeni kwenye moto, na viriba saba (au mara saba) vilifunguliwa kuleta joto zaidi. Muda mrefu kabla ya wakati huu, zana za chuma hazikutumika sana kwa sababu hazikuweza kuyafanya matanuri yaliyokuwa na uwezo wa kuyeyusha kufua chuma.

S: Kwenye Dan 3:25, ni nani aliyekuwa mtu wa nne hapa?

J: Huyu anaaminika kuwa ni Kristo mwenyewe aliyetokea kabla ya kufanyika kwake kuwa mwili. Ingawa kuna uwezekano kuwa alikuwa malaika, maelezo ya Nebukadneza kuwa mtu huyu "ni mfano wa wana wa miungu" yanatoa uwezekano kuwa alikuwa Kristo. Waandishi wa wakati wa kanisa la awali waliosema kuwa huyu alikuwa ni Kristo ni Irenaeus, Tertullian, Hippolytus, na Cyprian wa Carthage.
Hippolytus (mwaka 225-235/6 BK) kwenye fragment 3 (Maelezo ya Kitabu cha Danieli) sura ya 2.93, uk.188 pia inasema kuwa Yesu alikuwa kwenye tanuri pamoja na Shadraka, Meshaki na Abednego, ingawa Yesu alikuwa bado kuzaliwa na bikira hapa duniani. Baada ya baraza la kanisa la awali lililofanyika Nikea, Hilary na Augustine wa Hippo walisema vivyo hivyo. Jerome alisema kuwa hakuwa Yesu bali malaika aliyejionyesha kwa sura ya Kristo.

S: Kwenye Dan 3:26, ni kitu gani cha ajabu sana kwa Nebukadneza kumwita Bwana "Mungu Aliye juu", na "Mungu wa miungu, na Bwana wa wafalme" kwenye Dan 2:47?

J: Huyu ni Nebukadneza yule yule aliyetengeneza sanamu na kuiabudu kwenye Dan 3:1. Inaonekana kuwa jambo hilo halikueleweka akilini mwake kuwa endapo kuna Mungu Mwenye Enzi yote basi tunapaswa kuzingatia mambo anayosema, na kutoiabudu miungu mingine.

S: Kwenye Dan 3:30, nini ilikuwa hatima ya watu waliowashitaki Shadraka, Meshki na Abednego kwenye Dan 3:8? Unafikiri ni sababu gani kubwa iliyomfanya Mungu afanye hivyo?

J: Waliona vijana wa Kiyahudi wakipandishwa vyeo. Sababu kubwa huenda HAIKUWA malipo kwa Shadraka, Meshaki, na Abednego. Inaelekea kuwa ilikuwa kwamba jina la Mungu liinuliwe, na endapo watu wengine wangesikia kuhusu kupandishwa vyeo huku wangefanywa wapende kumsikiliza Mungu Mwenye Enzi yote. Jambo hili ni la kweli zaidi kwa Wayahudi, ambao wangeweza kujaribiwa na kupotoka na kufanyika kuwa kama Wababeli, wangetiwa moyo sana.

S: Kwenye Dan 4:1-3, je Nebukadneza alisema maneno haya kabla au baada ya mkasa wa Danieli?

J: Jambo hili lilitokea baada ya mkasa wa Danieli, kwa sababu maelezo haya ya Nebukadneza yenye kutumia nafsi ya kwanza yanatoka kwenye barua ambayo aliiandika baadaye.

S: Kwenye Dan 4:8-9,18, kwa nini mfalme aling'ang'ana kumwita Danieli Belteshaza, na kuwa roho ya "miungu watakatifu" ndani mwake?

J: Danieli alisema kuwa alimtumikia Mungu Mwenye Enzi yote (umoja), lakini Nebukadneza anaelekea alisikia kuwa Danieli anaitumikia miungu (uwingi). Mara nyingi tunaposema vitu, na watu wanasema kuwa wanatuamini, bado huwa wanayachambua maneno tunayosema kwa mtazamo wao, na wanayatafsiri upya maneno yetu ili yafanane na mawazo waliyokuwa nayo kabla.

S: Kwenye Dan 4:10-17, kwa nini unafikiri Mungu alimpa Nebukadneza ndoto hii?

J: Ndoto hii isingeaminika na mfalme endapo ingekuwa imetolewa kwa Danieli au mtu mwingine yeyote yule. Haikutolewa kwa Nebukadneza kwa sababu alikuwa mtu wa kiroho zaidi, au bora kuliko Danieli, au kwa sababu alikuwa mcha Mungu zaidi ya watu wote. Kutoa ndoto kwa mtu aliyefaa zaidi kupewa kulikuwa ni kwa ajili ya makusudi ya Mungu, na zi kustahili kwa namna yeyote ile kwa Nebukadneza.

S: Kwenye Dan 4:13,23, je "mlinzi" ni nani?

J: Huyu alikuwa ni aina ya malaika. Vitabu vya Kiyahudi vya kidini vya kubuniwa (Apokrifa) pia vinaelezea malaika walinzi, lakini vinaweza kuwa viliandikwa baada ya Kitabu cha Danieli. Jambo linaloweza kusemwa kwa uhakika zaidi hapa ni kuwa Wayahudi walifahamu dhana ya malaika walinzi.

S: Kwenye Dan 4:33-37, je ni wakati gani Nebukadneza alikiacha kiti chake cha enzo kwa sababu ya kuwa na wazimu?

J: Danieli 4 inasema kuwa miezi kumi na mbili baada ya ndoto hii, Mungu aliyashughulikia majivuno ya Nebukadneza na kutimiza unabii huu.
Neno la Kiarami hapa linaweza kumaanisha "muda au msimu" lakini pia "mwaka." Hivyo, 735 Baffling Bible Questions Answered, uk.195 inaonyesha kuwa huenda ulikuwa muda usiozidi miaka miwili badala ya miaka saba.
Believer's Bible Commentary, uk.1080-1081, 1092 inaongezea kuwa ugonjwa huu wa akili unaitwa ‘boanthropy' (yaani mtu-punda). Dr. R. K. Harrison anamwelezea mtu aliyekutana naye aliyekuwa na ugonjwa huu kwenye kitabu chake kiitwacho Introduction to the Old Testament, uk.1114-1117.

S: Kwenye 4:33-37, je kuna ushahidi wowote mbali ya Biblia kuwa Nebukadneza alipatwa na wazimu kwa muda?

J: Huenda. Ingawa kitabu cha mwenye kushuku Asimov's Guide to the Bible, uk.605 kinasema hakuna, The Expositor's Bible Commentary, juzuu ya 7, uk.63 inataja kipande chenye kufurahisha cha Hati toka Bahari ya Chumvi cha Kiarami kilichokutwa kwenye pango la 4. Hii ni sala ya Nabonidus inayosema, "Maneno ya maombi ambayo Nabunai(d), Mfalme wa Ashuri na Babeli, mfalme mkuu, aliyosali wakati alipopigwa na ugonjwa mbaya sana wa ngozi kwa amri ya Mungu Mwenye Enzi yote kwenye mji wa Teima: ‘Nilipigwa na ugonjwa mbaya sana wa ngozi kwa muda wa miaka saba . . . kwa jina la Mungu Mwenye Enzi yote.'" (Tafsiri hii ya kukisia, inayotegemea kuongezea herufi nyingi ambazo hazikuwepo kwenye hati, ilichapishwa na J. T. Milik kwenye Revue Biblique, uk.63 (1956): 408; linganisha na Saggs, Babeli, uk.154 kwa toleo la Kiingereza hapo juu). The Expositor's Bible Commentary, juzuu ya 7, uk.63 inasema jambo hili linaweza kuwa lilitokea baadaye, kinaweza kuwa kipande chenye masimulizi ya kimapokeo ambacho hakina uthibitisho wa wa kihistoria, kwamba huenda kina masimulizi ya kweli ama ya ugonjwa wa ngozi wa Nabonidus. Lakini inasema, ". . . uchunguzi wa kina wa kipande cha Nabonidus unaonyesha kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kuwa mapokeo ya baadaye yaliyonukuriwa na kuandikwa upya kwa njia inayochangnya ya ugonjwa wa Nebukadneza mwenyewe, kama kweli haya hayaongelii ugojwa wa baadaye uliomkuta Nabonidus (ambaye miaka yake kumi ya kufungwa kwenye mji wa Arabuni ya kaskazini wa Teima [Teman] inaweza kuwa imehusisha ugonjwa huu)."
The Expositor's Bible Commentary, juzuu ya 1, uk.246-247 inasema kuwa Maombi ya Nabonidus ni ya kubuniwa sana hata hayawez kusaidia, lakini yanaongezea mambo ambayo tunayajia kuhusu wazimu wa Nebukadneza kupitia Berossus, kuhani na mwana historia wa karne ya tatu wa Babeli, na mwandishi wa karne ya pili Abydenus, aliyesema kuwa Nebukadneza "alipagawa na mungu wa aina moja au nyingine", wakati alipotoa unabii na kutoweka Babeli.
Hivyo, ushahidi huu hauthibitishi jambo hili kikamilifu, lakini unaelezea kuwa rekodi rasmi za Babeli na hostoria ya Kigiriki havitoi maelezo yote ya tukio hili.

S: Kwenye Dan 4:33-37, je wazo la Nebukadneza kufanya vitu kama mnyama kunatokana na sanamu za Kiashuri za ng'ombe dume wenye vichwa vya binadamu na mabawa ya ndege, kama kitabu cha mwenye kushuku Asimov's Guide to the Bible, uk.605 kinavyosema ni kubunia kunakovutia?

J: Haielekei kuwa hivyo. Kwanza kabisa, wanadamu wenye vichwa vya ng'ombe dume walifahamika Misri na Krete za zamani kuanzia wakati wa Musa. Pili, hizi zilikuwa sanamu za Waashuri, si za Wababeli. Danieli angekuwa na sababu kidogo za kuandika kitu kuhusu "binadamu-mnyama", kuliko Musa aliyeishi Misri.

S: Kwenye Dan 5:1 na 30, Belshaza alikuwa ni nani?

J: Herodotus, mwana historia wa Kigiriki akiandika karibu miaka 90 baada ya kuanguka kwa Babeli, hakumtaja Belshaza kabisa na alisema bayana kuwa mfalme wa mwisho alikuwa Nabonidus. Hadi karne ya 20, hayo ndio yalikuwa maneno ya mwisho kuhusu swala hili mbali yale yaliyomo kwenye Biblia. Hili ni moja ya mambo ambayo Wakristo wanaafiki kuwa yatakuja kuelezwa siku moja, bila kujua maelezo yenyewe.
Hata hivyo, kwenye karne ya 20, wataalamu wa elimukale wamegundua jedwali la kikabari liitwalo "Aya ya Kiajemi inayomzungumzia Nabonidus." Belshaza alikwa mtoto wa kwanza wa kiume wa Nabonidus, na baada ya miaka mitatu ya kwanza ya utawala wake (mwaka 553 KK), Nabonidus alikwenda uhamishoni Tema Arabuni kwa hairi yake mwenyewe kwa miaka kumi, na Nabonidus alimteua Belshaza kuwa mtawala. Jambo la muhimu ni kuwa Wababeli walipoishinda Babeli, Nabonidus hata hakuwepo; alikuwa Tema sehemu ya kaskazini ya Saudi Arabia ya leo. When Critics Ask, uk.209 unahitimisha jambo hili, "Kwa kuwa Belshaza chini ya Nabonidus, jina lake lilisahauliwa, kwa sababu wana historia wa Babeli na Ugiriki za zamani walipenda kuongelea tawala za wafalme rasmi. Rekodi za Danieli zimehibitisha kuwa zina usahihi wenye kustaajabisha."
Encyclopedia of Bible Difficulties, uk.286 inataja "maandishi ya Nabunaid" yaliyovumbuliwa huko Uru. Haya yanaweza kuwa ni ile ile "Aya ya Kiajemi inayomzungumzia Nabonidus." Encyclopedia of Bible Difficulties, uk.286 pia unaongezea kuwa nyaraka za vikabari zinasema jinsi Belshaza alivyotoa sadaka za kondoo na ng'ombe kwenye mahekalu ya Sippar kama "matoleo ya mfalme."
Sasa Herodotus anachukuliwa kuwa sahihi kwa ujmla. Kama mtawala mwenza wa Belshaza (chini ya Nabonidus) hakuwa wa maana sana hata Herodotus, alipokuwa anaandika miaka 90 baadaye, alimsahau, ni kwa namna gani Kitabu cha Danieli kinaweza kutarajiwa kuandika jambo hili kiusahihi, isipokuwa kilikuwa tayari kimeishaandikwa kufikia muda huu? Kwa kuwa Danieli alijua jambo hili kuliko Herodotus, kama inavyoshangaza kuwa baadhi ya wanazuoni wenye kutilia shaka msimamo wa asili mwishoni mwa karne ya ishirini bado waliichukulia Danieli kuwa kitabu cha karne ya pili. Tazama 735 Baffling Bible Questions Answered, uk.193 kwa maelezo zaidi kuhusu jambo hili.
Kitabu cha mwenye kushuku Asimov's Guide to the Bible, uk.606 hakitoi maelezo haya, isipokuwa kinasema kuwa Belshaza (Bel-shar-utsur neno linalomaanisha "Bel, mlinde mfalme") alikuwa mtoto wa kwanza wa kiume wa Nabonidus.

S: Kwenye Dan 5:1, je ni hali gani ya hewa ya kisiasa ambamo Danieli aliishi wakati huu?

J: Baada ya Nebukadneza wa sura zilizotangulia kufa mwaka 562 KK, kulikuwa na nyakati za shida. Wana historia wanaiita himaya hii ‘Himaya ya Babeli Mpya', ili kutofautisha na himaya iliyopita iliyokuwa chini ya Hammurapi. Wafuatao ni wafalme wake:
Mwaka 627-605 KK Nabopolassar (Nabu-apal-
usur)
Mwaka 605-Aug/Sep 562 KK Nebuchadnezzar
II Nabu-kudurri-usur)
Mwaka 562-Aug 560 KK Merodach mwovu
(Amel-Marduk) mtoto wa kiume wa
Nebukadneza (aliuawa)
Mwaka 560-556 KK Neriglissar (Nergal-
Sharezer) mkwe wa Nebukadneza
May-June 556 KK (miezi 2) Labashi-Marduk
(aliuawa)
Mwaka 556-539 KK Nabonidus (Nabu-na'ia)
Mwaka 553-Okt 11 au Des 539 KK Belshaza
(Bel-shar-usur) (msaidizi wa mtawala
aliye badala ya mfalme [vice-regents]
kwenye himaya za kale za Umedi na
Uajemi)
Okt 11 au Des 539 KK Gavano wa Uajemi
Ugbar wa Gutium aiteka Babeli
Kwa mujibu wa mwanahistoria wa Kigiriki, Herodotus (1:191) njia waliyotumia kumtaka ilikuwa ya ubunifu mkubwa. Walijenga ziwa "kubwa" ili kuyahamisha maji kwa muda maji ya Mto Frati. Kisha usiku, walitembea chini ya ukuta ambapo Mto Frati ulikuwepo na kuwatokea Wababeli waliokuwa wanafanya sikukuu kwa kushtukiza.

S: Kwenye Dan 5:1, ni kwa jinsi gani Wababeli walikula sikukuu, wakati jeshi kubwa la Waajemi wa Umedi likiwa nje ya kuta?

J: Huenda yalikuwa ni majivuno yao ya jumla ya ulinzi wao, au ilikuwa ni onyesho la kushtukiza la ujasiri wenye lengo la kutisha. Kuta za mji zilikuwa kubwa, na sehemu ya ukuta ilikuwa (inavyoonekana) haiwezekani kushambulia kwa sababu Mto Frati ulipita chini yake. Mji ulijengwa kwa lengo la kuhifadhi chakula kwa muda wa miaka 20.
Pia mama wa Nabonidus alikuwa kuhani mkuu mwanamke wa Harani, mungu wa jua. Aliyafufua mahekalu mengi sana likiwemo hekalu la Sini la mungu jua Harani. Kwa hiyo sababu mojawapo ya kuchukua vyombo toka kwenye hekalu la Yerusalemu yawezekana ilikuwa ni kuonyesha ukubwa wa miungu yao. Sababu nyingine inayofanana nah ii huenda ikawa kuondoa athari ya Nebukadneza ya kumwinua Mungu wa Danieli.

S: Kwenye Dan 5:1-5, kwa nini unafikiri Mungu alichagua kuandika kimiujiza kwenye ukuta, na kutangaza hatima yao muda huu?

J: Kuna sababu mbili. Kwanza, walikuwa wanatumia vitu vya thamani vilivyotolewa kwa ajili ya hekalu la Mungu kutukuza miungu ya kipagani. Pili na huenda ikawa inafanana nay a kwanza, usiku ule wangeweza kuchinjwa na Waajemi. Kwa taarifa yako, Waajemi waliitwaa Babeli lakini hawakuiangamiza mpaka miaka ya baadaye.

S: Kwenye Dan 5:1-5, je Mungu alitimiza ahadi au unabii gani kwa kuandika kwenye ukuta?

J: Kwenye Yer 27:21-22, Mungu alisema vyombo vitakatifu vitahifadhiwa Babeli, mpaka siku atakayovitembelea, kisha vitarudishwa Yerusalem. Hata hivyo, Wababeli hawakupata fursa kubwa sana ya kuvitumia, kabla ya maandishi ya ukutani kutokea.

S: Kwenye Dan 5:2, je vyombo vya kunywea vya dhahabu vilitoka wapi awali?

J: Sulemani alifanya dhahabu na fedha nyingi sana kwa ajili ya Hekalu la Bwana karibu mwaka 950 KK. Kitu cha kufurahisha kuhusu dhahabu ni kuwa hata kama ikufunikwa kwenye udongo haichuji. Hatujui endapo walichukua vyombo vya kunywea vya fedha kutoka hekluni, na fedha ilizuiliwa kuchuja, au endapo vyombo vya kunywea vya fedha havikutoka hekaluni. Kwa uapnde mwingine, ingawa Septuajinti, Vulgate, na Theodotion wanasema vyombo vya kunywea vya dhahabu na fedha, toleo le Kiarami linasema vyombo vya kunywea vya dhahabu tu.

S: Kwenye Dan 5:10, kwa nini "malkia" anamtambulisha Danieli?
J: Belshaza hakufikira kufanya hivi, jambo ambalo linamaanisha kuwa hakuwa na ushirikiano na Danieli, na hakuuthamini ushauri wake. Wakati huu ni miaka 23 baada ya kifo cha Nebukadneza, kwa hiyo Danieli alikuwa na umri mkubwa sana sasa. Neno "maikia" hapa linaweza kuwa linamaanisha mama wa malkia, au pengine mke wa Nebukasneza, aliyemkumbuka Danieli na kumleta.

S: Kwenye Dan 5:25-28, je wageni waliweza kusoma maandishi ukutani?

J: Maneno manne yaliandikwa Kiarami, na Kiarami kilitumika sana Babelli na Uajemi, hivyo huenda watu wote waliokuwa wanajua kusoma waliweza kuyasoma maneno hayo. Hata hivyo, kulitambua fumbo hili kulikuwa hadithi nyingine.

S: Kwenye Dan 5:25-28, je Mene, Mene, Tekel, Upharsin inamaanisha nini?

J: Wanazuoni hawana uhakika wa maana ya maneno haya ya Kiarami. Kuna vitu vitatu vinavo wezekana, na kucheza na maneno kunaweza kuhusisha neno zaidi ya moja.
a) Ni maneno yanayoongelea fedha. Mina, shekeli, na nusu-mina zilikuwa sarafu zilizokuwa zinafahamika sana. Wycliffe Dictionary of Biblical Archaeology, uk.170 ina picha ya ‘mina' moja ya wakati wa Nebukadneza.
b) Maneno haya yalimaanisha umehesabiwa, umepimwa, na umegawanyika.
c) "u" kwenye upharsin inaweza kumaanisha "na." Pharsin ni uwingi wa peres, ambayo inatamkwa karibu sawa na neno lao lenye kumaanisha Waajemi (Persian).

S: Kwenye Dan 5:25-28, je maandishi ya ukutani yalimsaidiaje Danieli?

J: Watu wengi wangeweza kuelewa kwa uhakika kabisa kuwa Daniele alitabiri kuwa Waajemi wangewashinda Wababeli. Kitu cha kukisia ni kuwa endapo Waajemi wangesikia jambo hili wangefurahishwa sana na Danieli, na huenda wangependa kumwacha aendelee kuwa kiongozi wao wa ngazi ya juu.

S: Kwenye Dan 5:29, kwa nini Danieli alifanywa kuwa mtu wa tatu katika ufalme na si wa pili?

J: Belshaza hangeweza kumpa Danieli kitu chochote kikubwa zaidi, kama Nabonidus alikuwa kiongozi mkubwa zaidi, na Belshaza mwenyewe alikuwa wa pili.

S: Kwenye Dan 5:29b, je halikuwa jambo la kawaida kuwa na mtu wa tatu katika ufalme?

J: Hapana, maandishi ya Kiashuri na Kibabeli yanasema kuhusu kuwepo kwa mtu wa tatu katika ufalme. "Mtu wa tatu" anaweza kuwa kama waziri, au "meneja" chini ya mfalme na warithi wake. Kuwepo kwa watu wengi wenye uwezo wa kurithi kunaweza kuwa kwa salama zaidi inapotokea wafalme wawili wa juu wanakufa ghafla.

S: Kwenye Dan 5:30, orodha ya wafalme wa Babeli ni ipi?

J: Wana historia wanaiita himaya hii ‘Himaya Mpya ya Babeli', ili kuitofautisha na himaya ya zamani iliyokuwa chini ya Hammurapi. Wafuatao ni waflme wake:
Mwaka 627-605 KK Nabopolasa (Nabu-apal-
usur)
Mwaka 605-Aug/Sep 562 KK Nebukadneza II
(Nabu-kudurri-usur)
Mwaka 562-560 KK Merodaki mwovu (Amel
-Marduk) mtoto wa kiume wa
Nebukadneza
Mwaka 560-556 KK Neriglissar (Nergal-
Sharezer) mkwe wa Nebukadneza
Mwaka 556 KK (miezi 2) Labashi-Marduk
Mwaka 556-539 KK Nabonidus (Nabu-na'ia)
Mwaka 553-10/12/539 KK Belshaza (Bel-shar-
usur) (msaidizi wa mtawala aliye badala
ya mfalme [vice-regents] kwenye himaya
za kale za Umedi na Uajemi)

S: Kwenye Dan 5:30-51 na 9:1, kuna tofauti gani kati ya Umedi na Uajemi?

J: Swali hili ni gumu kuliko linavyoonekana kwa mara ya kwanza. Kuna mambo matatu ya kuzingatia katika kulijibu.
1.
Wamedi na Waajemi walikuwa jamii mbili tofauti lakini zilikuwa na uhusiano. Wamedi walihusiana kwa karibu zaidi na Wasinthia (walioishi ukanda wa zamani wa kusini mashariki mwa Ulaya na Asia) na waliishi Irani ya Kati, wakati Waajemi waliishi Elamu ya zamani kusini magharibi mwa Irani. Jamii hizi zilikuwa zinashirikiana kwa pamoja, huku Wamedi wakiwa washiriki wenye nguvu zaidi. Hali hii ilibadilika wakati wa utawala ya utawala wa Koreshi (Muajemi aliyekuwa na robo), wakati alipomshinda Astyges, babu yake Mmedi, mwaka 625 KK. Kuanzia wakati huo, Waajemi walikuwa na nguvu zaidi, na Herodotus 3.91-96 inasema Wamedi walitakiwa kuilipa Himaya ya Uajemi kodi ya mwaka.
2.
Hata hivyo, Herodotus 1.135 pia inasema Waajemi waliyafanya mavazi ya Kiajemi kuwa yao. "Kama Widengren anavyosema, ‘Mara nyingi Wagiriki waliwaita Wamedi na Waajemi ‘Wamedi', na ushahidi wa kuitwa hivi umeonekana wakati wa kukutana kwao na Wagiriki kwa mara ya kwanza huko Ionia na Wairani wa magharibi." Waajemi walijulikana kuwa Wamedi hadi kwenye enzi za Demosthenes, karne ya nne KK" (Persia and the Bible, uk.56-57).
3.
Kwenye Biblia, walichukuliwa kuwa jamii moja, "Wamedi na Waajemi", kwenye Dan 6:8, 12, 15, na "Waajemi na Wamedi" kwenye Est 1:3, 14. Persia and the Bible, uk.57 pia inasema kuwa majina haya yaliitwa "Wamedi" tu kwenye Isa 13:17 na kuendelea na Yer 51:11, 28).

S: Kwenye Dan 5:30-6:1 na 9:1 kwa ufupi sana, Dario Mmedi alikuwa ni nani?

J: Watu wengi wanafikiri alikuwa gavana wa kwanza wa Babeli, aliyeitwa Gubaru, ingawa wengine wanafikiri alikuwa ni Koreshi mwenyewe. Sababu ya kusema ni Dario ni ama:
a) kosa la kunakili wa hati yenye maandiko,
b) jina la kifalme la Koreshi, au
c) Wayahudi hawakuwa na tafsiri nzuri ya jina "Gubaru."
Angalia swali lifuatalo kwa jibu refu zaidi.

S: Kwenye Dan 5:30-6:1 na 9:1 huyu Dario Mmedi alikuwa ni nani?

J: Kwanza kuna mambo kadhaa ya kihistoria, kisha ya kibiblia, na mwishoni maoni matatu.
1. Mambo ya Kihistoria
1.1 Historia ya Wamedi
imetazamwa upya kutoka vyanzo vya Kiashuri, Kibabeli, Kiajemi na Kigiriki, kwani hakuna maandiko ya Kimedi ambayo yamegundulika. Mwana historia mwangalifu wa Kigiriki, Herodotus, alisema kuwa alisikia masimulizi manne tofauti ya maisha ya utotoni ya Koreshi. Ctesias alikuwa mwana historia mwingine wa Kigirik, lakini hakuwa anaaminika sana.
1.2 Mwaka 625 KK
, Wamdei waliwashinda
Waajemi na kuwatawala hadi mwaka 553 KK.
1.3 Kutoka mwaka 553 hadi 550 KK
, Muajemo Koreshi Mkuu aliasi na kufanikiwa kwa msaada wa Harpagus, chifu wa Kimedi (mwaka 550 KK). Wamedi bado walikuwa na nafasi ya juu zaidi baada ya Waajemi, na kama matoleo ya mwaka 1956 na 1972 ya Encyclopedia Britannica yanavyosema, "Wamedi wengi maarufu waliajiriwa kama viongozi, maliwali, na majemedari."
1.4 Astyages
(Kwa Kimedi, Ištumegu) alikuwa mfalme wa Kimedi aliyepinduliwa na Koreshi mwaka 550 KK. Mwana historia Ctesias anasema kuwa Koreshi alikuwa mwema kwa Astyages, na alimfanya kuwa liwali wa Barcania au Hyrcania, lakini Oebares (kwa Kibabeli Ugbaru) alimuua Astyages.
1.5 Kwenye Himaya ya Kiajemi,
Medi lilikuwa moja ya majimbo 20 ya Himaya ya Uajemi yaliyokuwa yanaongozwa na maliwali, lakini liligawanyika sehemu mbili kwa sababu za kodi. Kama wazo la ziada, majimbo haya 20 yaligawanywa kwenye wilaya 120, ambazo wakati mwingine nazo ziliitwa majimbo (satrapies), bali kwa kweli zilikuwa hyparchs.
1.6 Ugbaru,
gavana wa Kibabeli wa Gutium (kwa mujibu wa orodha ya matukio ya Nabonidus), alihamia upande wa Waajemi na kuwa jenerali wa jeshi la Uajemi liliiangusha Babeli tarehe 11 au 12 Okt mwaka 539 KK. Alikufa 6/11/539 KK, karibu mwezi mmoja baadaye. Ingawa hatujui ukoo wake, kamusi ya wenye kutilia shaka msimamo wa asili Anchor Bible Dictionary, juzuu ya 2, uk.39 kinasema kuwa Wababeli walitumia neno Gutium kumaanisha Kaskazini mashariki, na Wamedi waliishi sehemu ya kaskazini mashariki ya Himaya ya Babeli. Pia kinasema kuwa mwana historia Berossus alimworodhesha Gutium pamoja na watawal makatili wa Wamedi.
1.7 Koreshi mwenyewe
alikuwa na vikosi vingine huko Opis wakati Babeli ilipotekwa, na Koreshi hakuingia Babeli hadi 29/10/539 KK. Koreshi alisemekana kuwa mjukuu wa Astyages, kupitia binti wa Astyages aliyeitwa Mandane. Hata hivyo, the Wycliffe Bible Dictionary, uk.424 inaonyesha kuwa huyu hakuwa Mfalme wa Uajemi, kwa sababu Dario hapa inamaanisha "alifanywa mfalme." Danieli naye aliitwa "mfalme" kwenye Dan 5:29, na hakuwa mfalme.
1.8 Gubaru/Gaubaruwa
(ambaye Mgiriki Xenophon alimchanganya na Ugbaru), alichaguliwa na Koreshi kuwa gavana wa Babeli kwa mwaka mmoja au miwili.
1.9 Dario I, mtoto wa kiume wa Hystaspes/Vishtaspa
, alikuwa Muajemi (siyo Mmedi) aliyekuwa mfalme mwaka 522 KK, baada ya Koreshi na Bardiya wa uongo kutawala. Dario I alihusika na kuzimisha uasi huko Babeli mwaka 520 KK, miaka 19 baada ya Uajemi kuishinda Babeli. Encyclopedia of Bible Difficulties, uk.287 inaonyesha kuwa alikuwa na miaka ishirini na alipoanza kutawala, si miaka 62. Kamusi ya wenye kutilia shaka msimamo wa asili Anchor Bible Dictionary, juzuu ya 2, uk.39 inasema kuwa maandishi yake yanasema "Mimi ni Muajemi, mtoto wa kiume wa Muajemi."
1.10
Kwenye ulimwengu wa kale, wafalme wa Misri na sehemu nyingine walikuwa na majina waliyopewa wakati wa kuzaliwa, na jina la pili lilitolewa wakati wa kuanza kutawala.
1.11
Neno la Kiajemi Dario "Darayawush/Dareyawaes" linahusiana na neno la Kiajemi dara linalomaanisha mfalme. Encyclopedia of Bible Difficulties, uk.288 inasema hikli linaweza kuwa ni cheo na jina la mtu. Kamusi ya wenye kutilia shaka msimamo wa asili Anchor Bible Dictionary, uk.39 pia inasema kuwa darayarahu inamaanisha "Yeye ashikiliaye mema." Hii ndiyo sababu ya nadharia kuwa Dario lilikuwa ni jina la cheo.
1.12
Mwaka huo huo au miwili wa kuteka, Koreshi almfanya mtoto wake wa kiume Cambyses kuwa gavana wa Babeli, akichukua nafasi ya Gubaru.
1.13
Kwenye Agano la Kale kuna makosa kadhaa ya kunakili, hasa kwenye namba na majina. Kwa mfano, toleo la Kigiriki la Proto-Theodotion linasema "Artashasta (Artaxerxes)", na si "Dario" kwenye Dan 6:1. Kuna nyongeza kadhaa kwenye tafsiri ya Kigiriki (Septuajinti) kwenye Kitabu cha Danieli. Jerome anasema kuwa ingawa kanisa la awali lilitumia Septuajinti, hawakutumia Septuajinti ya Kitabu cha Danieli, lakini toleo la Kigiriki la Theodotion. Inaelekea waliona makosa mengi sana kwenye Septuajinti ya Danieli.
1.14
Nakala zetu zote za "Kiebrania" za Danieli zina zina sehemu ya kati ya Danieli, 2:4b-7:28, iliyoandikwa kwa Kiarami, si Kiebrania. Huenda iliandikwa Kiarami toka mwanzoni, au ilitafsiriwa kutoka kwenye hati yenye maandiko ya kale ya Kiebrania.
2. Mambo ya Kibiblia

Dario wa kwenye Kitabu cha Danieli alikuwa Mmedi, mwenye miaka 62, aliyekuwa na wilaya/majimbo 120 ya utawala chini yake. Alikuwa mtoto wa Ahasuero. Alikuwa na uwezo wa kutoa amri, na aliabudiwa. Kwenye Dan 6:6, aliitwa mfalme. Kutoka Dan 9:1, huyu Dario, alisistiziwa kuwa Mmedi, siyo Dario Muajemi. Encyclopedia of Bible Difficulties, uk.287 inasema kuwa kitenzi cha kawaida malak kinamaanisha fanyika kuwa mfalme, lakini kitenzi homlak hapa, ambacho ni kitendewa na kinamaanisha kufanywa mfalme. Kamusi ya wenye kutilia shaka msimamo wa asili Anchor Bible Dictionary, juzuu ya 2, uk.39 pia inaonyesha jambo hili. Hivyo, mtawala mwenye mwenye mamlaka makubwa zaidi amemfanya kiongozi. Pia, maneno "dunia yote" yanaweza kutafsiriwa kuwa "nchi yate."
3. Dario Mmedi ni nani hasa

Kwa kuwa Dario ndiye aliyeiteka Babeli, kuna mambo matatu yanayowezekana:
3.1 Koreshi:
Huyu alikuwa Koreshi hasa, na jina lisilokuwa sahihi liliandikwa, sawa na jinsi jina Yehoakimu lilivyoandikwa kimakosa kwenye Yer 27:1 kwenye nyingi ya hati zenye maandiko za Kiebrania wakati mandhari na hati zenye maandiko ya kazi za kale vinaonyesha kuwa ilikuwa Zedekiya. Ingawa Koreshi alikuwa Muajemi, mama yake, Mandane, alikuwa Mmedi na binti ya Astyages, na chifu wa Kiajemi Cambyses. Huenda ni kweli kuwa alikuwa robo Mmedi na mjukuu wa mfalme wa zamani, au alidai kuwa hivyo ili aungwe mkono na Wamedi.
3.1.1
Kwa kuwa wafalme wengi walikuwa na majina ya vyeo, Koreshi anaweza kuwa alikuwa na jina la cheo la Dario Mmedi. Dan 6:28 inaweza kutafsiriwa kuwa "utawala wa Dario, ‘hata' utawala wa Koreshi Mmedi." Maoni haya yanaungwa mkono na D.J. Wiseman, na John F. Walvoord anasifia maoni haya kwenye Daniel: The Key to Prophetic Interpretation, uk.134. The Bible Knowledge Commentary: Old Testament, uk.1347 pia inasema kuhusu maon haya lakini inapendelea maoni yanayofuata kuhusu Gubaru. Mifano mingine ya majina yanayofanana au majina ya vyeo yaliyotumiwa kwenye Biblia ni:
Yoramu kwa Yehoramu (2 Fal 8:23)
Yehoashi kwa Yoashi (2 Fal 12:1)
Koniya kwa Yekoniya (Yer 22:28)
Shalumu kwa Yehoahazi (Yer 22:11, 2 Fal 23:30-34)
3.1.2
Koreshi hakuwa na jina la cheo Dario. Jina Dario limekuja hapa kama kosa la kunakili, likichanganya Koreshi kuishinda Babeli mwaka 539 KK na Koreshi kuishinda Babeli mwaka 522 KK.
3.2 Gubaru
ametajwa hapa, kwa kuwa Koreshi alimteua kuwa gavana wa Babeli, kama When Critics Ask, uk.295 inavyoafiki. Hata hivyo, hatuna rekodi ya kihistoria inayosema ama Gubaru alikuwa Mmedi au la. Ama Dario ni namna Waebrania walivyomwita Gubaru, au mwandishi wa Kiebrania aliyekuwa amechanganyikiwa aliandika jina Dario. Ingawa jina Gubaru lilichukuliwa nafasi yake na jina Cambyses baadaa ya mwaka mmoja au miwili, Kitabu cha Danieli hakisemi kitu chochote baada ya mwaka wa kwanza. Magavana walikuwa wakiitwa "wafalme", kwa sababu Maandishi ya Behistuni yanasema kuwa Hystaspes "alifanywa mfalme" na Koreshi, kama Encyclopedia of Bible Difficulties, uk.287-288 inavyosema.
3.3 (si jibu) Dario
hapa watu wengine wanaweza kufikiri kuwa ni Dario I (Muajemi) wa kweli, na patakuwa na pengo la mika 19 kati wa kupinduliwa kwa Wababeli kwenye Dan 5:30, na Dario aliyeelezwa mwishoni. Hata hivyo, jambo halielekei kuwa hivyo kwa sababu kitabu hiki kinasema bayana kuwa Dario huyu alikuwa Mmedi. Isitoshe, hakuna aya ya Biblia inayosema kuwa Dario huyu alikuwa juu wa Wamedi na Waajemi wote, bali alifanywa mfalme kwa Wababeli tu.
Muhtasari:
Kwa kuwa maoni ya tatu hayana uwezekano wa kuwa kweli, mtu aliyekusudiwa hapa ni ama:
S1.
Gubaru, gavana wa kwanza wa Babeli chini ya utawala wa Koreshi, au
S2
. Koreshi. Ama Dario lilikuwa ni jina la cheo la Koreshi, ama waandishi walifanya makosa katika hati zao za maandiko, wakati ilitakiwa iandikwe Koreshi.
Makosa ya kunakili na mabadiliko si vitu vigeni kwenye Agano la Kale, na Septuajinti ya Kitabu cha Danieli ina mabadiliko kadhaa yanayofahamika.

S: Kwenye Dan 5:31, je Babeli ilitekwa lini?

J: Wataalamu wa mambo ya kale wanaamini kuwa ilikuwa usiku wa Oktoba 11 au 12, 539 KK. Hata hivyo, ni muhimu kuelewa kuwa Babeli haikubomolewa mpaka baada ya miaka kupita.

S: Kwenye Dan 5:31; 6:1 na 9:1, jina "Dario" linatamkwaje?

J: Cruden's Concordance na The New International Dictionary of the Bible, uk.254 zina da-RI-us, yenye ‘a' na ‘u' fupi, ‘i' ndefu, na kiinitoni kwenye silabi ya pili. Waebrania walilitamka daryawesh, na Wagiriki walilitamka Darious. Wamedi na Waajemi walilitamka jina la Dario sawa na "Darayawush / Dareyawaes."

S: Kwenye Dan 6:1, nani walikuwa maliwali 120?

J: Hawakuwa watoto wa kiume wa Dario, bali watawala 120. Kulikuwa na majimbo 20 yaliyoitwa ‘satraps', lakini yaligawanyika kwenye wilaya 120, ambazo wakati mwingine pia ziliitwa ‘satraps', ingawa walikuwa "wasaidizi wa mtawala aliye badala ya mfalme (vice-regents) kwenye himaya za kale za Umedi na Uajemi" kiuhalisi. Watu hawa hawakuwa majenerali wa majeshi lakini wahasibu, "ili kwamba mfalme asipate hasara." Hebu fikiri una mtu ambaye siyo tu mwenye busara, bali pia unajua kuwa unaweza kuamini uasilifu wake hata unapokuwa humwangalii. Bila shaka mfalme atakuwa alimthamini Danieli kwa kiasi kikubwa sana, nah ii ndiyo sababu alikuwa miongoni mwa viongozi wakuu wa uhasibu.

S: Kwenye Dan 6:1-5, kwa nini maliwali walikusudia kumtia Danieli matatizoni?

J: Huenda ni kwa sababu mbili:
Wivu:
Danieli alikuwa mgeni, Myahudi, aliyepandishwa cheo mara moja na kuwa juu yao.
Kutokuwa na upendo:
Hata kama hawakuwa na chuki au hisia mbaya dhidi ya Danieli, baadhi ya watu wasiokuwa waadilifu huwa hawaogopi kuwaondoa wandani wao ili kuweza kuendelea na mambo wanayoyafanya.
Kwa hiyo kitu cha kwanza walichokifanya ni kufanya uchunguzi wenye matumaini ya kupata habari. Kwa kuwa wengi wa viongozi hawakuwa waadilifu, walichunguza ili kufahamu uozo wa Danieli ili wautangaze. Huenda walifikiri kuwa kuutangaza uozo au uzemba wa Danieli watakavyochagua kutangaza ndilo jambo pekee walilotakiwa kulifanya. Hata hivyo, mawazo haya hayakuwa ya viongozi wote. Walipokuja kufahamu bila kutarajia kuwa hawakuona kitu chochote kibaya, kwenye mstari wa tano walitafuta ‘mpango mbadala', na kuangalia kitu kinachohusiana na sheria ya Mungu. Si kila mtu anayesoma neno la Mungu anakuwa amesukumwa na nia njema.

S: Kwenye Dan 6:6-9, je waliwezaje kuwafanya viongozi kwenye himaya yote kukubaliana na mpango huu?

J: Hawakuweza. Huenda walitegemea kuwa viongozi wengine watakubaliana na mpango huu bila kupinga. Kumbuka kuwa endapo kiongozi mpagani wa kawaida alikubali kupendekeza amri hii, asingeweza kujua kuwa lengo la mpango huu lilikuwa kumtega Danieli na huenda na Wayahudi wengine. Vinginevyo, wanaweza kuwa hawakuwahi kubaliana kabisa na walijua kuwa hawakuwasilisha ukweli kuwa walikuwa na uwezo wa kufikia makubaliano. Pia kumbuka kuwa walimdanganya Dario waliposema kuwa viongozi "wote" wamekubaliana. Danieli hakuwa amekubaliana na jambo hilo.

S: Kwenye Dan 6:6-9, kwa nini Dario alitoa amri hii kuwa mtu yeyote asiombe kwa mungu au mtu yeyote yule kwa muda wa siku thelathini?

J: Ingawa Maandiko hayasemi, tunaweza kukisia sababu kadhaa:
Kupitisha uamuzi bila kuuzingatia:
Dario aliambiwa (huenda kwa uongo) kuwa maliwali wengine wote walikubaliana na wazo hili. (Kwa hakika hawakukubali wote, kwani Danieli hakuwa amefanya hivyo). Kwa kuwa Dario aliwaamini watu wake, alisaini tu kitu walichosema.
Mshikamano wa himaya:
Kundi kubwa na lenye nguvu la watu waliokuwa wanatawaliwa na serikali ya kigeni, Wababeli, mpaka wakati karibu na huo walikuwa huru na wanapigana kwa ajili ya Himaya ya Uajemi. Jambo hili lingetia mkazo kwa Wababeli na watawaliwa wa zamani wa Himaya ya Babeli kuwa hawako chini ya Wababeli tena bali sasa wako chini ya Waajemi. Kwa hiyo walitakiwa kuacha kumwabudu Marduku, au miungu mingine ya Babeli kwa siku thelathini, kwa sababu Waajemi walichukuliwa kuwa wakuu kwani waliweza kutoa amri ya kusitisha ibada kwa miungu mingine. Watu ambao wangekataa wangetambuliwa kuwa waasi na kushughulikiwa ipasavyo.
Majivuno yasiyo na maana:
Dario angeheshimiwa, si tu kwamba watu walikuwa wanamwabudu na kumwomba, lakini hawangekuwa wanamwomba mungu au mtu mwingine yeyote yule kwa siku thelathini.

S: Kwenye Dan 6:6-9, kuna ushahidi wowote wa elimukale wa amri hii ya siku thelathini?

J: Hapana, lakini hili ni jambo ambalo Mfalme Dario hangependa likumbukwe.

S: In Dan 6:10, should we always kneel or do another posture when praying?

J: Ndiyo na Hapana. Hapana, Biblia haituamuru kutumia mkao wowote maalumu tunaposali. Wakati mwingine watu waliomba:
Huku wakipiga magoti
(Ezr 9:5-6; Dan 6:10; Luk 22:41; Mdo 7:59-60; Efe 3:14)
Kuanguka kifudifudi
(Mwa 17:17, 18; Yos 6:7-9; Mat 26:39)
Kupiga magoti au kuanguka kifudifudi
(Mak 14:35)
Kusimama wima
(Mwa 18:22-23; 24:11-13; Neh 9:4-5)
Kukaa
(2 Sam 7:18; 1 Fal 19:4)
Kulala kitandani
(2 Fal 20:2)
Bila kuweza kubadilisha mkao
(Amu 16:28; Neh 2:3-4; Yon 2:1; Mat 27:46; Mak 15:34; Luke 23:46).
Hata hivyo, tuna uhuru wa kutumia mkao wowote utakaoyafaa maombi tuombayo.

S: Kwenye Dan 6:10, je ni vizuri kuwa na muda maalumu wa kuomba?

J: Ndiyo. Ingawa Biblia haisemi tusali wakati fulani, waamini wengi wameona kuwa inasaidia zaidi kuwa na wakati maalumu wa kusali. Maombi ya mara kwa mara yanahitaji nidhamu, na kuwa na wakati maalumu wa kusali kunasaidia kufikia lengo hili.

S: Kwenye Dan 6:10, je tunapaswa kuelekea Yerusalemu wakati tunasali? Je Mungu anayasikia vizuri maombi tuyafanyayo tukiwa tumeelekea upande fulani?

J: Kwenye nyakati za Agano Jipya upande tunaoelekea wakati wa kusali hauna umuhimu wowote. Kwenye nyakati za Agano la Kale hakuna amri ya kuelekea Yerusalemu, au kuelekea kwenye hekalu wakati wa kusali, lakini Danieli alikuwa anafikiria maombi ya Sulemani ambapo alimwomba Mungu kuwasikiliza watu watakaomwomba kuelekea hekalu na kuelekea Yerusalemu kwenye 1 Fal 8:29, 42, 44, 48. Mungu alizungumza na kujibu ombi la Sulemani kwenye 1 Fal 9:3-9 kwa njia chanya na inayotia moyo, lakini Mungu hakusema kitu chochote kuhusu kusikia maombi vizuri zaidi ikiwa mwombaji ataelekea upande wowote ule. Mungu alisema kuwa ingawa hekalu lilikuwa zuri na lenye kuvutia, siku inakuja ambapo watatishwa na uwanja wa hekalu.

S: Kwenye Dan 6:10-11, je unaweza kufanya nini ikiwa unapenda kumcha Mungu kwa kufanya kitu fulani, ikiwa kuendelea kufanya hivyo kutaleta hasara kifedha, aibu, au hata kitu kingine kibaya zaidi?

J: Ningejaribu kuona endapo kuna njia ya kuendelea kufanya kitu hicho na kutokupata hasara. Hata hivyo, si tu kwamba Wakristo wasiwe waovu, bali pia waepushe kitu chochote chenye mwonekano wa uovu. Katika nyakati za kanisa la awali, Wakristo waliamriwa kutoa kafara kwa mfalme kama kwa Mungu. Wakristo wengi walichagua mateso na kifo kuliko kuabudu sanamu. Lakini wengine walikuwa wanyonge na walifanya dhambi kwa kutoa kafara. Ikiwa mtu alitoa rushwa ili kwamba asitoe kafara lakini alimhonga kiongozi wa umma aliyesema kuwa ametoa kafara, bado hangekuwa anamcha Mungu kwa sababu ya kuwa na mwonekano wa kufanya dhambi ya kutoa kafara.

S: Kwenye Dan 6:10-11, je Danieli alinunua mapazia? Kwa kutumia sitiari, ni wakati gani tunatakiwa kununua mapazia leo hii? Na vipi kuhusu kusali sirini?

J: Kusali sirini, mbali na watu wasio amini ni kitu kizuri, lakini Yesu alituagiza kusali sirini kwenye Agano Jipya (Mat 6:5-8) si Agano la Kale, na Agano Jipya lilikuwa bado halijatolewa wakati ule. Mapazia yasingeweza kusaidia kitu, kwa sababu watu wale waliishajua kuwa aliomba, na wangekuja kumwona, kama walivyofanya kwenye Dan 6:11.

S: Kwenye Dan 6:12, je simba hawa walifanana na kitu gani?

J: Simba walikuwa wanazunguka Mashariki ya kati hadi watu walipowawinda na kuwamaliza. Watu wengi, hasa Waashuri na Waajemi, walipenda kuwawinda. Samsoni alimuua simba Israeli kwenye Amu 14:5. Makala yenye kufurahisha sana yenye kichea ‘Simba wa Mwisho wa Asia' kwenye The National Geographic Magazine (Juni 2001), uk.46-61. Simba wa Asia walikuwa wadogo kiasi kuliko simba wa Afrika, walikuwa na manyoya mafupi, na walikuwa na fundo la ngozi kwenye pande zao za chini ambazo simba wa Afrika hawana. Eneo lao lilikuwa kuanzia kaskazini mwa India kupitia Iraki, hadi Ugiriki, Bulgaria na Albania.

S: Kwenye Dan 6:14, kwa nini Biblia inasema Dario alijaribu kumuokoa Danieli kwani kwenye Dan 6:16 mfalme aliamuru Danieli atupwe kwenye simbo la simba?

J: Kwa sababu aya zote zilikuwa sahihi. Huyu alikuwa mtu mwenye nguvu asiyeamini, ambaye anaweza kuwa alifikiri kuwa ni kiongozi mzuri na mwenye haki, ambaye kwa ujumla alipenda kumsaidia Danieli, lakini utiifu wake kwa mila ulikuwa mkubwa kuliko utiifu wake kwa mambo ya haki. Leo hii kuna watu wengi ambao mara nyingi hupenda kufanya mambo ya haki, lakini mila zao au mambo yaliyotangulia ndio kipimo chao kikuu, na cha muhimu zaidi kuliko dhamiri zao za kumfuata Mungu.

S: Kwenye Dan 6:24, je hakikuwa kitendo cha ukatili kuwatupa kwenye shimo la simba wake na watoto wa watu waliokuwa wamemshtaki Danieli?

J: Biblia haisemi kuwa Wababeli hawakuwahi kuwa wakatili, au kuwa walifanya vitu sahihi kila wakati. Lakini ikilinganishwa na Waashuri waliokuwa wanajisifu kwa kutesa watu, Waajemi walikuwa wapole.

S: Danieli 7 ilitokea kabla ya Danieli 6. Kwa nini unadhani mfuatano uko hivi?

J: Sura zilizotangulia zinaongelea maisha ya Daniele. Haya ni maono ambayo hayana uhusiano na maisha ya Danieli. Maono haya yalitokea karibu mwaka 556-553 KK.

S: Kwenye Dan 7:2, je pepo za mbinguni zinawakilisha kitu gani? Kwa nini kuna pepo nne?

J: Pepo nne zinaweza kuwa roho zinazoathiri himaya nne.
The Expositors Bible Commentary, juzuu ya 7, uk.85 inasema pepo nne zimedhibitiwa kwa namna fulani hadi wakati wa kuachiwa kwao, na malaika wanne kwenye Ufu 9:14. Hata hivyo, kuna ushahidi kidogo sana wa jambo hili.

S: Kwenye Dan 7:2, bahari inawakilisha kitu gani?

J: Bahari inaweza kuwa inawakilisha umati wa watu. The Expositor's Bible Commentary, juzuu ya 7, uk.85 inasema hivyo hivyo.

S: Kwenye Dan 7:3-7, 17-19, je wanyama wanne ni wapi?

J: Dan 7:17 inasema hawa ni wafalme au falme nne. Falme hizi ni Babeli, Uajemi ya Umedi, Ugiriki/Makedonia, na Rumi. Hivi ndivyo zinavyoendana na picha hii:
Simba mwenye mabawa:
Viumbe wanaoonekana kama simba wenye mabawa wakiwa wamelifunika lango lenye kuonekana vizuri sana la Ishtari huko Babeli. Pia, upande wa mbele wa chumba cha enzi ya Nebukadneza kwenye jumba la makumbusho la Verderasiatisches huko Berlin linaonyesha simba ambao awali walipakwa rangi za njano, nyeupe, bluu na nyekundu. Picha ya mchoro huu ipo kwenye kitabu kiitwacho Babylon kilichoandikwa na Joan Oates, uk.150.
Babeli iliitwa simba kwenye Yer 4:7. Farasi wa Babeli walikuwa wanakimbia haraka kuliko tai kwenye Yer 4:13. Babeli na Misri waliitwa tai kwenye Eze 17:3, 7. Baadaye, Wababeli waliwatenda mema Wayahudi, wakati Danieli alipokuwa kwenye makazi ya mfalme. Hab 1:8-9 haihusiki hapa, kwani farasi wa Wababeli wanalinganishwa na chui na mbwa mwitu na tai.
Dubu aliinuliwa upande mmoja:
Himaya ya Uajemi ya Umedi ilikuwa na sehemu mbili, huku upande wa Kiajemi ukiwa na nguvu zaidi.
Chui mwenye mabawa manne na vichwa vinne:
Ingawa chui ni mnyama mkubwa wan chi kavu mwenye kasi zaidi, anayefikia mwendo kasi wa km 97 (maili 60) kwa saa, chui mwenye mabawa manne atakuwa na mwendo kasi mkubwa zaidi. Alexander Mmakedonia aliishinda himaya yote ya Uajemi na hata sehemu za India katika miaka kumi na tatu ya kushangaza. Baada ya kifo chake, himaya iligawanywa miongoni mwa majemadari wake wanne. Ingawa chui wa Afrika hakuwa alama ya kawaida ya Wagiriki, hakuna mnyama mwingine muwindaji ambaye aliyeweza kuwakilisha mwendo kasi wa ushindi wa Alexander vizuri zaidi.
Mnyama mwenye meno ya chuma:
Mnyama wanne alikuwa tofauti, alikuwa na mapembe, na alikuwa na kiburi. Wafalme wa Rumi walijiita miungu, na hata sadaka za kila mwaka zilitolewa kwao.
Isitoshe, watu wengi wanaona utimilifu wa pande mbili wa unabii huu, huku mpinga Kristo akiwa anakuja kutokea himaya iliyofufuliwa ya Rumi.
Kitabu cha mwenye kushuku kiitwacho Asimov's Guide to the Bible, uk.610 kinadai kuwa chui alikuwa HImaya ya Uajemi, vichwa vyake vine vilikuwa wafalme wanne walikuwa wanajulikana na Danieli, na mnyama wanne alikuwa himaya ya Alexander. Asimov anasema hivi kwa sababu anajaribu kutenganisha Himaya ya Umedi na Himaya ya Uajemi. Hata hivyo, Wamedi, mbali na kuwasaidia Wababeli kuiangusha Ashuri, kupigana na Wasinthia, na kuungana na Waajemi, hawakuwa na mambo mengine yenye kuhusika na historia ya ulimwengu waliyoyafanya kama himaya uhuru.

S: Kwenye Dan 7:3-7, 17-19, badala ya Himaya ya Rumi, je mnyama wanne anaiwakilisha dola kamilifu ya Kiyahudi, kama kitabu cha mwenye kushuku Asimov's Guide to the Bible, uk.610-611 kinavyosema kuwa jambo hili linauwezekano mkubwa zaidi wa kuwa hivyo?

J: Hapana. Isipokuwa Asimov anafikiri kuwa Wayahudi walikuwa na mawazo kuwa dola kamilifu ya Uyahudi ilikuwa ni kitu kibaya na kiovu, Asimov amechanganyikiwa sana hapa. Dan 7:7 inasema, ". . . na tazama, mnyama wa nne, mwenye kutisha, mwenye nguvu, mwenye uwezo mwingi, naye alikuwa na meno ya chuma, makubwa sana; alikula na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake; na umbo lake lilikuwa mbali kabisa na wale wa kwanza, naye alikuwa na pembe kumi." Kwenye Dan 7:11 inasema, ". . . nalitazama hata mnyama yule [wa nne] akauawa, mwili wake ukaharibiwa, akatolewa akateketezwa kwa moto." Mungu ndiye aliyemuua mnyama wanne, hivyo ni dhahiri kuwa mnyama huyu si dola yenye kumcha Mungu.

S: Kwenye Dan 7:5, je mbavu tatu zinawakilisha kitu gani?

J: Kuna maoni matatu tofauti:
Uajemi iliyotangulia
ilikuwa na falme tatu: Misri, Ashuri na Babeli. Kwa mijubu wa vigezo vilivyopo, Uajemi haikuishinda Ashuri, kwa sababu Ashuri ilikuwa tayari imefanyika sehemu ya Himaya ya Babeli, ambayo Uajemi iliishinda.
Himaya zilizoshindwa na Uajemi
zilikuwa tatu: Misri, Babeli, na Lidia. Himaya nyingizaidi hadi kufikia wakati huu ziliishinda himaya moja tu iliyotangulia. Hata hivyo, Uajemi ilzishinda tatu.
Pembe badala ya mbavu
ndivyo toleo la Biblia la Kiingereza la NRSV linavyotafsiri maneno haya. Hata hivyo, majibu mawili yaliyotangulia yanaeza kutumika kwa pembe, kwa hiyo wazo hili ni lenye mjadala.
Hitimisho:
Kwa kuwa mbavu zilikuwa kwenye mdomo wa dubu, zitakuwa ni falme tatu "zilizoliwa" na dubu. Hivyo, Misri, Babeli na Lidia ni tafsiri sahihi.

S: Kwenye Dan 7:7-9, 20, 24, je pembe kumi ni nini?

J: Dan 10:24 inatuambia kuwa hizi ni falme tatu. Mfalme wa mwisho huenda akawa ndiye Mpinga Kristo kwenye himaya iliyofufuliwa ya Rumi. Pembe kumi kwenye mnyama mwekundu zimeongelewa kwenye Ufu 17:3, 12-14.

S: Kwenye Dan 7:9, je Mzee wa Siku alipokuja, kwa nini viti vya enzi (wingi) viliwekwa?

J: Viti kadhaa vya enzi kwa ajili ya Baba, Mwana wa Adamu. Hata hivyo, "hukumu ikawekwa" kwenye Dan 7:10b, kwa hiyo inaweza kuwa ni wazee na huenda hata sisi pia, tunaowahukumu malaika.

S: Kwa nini Dan 7:13-14 ni aya nzuri kuwashirikisha Wayahudi na Mashahid wa Yehova?

J: Inamtaja Mzee wa Siku (Mungu Baba), na mmoja kama mwanadamu akija kwa Mzee wa Siku, kisha mamlaka ilipewa kwa mwanadamu, na watu wanaomwabudu kiusahihi. Maneno haya yanamuongelea Yesu Kristo.

S: Kwenye Dan 7:16 na 9:21, Gabrieli ni nani?

J: Gabrieli ni malaika mkuu aliyetumwa kupeleka ujumbe kwa Danieli, na baadaye kwa Maria Mama wa Kristo kwenye Luk 1:19, 26.

S: Kwenye Dan 7:25, je muda wa watakatifu kutiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili na nusu wakati?

J: Muda huu ni sawa na kipindi cha miaka tatu na nusu ya mateso kwenye Dan 9:27 na Ufu 11:3; 12:6,14.

S: Kwenye Dan 8:2, Shushani ngomeni ni wapi?

J: Huu ulikuwa mji mkuu wa himaya ya zamani ya Elamu, ambayo ilikuwa kwenye sehemu ya kusini magharibi ya Irani ya sasa. Ulikuwa karibu na mji mkuu wa baadaye wa Himaya ya Uajemi.

S: Kwenye Dan 8:2, 16, je Mto Ulai uko wapi?

J: Leo hii tungeweza kuuita mfereji badala yam o wa asili. Ulitoka kaskazini na kuelekea kusini mbali kidogo na upande wa magharibi wa mji wa Susa (Shushani), kwa mujibu wa The Bible Knowledge Commentary: Old Testament, uk.1124.

S: Kwenye Dan 8:3-4, kondoo mume ni nini?

J: Huyu anawakilisha Himaya ya Uajemi ya Umedi. Pembe ndefu iliyotokea baadaye ni Uajemi, sehemu yenye nguvu zaidi ya himaya. Tazama Believer's Bible Commentary, uk.1084 na The Bible Knowledge Commentary: Old Testament, uk.1355-1356 zinazosema hivyo hivyo.

S: Kwa nini Dan 8:5 inaielezea himaya ya Alexander ya Makedonia kuwa mbuzi?

J: Maandiko hayaongelei jambo hili. Lakini, masimulizi yasiyokuwa na uhakika wa kihistoria kwenye kipindi cha Alexander yalisema kuwa Alexander alikuwa na pembe mbili zilizokuwa zimeota kichwani kwake ili kuonyesha hali yake ya kuwa nusu mungu.

S: Kwenye Dan 8:8, kwa nini pembe nne zilikua kuelekea kwenye pepo nne za mbinguni?

J: Hawa ni majenerali wanne wa Alexander walioitwaa himaya baada ya kifo chake. Cassander aliichukua Makedonia; Lysimachus aliichukua Thrace na Asia Ndogo; Seleucus aliichukua Shamu, Mesopotamia na Uajemi; na Ptolemy aliichukua Misri.

S: Kwenye Dan 8:9-11, je pembe ndogo ni ile ile ya Dan 7:8?

J: Hapana, kwa sababu pembe ya kwenye Dan 8:9-11 iliota kwenye himaya ya tatu, siyo ya nne. Waselesiudi na Warumi walikuwa na watawala waliokusudia kuwaangamiza watu wa Mungu.

S: Kwenye Dan 8:9-11, kwa nini pembe ndogo ilikua sana, badala ya kuwa sehemu tu ya pembe nyingine?

J: Pembe ndogo itakuwa ni mfalme wa Uselesiudi, Antiochus Epiphanes. Hakuwa mzao wa Seleucus. Antiochus Epiphanes anelzewa kiwazi hapa, lakini maneno haya yanaweza pia kuwa unabi wenye pande mbili, huku utimilifu wa pili ukiwa kwenye kipindi cha dhiki kuu.

S: Kwenye Dan 8:13-17, je nyakati za jioni na asubuhi 2,300 ni unabii wa miaka 2,300 kutoka amri ya Artaxerxes [inadaiwa kutolewa mwaka 457 KK] hadi kudhihirishwa kwa Bab mwaka 1844 BK kama Wabaha'i wanavyodai? (Some Answered Questions, uk.40-42)

J: Hapana, kuna matatizo manne kwenye maoni haya:
Aina isiyokuwa sahihi ya miaka:
1844 (BK) + 457 (KK) -1 (hakuna mwaka 0 BK) = 2300 (mwaka wenye siku 365.25). Hata hivyo, miaka ya kinabii kwenye Biblia ni miaka ya kidini yenye siku 360, si miaka yenye siku 365.25.
Urefu wa muda usiokuwa sahihi:
2,300 ni jioni na asubuhi, na hakuna kitu kwenye Kitabu cha Danieli kinachosema kuwa "jioni na asubuhi" ni miaka.
Muda usiokuwa sahihi wa kuanzia kuhesabu:
Amri ilitolewa mwaka wa 20 wa utawala wa Artashasta kwa mujibu wa Nehemia 2, hivyo mwaka wa kuanzia kuhesabu ulikuwa 445/444 KK, siyo 457 KK. Mwaka 457 KK ilikuwa ni amri tu kutoka kwa Artashasta ikithibitisha amri ya awali ya Koreshi kuwa Wayahudi wanaweza kurudi Yerusalemu.
Muda usio sahihi wa kuishia:
Kama utaangalia maneno yaliyobaki, si namba tu, jioni na asubuhi 2,300 ni wakati ambapo hekalu lilinajisiwa hadi wakati lilipowekwa wakfu tena. Wabaha'i wangependa kumaanisha kuwa hekalu la Mungu lilikanyagwa na kunajisiwa wakati Muajemi aliyeitwa Artashasta alipokuwa mfalme; lilibaki najisi wakati wa uhai wa Yesu hadi wakati wa Bab.
Hitimisho:
Mambo pekee ambayo Baha'u'llah aliyaelewa vibaya yalikuwa ni urefu wa muda, mwaka wa kuanzia kuhesabu, na mwaka wa kuishia kuhesabu. Kwa maneno mengine, ni kila kitu!

S: Kwenye Dan 8:16; 9:21; 10:13, 21 na 12:1, ni kitu gani kinachofurahisha kuhusu majina Gabrieli na Mikaeli?

J: Danieli ni kitabu pekee cha Agano la Kale ambacho kina majina ya malaika. Gabrieli na Mikaeli walitokea pia kwenye Agano JIpya. Gabrieli yupo kwenye Luk 1:19, 26, na Mikaeli yupo kwenye Yuda 9 na Ufu 12:7.

S: Kwenye Dan 8:17, kwa nini Danieli anaitwa mwanadamu?

J: Neno hili linamaanisha kuwa Danieli alikuwa binadamu, mwana wa Adamu. Mwana wa Adamu pia inamaanisha Kristo. Kwenye Dan 7:13-14, huyu Mwana wa Adamu (Yesu Kristo) anaabudiwa.

S: Kwenye Dan 8:23-25, kwa nini aliruhusu jambo hili?

J: Haya yanaonekana kuwa yatakuwa maafa makubwa sana. Waasi watakuwa waovu kabisa, patakuwa na uharibifu wa kushangaza sana, ukiwaangamiza watu wenye nguvu na watakatifu. Mfalme si kwamba ataruhusu uongo tu, bali pia kusababisha kushamiri. Isitoshe, unabii unajua Mungu alifahamu mambo yote haya na aliyaruhusu yatokee.

S: Kwenye Dan 8:27, kwa nini Danieli "aliyastaajabia" maono?

J: Danieli alilemewa na uharibifu wa maono haya, hata akaanguka kwa ajili ya msongo wa mambo. Ingawa Maandiko hayasemi kwa nini Danieli aishtushwa kiasi hicho, tunaweza kuona kitu kinachoweza kuwa sababu ya kufanya hivyo. Maono haya na mengine yalionyesha kuwa Mungu alikuwa anadhibiti historia. Lakini hata hivyo, Danieli alishtushwa na mambo mabaya yatakayo tokea kwa watu wa Mungu na hekalu la Mungu. Kwa kuwa Mungu alikuwa anadhibiti historia, kwa nini aliruhusu mambo haya yatokee?
Leo hii inawezekana kuwa tunaweza kushtushwana mambo ambayo Mungu anayaruhusu yatokee. Lakini tunapaswa kukumbuka kuwa Mungu anajua anachokifanya, - kuliko sisi tujuavyo.

S: Kwenye Dan 9:1, Dario Mmedi alikuwa ni nani?

J: Tazama maelezo ya Dan 5:30-6:1 ili kupata jibu la swali hili.

S: Kwenye Dan 9:2, miaka 70 ya kuvunjwa kwa hekalu la Yerusalemu ilikuwa ni ipi?

J: Miaka 70, itakuwa miaka yenye siku 360. Hii ni karibu miaka yetu 69. Hii ilikuwa kuanzia mwaka 605/604 KK hadi 538/537 KK. Tazama maelezo ya Yer 29:10 kwa habari zaidi.

S: Kwenye Dan 9:4-19, je maombi ya Danieli ya toba ya pamoja yanafananaje na t Neh 1:5-11?

J: Yafuatayo ni mambo saba yanayofanana.
1.
Wote waliomba kwa ajili ya mambo waliyoyaona kuwa yanakwenda kutokea lakini hayakuwa hivyo. Kwa upande wa Nehemia, lilikuwa ni tukio lenye kuonekana kwa nje la kutokujengwa kwa mji, na kwa upande wa Danieli lilikuwa ni tukio ndani la miaka 70 aliyoitabiri Yeremia kukaribia kwisha.
2.
Wote walifunga na kuomboleza - Danieli akiwa amevaa nguo za magunia na majivu, na Nehemia hakuwa amefanya hivyo, huenda ni kwa sababu alikuwa mnyweshaji wa mfalme.
3.
Wote wanaanza kwa kusema ukuu wa Mungu na rehema za agano lake.
4.
Wote wanaziweka pamoja dhambi za watu na adhabu ya Mungu.
5.
Wote wanataja kutokutii sheria ya Musa.
6.
Wakristo wote wanajua kuwa tunapaswa kufanya maombi ya toba, lakini kuna aina tofauti za maombi ya toba. Haya yote yalikuwa toba kwa ajili ya watu wote. Haya yalitoka kwenye "toba za kihistoria" tofauti za "toba za kihisia" kama kwenye Yeremia. Kutubu kwa kihistoria kunasistiza kitu walichofanya, hukumu za haki za Mungu, jambo walilofanya baada ya hapo, nk.
7.
Wote wanahitimisha kwa kumuomba Mungu kufanya kitu. Danieli anamwomba Mungu kugeuzia hasira yake mbali na Yerusalemu, wakati Nehemia alimwomba Mungu kumfanya mfalme asikilize ombi lake kwa uzuri.

S: Kwenye Dan 9:23, je maono haya yalijibuje swali la Danieli?

J: Danieli aliomba kuwa watu warudi na Yerusalemu ijengwe kama Mungu alivyoahidi kwenye Yer 25:11-14. Mungu si tu kuwa alimwambia tena Danieli mambo yatakayotokea, Mungu alimwambia undani wa baadhi ya mambo yatakayofuatia, na muda halisi wa jambo litakaloweka msingi wa muda ujao Masihi atakapokuja.

S: Kwenye Dan 9:24-27, ni kwa namna gani jambo hili linamwongelea Masihi?

J: Kwenye Dan 9:25, 26, neno "mpakwa mafuta" linatambuliwa na Wayahudi na Wakristo kuwa ni Masihi.

S: Kwenye Dan 9:24-27, kwa kuwa waandishi wa Agano Jipya walinukuu nabii za Agano la Kale kama ushahidi kuwa Yesu ni Masihi, kwa nini hakuna hata mmoja anayeongelea moja ya nabii zenye kushangaza sana za Masihi, Dan. 9:24-27?

J: Ingawa sifahamu kwa uhakika kwa nini waandishi wa injili hawakuongelea Dan 9:24-27, ninaweza kukisia. Kwa kiasi kikubwa waliandika mambo ambayo Yesu mwenyewe aliyasema. Yesu huenda hakuwa ameutaja unabii huo mbele ya watu kwa sababu hakupenda kuwafanya waelewe kimakosa kuwa walitenda sawa na mapenzi ya Mungu kumsulubisha, au kuwa walilazimika kufanya hivi kwa sababu ya unabii. Waliwajibika na kumsulubisha, na unabii uliotangaza ukweli huo haukuwapunguzia hatia.

S: Kwenye Dan 9:24-27, je majuma sabini ni yapi?

J: Yafuatayo ni maelezo ya majuma haya, yalipoanza, na yatakapo timizwa:
1. Haya ni majuma sabini ya miaka.
Endapo "majuma/saba" yalikuwa majuma ya siku, ingekuwa vigumu kuaminika kusema kuwa watu wangejenga upya mji wote kwa muda wa siku 42 za kazi. Hivi ndivyo Wayahudi wenyewe walisema kuhusu "saba", wakati unabii huu utakapo timia, na jinsi unavyohusiana na Masihi.
1a. Maimonides
(Rabi Moses Ben Maimon): "Danieli ametuelezea mambo ya siku za mwisho. Hata hivyo, kwa kuwa ni ya siri, wenye hekima [marabi] wamezuia kukakatua siku za kuja kwa Masihi ili kwamba umma usiofunzwa usije kupotoshwa wakati watakapoona nyakati za mwisho zimeisha kuja lakini hakuna ishara ya Masihi" (Igeret Teiman, sura ya 3, uk.24).
1b. Rabbi Moses Abraham Levi
: "Nimechunguza na kutafuta Maandiko yote matakatifu na sijaona wakati wa kuja kwa Masihi kuwa kumewekwa wazi kabisa, isipokuwa kwenye maneno ya Gabrieli kwa nabii Danieli, ambayo yameandikwa kwenye sura ya 9 ya unabii wa Danieli (The Messiah of the Targums, Talmuds and Rabbinical Writers, 1971), uk.141-142.
(Nukuu hizi mbili zilichukuliwa kutoka The Creator Beyond Time and Space, cha Mark Eastman, M.D. na Chuck Missler [The Word for Today, 1996]).
2. Muda wa kuanzia kuhesabu ni Machi/April 444 KK.
Dan 9:25 inaeleza wazi kuwa muda wa kuanzia kuhesabu amri ya kujenga upya kuta za Yerusalemu. Amri hii ilitolewa kwenye Nehemia 2, na hii ilikuwa mwaka 444 KK. Angalia kuwa si amri ya Koreshi ya mwaka 538/537 KK iliyoruhusu kurusi nyumbani, na siyo amri ya Artashasta ya mwaka 458 KK (Ezr 7:11-26) iliyowaruhusu Wayahudi kurudisha dhahabu na fedha ambayo Wababeli walizochukua kwenye hekalu la Sulemani. Julius Africanus, mwandishi Mkristo wa awali, akiandika mwaka 232-245 BK) pia anitaja amri wakati wa Nehemia kuwa muda wa kuanzia kuhesabu. (Ante-Nicene Fathers, juzuu la 6, uk.135).
3. Miaka ya siku 360 ilitumika.
Mwaka wa kidini wa Kiyahudi ulikuwa na miezi 12 yenye siku 30 kila mmoja. Hivyo, saba 7 ni 49 x 360 = siku 17,640. Kisha 7+62= saba 69, ambazo ni siku 173,880. Saba 1 ni siku 2,520. Ukiacha maelezo ya kubadilisha miaka yenye siku 360 kuwa miaka yenye siku 365.25 (na mwaka 1 KK kuwa mwaka 1 BK ni mwaka 1, siyo 2), hii inatupa tarehe ya:
3a. Mwaka 396/395 KK (Juni/Julai)
mji utajengea upya.
3b. Mwaka 32/33 BK (Machi/Aprili + siku 5)
Masihi atauawa. Believer's Bible Commentary, uk.1092 inasema kuwa Anderson alikokotoa na kupata Aprili 6, 32 BK. Dr. Harold Hoehner anapata mwaka 33 BK.
3c. Ukiacha kipindi kimoja
(kwa sababu zilizotolewa kwenye swali linalofuata), siku za mwisho zitakuwa kipindi cha 7 x 360/365.25 = miaka yetu 6.9.
Mungu alitaka kuwaonyesha watu wakati Masihi wake atakapokuja, na kwa wale waliopenda kuangalia, uko wazi kabisa.

S: Kwenye Dan 9:24-27, je juma hapa linaweza kuwa na siku saba badala ya miaka saba?

J: Hapana. Danieli alikuwa anaomba kuhusu unabii wa Yeremia, uliokuwa kwenye miaka. Pia kwenye Dan 9:25, ingekuwa vigumu kujenga mji kwa muda wa siku 7 tu. Hard Sayings of the Bible, uk.318-320 inasema kuwa kwa kuwa mwaka wa sabato ulikuwa ukienda kwa saba, kulinganisha "saba" na miaka haikuwa shida kwa wasikilizaji wa Kiyahudi, hasa kwa sababu Yubile ilikuwa mara moja kwa miaka saba kwenye Walawi 25.

S: Kwenye Dan 9:24-27, tunajuaje kuwa ipi ni amri sahihi?

J: Kulikuwa na amri tatu: Kwa Wayahudi kurudi mwaka 538/7 KK, amri ya Artashsta mwaka 458 KK kwa Wayahudi kurudisha dhahabu na fedha kwenye Hekalu lao, na amri ya Artashasta mwaka 444 KK. Hata hivyo, Dan 9:25 inasema wazi amri ya kuijenga upya Yerusalemu (siyo Hekalu). Amri ya Artashasta ya mwaka 444 KK ni amri pekee inayoendana na maelezo haya.
Julius Africanus, mwandishi Mkristo wa awali (mwaka 232-245 BK) pia anaelezea jambo hili kwenye Ante-Nicene Fathers, juzuu ya 6 Five Books of the Chronology of Julius Africanus, sura ya 16.1, uk.134. Anaelezea amri hii kipindi cha Nehemia kuwa ndiyo muda wa kuanzia kuhesabu (uk.135).

S: Kwenye Dan 9:24-27, je tunajuaje kuwa amri kwenye mwaka wa 20 wa Artashasta I ilitolewa mwaka 444 KK, na tunajuaje kuwa haikuwa ya Artashasta II?

J: Artashasta alipokuwa mfalme kwa kumshinda kaka yake Hystaspes huko Bactria, jambo hili lilifahamika mara moja Misri kufikia Januari 2/3, 464 KK, kama ambavyo Mafunjo ya Yebu (mkusanyiko wa hati za maandiko ya kale yaliyoandikwa kuanzia karne ya 5 KK) Cowley #6 inavyothibitisha. Mwaka huu wa kwanza "wa kutawala" ulihesabiwa kuanzia Aprili 13, 464 KK. Thucydides, jenerali wa Athene ambaye pia alikuwa mwana historia, aliandika kuhusu Artashasta I, kama walivyofanya wanahistoria Ctesias na Diodorus Siculus (karne ya 1 KK).
Tunajua huyu alikuwa Artashasta I (siyo II) kwa sababu makunjo yaliyopatikana kwenye kisiwa cha Yebu (Elephantine), Misri ya kale (Cowley #30), iliyoandikwa mwaka 407 KK inawataja watoto wa kiume wa Sanbalati, gavana wa Samaria. (Hapo palikuwa na ngome ya Kiajemi iliyokuwa na askari wa kukodiwa wa Kiyahudi hapo Yebu).

S: Kwenye Dan 9:24-27, kwa nini mwaka wa siku 360 ulitumika?

J: Kwa nini kutumia mwaka wa siku 365.25, kwani Biblia haiutumii kabisa? Mwaka wa kidini wa Kiyahudi kwa kawaida ulikuwa na miezi 12 yenye siku 30 kila mmoja. Mara kwa mara, Wayahudi waliongeza mwezi wa ziada kuufanya mwaka ufanane na misimu. Kwenye Biblia, mwezi wenye siku 30 ulianzia wakati wa Nuhu kwenye Mwa 7:11, 24; 8:3-4. Pamoja na kuongelea miezi ya kidini kwenye Agano la Kale, kwenye Agano Jipya siku 30 ni mwezi mmoja kwenye Ufu 11:3, 4. Julius Africanus, mwandishi wa Kikristo wa kale akiandika mwaka 232-245 BK) pia anataja kubadilisha kutoka mwaka wenye siku 365.25 kuwa mwaka wa Kiyahudi. Alisema mwaka wa Kiyahudi ulikuwa na siku 29.5, pamoja na miezi 3 ya ziada iliyoongezwa kila baada ya miaka 8 (Ante-Nicene Fathers, juzuu ya 6, uk.137).

S: Kwenye Dan 9:24-27, kuna mantiki gani ya kusema kuwa kuna pengo kati ya mwaka 69 na 70?

J: Kuna mambo manne ya kuzingatia katika kujibu swali hili:
1.
Hakuna kitu kwenye Kitabu cha Danieli kinachoonyesha kuwa saba ya mwisho inakuja baada ya saba hizi 69.
2.
Kinyume chake, Dan 9:25 inadokeza kuwa saba 7 na saba 62 ni kitu kimoja mpaka Masihi atakapokuja. Saba ya mwisho haijaelezwa kuwa inawekwa pamoja na kipindi kingine chochote.
3.
Baada ya Masihi kukatiliwa mbali na kutokuwa na kitu chochote, matukio kadhaa yameorodheshwa ambayo hayhusiani na ama kipindi cha kati (saba 62) au saba ya mwisho. Yaani, watu wa mtawala ambaye atakuja kuuvunja mji na Hekalu, mwisho utakuja, vita itakuja, na uangamivu. Saba ya mwisho haisemwi kuhusisha matukio haya. Inahusisha tu mtawala atakayekuja kufanya agano, na miaka 3 ˝ baadaye kuvunja agano.
4.
Wanathiolojia wengi wanaliita pengo hili kabla ya saba ya mwisho kwa kutumia neno bayana, ili kuelezea fumbo ambalo Mungu hakulieleza mpaka baadaye. Neno wanalotumia ni "enzi ya kanisa."
Hitimisho,
kuchukulia saba 69 kama kitu kimoja bila kuchukulia saba ya mwisho, na kutaja matukio kadhaa kati ya mwisho was aba 69 na mwano wa saba ya mwisho, inadokeza sana pengo kabla ya kuanza kwa saba ya mwisho.

S: Kwenye Dan 9:24-27, jambo hili linaendanaje na maoni kuwa Yesu alizaliwa mwaka 4-5 KK?

J: Unabii huu hauungi mkono wala kupinga maoni hayo. Biblia haisemi kuwa Yesu alikuwa na miaka thelathini alipoanza huduma yake. Badala yake, Luk 3:23 inasema kuwa Yesu alikuwa na miaka karibu thelathini.

S: Kwenye Dan 9:24, je aya hii inapaswa kusomeka "yeye aliye mtakatifu" au "mahali patakatifu zaidi?"

J: Biblia za Kiebrania na Kigiriki (Septuajinti) zinasema "mtakatifuzaidi."

S: Kwenye Dan 9:24-27, je kanisa la awali lilisema nini kuhusu majuma sabini?

J: Walisema sawa na Wakristo wa leo wanaoifuata wanavyosema, kuwa yanamhusu Masihi.
Hata waandishi wa Kiyahudi Maimonides kwenye Igeret Teiman na Rabbi Moses Abraham Levi kwenye The Messiah of the Targums, Talmuds and Rabbinical Writers. Dan 9:20-27 inamwongelea Masihi.
Irenaeus
(mwaka 182-188 BK) anaelezea nabii za Danieli na kusema, "na atakusudia kubadilisha nyakati na sheria; na atapewa [kila kitu] mikononi mwake mpaka wakati wa nyakati na nusu wakati,' yaani, kwa muda wa miaka mitatu na miezi sita, katika muda huu, atakapokuja, atatawala dunia" (Irenaeus Against Heresies, kitabu cha 5, sura ya 25.3, uk.553-554).
Clement wa Alexandria
(mwaka 193-202 BK) anasema kuwa Dan 9:24-27 inamwongelea Kristo (Stromata, kitabu cha 1, sura ya 21, uk.319).
Tertullian
(mwaka 198-220 BK) analinganisha mfuatano wa matukio ya kihistoria na Danieli 9 (Answer to the Jews, sura ya 8, uk.158-161).
Tertullian (mwaka 198-220 BK) "Kwa maana, baada ya kutokea kwake, tunasoma, kwa mujibu wa Danieli, kuwa mji wenyewe utapaswa kubomolewa kabisa; na tunaona kuwa jambo hili limetokea." Kisha Tertullian ananukuu Dan 9:26 (Answer to the Jews, sura ya 13, uk.169).
Hippolytus
(mwaka 222-235/6 BK) "‘Majuma sabini yameamuliwa juu ya watu wako, na juu ya mji mtakatifu, kuweka muhuri dhambi na kuondoa makosa, kuweka muhuru maono na nabii, na kumpaka mafuta yeye aliye mtakatifu; nawe utajua na kufahamu, kuwa kuanzia wakati wa kutolewa jibu, na kuijenga Yerusalemu, hadi wakati wa Kristo Mfalme, patakuwa na majuma saba, na sitini na majuma mawili'" (Visions of Daniel and Nebuchadnezzar, sura ya 12, uk.180).
Hippolytus, askofu wa Portus (mwaka 222-235/236 BK) Kitabu chenye maoni ya Nabii Danieli, sura ya 2.22.
Julius Africanus
(mwaka 235-245 BK) anaelezea majuma sabini ya Danieli na kusema kuwa unabii huo ulikuwa hadi siku za Yohana [Mbatizaji] (Five Books of the Chronology of Julius Africanus, sura ya 16.1, uk.134).
Origen
(mwaka 225-254 BK) Origen Against Celsus, kitabu cha 6, sura ya 46, uk.594-595.
Athanasius
(karibu mwaka 318 BK) "Danieli mwenye hekima, anayeonyesha muda halisi na safari ya kiungu ya Mwokozi akisema: ‘Majuma saba yamekatizwa juu ya atu wako, na juu ya mji mtakatifu, . . ." (Incarnation of the Word, sura ya 39, uk.57)
Lactantius
(karibu mwaka 303 hadi karibu mwaka 25 BK) Daudi alitabiri kuhusu Yesu kwenue Zab 16:10 kama alivyofanya Dan 7:13 (Epitome of the Divine Institutes, sura ya 47, uk.241). Pia anaongelea Isa 7:14 kwenye Epitome of the Divine Institutes, sura ya 44, uk.239.
Wakristo wa awali walisema maneno hayo hayo baada ya baraza la kanisa la Nikea, isipokuwa mtu wa kwanza anayefahamika kusema kuwa hakuwa Masihi alikuwa Julius Hilarianus [karibu mwaka 397 BK] ("Maoni yasiyo ya Masihi ya Danieli 9" kwenye Chronologia sive Libellus de Mundi Duratione iliyomo kwenye kitabu cha Jerome chenye kutoa maoni ya Kitabu cha Danieli).
Tazama makala iliyoandikwa na J. Paul Tanner: ‘Is Daniels' Seventy-Weeks Prophecy Messianic? Part 1" kwenye Bibliotheca Sacra, juzuu ya 166 (Aprili-Juni 2009), uk.181-200 kwa habari zaidi.

S: Kwenye Dan 9:25, je ni sahihi kusema kuwa Masihi Mwana wa Mfalme kuwa ni Koreshi wa Uajemi, kama kitabu cha mwenye kushuku kiitwacho Asimov's Guide to the Bible, uk.614 kinavyosema?

J: Hapana, Asimov anaelekea amechanganyikiwa kwenye wazo hili. Kwa mujibu wa Dan 9:25, kutakuwa na "saba" 69 za miaka kabla ya Masihi kuja. Koreshi alikuwa ameishakuja wakati Kitabu cha Danieli kinaandikwa. Pia, Masihi aliuawa (ondolewa) kwenye Dan 9:26.

S: Kwenye Dan 9:26, ni mafuriko gani ambayo Maandiko unayaongelea? Nimeona tafsiri inayosema "Mwisho wake utakuwa kama mafuriko", lakini nyingi za tafsiri zinasema "pamoja na mafuriko." Je Yerusalemu ilikumbwa na mafuriko mwaka 70 BK Warumi walipolibomoa hekalu? 

J: Yerusalemu ipo juu ya Mlima Sayuni, hivyo haipatwi na mafuriko ya maji, na hakuna mafuriko yaliyotokea mwaka 70 BK. Kwenye Maandiko ya Kiebrania, neno lenye kumaanisha "kama" halipo, lakini neno la Kiebrania linaweza kutafsiriwa ‘kufurika', kwa hiyo tafsiri kadhaa zimetokea kutumia maneno "kama mafuriko" kuonyesha neno hili, hakuna kitu chochote chenye kunyesha kuwa neno hili linahusika na maji.
The Expositor's Bible Commentary, uk.116 inasema, "Kwa kutafsiri ya neno kwa neno, sentensi hii inaweza kutafsiriwa kama: ‘Na mwisho wake utakuwa kwenye kufurika, na mwishoni kutakuwa na vita, kutambua uharibifu kiusahihi' au ‘kiasi kiasi cha uharibifu kilicho tambuliwa.' Maana ya jumla ya sentensi hii ipo kwenye kufana kwa kiasi kikubwa sana na utabiri wa Yesu kwenye mafundisho toka Mlima wa Mizeituni (Mat 24:7-22)."

S: Kwenye Dan 10:2-4, je Danieli alikuwa sahihi kuomboleza kwa muda wa majuma mazima matatu?

J: Ndiyo. Kuomboleza hakumaanishi msongo, au tatizo la kisaikolojia. Kuna nyakati za waamini kuomboleza, kama ambavyo kulivyo na nyakati za kufurahi.

S: Kwenye Dan 10:4, Mto Hiddekel uko wapi?

J: Hili lilikuwa ni jina linguine la Mto Tigris. Hatufahamu kwa nini Danieli alitumia jina lisilo la kawaida la mto huu, lakini wakati mwingine vitu vya kawaida vinawezakuonekana kuwa si vya kawaida tunapoweza kuona zaidi jinsi vitakavyokuwa siku za baadaye. Baadhi ya vyuo vikuu vyenye vitivo vizuri sana vya thiolojia kama Yale, Harvard na Princeton, vimebadilika na kutokufahamika sana karne moja au zaidi zilizopita.

S: Kwenye Dan 10:4-9, tunaweza kujifunza nini kuhusu huyu malaika hapa?

J: Kuna mambo angalau matatu:
Kimwili, malaika huyu alivaa nguo ya kitani, ambayo ni nyeupe na mkanda wa dhahabu. Malaika anaonekana pia kuwa mgumu kumwangalia. Uso wake kama radi ungekuwa mng'aavu sana hata usingependa kuuangalia.
Matokeo yake ni kuwafanya watu waingiwe na hofu hata kama hawakumuona malaika. Matokeo yake kwa Danieli yalikuwa kuishiwa nguvu zake, na kisha kunaguka na kulala usingizi mzito.
Hata kama malaika huyu alizuiliwa na Mkuu wa Uajemi kwa muda wa siku 21, hakuonekana kuwa mbaya zaidi kuwa kuzuiliwa kwa muda mrefu namna hii.
Sisi si malaika, na hatukuwa malaika wakati wowote ule. Hata hivyo, tunaweza kuona mambo kadhaa yanayofanana kati ya malaika na jinsi ambavyo sifa zetu zinatakiwa ziwe. Maisha yetu na ujumbe wetu vinatakiwa viwavutie na kuwapendezesha watu wengine. Lakini, watu watasikia kuhukumiwa watakaposikia sauti ya Mungu. Haja ya watu kufanya dhambi inatakiwa ipunguzwe wanapokuwa karibu nasi, endapo tuna athari ya namna fulani katika maisha yao.

S: Kwenye Dan 10:5 na Yer 10:9, je dhahabu safi ya Ufazi ni nini?

J: Hatujui, lakini kuna maoni mawili. Huenda Ufazi ilikuwa ni sehemu huko Afrika (Ofiri), au mahali pengine. Vinginevyo, huenda Ufazi haikuwa jina la sehemu yeyote ile, bali ni kisifa kinachoielezea dhahabu yenye ubora mkubwa zaidi.

S: Kwenye Dan 10:5-10, 13-21, Danieli alikuwa anaongea na nani?

J: Kiumbe huyu mwenye utukufu alikuwa ni malaika wa Mungu. Hatujui jina lake, na si lazima kuwa awe Gabrieli, aliyeongea na Danieli hapo awali.

S: Kwenye Dan 10:7, 8, 15-19, na Ufu 1:17, kwa nini watu wanaishiwa nguvu wanapoviona viumbe vya kimbingu?

J: Binadamu aliyepo duniani anapokutana na utakatifu wa Mungu, au utakatifu unaoonekana kwa malaika zake, hujiona si tu kuwa wenye dhambi na wadhaifu bali pia hupoteza nguvu zao za kimwili. Kwenye Isa 6:5, Nabii Isaya alitetemeka na kusema "Ole wangu."

S: Kwenye Dan 10:13, 21 na 12:1, malaika mkuu Mikaeli ni nani?

J: Dan 10:13 inasema tu kuwa ni mmoja wa wakuu wa ufalme. Dan 10:21 inasema ni "mkuu wenu" (mkuu wa ufalme wa Israeli), na Dan 12:1 inasema ni "jemadari mkuu." Agano Jipya linatueleza zaidi. Ufu 12:7 inasema ni malaika mkuu aliyeongoza majeshi ya mbinguni dhidi ya joka. Yuda 9 inasema alipambana na shetani kuhusiana na mwili wa Musa na alisema, "Bwana na akukemee."

S: Kwenye Dan 10:21, je jina "Mikaeli" linatamkwaje (kwa Kiingereza)?

J: Watu wengi zaidi wanasema "MI kel", kama kwa Kiingereza, ingawa nimewahi kusikia likitamkwa "mi KA el", kwenye mashindano ya mashindano ya kutaja herufi za maneno ya kwenye Biblia. (Mshindani wa darasa la saba [la mfumo wa Kimarekani] alitaja herufi namna hii kimakosa).

S: Kwenye Dan 10:21, Mikaeli ni mkuu wa nani?

J: Mikaeli alikuwa mkuu wa Wayahudi. Mara nyingine mbili ambazo Mikaeli ametajwa kwenye Maandiko, anapambana na kitu kingine. Kwenye Yuda Jude 9, Mikaeli malaika mkuu alimwambia shetani "Bwana na akukemee." Kwenye Ufu 12:7, ni Mikaeli anayepambana na joka mbinguni.

S: Kwenye Dan 10:21, je Mikaeli anaweza kuwa Yesu Kristo?

J: Hapana. Tofauti na Mashahidi wa Yehova wanavyosema, Mikaeli si Yesu Kristo. Sababu moja ni kuwa kwenye Yuda 9, MIkaeli alimwambia Bwana (Yesu) amkemee shetani; Mikaeli mwenyewe hakumkemea shetani.

S: Kwenye Dan 10:21, Maandiko ya kweli ndiyo yapi?

J: Kuna maoni mawili yanayofanana na haya:
a)
Biblia ambayo ilikuwa imefunuliwa hasi wakati ule. Hii ni pamoja na orati na sehemu kubwa ya manabii.
b)
"Rekodi ya Mungu ya kweli kwa ujumla, ambao Biblia ni moja ya vielelezi vyake" (Daniel: The Key to Prophetic Revelation, uk.250).

S: Kwenye Dan 11, je unafikiri anapendelea picha kubwa tu, au pia maelezo ya kina?

J: Unaposoma sura hii nzima, urefu wa kifungu hiki, na maelezo yake ya kina ya nani aliyemshinda nani, unaonyesha kuwa Mungu anapendelea maelezo ya kina licha ya kuangalia picha ya jumla.

S: Kwenye Dan 11, nabii nyingi zaidi kwenye Agano la Kale hazina utitiri wa maelezo; hata nabii nyingine kwenye Kitabu cha Danieli. Kwa nini unafikiri kuwa kulikuwa na maelezo marefu sana hapa?

J: Maandiko hayasemi, lakini kuna vitu viwili vinavyoelekea kuwa sababu:
Kwanza,
kama ukichora mstari ardhini wenye kuunganisha Shamu upande wa kaskazini na Misri upande wa kusini, mstari utapitia Israeli. Itakubidi uende mbali na njia yako ili upitie Amoni, Moabu na Edomu. Kwenye bembea hii ya mapambano na bahati, mapambano mengi yalikuwa Israeli.
Pili,
palikuwa na pengo la miaka 400 ambapo hapakuwa na manabii au nabii zilizotolewa kwa watu wa Mungu. Hatimaye pengo hili liliondolewa wakati alipokuja Yohana Mbatizaji, mtangulizi wa Yesu. Lakini katika karne hizi nne, watu wa Mungu hawakuvunjika moya, au kufikiri ukimya huu wa muda mrefu uliwaondoa kwenye mpango wa Mungu. Pengo hili linaweza kuwa limekusudia kujenga matarajio ya kuja kwa Yohana Mbatizaji, ambaye alijenga matarajio ya kuja kwa Masihi. Lakini hawakuwa wamesahauliwa kwenye kipindi hiki cha pengo; muda mfupi kabla ya hapa, Danieli alitoa maelezo ya kina yenye kuonyesha kuwa Mungu alifahamu kabla ya wakati historian a majeshi ambayo wataenda kupambana nayo.

S: Kwenye Dan 11:1 na 12:1, kwa nini Mikaeli aliitwa "mkuu" wakati alikuwa malaika?

J: Tunaona kuwa Mikaeli anaitwa mmoja wa wakuu kwenye Dan 10:13; malaika anaitwa mwanadamu kwenye Dan 10:5, au alionekana kama mwanadamu kwenye Dan 10:18. Gabrieli anaitwa mwanadamu kwenye Dan 9:21. Inasemekana kuwa mkono uliondika ukutani kwenye Dan 5:5 ulikuwa wa binadamu. Neno "malaika" limetumika kwenye Dan 3:28 tu (na Nebukadneza) na 6:22 (na Danieli). Danieli alipotumia neno malaika kwenye Dan 6:22, alikuwa anaongelea matokeo ya malaika kuifunga makanwa (midomo) ya simba, na si kitu kinachoonekana. Neno "mjumbe" limetumiwa kwenye Dan 4:13, 17, 23.
Kuhusu namna ya uandishi ya Danieli, anaandika kitu anachosema, ikiwa ni umbo la mtu au mkono. Danieli alitumia neno "malaika" mara moja tu, wakati hapakuwa na umbo la kimwili lililoweza kuonekana. Mungu hakumfanya malaika atokee bila sababu, lakini kila wakati ilikuwa kuwasilisha ujumbe. Labda hatupaswi kuhangaishwa sana na kuwaona malaika, bali kunufaika na matokeo yao maishani mwetu.

S: Kwenye Dan 11:1, kwa nini malaika alimtia nguvu Dario?

J: Usemi huu unaweza usiwe unamaanisha nguvu za kimwili au afya, bali kuiimarisha nafasi yake kuwa mfalme na kuendelea kuwa mfalme.

S: Je Dan 11:1 inatofautiana na historia inayosema kuwa mfalme wa Uajemi aliyeishinda Babeli alikuwa Koreshi I, siyo Dario I?

J: Si Koreshi I wala Dario I aliyeieka Babeli. Mtu aliyeiteka Babeli alikuwa jenerali chini ya Koreshi, jina lake ni Gubaru (Gobryas kwa Kigiriki). Huyu anaelekea mtu aliyetajwa hapa kama Dario. Gubaru alikuwa mtu anayefurahisha sana. Ni gavana Mbabeli wa Gutiumu aliyehamia kwa Wamedi na Waajemi.

S: Kwenye Dan 11:1-33, nani walikuwa wafalme wa Himaya ya Uajemi?

J: Walikuwa ni:
Koreshi Mkuu (mwaka 559 KK-Anshani, 550
KK
Uajemi ya Umedi - mwaka 530/529 KK
Cambyses II 530/529-523/522 B.C.
Pseudo-Smerdis (Guatama) mwaka 523/522 -
522/521 KK
Dario I mwaka 550-522/521- 486 KK
Ahashasta (Xerxes kwa Kigiriki) mwaka 486 -
465/464 KK
Artashasta I mwaka 464 - 423 KK
Dario II mwaka 423 - 404 KK
Artashasta II mwaka 404 - KK
Artashasta III - mwaka 336 KK
Dario III mwaka 336 - 331 KK
Kisha Alexander wa Makedonia aliishinda Uajemi.

S: Je Dan 11:1-33 inaongelea nini?

J: Inaongelea wafalme wa uajemi: Cambyses II (mwaka 530-522 KK), Pseudo-Smerdis (Guatama) mwaka 523/522-522/521 KK), Dario I (mwaka 550-522/521-486 KK), na Ahashasta (Xerxes kwa Kigiriki) (mwaka 486-465/464 KK). Kitabu cha mwenye kushuku Asimov's Guide to the Bible, uk.616 kinasema hivyo hivyo.
Mfalme wa nne, Xerxes, invaded Greece. aliivamia Ugiriki. Ilikuwa baadaye, kwenye mstari wa 3, kwamba Alexander Mkuu (mwaka 356-324 KK) aliishinda Himaya ya Uajemi.
Mwishoni, himaya ya Alexander iligawanyika sehemu nne. Cassander alitawala Makedonia
Lysimachus alitawala Thrace na Anatolia
Seleucus (mwaka 312-281 KK) alitawala Shamu, na
Ptolemy (I Soter) (mwaka 323-285 KK) alitawala Misri.
Dan 11:5-33 inaongelea viongozi wa Shamu na Misri, na siyo viongozi wale wale wawili katika kifungu chote.

S: Kwenye Dan 11:31, chukizo la uharibifu ni nini?

J: Unabii huu ulikuwa unamwongelea Antiochus Epiphanes na utimilifu ambao bado haujatokea wakati huu wa sasa.
Antiochus Epiphanes alilinajisi Hekalu. Aliingia patakatifu pa patakatifu, na kulingana na taarifa moja aliweka kichwa cha nguruwe hapo.
Kwa mujibu wa kipande cha 2 cha maandiko cha Hippolytus kutoka kwenye Commentaries yake (uk.184) ya mwaka 225-235/6 BK) chukizo la uharibifu la lililoongelewa na Danieli litatokea siku za mwisho wakati Mpinga Kristo atakapokuja.

S: Kwenye Dan 11:37-38, neno Mungu kwa Kihebrania linamaanisha nini hasa hapa?

J: Neno la Kiebrania, elohim, lina maana mbili. Linaweza kumaanisha Mungu mmoja wa Kweli, au linaweza kumaanisha miungu ya uongo. Neno la Kiingereza Mungu/mungu ni hilo hilo. Hata hivyo, tofauti na Kiingereza, elohim ni wingi, kwa hiyo ni "sisi ya kifalme" (the royal we) kwa Mungu Mmoja wa Kweli, na pia inaweza kumaanisha miungu (wingi). Kwenye Dan 11:37-38, "miungu wa baba zake" ni miungu sanamu za uongo, na "yeye anayetamaniwa na wanawake" inamaanisha mungu wa uongo (yaelekea ni Tammuzi).

S: In Dan 11:40-12:3, "Epiphanes" inamaanisha nini?

J: Linamaanisha maarufu, au inayojithibitisha yenyewe. Kama wazo la ziada, Believer's Bible Commentary, uk.1092 na The Bible Knowledge Commentary: Old Testament, uk.1369 zinasema Wayahudi walikuwa na jina lake jingine la utani, "Epimanes", lililomaanisha mtu asiye na akili timamu. Picha ya sarafu yenye kumwonyesha Antiochus Epiphanes, yenye jina la cheo, "Kujidhihirisha kwa Mungu" limo kwenye The Journey from Texts to Translations, uk.52.

S: In Dan 11:45, Kwenye Dan 11:45, Antiochus Epiphanes IV "alikujaje kwenye mwisho wake, bila kuwa na mtu wa kumsaidia"?

J: Antiochus IV (Epiphanes) alitawala kutoka mwaka 165-163 KK. Alidhalilishwa wakati Bunge la Rumi lilipomzuia kuivamia Misri tena. Mafunjo yenye maandishi Appian Syr. 66 yanasema kuwa Antiochus IV alijitoa na kwenda Tabae na alikufa kwa ugonjwa wa kifua kikuu mwishoni mwa 164 KK.

S: Kwenye Dan 12:1, je hiki ni kipindi gani?

J: Aya hii na Danieli 11 vinaongelea wakati ujao wa Dhiki Kuu, ambapo mpinga Krsito atatawala. Angalia Believer's Bible Commentary, uk.1091, The Bible Knowledge Commentary: Old Testament p.1372, The NIV Study Bible p.1318, The Nelson Study Bible, uk.1442-1443, The Expositor's Bible Commentary, juzuu ya 7, uk.149-152, na 1001 Bible Questions Answered, uk.287.
Wakati wa kanisa la kwanza, Hippolytus, askofu wa Rumi (mwaka 225-235/6 BK) kwenye maoni yake ya Danieli 12 pia anasema kuwa aya hii inaongelea kipindi cha mpinga Kristo.

S: Je, Danieli 12:2, inaonesha ufufuo tofauti wa Wayahudi wamchao Mungu?

J: Hapana kwa sababu mbili.
Ikiwa kifungu kinajadili jambo linalotokea kwa watu fulani, na kifungu cha pili kinataja jambo lile lile kuwa linatokea kwa watu wengine, kuyaweka makundi haya mawili ya watu pamoja haionyeshi endapo wote watafufuliwa kwa pamoja au nyakati tofauti.
Lakini katika swala hili hapa, Dan 12:2 inasema "watu wako – kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile." Ingawa maneno haya yanawezakumaanisha Wayahudi wateule tu, maana ya kawaida zaidi inaweza kuwa mteule yeyote.
Pamoja na hayo, marabi wa baadaye wa Kiyahudi walithibitisha kuwa maneno haya yanaongelea kufufuka kwa mwili ni Saaidah Gaon na Ibn Ezra.

S: Kwenye Dan 12:2, je ni watu "wengi" watakaofufuliwa au wote kama Ufu 20:5 inavyosema?

J: Wote, kwenye matukio yasiyopungua mawili. Wenye haki watafufuliwa kutoka kwa wafu kwanza, na kisha watu wote watafufuliwa kufikia mwisho wa miaka elfu moja ya utawala wa Kristo hapa duniani kwenye Ufu 20:5. Dan 12:2 ni kifungu cha zamani zaidi cha Maandiko kinachosema waovu watafufuliwa na wacha Mungu pia.

S: Kwenye Dan 12:6, je viumbe wawili ni kina nani hapa?

J: Hawa ni malaika wawili. Mto unaoongelewa hapa ni Hidekeli (Danieli 10:4), si Frati, ambao upo magharibi zaidi. Kwa hiyo, malaika hawa huenda wasiwekwe pamoja na malaika wanne kwenye Mto Frati kwenye Ufu 9:14-15.

S: Kwenye Dan 12:6, je malaika wanafahamu kila kitu?

J: Hapana, hawafahamu kila kitu kuhusu wakati ujao, kwa sababu malaika mmojawapo aliuliza mambo haya yatatokea lini. Kwenye 1 Pet 1:12, malaika walitamani kuyachungulia mambo yahusuyo kuja kwa Kristo.

S: Je Dan 12:6 inamuongelea Bab kama Wabaha'i wanavyodai, kwani alitokea miaka 1,260 baada ya Hijra ya Muhammad? (Some Answered Questions, uk.43)

J: Hapana. Wanadai hivi kwa sababu nyakati 3 ˝ au miaka 3 ˝ yenye siku zenye siku 360 zenye kufuata kaundama kwa mwezi ni 360 x 3 ˝ = siku 1260 za miaka yenye kufuata kuandama kwa mwezi kutoka Hijra ya Muhammad.
Kwanza kabisa siku hazimaanishi miaka hapa. Pili, muda wa kuanzia kuhesabu wanaotaka kuutumia si ule ambao Biblia inausema. Unapaswa pia kusoma muda wa kumalizia kuhesabu kwenye Dan 12:1-4. Kwa wakati huu, umati wa watu utafufuliwa kutoka usingizini kwenye mavumbi, na Mikaeli, anayewalinda Wayahudi atainuka. Jambo hili halikutokea kwa hakika; hasa kwa sababu mauaji ya Wayahudi wa Ulaya (Holocaust) yalitokea baada ya jambo hili.
Kimsingi, Wabaha'i wanauchukulia kila unabii unaoongelea ufahamu au ukombozi utakaofanyika siku za baadaye, na kuibua maswali ambayo bado hayajajibiwa kwa kusema kuwa jambo hilo linamwongelea Baha'u'llah. Kisha wanasema, "Tazama, unabii huu ulitimizwa, kwa hiyo Baha'u'llah alisema kweli."

S: Kwenye Dan 12:8-10, kwa nini Danieli mwenyewe hakuelewa mambo aliyokuwa anayaandika?

J: Danieli aliyafahamu maneno yaliyoyatumiwa, lakini hakuelewa maana wala umuhimu wake. Tofauti na maandishi mengi kwenye Biblia, sehemu hii "ilitolewa kwa njia ya imla", kwa maana ya kwamba Danieli aliandika mambo aliyoyasikia toka kwa malaika.
Leo hii, wakati mwingine watu wanakata tamaa kujifunza jambo endapo hawaelewi kila kitu kinachohusika nalo. Kama huelewi kila kitu kuhusu upendo, je hupaswi kumpendea mtu mwingine yeyote? Endapo huelewi kila kitu kuhusu Mungu, je, huwezi kuelewa kitu chochote kile? Si hivyo.

S: Kwenye Dan 12:9, je watu waliwekeaje mihuri mambo wakati ule?

J: Wakati hati au waraka mweingine muhimu ulihitajika, waandishi waliandika nakala mbili zinazofanana. Moja ilikuwa ya "watu wote" na nyingine ilitiwa muhuri na kuhifadhiwa mahali penye usalama. Waliitia muhuri hati kwa kuiviringisha, na kila mwandishi aliweka nta ya kutilia muhuri juu yake, ili endapo mtu angejaribu kuifungua au kuifungua bila idhini, muhuri ungevunjika. Endapo mtu yeyote angejaribu kubadilisha nakala ya watu wote, wangeenda kwenye nakala iliyotiwa muhuri na kuthibitisha maandishi ya awali.

S: Kwenye Dan 12:9; Ufu 6:1-3 na 10:4, kwanini Mungu anavitia vitu muhur?

J: Kuna mambo matatu yanayoweza kuwa sababu hapa:
a) Mungu hapendi watu wajue baadhi ya mambo, angalau hadi wakati wa baadaye. Lakini Mungu angeweza kutokusema kitu chochote kuliko kusema kitu ambacho kitatiwa muhuri.
b) Mungu anataka tuelewe sasa kuwa kuna jambo muhimu kulielewa, ambalo hatutalielewa hadi hapo baadaye.
c) Pengine Mungu hataki Shetani au mapepo wasikie habari hizi juu ya mambo ya baadaye.

S: Kwenye Dan 12:9 na 1 Pet 1:10-11, kwa kuwa manabii hawakuyafahamu mambo yote waliyokuwa wakiyasema, je jambo hili linaunga mkono kitendo cha viongozi wa Mashahidi wa Yehova kutoa nabii za uongo?

J: Hapana. Ingawa manabii hawakuelewa kila kitu, waliwasilisha kwetu kwa kweli, umakini na uaminifu kila kitu ambacho Mungu wa kweli alitaka watufunulie. Vile vile Yona hakuwa nabii wa uongo, kwa sababu kitabu cha Yona kinasema kuwa aliwasilisha ujumbe kwa usahihi, na kwamba unabii wa kuharibiwa kwa Ninawi ulikuwa na sharti la wao kutubu. (Ukweli ni kwamba, kuharibiwa kwao hakukuondolewa, bali kuliahirishwa tu).

S: Kwenye Dan 12:10 na Ufu 22:11, ni kwa jinsi gani walio safi wanatakaswa, na waovu wanaendelea kuwa waovu?

J: Mara tunapomgeukia Mungu na kutubu baadhi ya dhambi, Mungu bado huwa na kazi zaidi ya kufanya kujenga mwenendo wetu unaofanana na Kristo na kutuweka huru n dhambi nyingine. Hatupaswi pia kujikatisha tamaa sisi wenyewe ikiwa tutashindwa kuonyesha mwenendo wa Kristo kwa ukamillfu mara baada ya kumwamini Kristo. Pia tusikatishwe tamaa na ndugu na dada wengine katika Bwana, wanaposhindwa kuonyesha mwenendo wa Kristo kikamilifu mara moja.
Ufu 22:11 pia inasema kuwa mwenye kudhulumu azidi kudhulumu, na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa. Hapa hakuna hali ya kutokufanya kitu chochote au kutokubadilika tu bali pia tao la mtupo wa angani linalo waongoza watenda dhambi moja kwa moja kwenye dhambi zaidi, na wale wanaomtafuta Mungu kwenye haki.

S: Kwenye Dan 12:11, nini ni ishara ya siku 1,290 1,335?

J: Mwaka wa kidini ulikuwa na siku 360. Siku 1,290 zinazidi kidogo tu miaka 3 na miezi 7. Siku 1,335 ni siku 45 kamili baadaye.

S: Kwenye Dan 12:11-12, je siku 1,290 zinaashiria Baha'ullah kutokea miaka 1,290 baada ya Muhammad kutangaza kusudi lake kuu kama Bahai' alivyodai kwenye Some Answered Questions, uk.43-44?

J: Baha'ullah alidai hivi miaka 19 baada ya Bab, kwa hiyo tungeweza kusema ilikuwa miaka 1,279. Hata hivyo, kwa kuwa jambo hilo haliendanii na miaka 1,290, wanahamisha muda wa kuanza kuhesabu kuwa karibu na wakati Muhammad aliposema alikuwa nabii.

S: Kwenye Danieli, ungefanya nini endapo ungefahamu mapenzi ya Mungu kama Danieli alivyofahamu?

J: Danieli alifahamu kuliko watu wa wakati wake; zaidi kuliko mtu yeyote kiasi ambach mtu yeyote angeweza kufahamu kwa kawaida. Alitumia ufahamu wake kuwaelekeza watu wengine, kututia moyo sisi, na kuwaonya watu wengine, hata wafalme.
Lakini sisi sote tuna ufahamu mkubwa hata kuliko aliokuwanao Danieli. Pia tunafahamu kuhusu Masihi, na mengi zaidi kuhusu kurudi kwake siku zijazo. Lakini hatupaswi kujivuna kwa sababu ya ufahamu tulionao, bali tutumie ufahamu wetu kwa manufaa ya wengine kama Danieli alivyofanya.
Danieli alifahamu jinsi ya kupita salama kwenye tufani za maisha. Iwe amepelekwa mbali na kwao au salama, kwenye jumba la ufalme au shimo la simba. Danieli alikuwa mtu wa majira yote. Katika nyakati zozote tunazotokea kuishi, tunapaswa kuwa vivyo hivyo.

S: Ni aya zipi za Danieli zilizomo kwenye Hati za Kale toka Bahari ya Chumvi?

J: They are:
Dan 1:10-17 1Q71 (=1QDan a)
Dan 1:16-20 4Q112 (=4QDan a)
Dan 2:2-6 1Q71 (=1QDan a)
Dan 2:9-11, 19-49 4A112 (=4QDan a)
Dan 3:1-2 4Q112 (=4QDan a)
Dan 3:22-30 1Q71 (=1QDan a)
Dan 4:29-30 4Q112 (=4QDan a)
Dan 5:5-7, 12-14, 16-19 4Q112 (=4QDan a)
Dan 5:10-12, 14-16, 19-22 4Q113 (=4QDan b)
Dan 6:8-22, 27-29 4Q113 (=4QDan b)
Dan 7:1-6, 11(?), 26-28 4Q113 (=4QDan b)
Dan 7:5-7, 25-28 4Q112 (=4QDan a)
Dan 8:1-5 4Q112 (=4QDan a)
Dan 8:1-8, 13-16 4Q113 (=4QDan b)
Dan 8:16, 17(?), 20, 21(?)4Q114 (=4QDan c), 6Q7 (=6QpapDan)
Dan 10:5-9,11-16,21 4Q114 (=4QDan c)
Dan 19:8-16 6Q7 (=6Qpap Dan)
Dan 10:16-20 4Q112 (=4QDan a)
Dan 11:1-2,13-17,25-29 4Q114 (=4QDan c)
Dan 11:13-16 4Q112 (=4QDan a)
Dan 11:33-36, 38 6Q7 (=6Qpap Dan)
Tazama The Dead Sea Scrolls & Modern Translations of the Old Testament, uk.165 kwa maelezo zaidi. Tazama pia The Meaning of the Dead Sea Scrolls kwa maelezo zaidi.

S: Kwenye Danieli, ni nakala zipi za hati zenye maandiko ya kale zilizoandikwa zamani zaidi zilizopo leo?

J: Hati kutoka Bahari ya Chumvi: (mwaka 120 KK) nakala 8 tofauti kwa mujibu wa Dead Sea Scrolls Today, uk.30 na Wycliffe Bible Dictionary, uk.436-438. Hati ya zamani zaidi iliandikwa mwaka 120 KK.
1Q71
(=1QDan a) Dan 2:2-6; 3:22-30
1Q72
(=1QDan b)
4Q112
(=4QDan a) iliandikwa mwishoni mwa utawala wa Wahasmonea mwanzoni mwa utawala wa Herode. Hati hii inajumuisha Dan 1:16-20; 2:9-11, 19-49; 3:1-2; 4:29-30; 5:5-7, 12-14, 16-19; 7:5-7, 25-28; 8:1-5; 10:16-20; 11:13-16
4Q113
(=4QDan b) iliandikwa mwaka 20-50 BK. Hati hii ina Dan 5:10-12, 14-16, 19-22; 6:8-22, 27-29; 7:1-6, 11(?), 26-28; 8:1-8, 13-16
4Q114
(=4QDan c) iliandikwa mwaka 125-100 KK. Hati hii inajumuisha Dan 10:5-9, 11-16, 21; 11:1-2, 13-17, 25-29
4Q115
(=4QDan d), 4Q116 (=4QDan e) ina mabaki machache tu.
6Q7
(=6QpapDan) inajumuisha Dan 8:16; 17(?), 20, 21(?), 10:8-16; 11:33-36, 38. The Dead Sea Scrolls & Modern Translations of the Old Testament, uk.77 inasema imechakaa, lakini inakubaliana kwa ujumla na maandishi yaliyoandikwa kabla ya toleo la Kimasoretiki.
Kwa ujumla, aya zifuatazo za Kitabu cha Danieli zilizopo kwenye Hati za Kale kutoka Bahari ya Chumvi ni: 1:10-20; 2:2-6, 9-11, 19-49; 3:1-2, 22-30; 4:5?-9, 12-14, 29-30; 5:5-7,10-22; 6:8-22, 27-29; 7:1-7,11?,25-28; 8:1-8,13-16, 17?,20-21?; 9:12-15, 16?, 17?; 10:5-20; 11:1-2, 13-17, 25-29, 33-36, 38. Tazama The Meaning of the Dead Sea Scrolls, uk.423 kwa habari zaidi.
Theodotion
alikuwa Myahudi aliyeishi baada ya kupaa kwa Kristo aliyetafsiri Agano la Kale kwa Kigiriki. Kuna nakala za tafsiri yake ya Danieli, na vitabu vingine pia.
Christian Bible manuscripts,
kuanzia karibu mwaka 350 BK, yanajumuisha Agano la Kale, kikiwemo Kitabu cha Danieli. Karatasi za mafunjo za Chester (Chester Beatty Papyrii) IX na X (zilizoandikwa karne ya 2-4 BK) contain Daniel according to The Earliest New Testament Manuscripts p.367 and The Encyclopedia of Religious Knowledge p.746.
Karatasi la Mafunjo la Scheide (Scheide Papyrii) 1
linajumuisha Ezekieli, Danieli na Esta. Liliandikwa mwanzoni mwa karne ya tatu BK. Awali ilikuwa na makaratasi 118, 109 kati ya hayo yapo hadi leo. Kwa maelezo zaidi na picha yake tazama Manuscripts of the Greek Bible, uk.70-71.
Vaticanus
(mwaka 325-350 BK) inajumuisha Kitabu chot cha Danieli.
Hakuna sehemu yeyote ya Kitabu cha Danieli kwenye Sinaiticus (mwaka 340-350 BK).
Alexandrinus
(karibu mwaka 450 BK) inajumuisha Kitabu chote cha Danieli.
Waandishi wa kikristo pia walikinukuru Kitabu Danieli kwa kiasi kikubwa sana kama swali lifuatalo linavyoonyesha.

S: Ni waandishi gani wa awali walionukuru Kitabu cha Danieli?

J: Waandishi walioandika kabla ya kikao cha baraza la kanisa la Nikea walionukuru au kudokezea aya za Kitabu cha Danieli ni:
Clement wa Rome (mwaka 96-98 BK) [amesema lakini si moja kwa moja] "Kwani tutasema nini ndugu zangu? Je, Danieli alitupwa kwenye shimo la simba kama wale walomcha Mungu? Je, Anania na Azaria na Mikaeli walifungiwa kwenye tanuri la moto na wale walizingatia ibada nzuri na yenye utukufu ya Mungu Mkuu? Wazo hili na liwe mbali nasi!" Alinukuu Dan 6:16 na 3:20 (1 Clement, sura ya 45, uk.17).
Barua ya Barnabas
(mwaka 70-130 BK) sura 4, uk.138 "Kwa maana hiyo hiyo, da Danieli anasema kuhusu jambo hilo hilo, ‘Na nilimwona mnyama wa nne, mwovu na mwenye nguvu, na asiyefugika kuliko wanyama wote wa nyikani, na jinsi kutoka kwake zilivyochipuka pembe kumi, na kutoka kwenye pembe hizo ikachipuka ipembe nyingine ndogo, na jinsi ilivyojiweka chini ya moja ya tatu ya zile pembe kubwa."
Justin Martyr
(karibu mwaka 138-165 BK) "‘Kati ya maneno haya na mengine ya jinsi hiyo yaliyoandikwa na manabii, Ee Trypho,' alisema mimi, ‘wengine wameongelea ujio wa kwanza wa Kristo, ambamo anahubiriwa kama asiye na utukufu, asiyejulikana, na mwenye mwonekano wa mauti; lakini wengine wameongelea ujio wake wa pili, atakapokuja katika utukufu na juu ya mawingu; na taifa lako litamwona na kumjua yeye waliyemchoma, kama Hosea, mmojawapo wa manabii kumi na wawili, na Danieli walivyotabiri'" (Dialogue with Trypho the Jew, sura ya 14 uk.202).
Melito/Meleto wa Sardis
(mwaka 170-177/180 BK) anaorodhesha vitabu vyote vya Agano la Kale, na anajumuisha kila kitabu tulichonacho isipokuwa Nehemia na Esta (Kipande cha 4 From the Book of Extracts, uk.759).
Theophilus wa Antioki
(mwaka 168-181/188 BK) "Lakini kulingana na vipindi tunavyoviongelea, tunathibitishiwa na Berosus, mwanafalsafa wa Kikaldayo, aliyewafahamisha Wagiriki maandiko ya Kikaldayo, na kutamka mambo kadhaa kuhusu Mafuriko ya Nuhu, na mambo mengine mengi ya kihistoria, kwa mujibu wa Musa; na manabii Yeremia na Danieli pia, alikubaliana kwa kiasi kikubwa" (Theophilus to Autolycus, kitabu cha 3, sura ya 29, uk.121).
Irenaeus wa Lyons
(mwaka 182-188 BK) anukuru nusu ya Danieli 2:34 kama ya Danieli (Irenaeus Against Heresies, kitabu cha 3, sura ya 21.7, uk.453).
Clement wa Alexandria
(mwaka 193-205 BK) "Na nabii Danieli asema, ‘Fumbo ambalo mfalme anauliza, halimo kwenye uwezo wa wenye hekima, Mamajusi, waaguzi, Wagazareni, kumwambia mfalme; lakini ni Mungu aliye mbinguni anayefunua'" (Stromata, kitabu 1, sura ya 3, uk.304).
Tertullian
(mwaka 198-220 BK) "Na kisha kama inavyoyahusu mataifa yote hadi mwisho kabisa wa ulimwengu. Kwani baada ya kutangaza hivyo ‘Yerusalemu itakanyagwa na watu wa mataifa, hadi wakati wa watu wa mataifa utakapotimizwa'' –yaani, wale watakaochaguliwa na Mungu, na kukusanywa pamoja na watu waliosalia wa Israeli-Kisha anaendelea kuhubiri, dhidi ya ulimwengu na dispensheni (mpango uliowekwa na Mungu unaotawala kipindi husika cha historia) hii (hata kama alivyofanya Yoeli na Danieli na manabii wote kwa kauli moja), kwamba ‘panapaswa kuwa na ishara katika jua na katika mwezi, na katika nyota, dhiki ya mataifa na kuchanganyikiwa, bahari na mawimbi vikivuma, mioyo ya watu ikizimia kwa hofu, na kwa kutazamia mambo yale yanayotarajiwa kuja duniani'" (On the Resurrection of the Flesh, sura ya 22, uk.560-561).
Tertullian (mwaka 207/208 BK) "Pia alifunuliwa kwa Danieli mwenyewe kiwazi kama ‘mwanadamu, akija kwenye mawingu ya mbinguni' kama Hakimu, kama Maandiko yanavyosema pia" (Five Books Against Marcion, kitabu cha 4 sura ya 10, uk.359).
Hippolytus
(mwaka 225-235/6 BK) aliandika kitabu chenye maoni ya Kitabu cha Danieli. Kuna nukuu za sehemu za sura 1, 2, 3, 7, 9, 10, 12, vitabu vya kidini vya Kiyahudi vya kubuniwa (apokrifa) viitwavyo Song of the Three Children na Susannah.
Origen
(mwaka 225-254 BK) "Isitoshe, mtu yeyote anayependa anaweza kupata unabii kwenye Danieli unaomhusu mpinga Kristo" (Origen Against Celsus, kitabu cha 2, sura ya 50, uk.451).
Anonymous Treatise Against Novatian
(karibu mwaka 246-258 BK) sura ya 17, uk.662-663 "17. Kama mambo kwao pia asema Danieli:" na kisha anukuu Dan 7:9-10.
Cyprian
, askofu wa Carthage (karibu mwaka 246-258 BK) ananukuu "Danieli" kwenye Treatise 12, kitabu cha 10.
Firmilian wa Caesarea
akimwandikia Cyprian (mwaka 256 BK) Kwani neema ya Mungu ina uwezo wa kuhusisha na kuunganisha pamoja katika kifungo cha upendo na umoja hata vitu ambavyo vinaonekana kugawanyika kwa umbali mkubwa duniani, kulingana na njia ambayo awali pia nguvu za kimungu vilihusishwa katika kifungo kimoja Ezekieli na Danieli, ingawa baadaye katika enzi zao, na kutenganishwa nao umbali na muda mrefu, na Ayubu na Nuhu, waliokuwa kati ya watu wa kwanza; ili kwamba ingawa walitengwa na vipindi virefu, lakini kwa uvuvio wa kimungu walijisikia kweli ile ile" (Letters of Cyprian, Barua ya 74.3, uk.390).
Adamantius
(karibu mwaka 300 BK) ananukuu Dan 7:13 kama kazi iliyoandikwa na Danieli, akizifuatisha Septuajinti na Theodotion, kwenye Dialogue on the True Faith, Sehemu ya Kwanza, na.25, uk.69.
Victorinus of Petau
(aliyeuawa mwaka 304 BK) "Kutoka hapa anaweka, na kwa hapa anafanya upya, kile ambacho Bwana, akiyaonya makanisa yake kuhusu nyakati za mwisho na hatari zake, akisema: ‘Lakini mtakapoona shina la chukizo lililonenwa na nabii Danieli limesimama mahali patakatifu, asomaye na afahamu'" (Commentary on the Apocalypse kutoka Sura ya 13, na.13, uk.357).
Athanasius
(karibu mwaka 318 BK) "Danieli mwenye hekima zaidi, anayeonyesha muda halisi, na makazi ya muda ya Mwokozi akisema: ‘Majuma sabini yamefupishwa kwa watu wako, na kwa mji mtakatifu, . . ." (Incarnation of the Word, sura ya 39, uk.57).
Lactantius
(mwaka 315-325/330 BK) "Danieli alitabiri pia mambo yanayofanana na haya: ‘Nikaona, alisema, "katika maono ya usiku, na tazama, mtu mmoja kama mwanadamu akija na mawingu ya mbinguni, na akaja kwa Mzee wa Siku. Na wale waliosimama pale walileta karibu mbele yake. Na pale alipewa ufalme, na utukufu, na utawala; na watu wote, makabila yote, na lugha zote watamtumikia: na utawala wake ni wa milele, ambao hautaisha kamwe, na ufalme wake hautaharibiwa'" (The Divine Institutes, kitabu cha 4, sura ya 12, uk.111).
Baada ya Nikea

Eusebius wa Caesarea
(mwaka 318-339/340 BK) "Kwa kuwa Maandiko, kwenye Kitabu cha Danieli, yakiwa yametaja wazi namba fulani ya majuma hadi kuja kwa Kristo . . ." (Eusebius' Ecclesiastical History, kitabu cha 1, sura ya 6, uk.90).
Aphrahat Mshamu
(mwaka 337-345 BK) "Na tena Danieli pia alisema kuhusiana na jiwe hili ambalo ni Kristo." Na alinukuu Dan 2:34-35 (Select Demonstrations Demonstration 1, sura ya 8, uk.347).
Hilary wa Poitiers
(mwaka 355-367/368 BK) anataja watoto wa Kiyahudi kwenye miale na Danieli, "hawakuogopa kwenye shimo la simba" (On the Trinity, kitabu cha 10, sura ya 45-46, uk.194).
Life of Antony
(mwaka 356-362 BK) sura ya 82 uk.217 (huenda iliandikwa na Athanasius) inanukuu Dan 4:19 kwenye Septuajinti kama aya "iliyoandikwa kwenye Kitabu cha Danieli."
Synopsis Scripturae Sacrae
(mwaka 350-370 BK au karne ya 5).
Athanasius
(mwaka 367, 325-373 BK) anamworodhesha Danieli pamoja na vitabu vilivyobaki vya Agano la Kale kwenye Paschal Letter 39, sura ya 4, uk.552.
Ephraim
mwandika nyimbo wa Shamu (mwaka 350-378 BK) "Kwa sababu tazama, Danieli pia aliyeyushwa na kumiminwa kila upande mbele ya utukufu wa malaika, ambaye mng'ao wake mkubwa uliangaza ghafla juu yake" (Three Homilies, Homily 1, sura ya 27, uk.316).
Basil wa Cappadocia
(mwaka 357-379 BK)
Cyril wa Yerusalemu
(karibu mwaka 349-386 BK) inaitaja Dan 4:9 kuwa imo kwenye Kitabu cha Danieli (Catechetical Lectures, Mhadhara wa 16.31, uk.123).
Ambrose wa Milan
(mwaka 370-390 BK).
Gregory wa Nanzianzen
(mwaka 330-391 BK).
Pacian wa Barcelona
(mwaka 342-379/392 BK) "Kwa maombi Danieli aliuondoa upanga juu ya wenye hekima wa Babeli" (Letter 3, sura ya 24.1, uk.66).
Pacian wa Barcelona (mwaka 342-379/392 BK) anadokezea vitabu vya Esta na Danieli (Letter 2, sura ya 5.1, uk.33).
Gregory wa Nyssa
(karibu mwaka 356-397 BK)
Epiphanius wa Salamis
(mwaka 360-403 BK) anataja vitabu vyote vya Agano la Kale.
Rufinus
(mwaka 374-406 BK).
John Chrysostom
(alikufa mwaka 407 BK) anaitaja Dan 7:13-15 kuwa iliandikwa na Danieli kwenye juzuu ya 9 (Letters to the Fallen Theodore, sura ya 12, uk.101).
Sulpitius Severus
(mwaka 363-420 BK) anakitaja Kitabu cha Danieli kama Kitabu cha Danieli kwenye History, kitabu cha 2, sura ya 1-2, uk.97.
Jerome
(mwaka 373-420 BK).
Baraza la kanisa la Carthage
[maaskofu 218] (mwaka 393-419 BK)
Augustine wa Hippo
(mwaka 338-430 BK) anavitaja vitabu vya Danieli na Ezekieli kwenye The City of God, kitabu cha 17, sura ya 34, uk.380.
Mpelagia nusu John Cassian (mwaka 419-430 BK).
Theodoret wa Cyrus
[askofu na mwana historia] (mwaka 423-458 BK).
Jerome na Gennadius
(karibu mwaka 485-492 BK).
Gregory wa Rumi (mwaka 590-605 BK) (anadokezea)
Miongoni mwa vitabu vyenye mafundisho tofauti na vya uongo

Megethius
(karibu mwaka 300 BK) anukuu Dan 2:34-35, kama iliyoandikwa na Danieli, akifuata Septuajinti na Theodotion, kwenye mdahalo wake na Adamantius (Dialogue on the True Faith, Sehemu ya kwanza na.25, uk.68).

S: Kwenye Danieli, kuna tofauti gani ya tafsiri za Kiebrania na ya Kigiriki?

J: Kwa kutilia mkazo sura ya 9, tafsiri mbadala ya kwanza ni Biblia ya Kibrania (Agano la Kale), yaani Toleo la Kimasoretiki (Massoretic Text, MT), nay a pili ni Toleo la Kigiriki la Biblia ya Kiebrania (Septuajinti), isipokuwa imeelezwa tofauti.
Dan 1:2
"Kwa nchi ya Shinari" (Septuajinti, Theodotion) dhidi ya "Kwa nchi ya Shinari kwenda kwenye nyumba yake mwenyewe" (Kihebrania).
Dan 2:40 "Kama ambavyo chuma kipiga na kusaga kila kitu" (Septuajinti, Kishamu, Vulgate) dhidi ya "Kama ambavyo chuma kinapiga na kusaga kila kitu, na kama chuma kinachopiga" (Kiarami).
Dan 2:43
"Kwenye ndoa (nyingi za tafsiri) dhidi ya "Kwa mbegu za wanadamu (Kiarami).
Dan 3:15 "Niliyoifanya, nzuri nay a kupendeza" (nyingi za tafsiri) dhidi ya "Niliyoitengeneza" (Kiarami).
Dan 3:25 "Sura ya mungu" (nyingi za tafsiri) dhidi ya "Sura ya mwana wa miungu" (Kiarami).
Dan 4:9
"Sikia ndoto" (nyingi z tafsiri) dhidi ya "Sikia maono ya ndoto"" (Theodotion, Kiarami).
Dan 6:1
"Dario" (Toleo la Kimasoretiki, Septuajinti) dhidi ya "Artashasta" (matoleo yaliyomtangulia Theodotion).
Dan 7:1 "[Danieli] alisema/alieleza jumla ya mambo yote" (Toleo la Kimasoretiki) dhidi ya "[Danieli] jumla ya mambo yote" (4QDana).
Dan 6:6 "Aliandika ndoto kwa mtindo wa ufupisho" (MT) dhidi ya "Aliandika maneno" (Theodotion, kwa mujibu wa tafsiri ya Kiingereza Kipya (The NET Bible).
Dan 7:5
"Kwenye kinywa chake katikati ya meno yake" (MT) dhidi ya "Kwenye kinywa chake" (Septuajinti).
Dan 7:9-10
"Niliona kiti cha enzi kimewekwa, na Mzee wa Siku aliketi juu yake, na mavazi yake yalikuwa kama theluji, na nywele za kichwa chake kama sufu nyeupe: kiti chake cha enzi kilikuwa miale ya moto, na magurudumu yake yalikuwa moto uwakao. Mto wa moto ukuja mbele yake: maelf elfu walimtumikia, na maelfu elfu walisimama mbele zake: aliketi kuhukumu, na vitabu vikafunguliwa" (Anonymous Treatise Against Novatian [karibu mwaka 246-258 BK], sura ya 17, uk.662-663).
Dan 8:5
"Pembe ya maono" dhidi ya "Pembe moja" (Septuajinti, Theodotion).
Dan 9:1
"Alifanywa kuwa mfalme" dhidi ya "aliyetawala"
Dan 9:2
"Lililokuja kama neno" dhidi ya "Lililokuwa neno."
Dan 9:3
"Kutaka kwa maombi" dhidi ya "Kutaka kwa bidii kwa maombi."
Dan 9:4
"Wampendao . . . zake" dhidi ya "Wakupndao . . . zako."
Dan 9:7
"Haya ya uso" dhidi ya "Mchafuko wa uso."
Dan 9:8
"Haya" dhidi ya "Mchafuko."
Dan 9:10
"Kwa watumishi wake" dhidi ya "Kwa mikono ya watumishi wake ."
Dan 9:11
"Wasiisikilize" dhidi ya "na wamekataa."
Dan 9:13
"Hatukumwomba BWANA" dhidi ya "Hatukumsihi Bwana Mungu wetu."
Dan 9:13
"Na kuitambua kweli yako" dhidi ya "Na kuitambua kweli yako yote."
Dan 9:14
"Ameyavizia mabaya hayo, na akatuletea" dhidi ya "Pia ameyaangalia, na ametuletea [maovu] juu yetu."
Dan 9:16
"Ee Bwana, nakusihi, sawasawa na haki yako" dhidi ya "Ee Bwana huruma za yapita vyote; acha nikuombe."
Dan 9:16
"Hasira . . . hasira kali" dhidi ya "Ghadhabu . . . hasira."
Dan 9:16
"Maana kwa sababu ya dhambi zetu na maovu ya baba zetu" dhidi ya "Kwa kuwa tumetenda dhambi, na kwa sababu ya maovu yetu na ya baba zetu"
Dan 9:17
"Maombi" dhidi ya "dua"
Dan 9:17
"Kwa ajili ya Bwana" dhidi ya "Kwa ajili yako, Eh Bwana"
Dan 9:19
"Ee Bwana, usamehe" dhidi ya "Ee Bwana uturehemu"
Dan 9:20
"Kilio changu kinaanguka mbele" dhidi ya "Nilipokuwa nikiomba na kuiungama dhambi."
Dan 9:21
"Nikipanga maombi yangu" dhidi ya "Nikisema ombi langu."
Dan 9:21
"Mtu yule" dhidi ya "Tazama mtu yule."
Dan 9:21
"alinigusa katika kuchoka [kwangu] kukubwa mno" dhidi ya "[Alikuja] akirushwa upesi, alinigusa."
Dan 9:22
"Amekufanya ufahamu / kukupa ujuzi katika ufahamu" (Kiebrania) dhidi ya "Akaniagiza, akaongea nami" (Kiebrania, kwa mujibu wa maelezo chini ya ukurasa kwenye toleo la NET) dhidi ya "Alikuja / kukupa ufahamu" (Septuajinti, Kishamu). Maelezo chini ya ukurasa kwenye toleo la NRSV hayakubaliani kabisa na tafsiri ya Brenton).
Dan 9:23
"Itafakari" dhidi ya "Ifahamu."
Dan 9:24
"Ili kuyakomesha makosa, na kuishiliza dhambi, na kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu, na kuleta haki ya milele, na kutia muhuri maono na unabii" dhidi ya "Ili kutamatisha dhambi, na kuyatia muhuri makosa, na kutupilia mbali maovu, na kufanya upatanisho kwa ajili ya makosa, na kuleta haki ya milele, na kuyatia muhuri maono na nabii."
Dan 9:24
"Kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu" (Qere, Septuajinti, Kishamu, Vulgate) dhidi ya "Kutia muhuri Patakatifu pa Patakatifu" (Ketubim, Theodotion).
Dan 9:25
"Majuma 62. Njia kuu zake" dhidi ya "Majuma 62, kisha [wakati] atarudi na njia kuu."
Dan 9:25
"Naam katika nyakati za taabu" dhidi ya "Na nyakati zitadhoofishwa."
Dan 9:26
"Masihi atakatiliwa mbali, lakini si [kwa ajili yake yeye] Mwenyewe. Na watu wa mkuu atakayekuja watauangamiza mji na patakatifu. Na mwisho wake [utakuwa] pmoja na gharika, na hata mwisho ule vita [vitakuwapo]" dhidi ya "Masihi ataharibiwa, na hakuna hukumu ndani yake: na atauharibu mji na mahali patakatifu na mfalme anayekuja: watakatiliwa mbali na mafuriko, na mwishoni mwa vita itakayomalizwa haraka atateua [mji] wa uharibifu."
Dan 9:27
"Agano thabiti na watu wengi [kwa muda wa] juma moja" dhidi ya "Agano na wengi."
Dan 9:27
"Ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake [pa madhabahu] litasimama chukizo la uharibifu. Na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu" dhidi ya "na katikati ya juma sadaka yangu na sadaka ya kinywaji itaondolewa; na juu ya hekalu [kutakuwa] na chukizo la uharibifu; na mwisho wa muda uharibifu utaondoshwa."
Dan 10:1
"Uajemi" dhidi ya "Waajemi."
Dan 10:1
"Belteshaza" dhidi ya "Baltasar."
Dan 10:14
"Niliachwa huko pamoja na wafalme wa Uajemi" dhidi ya "Nilimwacha huko pamoja na wafalme wa Uajemi" (Septuajinti, Theodotion).
Dan 10:16
"Mfano wa mwanadamu" dhidi ya "Mfano wa mtoto wa kiume" (Thdototion, Vulgate), dhidi ya "Kitu kilichokuwa mfano wa mkono wa mwanadamu" (Septuagint, Hati za Kale kutoka Bahari ya Chumvi, Toleo mojawapo la Kiebrania la Kimasoretiki).
Dan 10:17
"Kwa maana kwangu mimi kuanzia sasa" dhidi ya "Kwa maana kwangu mimi, mara hazikusalia nguvu ndani yangu" (Septuajinti, NRSV).
Bibliografia ya swali hili: tafsiri ya Kiebrania ni ya Jay P. Green, Literal Translation na tafsiri ya Kigiriki (Septuajinti) ni ya Sir Lancelot C.L. Brenton, The Septuagint: Greek and English. The Expositor's Bible Commentary na maelezo chini ya ukurasa kwenye matoleo ya Biblia ya NASB, NIV, NKJV na NRSV pia yalitumika. Kitabu kingine kilichotumika ni The Dead Sea Scrolls & Modern Translations of the Old Testament.