Maswali ya Biblia Kitabu cha Mwanzo

 

Swali (S): Kwenye Mwanzo, tunajuaje kuwa Kitabu cha Mwanzo kinatakiwa kuwa kwenye Biblia?

Jibu (J): Pamoja na sababu nyingine, kwa sababu Yesu na watu wengine wengi kwenye Biblia walithibitisha ukweli wa Agano la Kale na walikielezea Kitabu cha Mwanzo kuwa ni Maandiko (Matakatifu).

 

S: Kwenye Mwanzi, ni nani aliyejibu maswali ya Kitabu cha Mwanzo?

J: Kwa kadri nijuavyo, mtu wa kwanza kuandika majibu ya maswali yahusuyo kitabu cha Mwanzo ni Philo, Myahudi wa Kiyunani (Kigiriki) wa Alexandria aliyeishi kutoka karibu mwaka 20 KK hadi 50BK. Leo hii tunayo tafsiri ya Kiarmenia ya kazi yake. Aliandika kazi yake yenye sehemu tatu, Questions and Answers on Genesis (Maswali na Majibu kuhusu Mwanzo). Tumetunza majibu yake kwa maswali 244 toka Mwanzo 1 hadi 17, kwa mujibu wa mtazamo wa Myahudi mcha Mungu ambaye aliathiriwa sana na falsafa za Kigiriki za Plato.

 

S: Kwenye Mwanzo 1, kwa kuwa vitu vingine vinapaswa kuwa kweli, kama 1 = 1, na 1 + 1 = 2, je Mungu aliumba hesabu na namba? Angeweza kuviumba kwa njia nyingine tofauti?

J: Mungu aliumba kilakitu; hata hivo, marudiorudio (tautology), kitu ambacho ni kweli sawa na maana yake ilivyo kama vitu vyekundu vina rangi nyekundu, si kitu. Tunaweza kukisia kuwa Mungu aliumba "kila kitu" kwenye hesabu na hii si marudiorudio.

 

S: Kwenye Mwanzo 1, kwa kuwa Mungu aliumba kila kitu, je aliumba giza, uovu, na mashimo ardhini? Kama aliumba uovu, haonyeshi kuwa mzuri mkamilifu. Kama sivyo, yeyote aliyeumba anaonyesha kuwa muumbaji pia.

J: Mungu aliiumba vitu vyote. Giza si kitu, bali ni kutokuwepo au upungufu wa mwanga. Uovu si kitu, bali kutokuwepo au kupotoa mambo mema. Mashimo, giza, na maovu hayakuumbwa moja kwa moja na Mungu, lakini yametokea kama marudiorudio, au "matokeo ya maisha" ya mada, mwanga na mambo mema. Hivyohivyo, kivuli si kitu kinachojitegemea, kikiwa na mada, nishati, au roho. Hata hivyo, mimea inaweza kufa kwenye kivuli.

 

S: Kwenye Mwanzo 1, kwa kuwa Mungu aliumba kila kitu kikiwa kizuri, kwa nini radi, milipuko ya magonjwa na majanga mengine hutokea?

J: Kila kitu kilikuwa kizuri mwanzoni. Lakini Warumi 8:20-22 inaonyesha kuwa tokea wakati wa anguko, dunia "ilitiishwa chini ya ubatili" pia. Ulimwengu wote upo chini ya utawala wa mwovu(1 Yohana 5:19), na mkuu wa dunia hii ni Shetani kwa mujibu wa Yohana 12:31; 14:30.

 

S: Kuna hoja gani ya umbo na muundo wa ulimwengu kwenye Mwanzo 1?

J: Kwanza, ifuatayo ni njia rahisi na yenye mantiki rahisi yenye kuelezea.

Huwezi kupata kitu bila kuwa na kitu (kingine). Kila kitu kilichoumbwa kilihitajika kuumbwa. Hata vitu vya kwanza kuumbwa vilihitajikwa kuumbwa na kitu/mtu mwingine ambaye aliisha kuwepo. Kwa hiyo, panatakiwa kuwa na kitu au mtu ambaye hajaumbwa na anaishi milele.

Yafuatayo ni maelezo makali; maana ni zangu mwenyewe.

Tunadhani kuwa kila mtu anaufahamu wa kutosha kuweza kuwa na maana inayofaa ya mantiki, kupingana na kutopingana, tukio, mchakato, "ndani ya", kitu, mkusanyiko, muda, mada, nishati, roho, chanzo, kilichosababishwa na, na matokeo.

Uwepo halisi kunafafanuliwa, katika makala hii, kuwa ni kuwepo kwenye ulimwengu huu, kuwa na uwezo wa kuathiriwa na kitu mojawapo hapa ulimwenguni, au kuwa na uwezo wa kuathiri kitu kimojawapo hapa ulimwenguni. Huu ni ufafanuzi mfinyu sana wa kuwepo/kuishi, kwani unashindwa kuhusisha mawazo, mienendo, na mambo mengine. Kwa hiyo, hebu na tuuite uwepo "halisi" na tufanye majadiliano yetu hapa yakomee kwenye uwepo halisi.

Kitu halisi kinafafanuliwa hapa kuwa ni kitu au mkusanyiko au mada, nishati, roho, au mchanganyiko wenye kuwa na uwepo halisi. Ukweli wa kimantiki, ukinzani wa kimantiki, na ushahidi wa kihesabu havichukuliwa kuwa vitu hapa.

Uwepo wa kimelea, kama kitu cha ndani, unfafanuliwa kuwa ni uwepo halisi wa vitu ambavyo si vitu halisi. Mashimo, giza, upungufu, kutokuwa sahihi, na maovu si mada, nishati, au roho, lakini kama ambavyo kivuli kinaweza kuua mimea ambayo inahitaji jua, au upungufu ea chakula unavyoweza kuua mtu, vivuli na upungufu wa chakula vina uwepo halisi licha ya kutokuwa vitu halisi.

Ulimwengu unafafanuliwa hapa kuwa ni mkusanyiko wa vitu halisi ambavyo vipo kiuhalisi. Tazama kuwa katika ufafanuzi huu, ulimwengu unajitisheleza, na Mungu (tuchulie kuwa Mungu yupo, ni roho na anaweza akaathiri vitu) yupo ulimwenguni.

Kutokwepo (nothing) kunafafanuliwa kuwa ni kitu ambacho hakijawahi kabisa kuwepo, au ambacho hakijawahi kuwa na uwepo wa kweli/kihalisi wakati wowote ule. Kwa maneno mengine, kabla hakijaumbwa [au baaday ya kuharibiwa], kitu halisi hakipo ulimwenguni, hakiuathiri ulimwengu, na hakiathiriki na ulimwengu.

Uumbaji unafafanuliwa hapa kuwa ni tukio au mchakato wa kufanya kitu halisi kipya. Kuumba kunatofautishwa na "kubadilisha", ambako hakuhitaji chanzo chochote mbali ya kitu chenyewe. Kuumba kitu halisi kipya kunaweza kuhusisha kubadilisha au kuharibu kitu halisi kilichowahi kuwepo, lakini hakulazimiki kufanya hivyo. Hata hivyo, angalia sehemu inayofuata.

Hakuna kitu kinachoweza kuwepo kutokana na kitu kisichokwepo. Kitu chochote halisi kilichoumbwa kinahitaji chanzo cha kuumbwa kwake. Kwa maneno mengine, hakuna kitu kinachoweza kuumbwa isipokuwa kitu/vitu vinginie vimekiumba.

Hakuna kitu kinachoweza kujiumba chenyewe. Hakuna kitu kinachoweza kujiumba chenyewe. Ingawa vitu halisi vinaweza kujibadilisha wakati mwingine, au kujiharibu vyenyewe, hakuna kitu kinachoweza kuwa chanzo cha kuumbwa kwake.

Chanzo cha kwanza. Ingawa vitu halisi vilivyoumbwa vinaweza kuumba vitu vingine halisi vilivyombwa, mwisho wa siku patahitajika kuwa na chanzo cha kwanza. Kwa maneno mengine, kwenye mlolongo wa vyanzo, chanzo walau kimoja kinatakiwa kuvitangulia vyanzo vingine vyote.

Kisichoumbwa. Kwa vile chanzo walau kimoja hakitakiwa kuwa na chanzo kilichokitangulia, na kila kiumbe kinahitaji chanzo, kuna kitu halisi walau kimoja ambacho hakijaumbwa na kimekuwepo toka milele iliyopita, kwa sababu kuna kitu halisi walau kimoja ambacho hakijaumbwa.

Mhutasari: Kila kitu halisi ambacho kinaishi ama kina wakati au kipindi fulana=i ambacho kiliwahikuishi, vinginevyo hakijawahi kuishi. Kama kimewahi kuishi, basi kuna kitu halisi ambacho ni chanzo cha kuwepo kwake.

Mipaka: Hoja hii haithibitishi kwamba chanzo cha kwanza ni kitu chenye uhai, au kwamba kuna chanzo kimoja tu ambacho hakijaumbwa, au kwamba vyanzo vyovyote ambavyo havijaumbwa bado vinaishi. Kitu ambacho hoja hii inasema ni kwamba kuna walau kitu kimoja halisi (nafsi iliyo hai au kitu kisichokuwa nafsi) ambacho kimekuwepo milele bila kuumbwa.

Moja ya waandishi wa kwanza aliyeiona hoja ya muundo na umbo la ulimwengu na kusema kuwa Mungu ni chanzo cha kwanza alikuwa Philo, Myahudi aliyeishi Alexandria, Misri, toka mwaka 15/20 KK hadi mwaka 50BK. R. C. Sproul na Norm Geisler wameandika kazi nyingi na nzuri kuhusiana na hoja ya muundo na umbo la ulimwengu.

 

S: Hoja kuwa "kushindwa kuelezeka kirahisi kwa ulimwengu kunaonyesha kuwa ni lazima kuwe na muumba" inaonekana nzuri, hadi inapochukuliwa kwenye hitimisho lake la kimantiki. Vipi kuhusu ugumu wa Mungu kueleweka? Kama kitu chenye utatanishi kinahitaji muumba basi Mungu lazima ahitaji muumba mkubwa zaidi, na kwa jinsi hiyohiyo na kuendelea. Je hoja hii inaishia wapi? Hoja hii inaishia na "kurudi nyuma kusikokuwa na ukomo," na hakuna jibu kwa hili? Ama je lipo?

J: Kabla ya kuijibu hoja hii, hebu nilikuze "tatizo hili" kwanza. Licha ya ugumu wa kuelezeka, suala hil pia ni aina iliyopotoka ya hoja ya muundo na umbo la ulimwengu. Kama kila kitu kina chanzo, basi Mungu naye pia ana chanzo.

Kwa kuwa kila kitu ni lazima kiwe na mwisho, vinginevyo hakitakuwa na mwisho, kuna majibu mawili tu yanayoweza kutolewa:

    hakuna mwisho wa kurudi nyuma kusikokuwa na ukomo hakuna mwisho wa kurudi nyuma kusikokuwa na mwisho, chanzo ambacho hakijasababishwa na kitu kingine chochote.

Kama a), kusingekuwa na mwisho wa kurudi nyuma kusikokuwa na ukomo, basi si kila kitu kingekuwa na chanzo kwa sababu kurudi nyuma kusikokuwa na mwisho kwenyewe hakuna chanzo. Kwa hiyo, kwa vyovyote vile kuna mtu/kitu ambacho hakina chanzo.

Kama b), kuna mwisho wa kurudi nyuma kusikokuwa na mwisho, basi ni lazima kuwe na chanzo cha kwanza, cha ugumu fulani wa kufahamika. Kwa ajili hiyo, jambo hili linamaanisha kuwa Mungu si nafsi iliyotokana na kitu kingine, si matunda ya uumbaji.

Hata hivyo nashangaa, kama Mungu angeiona hoja hii yote kuwa nyepesi namna hii, kw asababu tunafikiri kuhusu vyanzo ndani ya muda. Kama mungu anaishi nje ya muda na pia ndani yake, na kama muda ni kitu kimojawapo kilichoumbwa na Mungu, basi kusema kuwa hali ilikuwaje kabla ya kuwepo kwa Mungu ni kujipinga.

 

S: Kwenye Mwanzo 1, Mungu anaweza kuwa aliumba viumbe wengine na ulimwengu mwingine?

J: Aliumba viumbe wengine: malaika na mapepo. Kuhusu kuumba ulimwengu mwingine wenye viumbe ndani yake, Biblia haituambii haya yote tunayotaka kujua — na tunapaswa kuhakikisha kuwa walau tunasoma jambo hilo. Mungu angeweza kuwa ameumba ulimwengu mwingine, na huenda hizo ndizo mbungu na kzimu.

 

S: Kwenye Mwanzo 1, kwa nini Mungu aliwaumba Adam na Hawa, kwa kuwa Munug alijua kabla kwamba hawatamtii?

J: Pamoja na Mungu kujua kuwa watafanya dhambi, anatuambia vitu kadhaa kutuonyesha kuwa kwa nini aliumba watu.

Kwa utukufu wake: Mungu aliumba watoto wake kwa utukfu wake. Isaya 43:7; 61:34.

Watu wa kuwapenda: Mungu anatupenda sana. Zaburi 145:9,17; 1 Yohana 3:1.

Kuwa watoto wake: 1 Yohana 3:1-2; Wagalatia 3:28, Warumi 8:15-17.

Kuishi ndani mwetu: 1 Yohana 4:12-16; Warumi 8:9-11.

Mungu hataki mtu yoyote apotee. Ezekiel 18:23, 32; 33:11; 2 Petro 3:9. Hata hivyo, Mungu hajuti kwa kuwaumba watu ambao walipopewa nafasi walichagua kwa hiari zao wenyewe kumkataa. Mungu aliishajua kabla kuwa watafanya dhambi, na bado hakupenda kuingilia uchaguzi wao au "kutokuwaumba."

Huenda moja ya sababu ya Mungu kuwaumba viumbe ambao watakuwa na sura yake inafanana na sababu ya wazazi kuwa na watoto. Ni kweli, watoto wana gharamua: nepi, chakula, na kweli wanasababisha maumivu ya kichwa tokana na kuugua, kuumia, na kutokutii lakini pamoja na hayo yote upendo unawafanya wastahili kuwepo.

 

S: Kwenye Mwa 1:1, Mungu aliumba kwa sababu alihitaji kuumba?

J: Biblia haiungi mkono hisia hizi. Mungu hana uhitaji wowote ule, kwa maana ya kwamba atadhulika au kukoma kuwepo kama hangeumba vitu vingine. Kwa upande mwingine, lengo la Mungu lilikuwa kuumba, na Mungu alitimiza lengo hilo kwa kiasi kikubwa kikubwa sana.

 

S: Kwenye Mwa 1:1, je kulikuwa na uumbaji zaidi ya Mwanzo?

J: Maandiko hayasemi chochote kuhusu jambo hili, na Mungu Mungu anao uhuru wa kufanya kama apendavyo. Kama Mungu angeumba viumbe wengine, wangekuwa kama malaika, mapepo, kama Adam na Hawa kabla ya anguko, kama sisi, kama mapepo, kama wanyama, au kitu tofauti kabisa.

 

S: Kwenye Mwa 1:2, kama Roho ya Mungu ilikuwa inatulia juu ya uso wa maji, jambo hili linamaanisha Roho wa Mungu si nafsi hai yenye akili bali nguvu itendayo kazi kama Mashahidi wa Yehova wanavyodai?

J: Hapana. Kwamba Roho Mtakatifu hana mwili na anaweza kutembea juu ya maji haipingani na ukweli kwamba Maandiko yanamwonyesha Roha Mtakatifu kuwa kiumbe kinachoishi na chenye nafsi.

Yafuatayo ni marudio ya maelezo ya 1 Yohana 5:6-8.

Shahidi anaweza kuwa ni nafsi hai au kitu kisichokuwa na uhai. Kosa la Mashahidi wa Yehova (Jehovah's Witnesses) ni kwamba kwa kuwa Roho Mtakatifu ana sifa nyingi ambazo mwanadamu hana, basi (kwa kupanua hoja) Roho Mtakatifu hawezi kuwa na nafsi. Kwenye 1 Yohana 5:6-8 tunaona kuwa kuna mashahidi watatu wa ukweli kuwa Yesu alikuwa na mwili. Damu inayomaanisha kusulubiwa kwake, na Roho ni ushuhuda wa ndani kwa Wakristo. Maji yanamaanisha kubatizwa kwa Yesu na Yohana, au yawezekana maji yanayomzunguka mtoto wakati wa kuzaliwa.

Yafuatayo ni mambo mbalimbai ambayo Biblia inatufundisha kuhusu nafsi ya Roho Mtakatifu.

Parakletos (mfariji, yeye anayekuwa pamoja nasi - Yohana 14:16, 26; 15:26)

Hufahamu mawazo ya ndani ya Mungu (1 Korintho 2:10-11)

Huongea nasi (Mdo 13:2; Ebr 3:7)

Hutufundisha (Yohana 14:26)

Kama mzazi, ili kwamba tusiwe yatima (orphanos kwenye Kigiriki - Yohana 14:18)

Hutuongoza (Yohana 16:13)

Hutufundisha (Yohana 14:26; 1 Kor 2:13)

Huishi ndani yetu (1 Kor 3:16; 2 Tim 1:14; Rum 8:9, 11; Efe 2:22)

Mioyoni mwetu (2 Kor 1:22; Gal 4:6)

Hutuombea (vitu visivyo na uhai haviombi au kuombea - Rum 8:26-27)

Anaweza kufanyiwa jeuri (Ebr 10:29)

Humshuhudia Kristo (Yohana 15:26)

Anao ufahamu (Rum 8:27)

Anaweweza kuhuzunishwa (Isa 63:10; Efe 4:30)

Hufanya maamuzi (1 Kor 12:11)

Hupenda (Rum 15:30)

Anaweza kupendezwa na mambo (Mdo 15:28)

Huchunguza mambo ya ndani ya Mungu (1 Kor 2:9-10)

Huugua (na kwa ajili hiyo hutujali - Rum 8:26)

 

S: Kwenye Mwa 1:10, ilikuwaje Mung aumbe dunia wakati dunia ilikuwa tayari imeishaumbwa kwenye Mwa 1:1?

J: Neno la Kiebrania (eres) ni hilo hilo linalotumika sehemu zote. Kama ilivyo kwenye kiingereza, eres inaweza kumaanisha ulimwengu chini ya anga, na inaweza kumaanisha ardhi au nchi kavu. Kwa hiyo Mungu aliiumba sayari kwenye Mwa 1:1, na nchi kavu kwenye Mwa 1:12. Tazama Encyclopedia of Bible Difficulties uk.65-66.

 

S: Kwenye Mwaanzo 1 na 2, kwa nini inaonekana kana kwamba kuna matukio mawili ya uumbaji?

J: Mwanzo 1 ni uumbaji wa mbingu na nchi, na Mwanzo 2 ni uumbaji wa wanadamu kwenye bustani ya Edeni.

 

S: Kwenye Mwanzo 1 na sehemu nyingine, kwa nini Mungu anaitwa Elohim, wakati sehemu nyingine tena kama Mwanzo 2 Mungu anaitwa Yahweh?

J: Mungu ana idadi kubwa ya majina kwenye Biblia. Inaonekana kuwa jina Yahweh linaangalia zaidi uhusiano binafsi wa Mungu na sisi tofauti na Elohim, ambalo linaangalia zaidi haki na ukuu wake.

Lilikuwa jambo la kawaida katika jamii za zamani kuwa na majina zaidi ya moja kwa mungu huyohuyo. Hii hapa ni mifano:

Osiris – Wennefer, Khent-amentius, Neb-abdu

Bel – Enlil, Nunamnir

Sin – Nanna

El – Latpan

Baal – Larpan

 

S: Kwenye Mwanzo 1, je Mungu aliweza kuumba dunia kwa siku sita halisi zenye masaa 24 kila moja?

J: Bila kujali kama wanadhani dunia iliumbwa miaka mingi iliyopita au michache, Wakristo wote wanapaswa kujibu swali hili "ndiyo."

Badala ya siku sita, Mwenye enzi angeweza kuiumba kwa muda wa sekunde sita kama angependa kufanya hivyo. Suala hapa si jinsi gani Mungu alipaswa kuumba bali ni jinsi gani Maandiko na ulimwengu vinaonyesha alichagua kuumba.

Kama nyongeza, Maandiko hayasemi siku ina urefu gani kwa Mungu kwenye Mwanzo 1. Kumbukumbu 7:1 inaonyesha kuwa "siku" inaweza kuwa ni kipindi cha muda kinachozidi masaa 24, kama ilivyoeleweka kuwa "siku" za Musa. Zaburi 90:4; 2 Peter 3:8 zinaonyesha kuwa siku za Munugu zinaweza kuwa ndefu sana.

 

S: Kwenye Mwanzo 1, je kufanana kwa maelezo haya ya uumbaji na yale ya Wababeli kunathibitisha kuwa yote haya yametoka kwenye chanzo kimoja kilichotungwa na watu?

J: Maelezo ya Wababeli yanafanana kwenye ufafanuzi wa kinaganaga lakini karibu ni kinyume kabisa kuhusiana na chanzo. Tofauti na Marduk aliyekuwa anashindana na vurugu za joka kubwa Tiamat, Mungu anaamuru nini kitokee. Kama kuna kitu cha kweli kwenye jamii zisizokuwa za kibiblia jambo hili halipaswi kutushangaza. Isitoshe mtinod wa Mwanzo 1 unaelekea kuwa ni utofauti uliokusudiwa dhidi ya nadharia za kipagani.

 

S: Kwenye Mwa 1:26 na 3:22, kwa nini neno "tumfanye" linatumiwa kwa Mungu Mmoja wa Kweli?

J: Kuna majibu mawili yanayoweza kutolewa.

1. "Tumfanye" inaweza kuwa inamwelezea Mungu mmoja wa Kweli, lakini uwingi wa kitenzi ni namna ifaayo ya maongezi miongoni mwa nafsi za Utatu Mtakatifu.

2. "Uwingi wa kifalme" ulitumika kwa wafalme na miungu kuelezea mtu/nafsi mmoja. Kama mfano wa jambo hili kwenye dini ya Mashariki ya Kati ya Kiislam, Kurani inatumia kitenzi na pronomina za wingi wakati Allah anaongea kuhusu yeye mwenyewe. Waislam na watu wasiokuwa Waislam wanaweza kukubali kuwa kutumia "uwingi wa kifalme" kwenye Kurani hakumaanishi kuwa Muhammad alifundisha kuwa Allah alikuwa mungu zaidi ya mmoja.

Hata hivyo, Philo Myahudi (15/20 KK hadi 50 BK) alitafsiri uwingi wa kitenzi kuwa si "uwingi wa kifalme" bali kwamba Mungu alitumia wasaidizi kwenye wakati wa kuumba sura ya 24 na.75 uk.11.

 

S: Je Mwa 1:26 inamaanisha kuwa tunapaswa kupata elimu ili kuufikia ukamilifu wa kiungu na kiini cha baraka za kiungu, kama Wabahai wanavyofundisha kwenye Some Answered Questions uk.8, 9?

J: Hapana, kwa sababu Mwanzo 1:27 inasema kuwa Mungu alifanya kile alichosema kwenye Mwanzo 1:26. Wakati Adam na Hawa walipoumbwa, walikuwa wakamilifu bila dhambi kabla ya anguko, na hawakuhitaji elimu. Tukiwa tungali na sura ya Mungu, Mwanzo 1:26-28 inaongelea mambo ambayo Mungu ameisha yafanya.

 

S: Je Mwa 1:26 inamaanisha binadamu wenyewe ni "miungu wadogo", kama Kenneth Hagin na watu wengine wanaofundisha neno-imani wanavyosema?

J: Hapana. Neno lililopo kwenye kitabu cha Mwanzo ni "kama" siyo "ni." Hata waalimu wa neno-imani wanakubali kuwa viumbe kama sisi hawakupaswa kabisa kuabudiwa. Miili ya Adam na Hawa ilipewa maisha ya umilele unaoweza kupotezwa, haki inayoweza kuharibiwa, na upendo mkamilifu kwa Mungu ambao unaweza kutupwa mbali kama kipande cha zamani cha tunda.

 

S: Kwenye Mwa 1:26-27, je hayo yalikuwa ni maongezi ya nafsi za Utatu Mtakatifu, au viumbe vilivyoumbwa kama vile malaika?

J: Ingawa malaika wanaweza kuwa walisikia kwa mbali, maongezi haya yalikuwa kati ya nafsi za Utatu Mtakatifu. Kuumbwa kwetu hakukuwa kazi ya malaika bali Mungu katika Utatu Mtakatifu. Mwandishi wa kwanza wa kikristo anayejulikana kutambua kuwa maongezi haya hayakuwa ya malaika alikuwa Justin Martyr (aliyeandika karibu miaka 138-165 BK) kwenye kitabu chake kiitwacho Dialogue with Trypho the Jew sura ya 62.

 

S: Kwenye Mwa 1:26-27, kwa kuwa Mungu almewafanya watu kuwa wakubwa kuliko malaika, je baadaye Mungu angeweza kuumba viumbe vingine vikubwa kuliko binadamu?

J: Maandiko hayasemi lolote kati ya hayo, na Mungu an uhuru wa kufanya chochote anachopenda. Hata hivyo, Maandiko yanasema kuwa waamini ni "watoto wa Mungu" na "tutatawala pamoja na Kristo" na "tutakaa pamoja na Kristo" (Efe 2:6). Ni vigumu kwa viumbe wenye kikomo kuwa wakubwa kuliko hilo.

 

S: Kwenye Mwa 1:26, je Adam alikuwa "mtu mwenye uwezo kupita kiasi" mwenye nguvu mara milioni nyingi zaidi kuliko zetu, kama Watchman Nee alivyofundisha kwenye kitabu kiitwacho The Latent Power of the Soul (1933 uk.15)?

J: Maandiko hajawahi hata mara moja kufundisha mawazo haya ya ajabu. Pia haijawahi kufundusha kuwa Adam alikisha kuwa kama Mungu katika kuonekana kwake kwa nje, kama Watchman Nee anavyofindisha kwenye kitabu hichohicho ukurasa wa 18. Kwa bahati mbaya, watu mara nyingi hujaribu kuongezea mafundisho yao wenyewe kwenye mambo ambayo Mungu amesema.

 

S: Mwa 1:26, endapo tuliumbwa kwa sura ya Mungu, jambo hilo halithibitishi kuwa Mungu (au walau Mungu Baba) ana mwili wa kibinadamu? (Wamormon wanasema jambo hili.)

J: Watu wengi wataafiki kuwa Roho Mtakatifu hana mwili na kwamba Yesu hakuwa na mwili kipindi kile. Kama uwingi wa "tumfanye" inaongelea maongezi ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, basi sura haimaanishi mwili. Kwa taarifa yako, Mwanzo 9:6 inaonyesha kuwa tangia wakati wa anguko tungali tuna sura ya Mungu.

 

S: Kwenye Mwa 1:27, je wanadamu wangali wanaumbwa kwa sura ya Mungu tokea wakati wa anguko?

J: Ndiyo. Mwanzo 9:6, baada ya anguko, inaonyesha kuwa ingawa tumeharibiwa na dhambi, bado tungali tuna sura ya Mungu.

 

S: Kwenye Mwa 1:28, kwa kuwa mwanadamu alitakiwa kuijaza dunia na kuitawala, je jembo hili lilitoa kibali kwa mwanadamu kuharibu mazingira?

J: Sivyo kabisa. Hatujawahi kusikia kuhusu Mkristo au Myahudi aliyesoma Biblia na kuitafsiri namna hiyo. Tafsiri hii nyingine, iliyotolewa mwaka 1967 [tazama marejeo ya Kaiser mwishoni], inaeleweka tu endapo unasoma sehemu ya Mwanzo 1, na unafafanua "kutawala" kama "kuharibu" badala ya "kutawala kwa busara." Bibilia inasema mambo sita muhimu yanayohusu kutunza ardhi na wanyama.

1. Walikuwa "wapangaji" kwenye nchi ambayo ni mali ya Mungu

1a. Kwa hiyo, ardhi haikuweza kuuzwa moja kwa moja (Walawi 25:23)

1b. Vitu vyote ni mali ya Mungu (Zaburi 24:1)

2. Mungu atawahukumu wale wote wanaoharibu ardhi kwa ujumla

2a. Isaya 24:5 inasema dunia iliharibiwa na watu wake.

2b. Zekaria aliomboleza kwa ajili ya kuharibiwa kwa misitu mikubwa na majani mengi. Zaidi ya hapo, kuomboleza kwa ajili ya maangamizo ya kiroho ambayo kwa ajili yake maafa haya ya asili ni istiari (Zechariah 11:1-3).

3. Mungu anaonya dhidi ya kuiharibu ardhi

3a. Mungu atawaangamiza wale wanaoingamiza dunia (Ufunuo 11:18).

3b. Mungu atawahukumu "kondoo" wale ambao licha ya kula kile wanachohitaji, wanakanyaga majani yote. Hawanywi maji masafi tu bali pia wanayachafua kwa miguu ya (Ezekiel 34:17-22).

3c. Hesabu 5:3 inasema kuhusu kutokuchafua kambi, katika muktadha wa magonjwa ya kuambukiza.

3d. Hata wakati wa vita, usikate mti wa matunda unaoifanya nchi kuzalisha (Kumbukumbu 20:19-20). Mzeituni unaweza kuishi zaidi ya miaka 1,000.

4. Mungu huhukumu kuharibu ardhi kwa kuleta mabaya

4a. Hesabu 35:33-34 inatuamuru: "msiitie unajisi nchi" kwa maana ya kutokuua watu.

4b. Msiitie unajisi nchi kwa sanamu (Yeremia 16:18).

4c. Yeremia 32:34 inaelezea watu wanaolinajisi bonde la Topheth kwa kafara za watoto wachanga.

4d. Kwenye Ezekiel 7:22, watenda maovu watapanajisi mahali pa Mungu penye thamani sana.

5. Sheria ya Mungu inahusisha kusimamia rasilimali kwa busara

5a. Adam aliwekwa "katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza" (Mwanzo 2:15).

5b. Si ruhusa kupanda mazao ya aina mbili pamoja (Kumbukumbu 22:9). Badala yake, kubadilisha mazao kunapunguza wadudu waharibifu wa mazao.

5c. Kupumzisha ardhi kila mwaka wa saba wakati wa Jubilii (Walawi 25:3-7,11-12,18).

5d. Mungu ataihukumu Israel kwa kuvunja amri hii (Walawi 26:34-35).

6. Wanyama: wanamilikiwa na Mungu, wametolewa kwa matumizi yetu, lakini tunapaswa kuwachunga kwa upole

6a. Wanyama ni mali ya Mungu (Zaburi 50:10) na anawatunza (Zaburi 36:6; 104:11,14; 147:8-9).

6b. Kula nyama ni sawasawa, na sehemu nyingine kumeamriwa (Mwanzo 9:2-5; Matendo 10:13).

6c. Yesu hakutenda dhambi (Waebrania 4:15; 7:26; 1 Petro 3:22; 1 Yohana 3:5). Alikula samaki (Luka 24:42-43) na kwa vile alikuwa Myahudi mzuri alikula nyama kama ilivyomariwa wakati wa Pasaka (Kutoka 12:8-10).

6d. Kuvaa ngozi ni sawasawa, kama Yohana Mbatizaji alivyokuwa na mkanda wa ngozi kwenye Marko 1:6.

6e. Kuwinda ni sawasawa (Walawi 17:13).

6f. Kuua wanyama kwa ajili ya kafara kuliamriwa (Kutoka - Kumbukumbu).

6g. Tunapaswa kuwa wapole kwa wanyama (Mithali 12:10).

 

S: Kwenye Mwa 1:28, ingawa Biblia haisemi moja kwa moja kuwa tusiharibu zawadi ya Mungu ya mazingira yetu, je ukristo unadokeza kuwa tunaweza kuyaharibu mazingira?

J: Hapana. Huwezi kuulaumu ukristo kwa ajili ya matatizo ya kiikolojia yaliyosababishwa na ulafi wa mali na idadi iliyozidi ya watu kama ambavyo huwezi kuwalaumu watu wa Afrika wanaoamini kuwa vitu vyote vina roho, Wahindu wa India, Wafuasi wa Budha au Konfyushasi huko China, wala Waislam huko Indonesia na Mashariki ya Kati. Kuna matatizo ya kikolojia kwenye kila bara kama ambavyo kuna watu wenye kuyaharibu mazingira kwa ajili ya manufaa yao binafsi kwenye kila bara. Kwa ajili ya maelezo ya nini Biblia inasema kuhusu mazingira, angalia jibu la swali lililopita.

 

S: Kwenye Mwa 1:29, Adam na Hawa walipewa kila mmea wenye kuzalisha mbegu, au wasingeweza kula mti wa ujuzi wa mema na mabaya kama Mwa 2:17 inavosema?

J: Ingawa hatujui endapo mti wa ujuzi wa mema na mabaya ulkuwa na mbegu au la, jambo hili si la maana hapa. Kwa vyovyote vile, maana yake ilikuwa kwamba wanaweza kula mmea wowote wenye kuzalisha mbegu, isipokuwa mti wa ujuzi wa mema na mabaya.

 

S: Kwenye Mwa 2:2-3, kwa nini Mungu alipumzika siku ya saba?

A: "Kupumzika" hapa kunamaanisha kusimama/kuacha kufanya kazi ya uuumbaji. Maandiko hayajawahi kusema kuwa Munug alihitaji kupumzika, lakini alichagua kufanya hivyo.

 

S: Kwenye Mwa 2:2, je nadharia ya Sabato ina asili ya Kibabeli na iliwekwa kwenye mapokea ya Kiyahudi baadaye?

J: Majibu mawili, moja kwa Wakristo na moja kwa wasio Wakristo.

1. (Kwa Wakristo): Kama unadhani kuwa Yesu alitoka kwa Mungu kama ilivyothibitishwa na kufufuka kwake, kwa kuwa Yesu alikubaliana na usahihi wa asili na kuaminika kulikohifadhiwa kwa Agano la Kale, na maelezo kuhusu Sabato kwenye Mwanzo na Yeremia yanaweza kuthibitishwa kuwa yaliandikwa kabla ya kuja kwa Yesu, hayakuanzia Babeli, na hakuna kitu zaidi kinachotakiwa kusemwa.

2. (Kwa wasio Wakristo): Wababeli waliita siku ya 15 ya mwezi sappatu. Hiyo ilikuwa ni siku moja tu katika mwezi, siyo siku nne. Sabato ilionekana kuwa na umuhimu mdogo kwa Waisraeli kabla ya kwenda utumwani na yenye umuhimu mkubwa baada ya utumwa. Hata hivyo, kudhani kuwa Wayahudi wa wakati wa utumwa wa Babeli na wale wa baada ya utumwa walidanganyika a) kuamini kuwa kwenda kwao utumwani kulikuwa ni kwa sababu ya kushindwa kutii amri ambayo haikuwemo kwenye Maandiko, na b) hii iliongezwa kwenye sehemu 59 (35 kati ya hizo zikiwa kwenye Torati) bila mtu yoyote kutambua mambo mapya, ni jambo lisilo rahisi kuaminika. Kwa taarifa yako, si Wayahudi wote walioenda Babeli. Yeremia anarekodi kuwa baadhi yao walikwenda Misri. Hawa ndio ambao watoto wao walikuja kutafsiri Agano la Kale kuwa Kigiriki, na kwenye tafsiri ya Kigiriki ya Septuagint ina aya zinazoongelea Sabato pia.

 

S: Kwenye Mwa 2:4; 5:1; 6:9; 10:1; 11:10, 27; 25:12, 19; 36:1, 9 na 37:2; Hes 3:1; Ru 4:18, je neno la kiebrania (Toledot) lipo mwanzoni mwa kifungu au mwishoni?

J: Ama huwa linaongelea mwanzo, huwa linaongelea mwisho, au wakati mwingine linakwenda upande wowote kati ya hizo mbili.

Halieleweki: Hapa kuna "toledots" kadhaa zinazowe kutafsiriwa kwa njia yoyote kati ya hizo mbili: Mwanzo 2:4; 5:1; 36:9; 37:2.

Mwanzoni: Hapa kuna "toledots" kadhaa ambazo muktadha unazilazimisha ziwe mwanzoni: Mwanzo 6:9; 10:1; 11:10, 27; 25:12, 19; 36:1; Hesabu 3:1. Philo Myahudi (aliyeishi mwaka 15/20 KK hadi 50 BK) anaielezea Mwanzo 2:4 kama "inayataja maelezo yake [Musa] ya kuumbwa kwa ulimwengu" kwenye kazi yake iitwayo On the Creation 44:129 uk.18.

Mwishoni: Kuna "toledot" nyingi moja moja ambazo zinaweza kuwa zinatakiwa kuwa mwishoni mwa kifungu. Kwa hiyo, vifungu visivyoeleweka ni "toledots" za mwanzoni.

Uthibitisho wa hakika zaidi kuwa "toledot" inapaswa kuwa mwanzoni mwa kifungu ni Mwanzo 25:19, ambayo inasema ni maelezo ya Isaka. Kifungu kinachofuata kinaongelea watoto wa Isaka. Kifungu kinachotangulia kinamwongelea Ishmael na hakihusiani na Isaka kwa namna yoyote ile.

Tazama The Bible Knowledge Commentary : Old Testament (Victor Books 1985) uk.22-23 kwa maelezo zaidi kuwa kwa nini "Toledot" ni ya mwanzoni.

 

S: Kwenye Mwa 2:5-7, je Mungu aliumba mimea baada ya mtu, au kabla ya mtu kama Mwa 1:12, 26 inavyosema? (Mtu asiyeamini kuwa Mung yupo aliyeitea Capella aliuliza swali hili.)

J: Kuna mambo manne ya kuyazingatia katika kujibu swali hili.

1. Mimea kwanza: Mwanzo 1 inasema wazi kabisa mimea iliumbwa duniani kabla ya mtu. Mambo haya yanahususha nasaba ya mimea yote ya kisasa.

2. Ulimwengu dhidi ya Bustani: Mwanzo 1 ni maelezo ya uumbaji wa mbingu na dunia, wakati ambapo Mwanzo 2 ni maelezo ya uumbaji wa bustani ya Edeni.

3. Mazao baada ya binadamu: Mwanzo 2 inaonyesha kuwa vichaka vya nyikani vilikuja baada ya kuumbwa kwa binadamu, kwenye bustani ya Edene. Mara zote, neno la kiebrania litimikalo kwa "kichaka", saday, limetumiwa, badala ya kusema mimea tu.

4. Elimukale inathinbitisha mambo ambayo Mwanzo inaonyesha. Punje tuzitumiazo leo hazikuwepo hadi wakati binadamu alipozizalisha kwa ajili ya kuzipanda.

4a. Mahindi : Wataalamu wa elimukale wantuambia kuwa mahindi yalianza kulimwa kwa ajili ya kuzalisha chakula Marekani karibu mwaka 5000 KK. Yalitokana na punje zinazoitwa teosinte. Teosinte ina punje karibu 50 ambazo zimeshikiliwa kwa kiulegevu, na bunzi lake lina urefu usiofika inchi moja. Tofauti na mahindi ambayo siku hizi yana punje kunazia 500 hadi 1,000 ambazo zimeshikiliwa vizuri kwenye kila bunzi. Kwa kuwa punje zimeshikiliwa vizuri, mahindi, leo hii, hayawezi kukua maporini bila msaada wa binadamu.

4b. Ngano: Elimukale imewapata nasaba wa ngano kwenye upande wa masharki na kati ya Iraki karibu mwaka Inaitwa Emmer na inapoteza mbegu zake upepo unapovuma. Leo hii kuna maelefu ya uzao wa ngano. Kwa nyongeza, watu wengine wanaona tofauti ya miaka 2,000 kati ya muda wa kupanda ngano na mahindi kama moja ya sababu mbili za (farasi wakiwa sababu nyingine) kwamba Wahispania walipokuja Marekani, utamaduni wa kihindi ulikuwa na miaka 1,000 hadi 2,000 nyuma ya ule wa Ulaya.

4c. Mpunga ulikuwa ndio nafaka mpya zaidi kati ya nafaka kubwa tatu. Ulianza kuzalishwa kwa ajili ya chakula karibu mwaka 3500 KK.

Kama nyongeza, punje za ngano, shayiri, dengu na zabibu zilizosafishwa kwa mvuke na moto toka mwaka 4000 KK zimekutwa huko Beersheba.

Muhtasari: Mimea ilikuwepo kabla ya watu, lakini mazao na mashamba vilikuja baada ya binadamu kuumbwa.

 

S: Kwenye Mwa 2:7, je Mungu aliumba mada au "alizipanga tu" kama wengi wa Wamormoni wanavyofundisha, au mada haikuwa imeumbwa kwa sababu mada si kitu halisi, kama wafuasi wa Christian Science na baadhi ya makundi ya kidini ya mashariki yanavyofundisha?

J: Hapana. Kwa kuwa Mungu ni mwenye uwezo wote inamaanisha kuwa anaweza kufanya kitu chochote kile, na kwa kuwa Mungu ni muumba inamaanisha kuwa aliumba kila kitu. Mungu aliuumba ulimwengu "ex nihilo", yaani, kutoka kwenye kitu kisichokuwepo. Kwa hiyo, kwa ubayana zaidi, Mungu hakuumba "vitu vya mada na nishati" tu bali pia Mungu aliumba mada na nishati zenyewe.

 

S: Kwenya Mwa 2:7, 19 je Mungu alimuumba mwanadamu kabla ya wanyama, au baada ya wanyama kama Mwa 1:24, 27 inavyosema? (Capella, mwanadamu asiyeamini kuwa Mungu yupo aliuliza swali hili).

J: Kuna mambo matatu ya kuyazingatia katika kujibu swali hili.

Hapa duniani, Mungu alimuumba mwanadamu baada ya wanyama, kama Mwanzo 1:24, 27 inavyosema.

Kwenye bustani ya Edeni, Mungu atakuwa alimuumba mwanadamu kabla ya kumwonyesha wanyama.

Hata kwenye Bustani, wanyama wanaweza kuwa walikuwepo kabla ya mwanadamu. Mwanzo 2:19 inaongelea wanyama ambao walikuwa wameumbwa kufikia wakati ule. Haimaanishi kuwa wanyama hawakuumbwa hadi wakati ule.

 

S: Je Mwa Gen 2:7 inathibitisha kuwa watu hawana nafsi zinazodumu milele kama Mashahidi wa Yehova wanavyosema?

J: Hapana. Neno la kiebrania hapa, nephesh, linamaanisha "nafsi" kwenye baadhi ya na "maisha" kwenye sehemu nyingine kama hii hapa. Waumini watawezaje kuwa chini ya mimbari kwenye Ufunuo 6:9-10 endapo hawakuwahi kuishi baada ya kufa?

 

S: Kwenye Mwa 2:10-14, iko wapi mito iliyotoka kwenye Bustani ya Edeni?

J: Kwanza kabisa, Bustani ya Edeni haipo duniani leo. Hatujui Mto Pishon ulikuwa wapi, na mito Tigris naFrati iko Uturuki, Syria na Irak. Mto Gihon unadhaniwa kuwa ni Mto Nile, ulitokea ukanda wa Kushi, kusini kwa Misri. Hata hivyo, ungeweza kuwa mto mdogo unaotokea "Kushi" (Kashshu) magharibi mwa Elam, ambayo ipo karibu sana na Tigris na Frati. Wakasi (Greek: Kossaeans) walitokea huko.

 

S: Kwenye Mwa 2:15, kwa nini Mungu alisema unaweza kula (umoja) toka katika mti wowote wa kwenye bustani isipokuwa hampaswi kula (uwingi) toka katika mti wa ujuzi wa mema na mabaya?

J: Yeyeto kati yao angeweza mti wowote ule; hawakulazimika kula chakula kimoja. Hata hivyo, hakuna aliyeruhusiwa kula toka kwenye mti mmoja. Uwingi wa kitenzi unaongeza mkazo; amri hii haikuwa kwa Adam pekee, bali kwa kila mmoja.

Philo Myahudi (aliyeishi mwaka 15/20 KK hadi 50 BK) alijibu swali hili kwanza kwenye Questions and Answers on Genesis, I uk.794.

 

S: Kwenye Mwa 2:16, kwa nini Mungu alimuumba Adam hali alijua kuwa ataanguka dhambini?

J: Mungu anaweza kufanya kitu chochote kile, lakini mantiki ya kutokuwezekana si kitu. Mungu hawezi kumuumba kiumbe ambaye anachagua kumtii kama kiumbe huyo hawezi kuchangua kumtii Mungu. Kuweza kuchagua kumtii Mungu kunamaanisha kuwa na uwezo wa kuchagua kutokumtii Mungu.

 

S: Kwa kuwa Mwa 2:17 inasema "siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika?"

J: Kiroho na kisheria. Mambo matatu ya kuzingatia katika kujibu swali hili.

Kifo cha kiroho kilitokea siku ile.

Kisheria, siku ile hukumu za mauti ya milele na ya mwili zilitangazwadhidi yao. Nahau ya kiebrania inamaanisha uhakika wa kifo, sio uharaka wa kifo.

Kwa mfano wa matumizi ya nahau hii ya lugha tazama 2 Wafalme 2:37, ambapo Suleiman alitoa onya kama hili kwa Shimei siku aliyokuwa anaondoka Yerusalem.

Mtu wa kwanza tunayemjua ambaye alitoa jibu kwa swali hili alikuwa Philo Myahudi (aliyeishi mwaka 15/20 KK hadi 50 BK) kwenye Questions and Answers on Genesis, 1 uk.794, na Allegorical Interpretation, I 33 (105) uk.46-37, ambapo anaelezea kufa kwa nafsi.

Mwandishi wa kale wa pili ambaye alitoa jibu tofauti ni Irenaeus kwenye Against Heresies Kitabu cha 5 sura ya 23 (mwaka 182-188 BK) uk.551-552. Kwa kuwa Irenaeus anaonyesha kuwa kwa Mungu siku moja ni miaka 1,000, anaitafsiri hii kuwa ni moja ya siku za Mungu, na anaona kuwa ni muhimu Mwa 5:6 inasema kuwa Adam alikufa akiwa na miaka 930, ambayo ni pungufu ya miaka 1,000.

 

S: Kwenye Mwa 2:18, kwa nini Biblia inasema kuwa mtu alikuwa peke yake, kwa kuwa mtu alikuwa na Mungu pamoja na wanyama?

J: Adam alikuwa na mamlaka juu ya wanyama, na Adam alimwabudu Mungu, lakini Adam hakuwa na mtu yoyote mwingine aliyefanana naye. Alikuwa peke yake katika kutokuwa na mtu yoyote wa kuhusiana naye katika namna ya mlalo kama mtu anayelingana naye.

 

S: Je Mwa 2:18-22 inaonyesha kuwa wanawake waliumbwa kama wazo la pili, kama Born Again Skeptic's uk.164 inavyodai?

J: Hapana, inaonyesha tofauti kabisa na hivyo. Mungu alichukua muda mrefu wa kutosha, kwa Adama kutoa majina kwa wanyama and vitu vingine vyote, kumuonyesha Adam haja yake ya mwenzi. Vitu vingi zaidi kwenye Mwanzo 1 na 2 viliumbwa na maelezo machache. Hata hivyo, Mungu kwanza "aliandaa jukwaa" na kuelezea madhumuni ya mwanamke kama mtenda kazi mwenzi wa Adam kabla ya kumuumba Hawa.

 

S: Je Mwa 2:18 inaonyesha kuwa wanawake ni duni kwa wanaume, kwa sababu Hawa aliumbwa kwa tofauti na Adam?

J: Hapana haimaanishi hivyo. Mambo sita ya kuyazingatia katika kujibu swali hili.

1. Tofauti haimaanishi kutokuwa sawa. Watu tofauti wanazungumza lugha tofauti lakini hiyo haimaanishi kila lugha ni duni au bora kuliko nyingine. Kama Mkristo mmoja alivyosema, Hawa hakuumbwa kutoka mguu wa Adam ili awe chini yake, lakini aliumbwa kutoka katika upande wake ili awe naye.

2. Msaidizi haimaanishi kuwa mtu duni. Baadhi ya watu wanaweza kudhani kuwa Hawa alikuwa duni kwa Adam kwa sababu alikuwa "msaidizi" kwenye Mwanzo 2:18. Hata hivyo, Mungu ni msaidizi wetu kwenye Zaburi 70:5 na jambo hili halimaanishi kuwa Mungu ni duni kwetu! Kwa hiyo kutafsiri neno la kiebrania kama "msaidizi" si sahihi kabisa. Tafsiri nzuri ni ‘Nitafanya nguvu [au uwezo] unaoendana na mtu', kwa mujibu wa uchunguzi wa kina wa Walter Kaiser kwenye Hard Sayings of the Bible uk.92-94. Kwa hiyo mwanamke anapaswa kuwa "mwenzi mkamilifu" na si msaidizi tu.

3. Mwanzo 1:27 ianonyesha kuwa wote wana sura ya Mungu. Si Adam peke yake aliye na sura ya Mungu, bali wote mwanaume na mwanamke wana sura ya Mungu. Kuwa na "sura ya Mungu" hakuishii kuwa na miguu miwili, mikono miwili, tumbo, n.k. Badala yake, kama taswira ya pande mbili isivyokuwa muhtasari mkamilifu wa kitu halisi, tabia ya Mungu asiye na ukomo na hali yetu ya kuwa na ukomo vina mambo kadhaa yanayofanana.

4. Usawa wa asili, uthamani, umuhimu, n.k. Kwenye Biblia, Wagalatia 3:28 inasema, "Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu."

5. Lakini majukumu tofauti: Waefeso 5:22-24 inaonyesha kuwa wake wanapaswa kuwatii waume zao, kwa sababu mume ni kichwa cha mke wake. Waume wanapaswa kuwapenda wake zao kama Kristo alivyolipenda kanisa kwenye Waefeso 5:25-26. Paulo alisema kuwa wanawake wasiwafundishe wala kuwa na mamlaka juu ya wanaume kwenye 1 Timotheo 2:12.

6. Jambo hili linafanyikaje kwenye maisha ya siku kwa siku?

6.1 Deborah alikuwa mwamuzi wa Israel aliyemcha Mungu kwenye Waamuzi 4-5. Kwa kutokana na hili, sitasita kumpigia kura mwanamke kuwa raisi.

6.2 Waliweza kuruthi vitu, ikiwa ni pamoja na ardhi kwenye Hesabu 36:8.

6.3 Kwa maelezo ya kina zaidi ya namna ambavyo mke anatakiwa kuwa mwenzi mkamilifu wa mumewe, soma Mithali 31:10-31. Pamoja ni mambo mengine inasema:

Anafanya kazi kwa mikono yake mwenyewe (mstari wa 13, 22) na anapata faida kutokana na hili (m.24, 31).

Ananunua chakula (m.14) na kukipika (m.15)

Anawasimamia watu wengine (m.15)

Anaamua yeye mwenyewe kununua ardhi (m.16)

Anapanda shamba la mizabibu (m.16). Kumbuka kuwa familia haikumilika shamba lote la mizabibu kwa ajili ya kula wao wenyewe; ilikuwa ni chanzo cha mapato.

Ana nguvu za kimwili (m.17)

Pia anafanya biashara, si tu kwa ajili ya kupata mahitaji ya lazima lakini pia faida (m.18)

Anawasaidia maskini. (Alipaswa kusimamia hela ili aweze ufanya hivyo - m.20)

Anaisimamia nyumba (m.21)

Ana hekima, na anafundisha hekima (m.26)

Kwa ufupi: Wanawake si duni kwa wanaume kwa asili, uthamani au umuhimu. Wana majukumu tofauti na wanaume, kama ambavyo mwanamke yoyoye mjamzito anavyoweza kukuambia.

Tazama pia Today's Handbook for Solving Bible Difficulties uk.191-193 kwa maelezo zaidi ya jinsi ambavyo mwanamke alivyoumbwa "kama" mwanaume, na jinsi alivyo sawa naye.

 

S: Kwenye Mwa 2:19, ni kwa nini Adam alihitaji kuwaangalia wanyama wote hapa?

J: Mungu alimpa Adam mamlaka juu ya wanyama wote kwenye Mwanzo 1:26, na Mungu alitaka kuona jinsi ambavyo Adam atawapa majina kwenye Mwanzo 2:19.

Pamoja na hili, panaweza kuwa na sababu nyingine ambazo ni ngumu zaidi kuelezea. Kabla ya kumuumba Hawa, Mungu alijua umuhimu wa kujaza kitu kilichopunguka kwa Adam, lakini Adam hakujua. Kwa hiyo Adam aliweza kujifunza vitu vitatu kuhusu wanyama vinahusiana na hali yake ya wakati ule.

Familia:

a) Kumwonyesha Adam kuwa wanayama wote wakubwa wapo jike na dume kulionyehsa jinsi Mungu alivyowafanya wakamilifu na wenye uwezo wa kuendeleza kizazi chao.

b) Adam aliweza kuwaona viumbe wote, na kona kuwa hakuna hata mmoja aliyekuwa kama yeye.

c) Adam aliweza kuona kuwa alimhitaji mtu mwingine kumkamilisha.

Kwa kawaida, kuwafundisha watoto jinsi mimea inavyojizalisha, na jinsi wanyama wanavyojizalisha, ni njia nzuri ya kuwafundisha watoto jinsi ambavyo Mungu aliamuru watoto waumbwe.

Jumuiya:

a) Hata mbwa na paa wana jamii ambamo wanaishi.

b) Adam hakuweza kuona kuwa hakuwa na mtu yoyote kama yeye kwenye jumuiya ya wa kuweza kuishi naye, na watu wanahitaji watu wengine kuwa pamoja nao.

Uongozi:

    Kwa kuwa Mungu alimpa Adam mamlaka juu ya dunia, Adam alihitaji kujua wanyama waliokuwepo duniani. Kwa kuwa Adam alikuwa na mamlaka, Mungu alimpa heshima kwa kumruhusu awape majina wanyama wote hai. (Philo Myahudi alielezea hili kwenye Works of Philo uk.882.)

 

S: Kwenye Mwa 2:19-3:19, kuna ushahidi gani toka kwenye maandiko ya Wamormon wa mwanzo kuwa Wamormon waliamini mafundisho yasiyo ya kijinga kuwa Adam alikuwa Mungu?

J: Zifuatazo ni nukuu toka kwenye jarida la Wamormon liitwalo Journal of Discourses, zikifuatiwa na maandiko mengine kumi na mbili kama ushahidi.

a. Journal of Discourses juzuu ya 1, uk.50. (Mahubiri ya Brigham Young) "Sasa sikiliza, enyi wakazi wa duniania, Myahudi na mtu wa mataifa, Mtakatifu na mwenye dhambi! Baba yetu Adam alipokuja kwenye bustani ya Edeni, alikuja na mwili wa kimbinguni, na alimleta Hawa, mmoja wa wake zake, pamoja naye. Alisaidia kuuumba na kuupanga ulimwengu huu. Huyu ni Michael, Malaika mkuu, MZEE WA KALE! ambaye watakatifu wamesema na kuandika kuhusiana naye - YEYE ni BABA yetu na MUNGU wetu, na Mungu pekee TULIYENAYE. Kila mtu aliyepo duniani, Wakristo wanaokiri imani yao au wale wasiokiri wanapaswa kusikia jambo hili, na watalijua sasa au baadaye." (herufi ndogo na zile za mlazo zimo kwenye maandishi ya asili)

b. Journal of Discourses juzuu ya 1, uk.51. (Mahubiri hayo hayo) "Yesu, kaka yetu mkubwa, alizaliwa kimwili akiwa na tabia ileile iliyokuwepo kwenye Bustani ya Edeni, na ambaye ni Baba yetu aliye Mbinguni."

Kumbuka kwamba Wamormon hujibu kuwa hili ni kosa la uchapaji. Inafurahisha kuona kuwa juzuu za mhubira mashuhri wa kikristo Charles H. Spurgeon yalichapishwa karibu muda huohuo, na hayakuwa na makosa ya uchapaji kwenye kazi zake yaliyosema kuwa kiumbe mmoja aliyeumbwa alikuwa Mungu. Ufuatao ni ushahidi mkamilif kuwa nabii wa Kimormon kweli alisema hivi.

1. Journal la Wilford Woodruff chini ya 2/19/1854. (Tazama kwenye maktaba ya BYU)

2. Deseret Evening News 6/14/1873

3. Deseret Evening News 6/18/1873

4. Diary of Hosea Stout: On the Frontier juzuu ya 2, uk.438.

5. The Millennial Star juzuu ya 16, uk.543.

6. The Millennial Star juzuu ya 15, uk.769-770. Mwaka mmoja na nusu baadaye.

7. Journal of John Nuttall juzuu ya 1, uk.18-21.

8. Diary Journal of Abraham H. Cannon juzuu ya 11, uk.39 (iliyofundishwa kwa miaka 50)

9. Sacred Hymns and Spiritual Songs for the Church of Jesus Christ of Latter-Day Saints 1856 uk.375

10. Women of Mormondom uk.179

11. Journal of Discourses juzuu ya 4, uk.1 (Rais Heber C. Kimball anaongea tarehe 6/29/1856)

"...na pia najua kuwa kama hatutakuwa pamoja na kaka yetu Brigham, kiongozi wetu, hatutakuwa pamoja na Kristo. Naam, najua hili, na hisia zangu zipo na zimekuwa na kaka Brigham muda wote. Nimejifunza kwa vitendo kuwa kuna Mungu mmoja anayehusika na watu hawa, naye ni Mungu anayehusika na dunia hii - mwanadamu wa kwanza. Mtu wa kwanza aliyemtuma Mwana wake mwenyewe kuukomboa ulimwengu, kuwakomboa ndugu zake."

12. Mwisho, kitabu cha baadaye sana:

The Position of Adam in L.D.S. Scripture and Theology: "Kumfanya Adam kuwa ndiey Mungu Baba alikofanya Rais Brigham Young ni jambo ambalo haliwezi kukanushwa", uk.58.

 

S: Kwenye Mwa 2:20, Adam aliwezaje kutoa majina kwa wanyama wote, isipokuwa tu tunda lililozuilwa lilikuwa ni komyuta ya Apple Macintosh?

J: Mtu mmoja alitoa maoni ya kuchekesha kuwa kama Adam alitakiwa kutoa majina kwa aina zote za wanyama (ikiwa pamoja na wadudu milioni 1.5) kwa muda wa masaa 24 kwenye siku ya sita ya, si ajabu tunachanganya tunda lililozuiliwa na kompyuta ya Apple na vitu vingine vya aina hiyo!

Kwa upande mwingine, Paul S. Taylor amesema kwa usahihi kuwa msemo "aliwapa majina wanyama wote wafugwao, ndege wa angani na wanyama wa mwituni" kwenye Mwa 2:20 unaweza usimaanishe kutoa majina kwa viumbe wote duniani. Inaweza kumaanisha kutoa majina kwa aina za wanyama waliokuwa mahali ambapo Adam alikuwepo.

Kwa wale wanaopenda maelezo mengi yasiyo na umuhimu mkubwa, kuna karibu aina za viumbe hai 26,000 wenye uti wa mgongo duniani na ndege na mabaki ya aina 9,500 yanayofahamika duniani. (kati ya aina hizi za mabaki, karibu nusu yake ni aina za mijusi, na 1,000 walikuwa ndege).

Kuna karibu aina 5,600 za viumbe zilizopo dunia sasa, ikiwa ni pamoja na aina 1,900 za ndege. Kuna karibu aina 6,500 za mabaki yanayofahamika ya wanyama wa ardhini, ikiwa ni pamoja na aina 1,000 za nege na 1,500 za mijusi.

 

S: Kwenye Mwa 2:21-23, je Adam alikuwa mwanaume na mwanamke kabla ya kuumbwa kwa Hawa?

J: Hakuna kitu chochote kwenye Maandiko kinachosema hivi. Mwanzo 3:16 inasema kuwa mume atakuwa kichwa cha mke. Kwa kuwa jambo hili lilitokea baada ya anguko, jinsi gani "mwanaume" Adam alikuwa kabla ya Hawa haina umuhim wowote. Hata hivyo, kuhusiana na mamlaka ya kanisa kwa ujumla, Paulo anaona kuwa ni muhimu Adam aliumbwa kabla ya Hawa kwenye 1 Timotheo 2:13. Wazo la Paulo litakuwa linapotosha kabisa endapo Adam alikuwa mwanaume na mwanamke.

 

S: Kwenye Mwa 2:21-23, je maelezo kuwa Hawa aliumbwa toka kwenye ubavu yametoka kwenye shairi la Kisumeria la Dilmun?

J: Kwanza maelezo ya muktadha wa tukio, kisha jibu, na mwisho masomo mawili tunayoweza kujifunza toka kwenye jibu juu ya namna ambayo Mungu aliivuvia Biblia.

B1. Samuel Noah Kramer, kwenye The Sumerians (University of Chicago 1963), anaeleza kuwa neno la Kisumeria litumikalo kwa mbavu ni ti ambalo pia linamaanisha "kufanya kitu kiishi", na kwenye shairi la Dilmun, Nin-ti alikuwa "mwanamke wa ubavu" pia "mwanamke aliyefanya watu/vitu viishi" ambaye aliuponya ubavu wa mungu Enki uliokuwa unaumwa.

B2. Huu ni utani kwenye kisumeria, lakini siyo kiebrania, kitu ambacho kinafanya kufanana huku kuwa kwa ajabu sana.

B3. Ukiondoa "mwanamke aliyeponya ubavu" dhidi ya "Hawa aliyetoka kwenye ubavu wa Adam" kwenye Mwanzo, hakuna mambo mengi yote yanayofanana kati ya hadithi hizi mbili.

B4. Viba vyenye maandishi kutoka kwenye shairi la Dilmun viliandikwa mwaka 2400 KK au baadaye. Kwa vyovyte vile, bado vimemtangulia Abraham aliyeondoka Ur kabla ya mwaka 2050 KK.

B5. Hadithi hii inaweza kuwa ilifahamika sana nyakati za zamani.

Jibu: Mambo manne ya kuzingatia katika jibu la swali hili.

A1. Huu ni moja ya mifano kadhaa ya masimulizi ya matukio yaliyoelezwa kwenye Mwanzo. Mfano mwingne ni hadithi zaidi ya 200 za watu mbalimbali duniani za mafuriko yaliyosambaa dunia nzima.

A2. Kucheza na maneno kuhusu ubavu kunaweza kuonyesha kuwa jamii nyingine za kale zilikuwa na hazina ya habari hata zisizokamilika za kuumbwa kwa binadamu.

A3. Hata zaidi ya hapo, sehemu nyingine za Mwanzo 1 zinaonekana kuwa zimeandikwa kwa lengo maalum la kupingana na hadithi za kisumeria, kiakadia na mengineyo. Hadith nyingine zinawaonyesha miungu wakiwa wanagombana, kwenye Mwanzo Mungu mmoja tu anaumba kwa utulivu. Hadithi nyingine zinamwoonyesha shujaa akipigana dhidi ya fujo. Mwanzo inamwonyesha Mungu akitembea juu ya "vilindi/maji", na akitoa amri na kuelekeza.

A4. Ingawa kufanana kwa maelezo ya Mwanzo na shairi la Dilmun na kazi nyingine za kale kunawezakuwa kunaonyesha kuwa baadhi ya matukio yalijulikana na watu wote. Hata hivyo, ni vigumu kuthibitisha kuwa kazi moja ilinakiriwa na nyingne, si tu kwa sababu maelezo ya kina yanayofanana ni kidogo bali kwa sababu hakuna kufanana kwa maana ya maelezo ya kina.

Masomo ya kujifunza kutokana na jibu:

L1. Kitabu cha Mwanzo hakikuandikwa bila muktadha. Mungu hatufunulii ukweli tu, anatufunulia ukweli usio na kikomo cha muda, lakini kwa njia ya kivitendo, inayoendana na muda na jamii husika. Sababu mojawapo (lakini si sababu kubwa) Kitabu cha Mwanzo kinawezakuwa kilitolewa na Mungu ilikuwa ni kurekebisha maoni yasiyokuwa sahihi ya asili binadamu waliyokuwa nayo watu, huku kikitambua baadhi ya vitu sahihi vilivokuwepo.

L2. Mungu hutumia jamii za watu. Mungu hutumia hata matendo ya watu wabaya kwa ajili ya utukufu wake (Mwanzo 50:20). Tunawezaje hata kuthubutu kumzuia Mungu kutumia jamii za watu pia, kwa kadri anavyopenda. Musa alikuwa mtu aliyeelimika, na huenda akawa aliisoma hadithi hii, na Mungu alitumia kusoma huku kwa Musa kumwonyesha mambo yaliyokuwa ya kweli na yale ambayo hayakuwa ya kweli.

L3. Jambo la maana zaidi, usiuchuke msemo "Maandiko hayana makosa" kumaanisha kuwa Biblia ilitolewa kwa imla. Kwenye 1 Petro 1:21 Biblia inasema kuwa neno la unabii lilikuwa ni watu waliokuwa wanaongea kama walivyowezeshwa na Roho Mtakatifut. Kwa hiyo, sehemu tofauti za Biblia zinapoonyesha mitindo tofauti ya uandishi wa watu, jambo hilo haliukani utunzi wa Mungu wa Maandiko. Jambo hilo linaonyesha kuwa Mungu alitumia mitindo tofauti ya uandishi ya watu mbalimbali kwa kadri alivyoona inafaa.

 

S: Kwenye Mwa 2:22, je Lilith ni nani katika kipindi hiki?

J: Jina Lilith halijawahi kuelezwa hata maramoja kwenye Bibla. Kulikuwa na hadithi kwenye Enzi ya Kati kuhusu mwanamke aliyeitwa Lilith ambaye alikuwa mke wa kwanza wa Adam. Huyu alikataa kumtii Adam, kisha Mungu akamuumba Hawa. Lilith aligeuzwa kuwa pepo linaloua watoto wadogo.

Lilith pia alikuwa ni mnyonya damu kwenye hadithi za kubuniwa za kisumeria, kwa mujibu wa The Sumerians uk.198, 258. Civilizations of the Ancient and Near East uk.1890 kinasema kuwa mtu ambaye hajaoa/olewa aliyekufa alifanyika kuwa aina maalum ya mapepo yaliyoitwa lilu (mwanaume) na Lilitu (mwanamke). Hawa waliwaomba watu wanaoishi kuoana nao, wakiwaahidi utajiri, lakini kama watu wanaoishi walikubali walikufa mapema.

Kazi zote zenye Maandiko ya Biblia, za kiyahudi au kikristo, hazina kidokezi chochote cha Lilith wala Donald Duck.

 

S: Kwenye Mwa 2:22, Mungu angewezaje kumuumba Hawa kutoka kwenye ubavu?

J: Kwa njia yoyote ambayo Mwenyezi angeipenda. Kama Mungu alipaswa kutumia ubavu, na kama unafikiri kuwa Mungu alilazimika kuuchukua ubavu wote, basi nadhani utasema kuwa Hawa angekuwa anahesabu mbavu zote za Adam kila asubuhi!

Mungu anaweza kuwa hakuutumia ubavu wote; chembe moja ingeweza kutosha.

Kama Mungu angemuumba Hawa kwa kutumia udongo, mtu mwingine anaweza kusema kuwa wanawake wana utofauti wa asili (na pengine uduni kwa wanaume) . Hata hivyo, kwa kuwa Hawa aliumbwa toka kwenye ubavu, alikuwa sawa na mwanaume.

 

S: Kwenye Mwa 2:22-23, je wanaume wanapaswa kuwa na upungufu wa ubavu mmoja?

J: Hapana. Kama mtu atakatwa mkono, watoto na wajukuu wake watakaozaliwa baadaye hawatazaliwa bila mkono mmoja. Kwa jinsi hiyohiyo, kama utachukua chembe kadhaa toka kwenye ubavu wa mtu, bado wazazi na watoto watakuwa na namba ileile ya mbavu.

Tertullian akiandika mwaka 200-240 BK alitafsiri jambo hili kama Mungu "kukopa ubavu" kwenye Tertullian On Exhortation to Chastity sura ya 5 uk.53. Pia anaongeza kuwa Mungu angeweza kukopa mbavu zaidi kwa wake zaidi lakini alichagua kutokufanya hivyo, kama mfano kuwa ndo ya mke mmoja ndio kawaida na si wake wengi.

 

S: Kwenye Mwa 2:25, je mwanaume na mwanamke waliumbwa wakiwa uchi mwanzoni, na je walitakiwa kuvaa nguo?

J: Ndio. Waliumbwa wakiwa uchi na hawakuona aibu. Lakini, baada ya anguko, Mungu aliwavisha nguo, na wamekuwa wakivaa nguo tokea wakati huo hadi sasa.

 

S: Kwenye Mwanzo 3, kuna swali ambalo sijaweza kupata jibu lake. Biblia inasema kuwa Mungu alimwumba mwanaume. Mungu anamwambia mwanaume kutokula tunda lililokatazwa linalotoka kwenye mti wa ujuzi kwa sababu tunda lake litakufungua macho na kukufanya ujue mambo sahihi na yasiyo sahihi na mema au mabaya. Mwanadamu akala tunda lililokatazwa na akabadilika. Mwanadamu sasa anaona kuwa kuwa uchi ni kitu kibaya. Je kutomtii Mungu kuliwezaje kuwa dhambi ikiwa mwanadamu hakujua kitu sahihi au kisicho sahihi wakati alipokuwa anakula tunda lililokatazwa?

J: Ninapenda kujibu swali lako. Niruhusu nianze jibu la swali lako kwa kuuliza swali: tokea wakati uliofuata anguko, mtu anawezaje kujua jambo lililo sahihi na lisilo sahihi? Tunafahamu moja kwa moja kupitia yale yote ambayo Mungu ametufunulia kuhusu mambo sahihi na yasiyo sahihi, na kila mtu anao ufahamu wa kiasi fulani unaotokana na dhamira iliyomo ndani mwake. (Ni kweli mtu anaweza kuifanya dhamira yake kuwa butu.)

   Baada ya anguko, Adam na Hawa walikuwa na dhamira, hisia ya hatia kuwa wamefanya kosa kwa kutokutii, na wao pamoja na wazao wao walikuwa na asili ya dhambi. Matokeo ya anguko yalikuwa makubwa sana.

   Kabla ya anguko, hawakuwa nayo, na hawakufahamu jambo sahihi na lisilo sahihi. Asili yao ilikuwa nzuri, na jambo lolote walilofanya lilikuwa sahihi - karibu kila wakati. Hawakuwa na amri walizohofia kushindwa kuzitii isipokuwa moja: msile matunda toka kwenye mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Uchaguzi wao, wa kula ama kutokula, haukusimamia kwenye sahihi au siyo sahihi, kwa sababu hawakujua mambo haya (sahihi na si sahihi). Badala yake, uchaguzi wao ulikuwa rahisi sana ama kumtii Mungu ama kutokumtii.

   Mara nyingine siku hizi, watu wanaweza kuwa na mawazo ya ajabu kuhusu mambo sahihi na yasiyo sahihi, kama mababa wa Kiislamu wenye kufikiria kuwa ni sahihi kuwaua mabinti zao kwani wanaamini kuwa mabinti zao wameleta aibu katika familia yao, ikiwa ni pamoja na kufanya vitu kama kuolewa na watu ambao baba zao hawakuwakubali. Hata Wakristo wanaweza kuzidiwa na  fikra kuwa "je Biblia inaruhusu jambo hili." Jambo la maana zaidi kuliko kuuliza "je jambo hili ni sahihi au siyo sahihi" ni "je Mungu anapenda nifanye jambo hili" au "je jambo hili linampendeza Mungu." Jibu la swali hili linaweza kuwa sawa na "je jambo hili ni sahihi au siyo sahihi", lakini jambo la msingi lisiwe kufanya vitu kwa ajili ya kutuliza dhamira zetu, au kufuata amri kadhaa, lakini kumpendeza Mungu.

   Kwa hiyo, jibu fupi kwa swali lako ni kwamba Adam na Hawa hawakufanya dhambi kwa kuchagua jambo ovu badala ya jema, kwani hawakujua uovu au wema. Walifanya dhambi kwa kujua amri rahisi kabisa ya Mungu, na kuchagua kutokumtii Mungu.

 

S: Kwenye Mwanzo 3, kwa kuwa Mungu aliwaumba wanadamu ili wawe wakubwa kuliko malaika, je jambo hilo laweza kuwa ni sababu ya Shetani kuamua kuwaangusha?

J: Maandiko hayasemi lolote kuhusiana na jambo hilo, lakini kuna uwezekano wa kuwa hivyo.

 

S: Kwenye Mwanzo 3, je Adam na Hawa walikuwa na ngozi nyeupe, nyeusi, ya kahawia, ya manjano au nyekundu?

J: Biblia haisema kitu chochot kuhusiana na jambo hili. Kwa kuwa Adam na Hawa walikuwa wazazi wetu sisi sote haijalishi walikuwa na rangi gani. Watu wote ni uzao wa Adam na Hawa.

 

S: Kwenye Mwanzo 3, kwa nini Mungu aliruhusu Adam na Hawa kujaribiwa?

J: Biblia haisemi kitu chochote kuhusiana na jambo hili. Hata hivyo, tunaweza kuhisia kuwa Mungu hakupenda watu waliokuwa wanampenda tu bali pia ambao wamepewa ruhusa ya kufanya kitu tofauti lakini bado wamechagua kumpenda.

 

S: Kwenye Mwanzo 3, je jaribu hili halikuwa la haki, kwa kuwa Adam na Hawa walikuwa bado hawana ujuzi wa mema na mabaya, kama ambavyo Capella, mtu asiyeamini kuwa Mungu yupo anavyodai?

J: Hapana. Je ni haki kama kumjaribu mtu kwa kumwambia asitumie madawa haramu kama Cocaine kabla hajapata nafasi ya kuyatumia? Ndiyo ni haki! Kwa jinsi hiyohiyo, ilikuwa haki kwao kuzuiliwa kabla hawajatenda dhambi na kupata hatia. Ingawa mtu mwingine anaweza kusema kuwa hawakuwa wanajua kila kitu kuhusu mema na mabaya wakati huu, walijua kuwa Muumba wao amewaamuru kutokula mti ule, na kwamba ujuzi tu ulitosha kulifanya jaribu hili kuwa la haki.

Leo hii hatufahamu sababu zote za Mungu kutuzuia kufanya vitu mbalimbali, lakini Mungu ametuamuru tusifanye, tunajua mambo yote tunayotakiwa kujua ili tuweze kumtii Mungu.

 

S: Kwenye Mwanzo 3, kulikuwa na ubaya gani hasa kula tunda?

J: Suala si kwamba tunda fulani lilikuwa ovu; huenda wangeweza kula tunda hilo baadaye. Kama Theophilus, askofu wa Antioch (168-181/188 BK) alivyoandika kwenye baraua yake iitwayo To Autolycus kitabu cha 2 sura ya 25, uk.104 "Kwa sababu haukuwa mti, kama baadhi ya watu wanavyodhani, bali kutokutii kulikokuwa na mauti ndani yake." Ante-Nicene Fathers juzuu ya 2, uk.104. Watu wengine pia wanaona kwenye msemo "mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya", nia ya Adam na Hawa kujipatia haki au mamlaka ya Mungu ya kuweka mpaka wa mema na mabaya.

 

S: Kwenye Mwanzo 3, je jaribu hili lilikuwa kama wazazi kuweka betri lenye volti 40,000 sebuleni na kumwambia mtoto wao mdogo kutokuligusa?

J: Hapana. Hatari ilikuwa kwenye kukosa kwao kutii, siyo kwenye mti. Mambo manne yanayopaswa kuzingatiwa katika jibu la swali hili.

1. Tofauti na betri la hatari, si mti uliokuwa wenye hatari inayoweza kusababisha mauti. Ilikuwa ni kutokumtii kwao Mungu kulikokuwa na hatari yenye kusababisha mauti, na iliyowafanya wafe kiroho siku ile, na kimwili baadaye. Iliwezekana kuwa Mungu angeweza hapo baadaye hata kuwaruhusu kula matunda ya mti ule.

2. Adam na Hawa hawakuwa watoto wadogo. Waliweza kufikiri kama watu wazima wafanyavyo, walifahamu kabisa jambo walilokuwa wanalifanya na matokeo yake ambayo Mungu aliwaambia kuwa yatakuwa.

3. Adam na Hawa walitimiziwa mahitaji yao yote na hawakuwa na namna yoyote ya kutokumtii Mungu isipokuwa kwa kula tunda la mti huo. Ikiwa tunapenda au la, Mungu huwapa watu nafasi za kumtumikia au kutokumtumikia. Baadhi ya watu watafikiri kuwa "Mungu hapaswi kufanya hivyo, Mungu angetufanya kuwa maroboti yasiyo na uwezo wa kutokutii." Vyovote vile watu wanavyofikiri, Mungu anaweza kutanda kama apendavyo, na Mungu amempa kila mmoja utashi wa kutokumtii, na kupata madhara ya kutii au kutokutii kwao.

4. Tunda lingeweza kuliwa baadaye. Theophilus, askofu wa Antioch (168-181/188 BK) alifundusha kuwa kama Adam na Hawa hawangetenda dhambi, wangekua na kukomaa, na kuwa wakamilifu, na kupaa mbinguni wakiwa na hali ya umilele. Mwanadamu alikuwa na hali ya wastani, si wa milele kabisa lakini pia wenye maisha yenye ukomo, au Paradiso ilikuwa kati ya mbingu na dunia.. Theophilus to Autolychus kitabu cha 2 sura ya 22, uk.24, 104.

 

S: Kwenye Mwanzo 3, je tunapaswa kujivuna kuwa Hawa alikula epo (tunda), kama Laura Schlesinger anavyosema?

J: Hapana. Dr. Laura yuko sahihi katika vitu vingi sana lakini hayuko sahihi hapa. Yafuatayo ndiyo aliyoyasema kwenye Modern Maturity Septemba -Oktoba 1999, uk.67.

"Ninafahari kubwa kwamba (Hawa) alikula tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Kwa sababu kama asingekula, tungeendelea kuwa wanyama bustanini. Mungu hakuuweka ule mti ili kutoa kivuli tu. Tulifanyika kuwa wanadamu kwa hatua hiyo."

Kwanza kabisa, mti ule haukuwa wa ujuzi tu, lakini wa ujuzi wa mema na mabaya. Schlesinger yuko sahihi kuwa watu hawakubaki vilevile walivyokuwa. Mambo yote haya kama mauaji, vita, ukandamizaji, na kutokuwajibika kimaadili kulikofanywa na watu kumetokea baada ya jambo hili. Lakini, watu wataendelea kuwa watu mbinguni, ambako hawatafanya dhambi tena. Inawezekana kuwa mwanadamu kamili na kutokuwa mwenye dhambi, kama Adam na Hawa walivyokuwa kabla ya kula tunda, na kama Yesu Kristo alivyo.

Baadaye kwenye mahojiano, wakati Dr. Laura aliposema kuwa Adam alikosea alipojaribu kumlaumu Hawa, Schlesinger yuko sahihi, kwa kuwa Mwanzo 3:6 inasema kuwa Adam alikuwa na Hawa wakati Hawa alipokula tunda.

 

S: Kwenye Mwanzo 3, je tunda la mti ni sitiari ya uhusiano haramu wa kimwili kati ya Hawa na Shetani kama Mch. Moon wa kanila la Wamoon (Unification Church) anavyofundisha kwenye Divine Principle (toleo la tano, 1977), uk.75-79?

J: Hapakuwa na sitiari ya ngono kwenye mti, tunda, au Shetani. Kama Mch. Moon alikuwa sahihi basi:

Je miti mingine yote iliyoruhusiwa ilikuwa nini?

Hawa alimpuuzia Shetani alipokula tunda la mti

Kwenye Mwanzo 3:13, Hawa, akijaribu kumtupia nyoka lawama zote, alisema tu kwamba nyoka alimdanganya. Hakusema kuwa nyoka alifanya kitu chohote kila kwake.

Tazama pia swali lililotangulia.

 

S: Kwenye Mwanzo 3, kuna jamii zozote zenye hadith kama hiyo ya watu wa kwanza, kwenye bustani, wakila tunda lililozuiliwa?

J: Ndiyo. Kuna walau mifano mitatu hapa.

Sgaw Karen watu wa Burma: Mwenyezi, Mungu ajuaye vyote ambaye anaitwa Y'wa aliumba kila kitu. Aliumba watu wawili, mtu aitwaye Thanai na mwanamke alieitwa Eeu, na aliwaweka kwenye bustani iliyokuwa na aina saba za miti ya matunda. Lakini hawakuruhusiwa kula aina moja ya miti. Mwovu Mu-kaw-lee aliwadanganya watu hawa wawili akiwaambia kuwa watakuwa na nguvu za kimiujiza na kupaa mbinguni. Mu-kaw-lee aliwashawishi kula tunda la mti wa majaribu. Walikula na wakawa na uwezo wa kupata magonjwa, uzee na kifo.

Don Richardson anaelezea uwezekano kuwa hadithi hii inaweza kuwa imetokana na ushawishi wa Wanestoria au kanisa Katoliki, na anahitimisha kwa kusema kuwa haikutokana hivyo, kwa sababu Richardson hakukuta nadharia ya kufanyika mwili au mkombozi anayekufa kwa ajili ya mwanadamu na kufufuka toka kwa wafu. Tazama Eternity in Their Hearts uk.77-83 kwa habari zaidi.

Santal wa India: Walimwamini "Thakur Jiu" (Thakur = wa kweli, Jiu = Mungu), ambaye aliwaumba wanandoa wa kwanza, mwanaume aliyeitwa Haram na mwanamke aliyeitwa Ayo na aliwaweka Hihiri Pipiri, iliyokuwa magharibi mwa India. Mwovu Lita aliwajaribu kuwa watengeneze pombe ya mchele na kumwaga sehemu yake ardhini kama sadaka kwa Shetani. Walifanya hivyo, na wakanywa sehemu ya pombe iliyobaki na kulewa. Walipoamka, walijua kuwa wako uchi na walishikwa na aibu. Baadaye walipata watoto saba, wavulana kwa wasichana. Kizazi chao kilikuja kuwa cha uharibifu, hivyo Thakur Jiu aliwaficha "wanandoa hao watakatifu" kwenye Mlima Harata (=Ararat?), na kuwaharibu waliobakia kwa mafuriko. Hatimaye mababu zao walikwenda (mashariki) kutoka msitu hadi msitu, mpaka walifika kwenye milima mirefu iliyozuia njia yao. Mwishowe walipita (huenda njia ya Khyber) na kufika nyumbani kwao karibu na Calcutta.

Wasumeria: Wasumeria waliamini kuwa walitokea Paradiso waliyoiita Dilmun. Hata hivyo hakuna vitu vingine vingi vinavyofanana na Bustani ya Edeni. Dilmun palikuwa ni mahali ambapo miungu wote walikuwepo, pia Ziusdra, mtu aliyepata hali ya kutokuwa na ukomo. Shairi la Dilmun liliandikwa karibu mwaka 2400 KK.

 

S: Kwenye Mwanzo 3, kwa kuwa Adam na Hawa walikuwa wakamilifu, inawezekanaje watu wakamilifu wanafanya vitu visivyo vikamilifu, kama dhambi?

J: Bila kujali mtu anafafanua "kamilifu" kwa namna gani, Biblia haijasema mahali popote pale kuwa Adam na Hawa walikuwa wakamilifu. Pia haijawahi kusema kuwa hawakuwa na uwezo wa kufanya dhambi. Badala yake Biblia inaonyesha kuwa walikuwa watu wazuri sana, na "hawakuwa na dhambi", kwa maana ya kuwa hawakuwa wamewahi kufanya dhambi. Walikuwa bado na uwezo wa kutumia uhuru walionao na waliweza kufanya uchaguzi kuhusu dhambi.

Clement wa Alexandria (aliandika mwaka 193-217/220 BK kwenye kitabu chake kiitwacho Stromata kitabu cha 6 sura ya 12, uk.502) alikuwa ni mtu wa kwanza kujibu swali hili. Alisema, pamoja na mambo mengine, kuwa mwanadamu "hakuwa mkamilifu wakati wa kuumbwa kwake bali alizoezwa kupokea maadili. ... Sasa mtihani ni mwendo wa kuelekea uadilifu, si uadilifu wenyewe. Mambo yote, basi, kama nilivyosema, yanahusishwa na kupata uadilifu."

 

S: Kwenye Mwanzo 3, kwa kuwa Mungu mkamilifu anaumba watu wakamilifu, ilikuwaje Adam na Hawa wafane dhambi?

J: Mambo matano ya kuyazingatia kwenye jibu la swali hili.

Tertullian alijibu swali hili zamani sana mwaka 207 BK kwenye kazi iitwayo Against Marcion kitabu cha 2 sura za 5-9. Jibu lefu la Tertullia linaweza kufupishwa kwa kutumia maneno yake mwenyewe: "Kwa hiyo ilikuwa vema kuwa [mwanadamu] sura na mfano wa Mungu aumbwe akiwa na utashi huru na uwezo wa kujidhibiti yeye mwenyewe; ili kwamba jambo hilihili - yaani uhuru wa kuamua na kujiamrisha - viweze kutambuliwa kuwa ni sura na mfano wa Mungu ndani yake." Kwa maneno mengine, ilikuwa vema kwa Mungu mkamilif kuumba viumbe kama Yeye mwenyewe, vyenye kuwa wa utashi huru.

Theophilus askofu wa Antioch (168-181/188 BK) alijibu swali linalofanana na hili, kuwa Adam na Hawa walikuwa na hali ya kuishi bila ukomo au na ukomo, kwa kuonyesha kuwa walikuwa kwenye mchakato na walikuwa na uwezo kuelekea upande wowote. (Theophilus to Autolychus kitabu cha 2 sura ya 27, uk.105).

Si maroboti: je ungependa Mungu mkamilifu awekewe mipaka na kuumba maroboti na kutokuwa na uwezo wa kuumba watu wenye utashi huru? Mungu haumbi mantiki zisizowezekana, na ili aumbe watu ambao wamechagua kwa hiari kumtii na kumpenda, Mungu pia aliwaumba wakiwa na uwezo wa kutokumpenda na kutokumtii. Biblia haisemi hata mara moja kwamba Adam na Hawa walikuwa "wakamilifu" kwa maana ya kwamba wakiwa hawana uwezo wa kutenda dhambi. Badala yake Biblia inasema kuwa walikuwa "wazuri sana" na "bila dhambi", kwa maana ya kuwa walikuwa hawajwahi kutenda dhambi.

Ukamilifu wa Mungu: Kati ya wanadamu na mapepo, Biblia iko wazi kabisa kwamba ukamilifu wa Mungu haumzuii kuumba viumbe wenye uwezo wa kutokumtii.

Ni ufafanuzi wa nani? Kama ufafanuzi wa mtu wa Mungu mkamilifu utakuwa ni yule ambaye hana uwezo wa kuumba watu wenye uwezo wa kufanya maamuzi ya kimaadili, basi wajibu wa kuthibitisha utakuwa kwao kutafuta angalau aya moja inayounga mkono mawazo hayo. Vinginevyo, ufafanuzi huo haufanani na Mungu wa kwenye Biblia. Suala la msingi hapa ni:

a) uweke ufafanuzi wako wa "ukamilifu wa Mungu" kwa Mungu wa kwenye Biblia, au

b) Umwache Mungu ajisemee mwenyewe kwenye Biblia jinsi alivyo mkamilifu na namna alivyochagua kuumba.

Kuhusu sababu ya Mungu kuchagua "kupitia matatizo" ya kuwaumba Adam na Hawa, huku akijua kuwa watafanya dhambi. Tazama maelezo kuhusu Mwanzo 1.

 

S: Kwenye Mwanzo 3:1 na 2 Kor 11:3, kwa nini Adam na Hawa walijaribiwa na Shetani aliyekuwa na umbo la nyoka, badala ya kitu kingine kama simba, au mtoto wa sungura?

J: Maandiko hayasemi kitu chochote, lakini tunaweza kuhisia. Wanyama wakubwa wanaweza kutisha watu na kuwafanya watafute namna ya kujilinda. Wanyama wadogo wanaweza kupuuzwa kuwa hawana umuhimu. Nyoka anaweza kumaanisha kuwa "edanganyifu" unaruhsiwa. Kwa sababu ili watu wengi kwenye jamii waende kufanya dhambi kwa pamoja ni dhahiri kuwa watu wengi wanaamini kuwa dhambi hiyo haina ubaya.

Bible Difficulties and Seeming Contradictions uk.96 inatoa wazo la kufurahisha kuwa baadhi ya watu wanamwona nyoka kuwa kama ufananisho wa uwezo wa akili usiokuwa na dhamira. Nyoka anashangaza jinsi anavyosubiri kwa udanganyifu na kujiingiza kwenye mawindo yake. Mathayo 10:16 inasema tunapaswa kuwa wenye busara kama nyoka na wapole kama njiwa.

 

S: Kwenye Mwa 3:1, inawezekanaje mnyama asiyekuwa na aikili na asiyeweza kusema kama nyoka awadanganye Adam na Hawa?

J: Huyu hakuwa nyoka wa kawaida. Shetani alichukua umbo la nyoka, na Shetani anaweza kuongea na ana akili sana. Shetani pia ameitwa nyoka kwenye Ufunuo 12:9, 14, 15 na Ufunuo 20:2. Kuna njia tatu ambazo Shetani angeweza kuwa nyoka, na tafsiri rahisi zaidi inaonyesha kuwa zote hizi ni kweli.

Kujigeuza kimwili: Shetani ama alijigeuza mwenyewe ama aligezwa na kuwa na umbo la kimwili la nyoka hata akaweza kuongea.

Mfano: Bila kujali endapo nyoka ambaye Hawa alimwona alikuwa Shetani mwenyewe au nyoka wa kawaida, Shetani "aliongea kupitia" kupitia umbo hili kuoyesha udanganyifu wa nyoka.

Sitiari: Shetani aliitwa nyoka kwa sababu ya njia ya ujanja aliyotumia kumwendea Hawa.. Tazama swali lililotangulia kwa maelezo zaidi.

 

S: Kwenye Mwanzo 3:1-16, kuna mambo gani makuu tunayoweza kujifunza kuhusu dhambi tokana na mfano huu?

J: Tunaweza kujifunza mambo mengi sana, lakini hapa yapo machache tu kati ya hayo.

1. Dhambi ina madhara. Mungu aliwasamehe, lakini bado walipaswa kufa, na hawakuirudia zawadi ya mti wa uzima. (Angalau hadi Ufunuo).

2. Maandiko hayasemi endapo walikufa kabla Mungu hajaaua baadhi ya wanyama ili awavishe ngozi. Dhambi haikuweza kufunikwa na matawi kadhaa ya miti ambayo yalikua tena mwaka uliofuata. Inaweza kufunikwa na damu tu, kwenye mnyama aliyekufa.

3. Wangeweza kula toka katika mti wowote wa kwenye bustani, lakini walifikiri Mungu alikuwa mchoyo kwa sababu aliwazuilia mti ule mmoja. Baada ya anguko, Mungu alikuwa mwenye rehema hata akawasamehe na kuwavisha ngozi za wanyama, lakini walikuwa na shida kwani ardhi ilikuwa choyo kwao sasa.

4. Hata madhara ya dhambi yao yalikuwa ni rehema ya Mungu. Haddon Robinson anasema kuwa uchungu umechukua nafasi ya juu kwenye ngome ya moyo wa uasi.

5. Hata baada ya dhambi, Mungu bado alikuwa na mpango wa ukombozi. Hata baada ya kuharibu kabisa, ahadi ya Warumi 8:28 bado ipo. Hata kwenye sura hii ya giza, Mungu ana ahadi kwenye Mwanzo 3:15.

Kwa maelezo zaidi kuhusu Mwanzo 3, agiza mahubiri ya Gary Brandenburg ya 5/27/2005 toka www.FBCDallas.org.

 

S: Kwenye Mwa 3:1,14, kwa kuwa nyoka alilaaniwa kuwa atatambaa kwa tumbo lake, je jambo hilo linamaanisha kuwa nyoka walikuwa na miguu?

J: Hapana. Ingawa baadhi ya wanyama wadog wa majini walio kama mijusi wana mikono lakini hawana miguu, hivi sivyo ilivyokusudiwa hapa. Ingawa Maandiko hayako bayana Shetani alilaaniwa kwa kupewa njia ya kutembea iliyohafifu na isiyokuwa na heshima. Shetani alichukua umbo la Shetani ambaye ni mdogo kwa heshima, na Mungu alimwadhibu Shetani kwa laana kwa kumpa baadhi ya sifa za nyoka.

Watu wanapofanya dhambi, hitaji la msamaha kwa tendo la nje lililofanywa ni sehemu tu ya tatizo. Asili ya dhambi iko hivi sehemu ya dhambi inashikamana na mioyo yetu kwa ndani, na tunahitaji pia kusafishwa.

 

S: Kwenye Mwanzo 3:1, 14-15, je nyoka alikuwa na miguu kabla ya kulaaniwa?

J: Kuna maoni makubwa mawili.

Ndiyo: Huenda "nyoka" huyu wa bustanini alifanana na kenge ambaye hatambai kwa tumbo, na Mungu alimfanya kiumbe huyo akose miguu yake yote. Hawezi kuwa alibadilika kutoka kuwa kama "kenge‘ na kuwa kama mamba anayetambaa kwa tumbo, kwa sababu matumizi ya neno linalofahamika sana "nyoka" yanadokeza kutokuwepo kwa miguu. The Nelson Study Bible uk.10 inasemas, "Maneno halisi ya mwandishi ... yanadokeza kuwa kabla ya hapa nyoka alikuwa na namna nyingine ya umbo la mwili."

Hapana: The New International Bible Commentary uk.117 ina maoni kuwa "Adhabu ya nyoka (m.14) inatakiwa kueleweka kuwa kipindi fulani nyoka alikuwa na miguu. Badala yake, kitu ambacho kimeonekana kuwa cha kawaida na kizuri sasa kinakuwa ukumbusho wa siku zote wa kitu ambacho nyoka alikifanya." The Expositor's Bible Commentary juzuu ya 1, uk.55 inasema, "Laana hii haimaanishi kuwa nyoka alikuwa anatembea kwa miguu kama wanyama wengine wanaotembea ardhini. Jambo linalomaanishwa ni kuwa tokea wakati huo, kama matokeo ya laana, wakati nyoka anatambaa kwa tumbo lake, kama ambavyo nyoka anafanya, "atakula mavumbi." Mkazo upo kwenye nyoka ‘kula mavumbi', na maelezo ambayo sehemu nyingine yanamaanisha ‘kushindwa kabisa' (linganisha na Isa 65:25; Mik 7:17)."

Hata hivyo, wazo ni kuwa nyoka aliyekuwa mjanja (‘arum kwnye Mwanzo 3:1), sasa amelaaniwa (‘arur kwenye Mwanzi 3:14). Neno ‘amelaaniwa' limetumiwa kwa nyoka na kwa ardhi, lakini si kwa mwanaume na mwanamke.

 

S: Kwenye Mwanzo 3:3-24, kwa nini Adam na Hawa waliadhibiwa vikali zaidi kuliko watu wengi leo?

J: Mungu hakuwaadhibu kwa kitendo chao cha kuchuma; isitoshe wangeweza kuchuma matunda ya miti mingine. Mungu aliwaadhibu kwa sababu ya kutokuwa na hali ya dhambi lakini bado walikosa kumtii Mungu.

Ukubwa wa adhabu yao unaonekana kuwa wa haki ukizingatia kuwa Mungu huadhibu watu kwa kutegemea kiwango ambacho watu wanajua na walikuwa na uwezo wa kufanya. Tofauti na watu wa leo, Adam na Hawa walikuwa kwenye uwepo wa moja kwa moja wa Mungu, na bado hawakutumaini kuwa Mungu alijua kitu kilichokuwa bora zaidi kwao. Tofauti na watu wa leo, hawakuwa na hali ya dhambi, ambayo ingekuwa inawavuta kwenye dhambi mara kwa mara na kwa nguvu.

Tazama Today's Handbook for Solving Bible Difficulties uk.193-195 kwa jibu tofauti kabisa ambalo linafikia kwenye hitimisho hilihili.

 

S: Kwenye Mwanzo 3:3-6, je Adam na Hawa walikula epo?

J: Maandiko hayajasema kuwa walikula epo. Lilikuwa ni tunda lililozuiliwa, tunda la ujuzi wa mema na mabaya, ambalo linaweza kuwa halipo tena duniani leo.

Watu wengine wanafikiri kuwa kuchanganya tunda lililozuiliwa na epo kwenye Enzi ya Kati kulitokea kwa sababu neno la kilatini la uovu ni "malum" na neno la kilatini la epo ni "malus." Kwa jinsi yoyote ambayo wazo hili limejitokeza, hakuna msingi wa kibiblia wa kiini cha wazo hili, kwa vyovyote vile utakavyolichambua.

 

S: Kwenye Mwanzo 3:5-22, je Adam ni anaashiria roho ya mbinguni, Hawa anaashiria roho ya duniani, na nyoka anaashiria kushikamana na ulimwengu wa binadamu kama Wabahai' wanavyofundisha kwenye Some Questions Answered uk.123?

J: Hapana. Watu wamekuwa wakujaribu kupata maana za kiroho tofauti na maana wazi ya Mwanzo kwa karne nyingi sana. Adam ni mwanadamu mwanaume, na Hawa ni mwanadamu mwanamke, na kuongezea tafsiri hii isiyotakiwa kunawafanya wanaume wawe "roho za kimbinguni" kubwa na wanawake "roho za kidunia." Badala yake, wanaume na wanaume uthamani mmoja na unaofanana mbele ya macho ya Mungu (Wagalatia 3:28).

 

S: Kwenye Mwanzo Gen 3:5, 22, endapo Adam na Hawa wangekuwa "kama miungu" kama wangekula tunda, je kuna Mungu zaidi ya mmoja kama Wamormon wanavyofundisha?

J: Ilikuwa tu baada ya wakati ule wangepata ujuzi wa mema na mabaya. Mwanzo 3:5 inasema kama Mungu. Kwenye kiebrania ni Elohim, jina la Mungu. Tazama Mwanzo 3:5 haithibitishi uwingi wowote ule.

 

S: Kwenye Mwanzo 3:5, 22, je watu wangeweza kujua kila kitu, kama Mungu?

J: Hapana. Shetani hata hakudokeza kuwa watakuwa kama Mungu kwa kila kitu (kuabudu, Mwenyezi, Utatu Mtakatifu, n.k.). Badala yake Shetani aliwaahidi kuwa watakuwa kama Mungu kwa maana ya kuwa watajua mema na mabaya. Kabla ya kula tunda walifahamu mema tu. Baada ya kula tunda, walijua kuhusu mema na mabaya. Kwa hiyo, kwa namna fulani Adam na Hawa walijuta sana, nyoka alikuwa sahihi.

Kuna vifungu vingine vitano vinavyoelezea kujua mema na mabaya: Kumbukumbu 1:39; 2 Samuel 14:17; 19:35; 1 Wafalme 3:9; na Isaya 7:5. Hivi vinaonyehsa kuwa Mungu ndie anayeamua kitu gani ni chema na kitu gani ni kiovu, na huenda Shetani alikuwa anawaahidi "tamko la uhuru" ambapo wangeamua wao wenyewe vitu gani ni vyema na vitu gani ni viouvu. "Tamko hili la uhuru" liliwanasa kwenye hukumu.

Shetani anatoa ahadi kama hizo leo. Kwa namna nyingi za uhindu, lengo likiwa kuwa na uhusiano na Mungu, au kuwa "mwema." Badala yake lengo ni kupata "uzoefu", kuzoea mema na maovu. Wakati mwingine watu wanashangazwa kumkuta mwalimu wa dini ya kihindu (guru) ambaye si mwaminifu na anadanganya mtu mwingine. Guru anaweza kuwa anafanya sawa na dini yake. Kwa baadhi ya watu, lengo ni kujua mema na mabaya.

 

S: Kwenye Mwanzo 3:6, kwa nini Hawa aliadhibiwa kwa kutafuta maarifa kwa kula tunda, kwa sababu kupata maarifa kunachukuliwa kuwa kwema wakati wote?

J: Kutafuta maarifa si kitu chema peke yake. Kutafuta maarifa kutoka kwa Mungu ni kwema, lakini maarifa yanayopatikana kupitia kutokutii si njema. Wakristo kwa ujumla hawajajifunza na kupitia maovu ya aina mbalimbali, na wala hawapendi kufanya hivyo.

Kama Theophilus, askofu wa Antioch (168-181/188 BK) aliivyoandika kwenye barua yake To Autolychus 2:250 "Kwa sababu haukuwa mti, kama wengine wanavyodhani, bali kutokutii, kulikokuwa na mauti ndani yake. Kwani hakuna kitu kingine kwenye tunda zaidi ya ujuzi; lakini ujuzi ni mzuri unapotumika kwa busara. Lakini Adam, kwa kuwa kwake mtoto mchanga kiumri, alikuwa bado, kwenye tukio hili, bado hajawa na uwezo wa kupokea ujuzi kwa namna inayostahili." Ante-Nicene Fathers 2, uk.104.

 

S: Kwenye Mwanzo 3:6, majaribu ya Shetani kwa Hawa yanafananaje na majaribu ya Shetani kwa Yesu kwenye Mt 4:1-11 na Lk 4:1-13?

J: Ingawa hayafanani, Shetani mara nyingi hutumia mbinu zinazofanana mara kwa mara , na hii huenda ni kwa sababu mbinu hizo hazijashindwa kufanya kazi.

Hawa aliona tunda lililokatazwa kuwa

1. Zuri kwa chakula [haja ya mwili ya chakula]

2. Linavutia macho [uzuri, tamaa ya macho]

3.Linatamanika kwa maarifa [macho yatafunguliwa, na kama Mungu, utajua mema na mabaya. [nguvu kama ya Mungu baada ya kuifuata amri ya Shetani].

Yesu, aliyekuwa anafunga, alijaribiwa na

1. Mawe yawe mkate [haja ya mwili ya kula]

2. Kujitupa toka kwenye kinara cha hekalu [kujionyesha]

3. Mamlaka juu ya falme za dunia [nguvu kama za Mungu zilizo chini ya amri ya Shetani].

Kwenye 1 Yohana 2:16 zimeelezwa aina tatu za dhambi duniani, tamaa ya mwili, tamaa ya macho, na kiburi cha uzima.

 

S: Kwenye Mwanzo 3:8, kwa Mungu yupo kila mahali (Zaburi 139), Adam angewezaje kuwa mbali na uwepo wake?

J: Kuwepo kwa uwepo wa Mungu mahali pote hakutuzuii kuwa na uwepo wake wa moja kwa moja mahali tulipo ili kuhusiana naye. Kuna mifano mingi mingine ya Mungu kujidhihirisha sehemu mbalimbali kupitia vitu tofauti tofauti. Hivi ni pamoja na maono ya Abraham ya wageni watatu (mwanzo 18:1-33), kichaka kilichokuwa kinaungua (Kutoka 3:2-22), wingu zito (Kutoka 19:9), pale Mlima Sinai (Kutoka 19:11-12), kwenye Sanduku la Aganoa (1 Wafalme 8:11-13), kuondoka kwenye hekalu (Ezekiel 10:3-18), na kuja kwa Yesu duniani.

 

S: Kwenye Mwanzo 3:8, kwa kuwa Mungu yupo kila mahali, Adam na Hawa waliwezaje lumsikia akitembea bustanini?

J: Mungu yupo kila mahali, na anaweza akafanya kitu chochote kile; kitu chochote ikiwa ni pamoja na kuufanya uwepo wake uwe mahali fulani. Huyu anaweza kuwa Mungu kwenye Utatu, lakini Wakristo wa mwanzo, kama Theophilus wa Antioki (168-181/188 BK) kwenye barua yake iitwayo Letter to Autolychus kitabu cha 2 sura ya 22, uk.103 anasema kuwa huyu alikuwa ni Yesu Kristo. Kutokea kwa Yesu kabla ya kuzaliwa kwake na bikira kunaitwa Christophanies na wataalam wa thiolojia.

 

S: Kwenye Mwanzo 3:9, 11, kwa kuwa Mungu anajua kila kitu, kwa nini alihitaji kumuuliza Adam yuko wapi na amefanya nini?

J: Mungu anajua kila kitu. Kama mzazi anavyoshughulika na watoto, wakati mwingine Mungu huuliza maswali ambayo tayari anajua majibu yake ili kuwapa watu nafasi ya kumkiri. Wakati ule, Mungu aliwauliza maswali manne:

1. Uko wapi?

2. Nani aliyekuambia kuwa uko uchi (umejifunza jambo hili wapi)?

3. Je umekula (umekosa kunitii)?

4. Umefanya kitu gani?

Maswali ya Mungu yaliwaongoza kwa upole kwenda kwenye toba. Mungu aliwasamehe bure, lakini walipata matokeo ya uovu wao na hawakurudishiwa zawadi ya mti wa uzima.

Today, God asks people the same four questions!

1. Uko wapi? Mara nyingi watu wanaokuwa kwenye dhambi huwa hawajui wako wapi, ingawa Mungu na watu wngine karibu yao wanaweza kuona jinsi wanavyoyafanya maisha yao wenyewe kuwa mabaya sana. "Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, tulikuwa waasi, tumedanganywa, huku tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukiishi katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana. Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa, alituokoa..." (Tito 3:3-4a).

2. Nani aliyekuambia (umejifunza jambo hili wapi)? Watu leo hii wanaamini wanamazoea ya kuamini uongo mwingi badala ya ukweli toka kwa Mungu. "Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyoofu na usafi wa Kristo. Maana yeye ajaye akihubiri Yesu mwingine ambaye sisi hatukumhubiri, au mkipokea roho nyingine msiyoipokea, au injili nyingine msiyoikubali, mnatenda vema kuvumiliana naye" (2 Wakorintho 11:3-4).

3. Je umekula (umekosa kutii)? Iwe ni chanzo kilichozuiliwa (na mara nyingi huwa uongo) ujuzi, au kitendo kilichozuiliwa, au moyo uliojiweka kwenye vitu duni, Roho Mtakatifu anauliza: "je unakosa kutii?"

4. Umefanya nini? Matatizo ya kujitakia (kimaadili na kimwili) hayatokei kwa ghafla tu kama pulizo linalopasuka mara, bali yanakuwa na msingi wa dhambi uliojengwa kwa muda mrefu, kama pulizo lenye kuvuja kidogo kidogo. Yakobo 1:15 inasema kuwa tamaa ikitunga mimba huzaa dhambi, na dhambi ikikomaa huzaa mauti. Hata kama mtu mkosaji hana sababu ya kujitetea, angalia nyuma na kuona maamuzi ambayo amekuwa akiyafanya na fikra za moyo zilizopelekea kwenye tatizo hilo.

Waandishi wa mwanzo wa kikristo pia waliona maswali ya Mungu yakiwa yanajifunua kwao kwenye sehemu walizokuwemo na kuwaita kutubu.

Theophilus (askofu mwaka 168-181/188 BK.) kwenye Letter to Autolychus, alikuwa mtu wa kwanza kungelea swali hili. Alisema, "Na kama Mungu alivyoita na kusema, "Uko wapi Adam? Mungu alifanya hivi si kwa sababu ya kutokujua kwake jambo hili; bali, akiwa mvumilivu, alimpa nafasi ya kutubu na kukiri." (Ante-Nicene Fathers uk.105).

Tertullian kwenye kazi yake Against Marcion (mwaka 207 BK) anajibu swali hili kwa namna hii. "...Mungu hakuwa hana uhakika (alikuwa na uhakika) kuhusu kufanyika kwa dhambi wala hajui mahali Adam aliko. Ilikuwa sahihi kabisa kumwita mkosaji, aliyekuwa anajificha toka na kuelewa kwake dhambi, na kumleta kwenye uwepo wa Bwana, si tu kwa kumuita kwa jina lake, bali kwa kuishambulia kwa nguvu dhambi ambayo ilifanywa wakati ule. Kwa sababu swali halipaswi kusomwa kwa namna ya kuuliza tu, Uko wapi Adam? Lakini kwa sauti kubwa na ya msistizo, na pumzi ya kuzuilia (imputation???). Ewe Adam uko wapi? - kwa ukaribu unaowezekana: haupo hapa tena, umekwenda kwenye hukumu ya milele- kwa hiyo sauti ni tamko lake Yeye akaripiaye na kuhuzunika." (Against Marcion kitabu cha 2 sura ya 26).

 

S: Kwenye Mwanzo 3:14-15, Bwana Mungu alimlaani nyoka kuwa "atakula mavumbi siku zote za maisha yake." Nashindwa kuhusanisha jambo hili na ushahidi wa kizoolojia kwamba nyoka ni wanyama wanaokula nyama na wanakula vyura, ndege, n.k. Sijaribu kusema kuwa Mungu hayuko sahihi; naamini Yeye huwa hafanyi makosa, lakini unaweza kusema mstari huu unamaanisha nini hasa? Je kuna sitiari yoyote iliyokusudiwa hapa?

J: Hebu tuwaangalie nyoka kwanza kisha sitiari yake. Tofauti na minyoo, nyoka hawapati virutubisho vyao toka kwenye kula vumbi. Lakini nyoka wengi huwa wanatambaa ardhini; chakula chao ni kile tu kinachoanguka mavumbini. Si tu chakula chao, bali pia maisha yote ya nyoka ni duni, yamezungukwa na uchafu na vitu visivyokuwa muhimu. Neno la kiebrania hapa, nacash, hutumika sana kwa nyoka, likiwa limetokana na kitenzi chenye kumaanisha toa sauti ya kutokukubaliana au kunong'ona. Linamaanisha kutoa sauti ya uchawi. Kwa hiyo, neno hili linakazia kunong'ona kwa nyoka, na Mwanzo inakazia mavumbi, kwa hiyo picha ni hapa ni "mara unaponong'ona mavumbi, utanong'ona mavumbi siku zote."

The New Geneva Study Bible uk.13 inasema kwamba vumbi linaweza kumaanisha "kudhalilishwa kubaya sana." Vumbi inaweza pia kuwa ishara ya mauti.

Sasa nyoka aliyewajaribu Adam na Hawa hakuwa nyoka wa kawaida; alikuwa ni Shetani mwenyewe. Kuna vitu viwili vya kuchagua: ama Shetani alitokea kama nyoka, au alitumia mwili wa nyoka aliyekuwepo. Wakati Mwanzo 3:14-15 inawezakuwa inawaongelea nyoka wote, au nyoka.mjusi mmoja na uzao wake wote, inaweza kuwa inamwongelea Shetani akiwa anaonekana na namna hiyo ya mwili, kwa sababu aliitumia wakati ule.

Mkazo muhimu zaidi kwenye Mwanzo 3:14-15 ni hukumu dhidi ya Shetani. Kama ambavyo nyoka anatambaa kwa namna duni na isiyokuwa na heshima, na kula vitu vichafu, Shetani, aliyechagua kuwa na umbo la nyoka, vivyo hivyo hataacha kutambaa kwenye mavumbi kutoka kwenye mahali pake pa juu pa zamani kule mbinguni.

The Bible Knowledge Commentary : Old Testament uk.33 inasema kuwa kitendo cha watu kumwona nyoka anatambaa na kula mavumbi kinawakumbusha anguko.

Wakati wa milenia kwenye Isaya 55:25, mbwa mwitu, mwana kondoo, na wanyama wengine watabadilishwa na kubarikiwa, lakini nyoka ataendelea "kula vumbi." Ingawa hakuna atakayemdhulu, na hakutakuwa na wanyama wenye kula nyama kwenye mlima mtakatifu wa Mungu, nyoka ataendelea "kula mavumbi." Ufunuo 20:1-10 inatuambia kuwa waamini watatawala duniani pamoja na Kristo kwa muda wa miaka 1,000, lakini mwishoni mwa miaka hiyo 1,000, Shetani ataendelea kutoa "sauti" akiyashawishi mataifa kumpinga Mungu.

 

S: Je Mwa 3:15 inamaanisha kuwa Bikira Mariamu hatakuwa na dhambi, kama baadhi ya Wakatoliki wanavyodai?

J: Hapana, kwa sababu mbili.

Hawa anaongelewa hapa, si Mariamu. Hawa hakuwa bila dhambi, lakini hakuna shida kwani aya hii hasemi kuwa hakuwa na dhambi.

Mbegu, yaani Yesu, ni mkazo wa aya hii. Hakuna kitu chochote hapa, au sehemu nyingine yoyote ile ya Biblia inayosema kuwa mama yake Yesu hatakuwa na dhambi. isitoshe, hakuna rekodi kumbukumbu yoyote ya Mkristo wa miaka iliyotangulia Nikea (pre-Nicene Christian) aliyesema Mariamu hakuwa na dhambi.

 

S: Kwenye Mwa 3:15, nani hasa ni mzao wa Shetani?

J: Kwenye Yohana 8:41, 44 Yesu anaonyesha wazi kuwa ni wale wanaomkataa Yesu.

 

S: Je Mwa Gen 3:16 inapaswa kutafsiriwa kuwa "Mtego umezidisha huzuni na majonzi yako" au kwa namna ile ya kawaida "nitakuzidishia uchungu wako"?

J: Konsonati za kiebrania ni karibu sawa kwenye misemo hii miwili. Voweli ziko tofauti sana, lakini alama za voweli ziliongezwa miaka mingi baada ya kuja kwa Kristo. Tofauti pekee kwenye konsonati ni kuwa tafsiri ya kawaida haina konsonatni mbili. Ama konsonatni zinazopungua ni makosa ya uchapaji au tafsiri nyingine iko sahihi.

Kama tafsiri nyingine ("mtego") ni sahihi, basi Shetani atakuwa ndie mtego. Hata hivyo, kuwa na watoto si jambo ovu, na lilikuwa sehemu ya mpango wa awali wa Mungu kwao (Mwanzo 1:28) na anguko halikubadilisha jambo hili.

 

S: Je Mwa 3:16 inatakiwa kutafsiriwa kumaanisha kwamba mwanamke alilaaniwa kwa haja [ya kimwili/tendo la ndoa] inayotisha kwa mume wake? Au, neno "kugeuka" badala ya "haja"?

J: Ingawa neno linawezakuwa na maana yoyote kati ya hizo mbili, muktadha unaonyesha kugeuka, kudhibiti, au kutawala. Katika mara zote 120 ambazo maneno ya kiingereza tamaa/haja/kutamani/yenye kutamanisha yametumiwa kwenye Agano la Kale, neno hili maalum la kiebrania la haja, teshuqah (namba 8669 kwenye itifaki ya Strong) limetumika mara tatu tu: Mwanzo 3:16; Mwanzo 4:7 na Wimbo Ulio Bora 7:10. Kwenye Wimbo Ulio Bora, neno hili linamaanisha haja ya mtu kwa mpenzi wake, na kwenye Mwanzo 4:7 Mungu anamwonya Kaini kuwa dhambi inatamani kumpata.

Kwa mujibu wa Walter Kaiser, mababa wa kanisa Clement wa Rumi, Irenaeus, Tertullian, Origen (mwaka 225-254 BK), Epiphanius, na Jerome, na Philo Myahudi, walilitafsiri kuwa "kugeuka", na hawakujua tafsiri ya "tamaa." Kwa hiyo, kifungu hiki kinamaanisha kuwa wanawake watageuka wakiacha kumtumaini Mungu na kutumaini waume zao badala yake. Kaiser anasema kuwa Katherine C. Bushnell aligundua kuwa matumizi ya kwanza ya "haja/tamaa" kwenye kifungu hiki yalifanywa na mtawa wa kidominika wa Italia aliyeitwa Pagnino. Ingawa Wycliffe Bible ilitafsiriwa kabla ya hii, kwa bahati mbaya, Biblia nyingine zote za kiingereza kuanzia toleo la Coverdale hadi toleo la Mfame James (King James Version) na kuendelea zinatafsiri neno hili kuwa "tamaa."

Sababu tano zenye kuonyesha kuwa neno hili linamaanisha kugeuka, kudhibiti, au kutawala dhidi ya tamaa ya ngono

1. Ulinganifu wa "tamaa ya mume wako", na "atakutawala

2. Ukaribu wa maana hiyohiyo kwenye Mwa 4:7

3. Kama lilimaanisha tamaa ya ngono, kwa nini hakuna maelezo kuwa mwanaume atamtamani mwanamke pia?

4. Agano Jipya: wake wanapaswa kuwatii waume wao na waume kuwapenda wake wao kama Kristo alivyolipenda kanisa kwenye Waefeso 5:22-33. Kwenye 1 Timotheo 2:11-14 Biblia hata inasema kuwa wanawake wasifundishe au kuwa na mamlaka juu ya wanaume kwa sababu Hawa ndiye aliyedanganywa.

5. Maovu katika historia: Wanaume wamekuwa wakiwatawala wanawake kwa njia za unyonyaji na zisizofaa pia. Wakati mfalme wa kisumerian au kichina alipokufa, wake zake waliuawa naye mara kwa mara. Kabla ya Waingereza kuja, mwanaume wa kihindu alipokufa, mke wake alichomwa akiwa hai kwenye mazishi ya mumewe (yaliyoitwa suttee). Wagiriki hawakuwachukulia wanawake vema zaidi kuliko Waarabu na Waiskam: mtu alipopewa mwanamke, mtumwa, au mnyama, alishika kichwa chake na kuomba kwa Mungu. Ibn-i-Majah juzuu ya 3 na.1918, uk.157. Kwa mujibu wa sharie za kiislam (Sharia), ushahidi wa mwanamke ulikuwa sawa na nusu ya ushahidi wa mwanaume, "kwa sababu ya ufanisi wa mawazo ya mwanamke." (Bukhari juzuu ya 3 na.826, uk.502).

 

S: Kwenye Mwa 3:16, je mwanamke atakuwa na maumivu makubwa wakati wa kuzaa mtoto, au kuzaa watoto ni baraka kama Mwa 1:28 inavyosema?

J: Yote ni kweli. Mambo matatu ya kuzingatia kwenye jibu la swali hili.

Kabla ya anguko la Adam na Hawa, kuzaa mtoto kulikuwa baraka bila ya maumivu yoyote ya kimwili wala kihisia.

Baada ya anguko, Mwa 3:16 inasema kutakuwa na maumivu ya kimwili. Pia kutakuwa na maumivu ambayo watoto wataleta kwa sababu a dhambi zao. Kuna uwezekano mkubwa sana kuwa maumivu ni mchakato mzima wa kulea watoto hadi wanapkuwa watu wazima. Uchungu ambao Hawa aliupata wakati wa kuwazaa Kaini na Abeli utakuwa mdogo kuliko uchungu wa kujua kuwa Kaini kamuua Abeli.

Hata hivyo, baraka haijaondolewa kabisa. Watoto bado ni baraka toka kwa Bwana (Zaburi 127:3-5).

 

S: Kwenye Mwa 3:16, kwa nini lawama zote zilielekezwa kwa Hawa? (Muslam mmoja amedai hivi)

J: Si kila lawama ilielekezwa kwa Hawa. Ingawa Hawa alikula kwanza, na Hawa aliadhibiwa, Adam naye pia aliadhibiwa. Alitakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kupata kitu ambacho hapo awali kilikuja kiurahisi kabisa.

Kwenye thiolojia ya Biblia hakuna kidokezo chochote cha Hawa kuumbwa akiwa "mjinga zaidi." Lakini kwa kuwa Muislam ameleta hoja hii, mwana historia na thiolojia wa kale wa kiislam al-Tabari alisema kuwa Hawa alikuwa na akili mwanzoni, Allah alimfanya (lakini siyo Adam) mjinga baada ya anguko la Adam na Hawa (al-Tabari juzuu ya 1, uk.280, 281). Pia Muhammad alisema kwenye Hadithi kuwa mkojo wa mtoto wa kiume ni msafi zaidi ya ule wa mtoto wa kike. Ibn-i-Majah juzuu ya 1 na.522, 525, 526, uk.284, 285, 286. Sababu ni kwamba: "(Nabii) alisema, ‘Hakika, Allah aliyetukuka alimuumba Adam na Hawa (Hawwa') aliumbwa toka kwenye ubavu wake mdogo. Kwa hiyo, mkojo wa mvulana mdogo ulitoka kwenye maji na udongo mfinyanzi na mkojo wa msichano mdogo ulitoka kwenye nyama na damu.'" Kumbuka kuwa jambo hili halitokani na kitu chochote kinachohusiana na anguko, lakini na kuumbwa kwa Hawa.

 

S: Kwenye Mwanzo 3:20, pamoja na tofauti zote walizonazo, inawezekanaje watu wa rangi zote watokane na Adam na Hawa?

J: Mwanzo 3:20 inasema Hawa atakuwa mama wa wote wenye uhai. Urefu, rangi ya nywele na ngozi ni tofauti ndogo, si tu kwa watu, bali pia kwa mbwa, paka, na farasi. Kwa kuangalia ainasafu, wanadamu wote wanafanana sana. Uchunguzi wa ainasafu wa aina 67 za mbwa uliotolewa kwenye toleo la Juni 1997 la Science unaonyesha kuwa mbwa wote walikuwa na chanzo kimoja pia.

Aya nyingine zenye kuthibitisha kuwa watu wote wametoka kwa Adam na Hawa ni Mathayo 19:4-5; Warumi 5:12-19 na 1 Timotheo 2:13-14.

 

S: Kwenye Mwa 3:20, kama Adam na Hawa hawangetenda dhambi je wangekuwa bado wanaweza kupata watoto? (mke wangu ameuliza swali hili)

J: Ndiyo. Hatujui Adam na Hawa walikuwa na umri gani wakati walipofanya dhambi; inaweza kuwa walikuwa watoto wadogo, matineja, au watu wazima. Kutokuwepo kwa watoto kabla ya anguko hakumaanishi kuwa Mungu aliwaumba bila uwezo wa kupata watoto isipokuwa tu wamefanya dhambi.

Maandiko mawili tofauti yanathibitisha kuwa wangeweza kupata watoto, hata kama anguko lisingitokea.

Kwenye Mwanzo 1:28, kabla ya anguko, Mungu aliwaamuru kuzaa na kungezeka. Isipokuwa tu Mungu alikuwa anaongelea hisabati, aliwaamuru kupata watoto.

Kwenye Mwanzo 3:16, Hawa alilaaniwa kwa kuongezewa maumivu wakati wa kuzaa. Alilaaniwa na ongezeko la maumivu au huzuni wakati wa kuzaa, siyo kuzaa kwenyewe.

 

S: Kwenye Mwanzo 3:21, kwa nini Mungu aliwavisha Adam na Hawa ngozi za wanyama?

J: Maandiko hayasemi moja kwa moja, lakini tunaweza kuona kafara hii ya kwanza ya wanyama kuwa ishara kwamba Mungu atatumia kafara ya kiumbe hai kama kifuniko cha dhambi zetu.

 

S: Kwenye Mwanzo 3:21 kwa nini Mungu "alihitaji" mavumbi ya ardhini kumuumba Adam, na ubavu kumuumba Hawa kama Born Again Skeptic's uk.192 inavyosema?

J: Biblia inasema Mungu alichagua kutumia hivyo, lakini haisemi kuwa Mungu litakiwa kutumia mavumbi na chembe toka kwenye ubavu. Mungu anaweza kutumia kitu chochote anacotaka.

 

S: Kwenye Mwanzo 4:3-6, kwa nini Mungu aliikataa sadaka ya Kaini?

J: Wycliffe Bible Commentary uk.284 inasema kwamba ingawa Abeli anaweza kuwa alitoa sehemu bora zaidi ya alivyonavyo na Kaini hakufanya hivyo, hakuna kitu chochote chenye kuonyesha hivyo kwenye Mwanzo.

Waebrania 11:4 inasema kuwa Abeli alitoa kwa imani. Licha ya kuwa na fikara mbaya moyoni mwake (kama ambavyo matendo yake yaliyofuata yanavyoonyesha), inawezekana pia kuwa Mungu alitaka kafara ya damu, si mimea, kama ishara ya kifo cha Yesu.

Hii huenda ikawa ndio tofauti kati ya ibada ya kweli ya Abeli na ibada ya kidesturi ya Kaini. Sadaka ya Abeli ya "sehemu zilizonona" za "wazaliwa wa kwanza" zilikuwa ni sehemu nzuri zaidi za wazaliwa wa kwanza. Kaini alileta mazao "kiasi", sio mazao ya kwanza.

 

S: Kwenye Mwanzo 4:10, damu ya Abeli iliwezaje kulia?

J: Hii ni sitiari ya dhuluma dhidi ya Abeli na hatia ya Kaini. Kuchukua maana iliyo wazi ya Biblia kunamaanisha kuisoma kama waandishi walivyokusudia. Kutokutambua sitiari na istiari kwenye Biblia kunaitwa kuichukua Biblia kwa uwazi uliovuka mipaka. Tazama utangulizi kwa maelezo zaidi ya uwazi unaovuka mipaka dhidi ya kuichukua Biblia kama ilivyokusudiwa, na kama Yesu alivyoichukulia.

 

S: Kwenye Mwanzo 4:12, kwa nini Kaini hakuuawa kwa kuua? (mke wangu aliuliza swali hili)

J: Adhabu ya kifo iliamriwa kwenye Agano la Kale, siyo tu kwenye Amri Kumi, bali mara baada ya mafuriko ya Mwanzo 9:5-6. Hata hivyo, mambo haya yote yapo baada ya muda wa Kaini na Abeli. Mbali ya hapo, Mungu anajua mazingira yote, na Mungu Mwenyewe hazuiliwi na sheria kwa ajili yetu.

Wakati ule ambao Kaini alikuwa hajaambiwa lolote kuhusu sheria ya kuuawa kwa muuaji, na Mungu alimshughulikia kwa kumtoa toka kwenye udongo.

 

S: Kwenye Mwanzo 4:13, kwa nini Kaini alifikiri kuwa mtu yoyote atakayemwona atapenda kumuua?

J: Inafurahisha sana kwamba Biblia haisemi kuwa Mungu au mtu mwingine yoyote alimwambi Kaini jambo hili. Kwa sababu maovu mengi ikiwa ni pamoja na mauaji, watu wana dhamira ndani yao inayowaambia kuwa jambo hili ni ovu. Kaini anaweza kuwa alijiuliza kuwa kama alimuua binadamu mwenzake, ambaye aliumbwa kwa mfano wa Mungu, itakuwa haki kwake kuuawa pia. Kwenye Mwanzo 4:15, Mungu anaonekana kuthibitisha fikra hii, na ndio maana alichukua tahadhari ya ziada kwa kumwekea alama Kaini, ili watu wajue na wasimuue.

Mchezo wa kuigiza wa kwenye video uitwao Growing Kids God's Way, uliotungwa na Gary na Anne Marie Ezzo, onyesho la 6, una mafundisho mazuru sana kuhusu dhamira ya mwanadamu.

 

S: Kwenye Mwanzo 4:13-16, alama ambayo Mungu aliiweka kwa Kaini ilikuwa ni nini?

J: Maandiko hayasemi kitu chochote, isipokuwa kwamba ilikuwa kitu ambacho watu wengine wangeweza kukutambua. Hata hivyo, Today's Handbook for Solving Bible Difficulties uk.202-203 inasema kuwa alama hii haikuwa sehemu ya laana ya Kaini. Badala yake, ilikuwa neema ya Mungu kwa kumpa Kaini alama ili kwamba watu wengine wajue na wasimuue.

 

S: Kwenye Mwanzo 4:13, je kulikuwa na mtu yoyote duniani mbali ya Adam na Hawa na Kaini?

J: Jambo hili haliongelei tu mabinti ambao wangeweza kuwepo na ambao miongoni mwao Kaini alimpata mke wake, lakini pia watu waliozaliwa baada ya mauaji. Ingawa watu wote walitokea kwa Adam na Hawa (Mwanzo 3:20; Matendo 17:26; Warumi 5:14-15), Adam na Hawa walikuwa na watoto wengine wavulana kwa wasichana, kwa mujibu wa Mwanzo 5:4.

 

S: Kwenye Mwanzo 4:16-22, watoto wa Adam na Hawa walipata wapi wake? Je ndoa za maharimu haijazuiliwa?

J: Mwanzo 5:4 inasema kuwa Adam na Hawa walikuwa na watoto wengine wavulana na wasichana. Ndoa za maharimu hazikuwa zimezuiliwa wakati ule: kama jeni zetu zisingekuwa na hitilafu, uharimu usingeleta magonjwa ya kijeni kama unavyofanya leo.

 

S: Kwenye Mwanzo 4:16-17, Kaini alimpataje mke toka kwenye nchi ya Nod?

J: Kuna mambo mawili ya kuyazingatia katika kujibu swali hili.

1. Hata kudhania kuwa Kaini alipata mke toka kwenye nchi ya Nodi, bado atakuwa ni mzao wa Adam na Hawa, kwa sababu watu wote wametoka kwa Adam (Matendo 17:26) na Hawa alikuwa mama wa wote weny uhai (Mwanzo 3:20).

2. Biblia haijasema kuwa Kaini hakumpata mke wake Nodi. Kaini anaweza pia kuwa aliishaoa, na mke wake alisafiri pamoja naye kuelekea Nodi.

 

S: Kwenye Mwanzo 4:17-24, je hii ni orodha ya vizazi vya Adam, au Mwanzo 4:25-32 ndiyo orodha ya vizazi vya Adam? (Mtu mwenye fikra kuwa maoni yaliyotoka kwa waumini wa kale hayana uhakika alileta hoja hii kama neno kikoa likionyesha watunzi wengi wa Kitabu cha Mwanzo)

J: Mwanzo 4:17-24 ni orodha ya vizazi vya Kaini, ambamo Seth haelezewi. Mara baada ya hii, Mwanzo 4:25-5:32 inatoa orodha ya vizazi vya Seth ambayo haimwelezei Kaini. Hakuna kuingiliana au maneno kikoa hapa.

Kama hii haieleweki vizuri, unaweza kuangalia kwenye mfano wa pili. Kwenye 1 Nyakati 5:1-10 kumetolewa orodha ya vizazi vya Rubeni, mmoja wa watoto wa Yakobo. Mara baabda ya hiyo, 1 Nyakati 5:11-22 ni orodha ya vizazi vya Gadi, mtoto mwingine wa Yakobo.

 

S: Kwenye Mwanzo 4:22, metali ziliwezaje kutumika mapema kiasi hicho?

J: Shaba (nyeusi) imekutwa: Thailand–4500 KK, Yugoslavia–4000 KK, Ugiriki–3000, na Anatolia–kabla ya mwaka 3000 KK. Wamisri walitumia chuma iliyotoka kwenye mawe yaliyotokana na nyota kama urembo na visu vya kupigania kabla ya mwaka 3000 KK.Pia kwenye jiji la Eshnunna, karibu na Babeli, wataalamu wa elimukale waliugundua wembe wa chuma toka mwaka 2700 KK.

 

S: Kwenye Mwanzo 4:22, je jina la "Tubal-Cain" linahusiana na ukanda wa "Tubal" kwenye Uturuki ya sasa?

J: Ingawa haiwezi kuthibitishwa kwa yoyote kati ya hizo mbili, kuna uwezekano kuwa havihusiani. Tubal lilikuwa pia ni jina la Yafeti, na watu watu wa Tubal wana uwezekano wa kuhusiana naye. Watu wa "Tubal" walielezwa kwenye kumbukumbu za kiassyria wakati wa Shalmaneser III (mwaka 859-824 KK na Sargon karibu mwaka 732 KK.

 

S: Kwenye Mwanzo 4:23-24, kwa nini mtu mmoja alimjeruhi Lameki?

J: Hisia tatu kuhusiana na mtu huyo ni:

Wazo la ujanja alikuwa anafanya jambo jema kwa kuwaua wazao wa Kaini. Lakini, Mungu alionyesha wazi kabisa kuwa mtu yoyote asimlipize kisasi Kaini kwenye Mwanzo 4:15, kwa hiyo wasiwalipize kisasi hata watoto wake.

Kisingizio kwa mnyang'anyi kujaribu kuchukua mali za Lameki kilikuwa Lameki alikuwa mzao wa Kaini.

Haikujalishi Lameki alikuwa mzao wa nani; huyu mtu alitaka kumpora na kumuua Lameki tu.

Hata hivyo, Maandiko hayaweki umuhimu kwenye sababu ya huyu mtu kujaribu kumjeruhi Lameki. Wazo la Mwanzo 4:23-24 lilikuwa kuonesha kuwa baada ya mauaji ya kwanza, Kaini na wazao wake waliishi kwa uadui na watu wengine.

 

S: Kwenye Mwanzo 4:23-24, je mtu akliyemjeruhi Lameki alikuwa wa uzao upi, na Sethi alizaliwa lini?

J: Maandiko hayasemi, kwa hiyo kuna vitu vitatu ambavyo vinawezakana.

Abeli alikuwa na watoto kabla hajauawa.

Sethi alikuwa mhenga wake. Hakuna kitu kisemacho kuwa Mwanzo 4:23-24 ilitokea kabla ya Mwanzo 4:25-26.

Kaini alikuwa mhenga wa kijana.

 

S: Kwenye Mwanzo 5, je "miaka" inaweza kuwa miezi?

J: Hapana. Kama ingekuwa hivyo, basi Henoko angekuwa na miezi 65 tu (miaka 6 ½) alipomzaa Methuselah! Tazama 1001 Bible Questions Answered uk.323 kwa jibu kama hili hili.

 

S: Kwenye Mwanzo 5, je kitabu cha Mwanzo kinachukulia kuwa kila mtu alingea kebrania kabla ya Abraham (kuzaliwa)?

J: Hapana, ni kinyume cha hapo. Mwanzo 11 inasema kuwa baada ya mafuriko watu tofauti walizungumza lugha ambazo hazikuweza kueleweka. Abraham mwenyewe huenda hakuongea kiebrania. Alitoka Ur, mji wa Sumeria. Kisumeria kilifanana na kiebrania, kwa sababu kiebrania kilitokana na kisumeria na kilikuwa na athari kubwa ya Waaremi.

Wataalam wa lugha isiyokuwa ya kidini wanaamin kuwa nyingi za lugha za magharibi, ikiwa pamoja na kisanskrit cha India, zilkuwa na chanzo kimoja karibu mwaka 4000 KK.

 

S: Kwenye Mwanzo 5:3-29, majina yote haya yanamaanisha nini katika kiebrania?

J: Zifuatazo ni maana zake, kwa kutumia etimolojia (asili na historia ya maneno) iliyochukuliwa kutoka Strong's Concordance na nyakati nyingine, maelezo ya kitabu cha Mwanzo kuhusu maana ya neno.

Adam - mtu/binadam. Strong's Concordance inasema nyekundu, au binadamu. Mwanzo 2:23 inaonyesha kuwa Adam = binadam.

Sethi - iliyo wekwa/teuliwa/wekwa badala ya. Mwanzo 4:25 inasema Hawa alimwita jina lake Sethi kwa sababu Mungu aliteua mahali pengine pa Abeli.

Enoshi - yenye ukomo. Jina, kama "Adam" linamaanisha "binadam."

Kaini/Kenan - imetulia sehemu moja (kama kiota au makazi)

Mahalaleel - Msifu Mungu, Msifu Mungu.

Yared - nasaba

Henoko - Aliyeingizwa katika kundi, wekwa wakfu, funzwa

Methuselah - mtu wa kigumba (dart)

Lameki - toka kwenye chanzo kisichotumika cha maana isiyokuwa na uhakika.

Nuhu - Strong's Concordance inasema pumziko, na Mwanzo 5:26 inasema faraja, ambayo inafanana sana.

Irad - mkimbizi

Ham - moto

Shem - jina?

Yafethi - kutanuka. Kwa mujibu wa Wagiriki wa zama za kabla ya ukristo, Japetos alikuwa mhenga wao.

Jambo moja tunaloweza kujifunxa toka kwa Japetos, ni kwamba si kila jina lenye etimolojia au maana iliyo muhimu

.

Jambo la pili tunaloweza kujifunza toka kwa Sethi na Nuhu ni kwamba maana ya baadhi ya majina ni muhimu.

 

S: Kwenye Mwanzo 5:21-27, kuna sababu yoyyote ya kumfanya Methuselah awe binadamu mwenye umri mkubwa zaidi kwenye Biblia?

J: Huenda. Mafuriko yalitokea mwaka ambao Methuselah alikufa. Huenda hii ilikuwa ishara ya rehema za Mungu katika kuchelewesha mafuriko kwa kumpa Methuselah maisha marefu.

 

S: Kwenye Mwanzo 5:24, kwa nini alimchukua Henoko, mtu mwenye kumcha Mungu?

J: Huenda ni kwa sababu hiyohiyo tunayo peleka maua mazuri kwenye nyumba zetu. Siyo lazima kuwa Henoko alikufa; Mungu alimchukua Henoko na kumpeleka mbinguni ili awe naye, sawa na Elia kwenye 2 Wafalme 2:11-12. Kielelezo kingine kilikuwa kwamba kama marafiki wazuri Henoko na Mungu walikwenda kutembea, saa zilikuwa zimeenda, na Mungu alisema, kwa kuwa upo karibu na nyumba yangu kuliko yako kwa nini usije kwenye nyumba yangu sasa. Lakini Mungu huwafanya wengi wa watumishi wake wafe ili waweze kwenda mbinguni. Jambo hili si halimaanishi kuwa Mungu amewapuuzia, lakini Zaburi 116:15 inasema "Ina thamani machoni pa Bwana mauti ya wacha Mungu wake."

 

S: Kwenye Mwanzo 6, kwa nini mafuriko ya Nuhu yanafanana na taarifa nyingine?

J: Yatafanana endapo yamerekodi tukio moja. Taarifa ya Babeli inafanana kwenye undani wa habari lakini ni tofauti sana kwenye sababu zilizotolewa. Kwa mujibu wa taarifa hii, miungu ilimwangamiza binadamu kwa sababu alipiga kelele nyingi sana, lakini baadaye walijutia jambo hili na wakakusanyika huku wakiwa na njaa kali kuzunguka kafara za "Nuhu."

Kufanana kwa pekee Biblia ni pale inaposema Nuhu alikuwa na watoto watatu Ham, Shem na Yafethi. Institutes of Manu ya Arya inasema Satyaurata alinusurika kwenye mafuriko pamoja na watoto watatu: Jyapeta, Sharma, na C'harma. Mwandishi wa Kigiriki Aristophanes anarekodi kuwa Japetos (Iepetus Mtita) alikuwa mhenga wa Wagiriki. Huu wote ni ushahidi unaothibitisha tukio moja.

 

S: Je Mwanzo 6:3 inamaanisha kuwa Roho wa Mungu anaweza kumuacha mtu na kutokurudi tena?

J: Hapana. Mwanzo 6:3 inasema kwamba roho iliyopewa na Mungu itauacha mwili wa mtu baada ya miaka 120.

 

S: Je Mwanzo 6:3 inamaanisha kuwa urefu waa maisha ya mtu utakuwa miaka 120 tu, au kwamba kutakuwa na miaka 120 ya neema kabla ya mafuriko?

J: Inaweza kuwa namna yoyote kati ya hizo mbili, kwa sababu hakuna ushahidi dhidi ya maoni yoyote kati ya hayo. Inawezekana kuwa namna yoyote ile kwa mujibu wa maelezo ya baadhi ya waandishi. Watu wengine wanapendelea iwe urefu wa maisha ya binadamu.

 

S: Kwenye Mwanzo 6:3, je Mungu aliweka urefu wa maisha kuwa miaka 120, au 70 hadi 80 tu kama Zaburi 90:19 inavyosema?

J: Baadhi ya mambo ni vigumu kuelewa hadi utakapoona kwamba Mungu ana uhuru wa kuweka kanuni tofauti kwa nyakati tofauti. Urefu wa maisha wa wastani wa watu umebadilika. Mungu aliweka wastani wa urefu wa maisha wa miaka 120 kabla ya mafuriko. Miaka mingi baadaye, Zaburi 90:10 inaonyesha kwamba ilifupishwa. Inasemekana kwamba mtu ataishi miaka 70, 80 kama ana nguvu. Mpango wa urefu wa maisha uliotolewa kwenye kitabu cha Mwanzo unapungua kwa kipe husisho.

Wanasayansi hawana uhakika wa jinsi kuzeeka kunavyotokea: vijiumbe maradhi havizeeki. Wakati kuondoa kundi la methyl toka kwenye DNA kunaweza kuwa ni jinsi moja ya kutenda, inaonekana kuwa namna inayotumika zaidi ni kufupisha ncha ya DNA. Kila mara DNA kwenye chembe ya mnyama inapojigawa baadhi ya miisho yake hufupishwa. Sasa kuna vitu vya nje kwenye miisho, na vijiumbe maradhi vina kimeng'enya, telomerase, zinazorejesha miisho. Hata hivyo, telomerase haielekei kurejesha miisho ya DNA za wanyama.

 

S: Kwenye Mwanzo 6:3, jambo hili linafanaje na wataalam wa mambo ya kale wanaosema kuwa watu wa zamani waliishi maisha mafupi?

J: Kuna baadhi ya dosari katika madai haya ya usayansi unaojifanya kuwa sayansi.

1. Kumbuka kuwa hawajawahi kusema msingi wanaotumia udai kuwa watu walikuwa na urefu mdogo wa maisha.

2. Hawatoi ushahidi wowote kwamba wana sampuli kielelezo iliyo kweli kitakwimu na isiyo na upendeleo. Kwa mfano, mtaalam wa baadaye wa kubuniwa wa mambo ya zamani, karne kadhaa kuanzia sasa, anaweza kuchimba mabaki toka kwenye zahanati za kutoa mimba, na "kuthibitisha" kwamba urefu wetu wa wastani wa maisha ulikuwa chini ya mwaka mmoja. "Ushahidi" huu pia utakuwa na upendeleo kitakwimu.

3. Makadirio ya urefu wa maisha yanapaswa kuelez endapo yanahusisha au hayahusishi vifo vya watoto. Kwa mfano, katika miaka ya 1970, urefu wa maisha katika nchi nyingi za afrika ya kati ulikuwa chini ya miaka 30. Hata hivyo, kama ukienda kwenye nchi mojawapo, bado utawaona watu watu wengi wazee. Kama kungekuwa na nchi kubuni, ambayo kila mtoto anayeanza kutembea aliishi na kufikisha miaka 60, lakini theluthi mbili (2/3) ya watoto wote walikufa, wastani wa urefu wa maisha utakuwa miaka 20 tu.

S: Kwenye Mwanzo 6:3, kwa kuwa Mungu hakuweza kuwa mwili, ni jinsi gani Yesu alkuja duniani? (Mtu asiyeamini kuwa Mungu yuko aliuliza swali hili)

J: Mwanzo 6:3 haisemi kitu kama hiki. Inasema tu kuwa wanadamu ni mwili kweli. Sasa ni kweli kwamba Mungu ni Roho, na Yesu alijifanya kuwa hana utukufu na kuja duniani katika mwili, lakini Mwanzo 6:3 yenyewe haithibitishi au kukanusha chochote kuhusu Mungu kuja katika mwili.

 

S: Kwenye Mwanzo 6:2, 4-5, Wanefili au "wana wa Mungu" ni watu gani ?

J: Unefili maana yake watu waliwaita "wana wa Mungu" na zifuatazo ni baadhi ya nadharia.

Uzao wa kiungu wa Sethi, au waamini ambao walifanya dhambi kwa kuwaoa watu wasioamini kutoka kwa Kaini. Kitabu kiitwacho 1001 Bible Questions Answered uk.65, 348 kinaunga mkono wazo hili na kusema kuwa huu ulikuwa mtazamo wa Scofield. Mtazamo huu ulianzia zamani za Julius Africanus aliyeandiaka mwaka 232-245 BK, kwenye Ante-Nicene Fathers juzuu ya 6 kipande cha 2, uk.131.

Wafalme wenye nguvu ni tafsiri ya Kiaremi ya Targumi.

Mbari nyingine kama vile Neanderthals au pengine Homo erectus.

Waliondelea kiteknolojia: Mwandishi mmoja alidhani kuwa Wisraeli waliwaita majitu kwa sababu ya kuta zao ndefu na silaha zao za teknolojia ya juu.

Watoto wa wanawake na wanaume waliopagawa mapepo.

Baadhi ya mapepo yanaweza kuzaa na wanadamu viumbe wengine interbreed ilikuwa ni imani ya Wayahudi Philo, Josephus (kabla ya mwaka 100 BK), na mwandishi wa 1 Enoch sura ya 6. Wakristo ambao wamefundisha jambo hili ni pamoja na Second Apology of Justin Martyr sura ya 5, uk.190, On the Veiling of Virgins sura ya 7, uk.32, The Instructions of Commodianus (karibu mwaka 240 BK) sura ya 3, uk.203, na Ambrose (karibu mwaka 378 BK).

   Hili huenda likawa ni jaribio la Shetani kwa kubadilisha jeni zetu. Hata hivyo, kama pepo anaweza kuzaa na mwanadamu ni jinsi gani Yesu anaweza kuleta nusu upatanisho kwa viumbe ambao ni nusu-watu, nusu-mapepo? Hank Hanegraff alieleza hili kwenye mahubiri mazuri sana kwa njia ya redio, the Bible Answer Man 10/29/97.

 

S: Kwenye Mwanzo 6:6, Mungu anatubuje?

J: Neno hili linaweza kutafsiriwa pia kama "kuhuzunishwa." Mungu huonyesha hisia zake nyakati zingine matukio yanapotokea.

 

S: Kwenye Mwanzo 6:9, Nuhu alikuwaje mkamilifu katika kizazi chake?

J: Hakuna kitu chenye kuonyesha kuwa ukamilifu hapa inamaanisha kutokuwa na dhambi kabisa. Badala yake, neno la Kiebrania linamaanisha "kulingana na kiwango, na wazo awali inaweza kuwa kunyooka. Neno hilohilo, likiwa na alama tofauti za vokali, limetumika katika Mambo ya Walawi 19:15 kumhukumu jirani yako kwa haki."

 

S: Kwenye Mwanzo 6:12, kwa kuwa wote walipotoka katika njia zao, Nuhu aliwezaje kuwa mkamilifu kwenye Mwanzo 6:9 na 7:1?

J: Muktadha inaonyesha wazi kabisa kwamba "wote" inamaanisha isipokuwa Nuhu na familia yake. Kumbuka kuwa Lameki, baba yake Nuhu, pia alikufa katika mwaka wa mafuriko.

 

S: Kwenye Mwanzo 6:13 na 7:1, Nuhu aliwezaje kuju kuwa Mungu alikuwa anaongea naye, kwa kuwa hakuwahi kumwonw Mungu?

J: Mara nyingi, watu wanaokuwa na miaka mingi ya uhusiano na Mungu wanajua Mungu anaposema nao. Angalia 1 Wafalme 19:11-13 kwa mfano mwingine.

   Onyo pekee ambalo watu walikuwa nalo kuhusu gharika alikuwa ni Nuhuwatu walikuwa alikuwa Nuhu, mtu mwenye ujasiri na dhamira ya kujenga safina jangwani. Kutokana na mtazamo wa Nuhu, angeweza kuwa ama shujaa mkubwa zaidi au mpumbavu mkubwa zaidi ambaye kizazi chake kimewahi kumuona. Hivi ndivyo imani kubwa kwa Mungu inavyokuwa. (Mahubiri ya Bill Counts 11/5/2005).

 

S: Kwenye Mwanzo 6:14, Nuhu angewezaja kujenga safina kubwa namna hii?

J: Alikuwa na miaka 100 ya kuijenga yeye pamoja na watoto wake watatu. Safina ilikuwa karibu futi 450 urefu, futi 75 upana, futi 45 kimo. Ilikuwa na eneo la futi mraba 101,250. Kitu chenye urefu wa futi 10 kwa 15 kwa 6 2 / 3 kina futi za ujazo 1,000. Meli ya Malkia Elizabeth 2 ina urefu wa futi 963 na upana wa futi 105.

 

S: Kwenye Mwanzo 6:14, tunajuaje kuwa dhiraa ni inchi 17.5?

J: Kwa mujibu wa Today's Handbook for Solving Bible Difficulties uk.215-216, wakati Mfalme Hezekia alipujenga mfereji wa Siloamu karibu mwaka 700 KK, wafanyakazi wake waliuchonga ili uwe na urefu wa dhiraa 1,200. Kwa kuugawa urefu katika inchi kwa dhiraa 1200 kunatupa karibu inchi 17.5 kwa dhiraa. Dhiraa katika wakati wa Musa ingeweza kuwa kubwa zaidi au ndogo zaidi. Jambo hilo lingeifanya safina kubwa zaidi au dogo zaidi.

 

S: Kwenya Mwanzo 6:14 safina iliwezaje kusalimika kwenye mafuriko ya Nuhu?

J: Kuna walau sababu tatu.

Mbao za mvinje zinaweza kuwa aina ngumu ya mbao, lakini inaweza kuwa mbao iliyotiwa dawa maalum pia. Mbao nzito ni chaguo zuri kwa sababu linatoa fursa ya mawazo mapya.

Umbo lilifaa kweny mikikimikiki ya maji (1:1.67:10).

Mungu angeweza, bila shaka, kuilinda safina kwa kadri ilivyohitajika.

 

S: Kwenye Mwanzo 6:19, Je Nuhu alikuwa aweke wanyama wawili kwa kila aina au wanyama saba kwa kila wanyama safi kama Mwanzo 7:2 inavyosema?

J: Yote mawili. Nuhu alitakiwa kuleta wanyama kwa kila aina, na pamoja na hao wanyama saba kwa kila aina safi. Mwanzo 6:19 inasema "wawili" haisemi, "si zaidi ya wawili." Wanyama wa ziada walikuwa kwa ajili ya chakula na sadaka kwenye Mwanzo 8:20. Huku si kukosa usahihi kwa upande wa Biblia bali ni mfano wa njia ya Mungu ya kutufundisha. Mungu huhakikisha kuwa tumeelewa dhana ya jumla "wawili kujazia tena" ,na kisha anaongeza dhana ya pili "saba zaidi wa sadaka." Ni sawa na wanafunzi wanapojifunza hesabu. Kwanza wanajifunza kutoa namba ndogo kutoka kwenye namba kubwa. Baadaye wanajifunza kuhusu namba hasi na kwamba unaweza kutoa namba kubwa kutoka kwenye namba ndogo.

 

S: Je Mwanzo 6:19-20 inatoka kwenye chanzo cha "kikuhani (Priestly)" cha karibu mwaka 450 KK, na Mwanzo 7:2-3 inatoka kwenye chanzo cha "Kiyahwe (Yahwistic)" cha karibu mwaka 850 KK?

J: Hakuna ushahidi kwamba kulikuwa na maelezo mawili tofauti, isipokuwa kwa tukio lililotokea mara mbili. Hata hivyo, marudio ni mbinu ya kiandhishi ya kukazia wazo. Wakati ule, hawakuwa na mithali ya kisasa, "Waambie kitu unachokwenda kuwaambia, waambie, na kisha uwaambie kitu ulichowaambia", lakini walifahamu kwa hakika nguvu ya kurudia, kama ambavyo hata kutazama kwa ufupi kwenye Zaburi na Mithali kunavyoonyesha.

Ni vigumu kwa wanazuoni wanaopinga mtazamo wa asilia wa kanisa kusema hadithi ya gharika ya Nuhu iliandikwa ama mwaka 850 KK au mwaka 450 KK, kwa kuwa Gilgamesh Epic ya Kisumeria ina maelezo kadhaa yanayofanana kuhusu mafuriko ya duniani yote, na iliandikwa kabla ya mwaka 2500 KK (Nakala Kibabeli ya Jedwali la 11 la shairi lenye majedwali 12 lilikuwa katika jumba la Ashurbanipal huko Ninawi. Picha yake iko kwenye Wycliffe Bible Dictionary uk.6126).

Hata hivyo, kuitendea haki nadharia ya JEPD ya wanazuoni wanaopinga msimamo wa asili wa kanisa kwamba gharika ya Nuhu ilitoka kwenye vyanzo viwili ilianza karne ya kumi na tisa, kabla ya Gilgamesh Epic haijajulikana kwenye ulimwengu wa kisasa. Sababu pekee swali hili linaongelewa kwenye kazi hii ni kuwa kuna "Wakristo" kdhaa wenye kupenda fikra mpya wanaoamini nadharia ya JEDP.

 

S: Kwenye Mwanzo 7:1, je watu wengine "hawakuwa na nafasi" ya kutubu kama watu wasioamini uwepo wa Mungu wanavyodai?

J: Hapana, karne moja ni muda wa kutosha kutubu. Walipoona safina inajengwa, wangeweza kumsikiliza Nuhu, "mhubiri wa haki" (1 Petro 3:20). Ilichukua miaka 100 kujenga safina, na miaka zaidi ya mia ni muda wa kutosha kupata nafasi ya kutubu. Pengine hii ni moja ya sababu 1 Petro 3:20 inasema Mungu alikuwa akisubiri kwa uvumilivu wakati safina ilipokuwa inajengwa.

 

S: Kwenye Mwanzo 7:2, je Nuhu aliwezaje kujua namna ya kuwachukua wanyama wasafi, kwa kuwa bado hapakuwa na sheria ya Agano la Kale?

A: Nuhu hawakuwa na Maandiko ya Agano la Kale; bali Nuhu aliongea na Mungu mwenyewe. Ingawa hatujui hasa ni kiasi gani Mungu alimfundisha Nuhu kuhusu vitu vitakavyokuwemo kwenye sheria ya Musa, Mungu mwenyewe alijua, na alikuwa na uwezo wa kumweleza Nuhu wanyama gani achukue saba.

Katika maongezi haya ya mtu-na-mtu na Nuhu, hatujui kama Mungu alitumia ufafanuzi wa (wanyama) safi unaofanana na ule ulio kwenye sheria ya Musa. Vyovyote ilivyokuwa, Nuhu aliambiwa wanyama gani wa kuchukua.

Kuna somo kwa ajili yetu katika swali hili. Wakati wowote Mungu anapotuambia kufanya kitu huwa hatujui undani wa kila kila jambo. Tunaweza kuahirisha au kutii kile tu ambacho tunakijua, na kumtumaini Mungu kuturekebisha inapobidi huku tukimtii. Kama tutasubiri hadi tutakapojua undani kila kitu, tunaweza kushinda kabisa kutii.

 

S: Kwenye Mwanzo 7:4 - 8:12, kuna jambo lisilokuwa la kawaida kuhusu muundo wa fasihi hapa?

J: Hii inaitwa chiasm, ambayo ni ya kawaida kwenye kazi za Kiyahudi, si kazi za Kigiriki wala za kisasa, ambamo kila usemi (isipokuwa wakati mwingine wa kati) ina usemi ambao ni kioo cha ulinganifu. Ufuatao ni muundo

7:4 - siku 7 za kusubiri gharika

7:10 - - siku 7 za kusubiri gharika

7:17a - - - siku 40 za gharika

7:24 - - - - siku 150 za kupanda kwa kina cha maji

8:3 - - - - siku 150 za kushuka kwa kina cha maji

8:6 - - - siku 40 za kusubiri

8:10 - - siku 7 za kusubiri

8:12 - siku 7 za kusubiri

 

Pamoja na hayo, Mwanzo 7:21-23a ni chiasm ndani ya chiasm hii.

- Wote wenye mwili wanakufa

- - Ndege

- - - Wanyama wa kufugwa na wanyama pori

- - - - Viumbe vitambaavyo

- - - - - Binadamu

- - - - - - Kila kitu kwenye nchi kavu

- - - - - - Viumbe hai vyote juu ya uso wa nchi

- - - - - Binadamu

- - - - Wanyama

- - - Viumbe vitambaavyo

- - Ndege wa angani

Waliangamia wote

S: Kwenye Mwanzo 7:12, 24, je gharika ilidumu siku 40 au 150?

J: Mwanzo 7:12 inasema ilinyesha kutoka mbinguni kwa muda wa siku 40, lakini maji yalifurika duniani kwa jumla ya siku 150.

 

S: Kwenye Mwanzo 8, kwa nini Biblia inaonyesha kufundisha kuwa binadamu walianza kuwepo karibu miaka 6,000 iliyopita?

J: Kwa mujibu wa njia za mionzi za kutambua tarehe, binadamu wa kwanza, ambao wanasayansi wanawaita Cro-Magnon, waliishi kutoka karibu miaka 400,000 iliyopita hadi leo. Nenderthals walikuwa wazao wa Cro-Magnon na waliishi kutoka miaka 130/100, 000 hadi 35 / 30, 000 iliyopita.

Hata hivyo, bila kujali muda ambao Mungu alimuumba mtu, orodha za vizazi za Kitabu cha Mwanzo ina mapengo yasiyoweza kufahamika, kwani neno "mwana" pia linamaanisha "uzao wa" na neno "baba" pia linamaanisha mhenga. Isaya 51:2 inasema Ibrahimu ni baba wa Wayahudi, na Wayahudi walimwambia Yesu Ibrahimu alikuwa baba yao kwenyea Yohana 10:53.

Kama nyongeza, tunaweza kusema kwa uhakika kuwa dunia iliumbwa kwa muda wa siku sita, lakini siku moja ya Mungu ina urefu gani? 2 Petro 3:8 anasema kwa Mungu siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja. Zaburi 90:4 inasema miaka elfu mbele ya Mungu ni kama siku moja au lindo moja la usiku. Irenaeus kwenye Against Heresies Kitabu cha 5 sura ya 23 (mwaka 182-188 BK) uk.551-552 anatafsiri kuwa siku moja ya Mungu kwenye Mwanzo ni miaka 1,000.

 

S: Kwenye Mwanzo 8:1 na Kutoka 6:5, Mungu angewezaje kukumbuka isipkuwa alisahau kwanza?

J: Mungu anjaua vyote. Ingawa Nuhu anaweza kuona kuwa amesahauliwa, hii ni njia ya kuonyesha kwamba Mungu hakumsahau Nuhu. Tunapomkumbuka mtu kwenye maadhimisho ya ndoa yake au siku ya kuzaliwa, haimaanishi kuwa tumewasahau muda mwingine wote wa mwaka.

 

S: Kwenye Mwanzo 8:11, jani la mzeituni lina umuhimu gani?

J: Jani linadhaniwa kumea baada ya gharika, na mizeituni huwa haikui katika maeneo ya mwinuko. Mzeituni mara nyingi ni ishara ya watu wa Mungu.

 

S: Kwenye Mwanzo 8:15, je mbari zote zilitoka kwa Nuhu?

J: Kwa upande wa baba ndiyo, lakini kwa upande wa mama hapana. Mke wa Nuhu, watoto wao watatu, na wake zao walikuwa kwenye safina pia. Tofauti si kubwa sana, ikichukuliwa kuwa kwenye ndoa za watu wenye rangi mchanganyiko, ndugu wawili wanaweza kuwa weupe sana na weusi sana.

 

S: Kwenye Mwanzo 8:15-21, kuna vitu gani vinavyofanana na Mwanzo 12:1-7?

J: Kuna vitu vingi sana vinavofanana kati ya kuitwa kwa Nuhu na Mungu na kuitwa kwa Abramu na Mungu.

Mungu anasema kwake (Mwa 8:15; 12:1)

Toka katika safina / nchi (Mwa 8:16; 12:1)

Hivyo akatoka (Mwa 8:18; 12:4)

Kisha akajenga madhabahu (Mwa 8:20; 12:7)

Mungu alimbariki (Mwa 9:1; 12:2)

Ongezeka / kuwa taifa kubwa (Mwa 9:1; 12:2)

Weka agano / Mungu awapa ardhi (Mwa 9:9; 12:7)

 

S: Kwenye Mwanzo 8:21-22, je maji yatafunika uso wa dunia nzima tena?

J: Hapana, kwa sababu Isaya 54:9 inatukumbusha kuwa hayatafunika. Hii ni hoja nyingin dhidi ya maoni ya gharika inayohusisha eneo dogo la nchi, kwa sababu Mungu alisemaa hapakuwa na gharika nyingine itakayoifunika dunia nzima tena. Kama gharika ya Nuhu ingekuwa inahusisha eneo dogo tu, basi pamekuwa na mafuriko mengine makubwa yaliyohusisha maeneo madogo ya dunia.

 

S: Kwenye Mwanzo 8:21, je Mungu ataangamiza viumbe wote wenye uhai tena, au vitu vyote vitaangamizwa tena kwenye 2 Pet 3:7,10?

J: Mwanzo 8:21 inasema Mungu aliahidi kutoangamiza viumbe vyote vyenye uhai "... kama nilivyofanya", na Mwanzo 8:22 inaongeza "...muda nchi idumupo." Mungu ataiangamiza dunia kwa moto, akiwaacha waamini.

 

S: Kwenye Mwanzo 8:22, kwa nini bado kuna majanga ya njaa?

J: Mwanzo 8:22 inasema kuwa majira ya kupanda mbegu na kuvuna hayataisha. Ingawa pamekuwa na majanga mengi ya njaa, hapajawa na janga la muda mrefu la njaa lenye kuihusisha dunia nzima.

 

S: Kwenye Mwanzo 9, wanyama wote waliwezaje kurudi kwenye sehemu walizotoka?

J: Wakristo hawakubaliani kama gharika ilitokea mwaka 2600-3000 KK, karibu mwaka 7000 KK, karibu mwaka 14,000 KK au karibu miaka milioni iliyopita. Wale wanaoamini gharika ilitokea kutoka mwaka 2600 hadi 3000 KK wanaamini akiolojia na njia za mionzi zimechanganywa hata hapatakuwa na vigezo vya kuthibitisha kuwa wanyama walirudi sehemu ileile waliyotoka au la.

Hata hivyo, kama gharika ilitokea karibu miaka 14,000 iliyopita, wanyama wote hawakuishi mahali pamoja. Daraja la ardhi liliiunganisha Amerika na Asia. Baada ya hapo, tembo wa kale na farasi walikufa katika Dunia Mpya.

Hata hivyo, bila kujali lini gharika ilitokea, Wakristo wote wanaweza kukubaliana kuwa Mungu ana nguvu ya kuwafanya wanyama waende mahali anapotaka.

 

S: Kwenye Mwano 9:3, je watu wanaweza kula nyama, au mboga za majani tu?

J: Mwanzo 1:29 inasema Adam aliweza kula mboga za majani. Baada ya gharika, Mwanzo 9:3 inasema sasa tunaweza kula nyama. Tazama maelezo kwenye Mwanzo 1:28 kwa habari zaidi.

 

S: Kwenye Mwanzo 9:4, kunywa damu kumezuliwa leo?

J: Kuna watu wanaosema hapana, kwa sababu ukristo uko juu ya sheria, na kwenye Matendo 10:11-16, "vyakula" vyote viliitwa safi.

Wengine wanasema ndiyo, kwa sababu agizo hili lilitolewa kabla ya sheria ya Musa kwenye Mwanzo 9:4. Kwenye Matendo 15:20,29 kanisa la mwanzo liliamini kuwa Wakristo wanapaswa kujiepusha na damu. Kiasi kidogo cha damu ni sawa, kwa sababu Wayahudi waliruhusiwa kula wanyama waliowawinda na kuwatoa damu [kwa haraka] nyikani kwenye Walawi 17:13. Tazama Encyclopedia of Bible Difficulties uk.84-86 kwa hoja hii.

 

S: Kwenye Mwanzo 9:4, Walawi 7:26-27, Walawi 17:11-12, na Kumbukumbu 12:16, 23-25, je zuio la kunywa damu linamaanisha watu wasitoe wala kuongezewa damu kama Mashahidi wa Yehova wanavyofundisha?

J: Hapana. Hatupaswi kuwa watu wanaokula watu, lakini kutoa viungo ni sawa. Kadhalika, watu walizuiliwa kula damu, na kutoa au kuwekewa damu ni sawa.

Kama Jehovah's Witnesses Answered Verse by Verse uk.22-23 inavyosema, hata shirika la Mashahidi wa Yehova (Jehovah's Witness Watchtower) halikuzuia kutoa na kupokea damu hadi mwaka 1944. Mwaka 1967, walizuia pia kuto au kupokea viungo (Gazeti la Watchtower Desemba 15, 1967, uk.702-704). Kisha walibadilisha mawazo yao mwaka 1980 (Gazeti la Watchtower Machi 15, 1980, p.31). Pia hawakuruhusu chanjo kuanzia mwaka 1931 hadi 1952.

 

S: Je Mwanzo 9:6 inazuia adhabu ya kifo kwa wahalifu leo?

J: Si hivyo kabisa. Mwanzo 9:6 inakatazo uuaji, na inaamuru adhabu ya kifo kwa wauaji. Kumbuka kwamba kitabu cha Mwanzo kilikuwa moja ya vitabu vya Musa, na kwenye Kutoka hadi Kumbukumbu makosa kadhaa ya jinai yamepewa adhabu ya kifo. Tazama pia swali linalofuata.

 

S: Je Mwanzo 9:6 inaongelea adhabuya kifo?

J: Ni dhahiri anaongea ya adhabu ya kifo. Ina maana kunyonga na si kufa kimwili tu ambako hutokea kwa wauaji na watu wasiokuwa wauaji pia.

 

S: Kwenye Mwanzo 9:12-13, je upinde wa mvua, kama ishara ya agano la Mungu, unaonyesha kuwa hapakuwa na upinde kabla ya gharika?

J: Inadokeza hivyo lakini haithibitishi. Kama Today's Handbook for Solving Bible Difficulties uk.220-221 inavyosema, kwa kutumia ishara Mungu hakuthibitisha moja kwa moja kuwa haikuwahi kuwepo kabla ya wakati huo. Kwa mfano, tohara ilifanywa na watu wengine kama Wamisri na Waethiopia kabla ya Abrahamu (Herodotus kwenye History kitabu cha 2 sura ya 104, uk.69). Ilifanywa na Wamisri kwa mujibu wa Letter of Barnabas (mwaka 100-150 BK) sura ya 8, uk.142.

 

S: Kwenye Mwanzo 9:20-21, jinsi mtu mcha Mungu kama Nuhu anawezaje kulewa?

J: Kwanza, Biblia haifichi ukweli kwamba watu wa Mungu wanafanya dhambi pia. Pili, udogo wa shinikizo la hewa karibu na kilele cha mlima baada ya mafuriko, ni rahisi kulewa.

 

S: Kwenye Mwanzo 9:20-21, kwa nini hadithi hii mbaya ya kulewa kwa Nuhu imo kwenye Biblia?

J: Biblia haituonyeshi tu umuhimu wa kutenda haki, lakini pia inatoa mifano ya matokeo ya kufanya vitu vibaya. Clement wa Alexandria (mwaka 193-217/220 BK) alijibu swali hili vizuri sana. "Kulewa kwa Nuhu kulirekodiwa kimaandishi ili kwamba tukiwa na maelezo wazi yaliyoandikwa ya dhambi yake, tuweze kujilinda kwa nguvu zote dhidi ya ulevi", The Instructor kitabu cha 2 sura ya 2 uk.246.

 

S: Kwenye Mwanzo 9:21-25, je Mwanzo ni toleo liliofupishwa la hadithi ya asili ambapo Ham almhasi Nuhu ili kumzuia kupata watoto zaidi, sawa na hadithi ya kubuniwa ya Kigiriki ambapo Chronos alimhasi baba yake Uranus kama mtu asiyeamini uwepo wa Mungu (Capella) alivyopendekeza?

J: Hapana, hakuna dokezo lolote la kuhasiwa, hapa. Kuhusu utamaduni wa Kigiriki, kumbuka kwamba utamaduni pekee wa Kigiriki wakati wa Musa ulikuwa ni Wagiriki wa mwanzoni wa Mycenea. Mengi ya hadithi za kubuniwa za Kigiriki yalitokea baada ya wakati huo. Kwa kumbukumbu, vita vya Trojan ya Homer vilikuwa karibu mwaka 1200 KK, kiasi cha miaka 450 baada ya Kutoka (kwa Waisraeli Misri).

Kwa hiyo, kuna uwezekano kuwa hakukuwa na kunakiri matukio hapa. Kama mtu ataendele kusisitiza kuwa kulikuwa na kunakiri, mtu aliyeishi miaka ya baadaye atakuwa amenakiri toka kwa walioishi miaka iliyopita, na hadithi Kigiriki hapa ina uwezekano mkubwa wa kutungwa baada ya wakati wa Musa.

 

S: Kwenye Mwazno 9:22 kulikuwa na kosa gani Ham alipoona utupu wa baba yake?

J: Watoto hawapaswi kutangaza madhaifu ya wazazi wao, na fikra za Ham hazikuwa na heshima kwenye Mwanzo 9:22. Ham alijifunza kuwa mtoto wake mwenyewe atakuja kuwa fedheha kwake. Fikra ya Ham ilikuwa ya mzaha kwa mujibu wa Methodius (mwaka 260-312 BK) kwenye Banquet of the Ten Virgins sura ya 2 na Justin (mwaka 138-165 BK) Dialogue with Trypho sura 139.

 

S: Kwenye Mwanzo 9:22-23, unafanyeje ikiwa utaaibishwa na wazazi wako?

J: Kwanza elewa kwa nini umeaibishwa. Je wazazi wako wanafanya kitu ambacho ni kibaya kimaadili, ni jambo ambalo unatafuta kasoro kupita kiasi, au ni kitu kiicho kati ya hivi viwili. Unapaswa kuwaheshimu wazazi wako (Kutoka 20:12; Waefeso 6:2), lakini pia hupaswi kuunga mkono dhambi. Unatakiwa kuwatiini wazazi wako katika Bwana (Waefeso 6:1). Hii inamaanisha uwatii, lakini wanapoamuru kitu kilicho kinyume na Mungu, unapaswa umtii Mungu kwanza.

S: Kwenye Mwanzo 9:22-23, unafanyaje endapo watoto wako wameaibishwa na wewe?

J: Kuna njia walau nne ambazo wanaweza kuaibishwa:

1) kwa sababu ya msimamo wa kimaadili unaouchukua ni sahihi

2) kwa sababu ya kitu kinachohusiana na mtindo, matakwa binafsi, au mada nyingine ya kimaadili isiyo ya upande wowote ambayo ni sahihi

3) kwa sababu ya kitu kisichokuwa sahihi ulichokifanya

4) kwa sababu ya kitu ambacho si sahihi, lakini hakifai au hakina heshima kwa hisia zao

Kwa sababu ya kwanza, unaweza kueleza tu kwa nini umechukua msimamo wako. Kwa sababu ya pili, usiruhusu kitu chema kusemwa kuwa kiovu (Warumi 14:16), lakini kwa upendo unaweza kuchukuliana nao (Warumi 14:14-15).

 

S: Kwenye Mwanzo 9:22-23, tufanyeje watu wengine wanapofanya dhambi?

J: Kwa vyovyote vile, hatupaswi kutoa namna yoyote ya kuunga mkono dhambi, lakini bado tunaweza kumpenda mwenye dhambi. Tusiwe mahali ambapo tunajaribiwa sisi wenyewe. Licha ya hiyo, kuna tofauti endapo mwenye dhambi ni mtoto wako, mzazi wako, mtu mkubwa kuliko wewe, Mkristo, au mtu asiyeamini.

Usikubali mashtaka juu ya mzee, ila kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu (1 Timotheo 5:19).

Adhabu ya kupiga viboko inaweza kutumika kwa watoto wako, lakini si watu wengine (Mithali 22:15; Waebrania 12:7-11)

Mzee usimkemee, bali umwonye kama baba (1 Timotheo 5:1)

 

S: Kwenye Mwanzo 9:25, kwa nini Kanaani, sio Ham, alilaaniwa?

J: Ham alijifunza kuwa wazao wake watakuwa mfano wa matokeo ya dhambi. Expositor's Bible Commentary juzuu ya 2, uk.97 inasema kuwa njeo ya Kiyahudi ni ile isiyokamilifu na si amri (jussive), "kwa hiyo maana ni zaidi ya utabiri (‘atakuwa') badala ya laana (‘na awe'). Hivyo maneno ya Nuhu yanatarajia mada kuu ya simulizi zinazofuata - kutenya mbegu iliochaguliwa kutoka kwenye mbegu ya Wakanaani."

Tazama Dialogue with Trypho ya Justin Martyr [iliyoandikwa karibu mwaka 138-165 BK], sura ya 139 kwa maelezo zaidi.

 

S: Kwenye Mwanzo 9:25-26, laana ya Kanaani ilikuwa nini?

J: Mwanzo inasema tu kuwa atakuwa mtumwa wa chini kabisa kwa ndugu zake. Kumbuka laana haipo kwa Hamu bali Kanaani. Hakuna maandiko ya Kigiriki au Kiyahudi yanayosema ilikuwa ni Hamu, ni tafsiri Kiarabu tu inayosema hivyo. (Kwa mujibu wa Origin of the Bible uk.307, toleo la kwanza la Kiarabu la vitabu vitano vya kwanza vya Biblia lililotafsiriwa na Saadya Gaon, aliyeishi kutoka mwaka 892 hadi 942 BK).

   Kama Hamu alivyomfanya Nuhu baba yake aaibike, Kanaani na wazao wake walimfanya Ham baba yake aaibike..

 

S: Kwenye Mwanzo 10, ni kina nani hawa watu 68 na hii moji 16?

J: Haya ni maelezo ya kiasayansi kuhusu mbari ya zamani zaidi ambayo yamehifadhiwa. Wasomi wanaamini kuwa wanaweza kutambua watu 51 kati ya 68 na wataalam wa elimukale wamegundua miji 11 kati ya 16. Sodoma na Gomora iliharibiwa sana hata haijaweza kupatikana. Hata hivyo, vibai vyenye maandiko vya Ebla, vilivyoandikwa mwaka 2400-2250 KK vinaitaja miji ya Si-da-mu (Sodoma) na I-ma-ar (Gomora). Pia, madhabahu iitwayo Bab ed-Dra ilikutwa kusini mwa Bahari ya Chumvi. Ilitengenezwa kati ya mwaka 2800 na 1800 KK.

 

Hawa ni watu ambao wanafahamika au kudhaniwa.

 

Yafethi - Wagiriki wanasema mhenga wao ilikuwa Japetos

|->Gomeri - Gimirra/Kiasiria Cimmerian/Kigiriki

| |->Ashkenazi - As-gu-za-a/Kiasiria = Scythians

| |->Rifathi - ? aliishi Urusi?

| |->Togama - ama mji wa Tegarama wa Asia ndogo, wahenga wa Waamenia, au vyote

|->Magogu - Scythians? kwa mujibu wa Josephus

|->Madai - Wamede

|->Yavani - Wagiriki wa Ion

| |->Elisha - Waeolia? kwa mujibu wa Josephus

| |->Tarshish - mji wa Asia ndogo au Hispania

| |->Kitimu - Cyprus

| |->Rodani - Kisiwa cha Rhodes

|->Tubal - Watabali huko Cappadocia

|->Mesheki - Mushki/Kiasiria awali kati ya

| Cilicia na Bahari ya Caspia

|->Watiira - huenda ni Wathrusa walioivamia Misri mwaka 1250 KK

Hamu - Hana kabila, wazao tu

|->Wakushi - Wasudani (Wakushi hapo zamani)

| |->Seba - Kaskazini mwa Ethiopia. Jina la

| mahali linaloweza kuwa limetoka kwa wakoloni | wa Kisabe waliokuja baadaye

| |->Havila - Ama karibu na Mto Indus River | huko Pakistan, au karibu na Sheba na Hadramaut

| |->Sabta - ? huenda aliishi kaskazin mwa | Sheba

| |->Raama - Wanaweza kuwa Warhama wa | kusini magharibi mwa Arabia (Strabo 16.4.24)

| | |->Sheba - Sheba kona ya kusini magharibi | mwa rasi ya Arabuni

| | |->Dedan - Kaskazini mashariki mwa | Ghuba ya Uajemi. Imeelezwa na Wakaldia na | Waasiria

| |->Sabta - ? haifahamiki

|->Mizraim - Misri

| |->Waludi - ? hawafahamiki

| |->Waanami - ? wafahamika 1 Nya 1:11 tu

| |->Walehabi - Walibu walikuwa kabila maadui | magharibi mwa Misri

| |->Wanaftuhi - ? hawafahamiki

| |->Wapathrusi - Pathros ilikuwa kusini mwa | Misri

| |->Wakasluhi - Wafilisti walitokana nao

| |->Wakaftori - Visiwa vya Krete / Aegea

| | (Akadia/Mari/Ugarit/Misri)

|->Put - Libya kwa mujibu wa rekodi za Babeli na | Uajemi

|->Kanaan - Wakanaani

| |->Sidoni - Mji wa Foinike

| |->Wahiti - Waliishi kaskazini mwa Yerusalem

| |->Wayebusi - Waliishi Yerusalem

| |->Waamori - Waliishi Kanaan. Amurru kwenye Kiakadia inamaanisha mtu wa magharibi

| |->Wagirgashi - Waliishi Kanaan, wanawea kuwa Waqirkishi/Waasiria

| |->Wahiivi - Waliishi karibu na Tiro, Sidon, na

| Shekemu. Suleiman aliwatumia katika kujenga | hekalu

| |->Warki - Bandari ya ‘Arqah kaskazini mwa | Syria

| |->Wasini - Bandari ya Siannu kaskazini mwa | Kanaani

| |->Warvadi - mji wa Arvadi kaskazini mwa Foinike

| |->Wazemari - Mji wa Kikanaan wa Simura | ulio maili 6 kusini mwa Arvadi

| |->Wahamathi - Moja ya miji ya zamani sana | ya Syrian

Shemu - yaweza kuwa Sumer

|->Elamu - Waelami, mji mkuu ulikuwa Susa

|->Washuri - Mji mkuu wa kwanza wa Asiria

|->Arphaxad - ? Ptolemy aliuelezea ukanda wa | Arrapachitis kati ya maziwa Van and Urmia

| |->Shela - Hakuna kabila linalofahamika, | wazao tu

| | |->Eberi - Hakuna kabila linalofahamika, | wazao tu

| | |->Peleg - Hakuna kabila linalofahamika, | wazao tu

| | |->Joktan - makabila mengi ya Arabia au kabila la Qahtan la kusini mwa Arabia

| (al-Tabari juzuu ya 6, uk.xxii; juzuu ya 20, uk.xv)

| | | |->Almodadi - huenda? ni kabila la kusini | mwa Uarabuni

| | | |->Shelefu - Kabila la Kiyemeni kusini | mwa Uarabuni

| | | |->Hazarmavethi - Hadrumaut Arabia

| | | |->Jerah - Linaweza kuwa kabila la | Arabia?

| | | |->Hadoramu - ? haifahamiki

| | | |->Uzali - ? haifahamiki

| | | | Hata hivyo, Uzal/Auzal ni jina la | zamani la Sa'na huko Yemen.

| | | |->Diklah - inamaanisha "mtende." | | | | Huenda? waliishi Wadi Sirhan,

| | karibu maili 250 kusini mashariki mwa | Bahari ya Chumvi.

| | | |->Obal - haifahamiki nje ya 1 Nya 1:22

| | | |->Abimael - ? haifahamiki

| | | |->Sheba - Wasabea kusini mwa Arabia

| | | |->Ophir - Huenda ni Somalia au kusini | | | | magharibi mwa Arabia

| | | | Josephus and Jerome walidhani | | | | | | ilikuwa India

| | | |->Havilah - Huenda ni Arabia ya kati

| | | |->Jobab - ? haifahamiki

|->Lud - Ama Walidia au nchi ya Waludi

| kati ya Tigris ya juu na Frati

|->Aram - Waarami wa Syria

|->Uz - Kabila la Ausitai? waliishi magharibi | | | mwa Frat.

|->Hul - ? haifahamiki

|->Gether - ? haifahamiki

|->Mash/Meshech - ? Ama jangwa la Syria-Arabia la Mash lilifahamika na Wasiria, mlima wa Lebanoni wa Masius, au Mesheki ilikuwa ni mchanganyiko wa wahenga wawili

 

S: Kwenye Mwazno 10, kwa nini Wahindi an Wachina hawajatajwa kwenye orodha ya mataifa?

J: Kwanza kitu gani si jibu, kisha kitu gani ni jibu.

Si jibu: Ingawa Wasini wametajwa, hawa huenda wasiwe Wachina bali wanatoka bandari ya Kanaani ya Siannu kaskazini mwa Syria. Josephus na Jerome walifikiri Ofiri ilikuwa India, lakini inawezekan zaidi kuwa Afrika.

Jibu: Wote walitoka kwa Adamu, kwa kuwa wote walilaaniwa pamoja na Adamu. Kitabu cha Mwanzo hakidai kuorodhesha kila kundi la watu, na wa mamia ya makundi ya watu, Mwanzo inayataja mataifa ambayo wengi wa Waisraeli watayatambua. Angalia Today's Handbook for Solving Bible Difficulties uk.224-226 kwa jibu la kina zaidi.

 

S: Kwenye Mwanzo 10, je Wasumeri wa Mesopotamia wameelezwa?

J: Ndiyo, pengine wameelezwa kama "Shemu." Nchi ya Sumeri, mara nyingi hutamkwa bila ya "r", na Sum inaweza kuwa Shemu kwa urahisi. Kwa uthibitisho wa kitaalamu wa hii, rejea kwenye The Sumerians na Samuel Noah Kramer uk.297-298. Kramer pia ananukuu American Journal of Semitic Languages (58 [1941] uk.20-26).

 

S: Kwenye Mwanzo 10:2, Wagomeri walikuwa ni watu gani?

J: Wycliffe Bible Dictionary uk.710 inasema hawa ni watu walioitwa "Gimirra" na Waashuri na Cimmerians na Wagiriki. Gomeri aliishi Ukraine na kusini mwa Russia.

 

S: Kwenye Mwanzo 10:2 kwa nini Wamedi (Madai) wameelezwa, kwa kuwa watu hawakuelezwa sehemu nyingine yoyote hadi mwaka 836 KK kwenye maandishi ya Shalmaneser III?

J: Maandishi ya Shalmaneser III yaliandikwa baada ya muda wa Musa wa mwaka 1407 KK, lakini ukimya kwenye maandishi ya kale yaliyopo haumaanishi kutokuwepo kwake. Waashuri waliandika tu wakati walipopigana na kufanya biashara na Wamedi kwa farasi. Kwa mujibu wa Persia and the Bible uk.35, "I.M. Diakonoff anaamini kuwa kuwasili kwa makabila Kihindi-Kiirani kwenye milima ya Iran kulitokea nusu ya kwanza ya milenia ya pili KK [miaka ya 2000-1500 KK]. Lakini ushahidi wa kale zaidi wa elimukale wa wageni unaelekea kuonyesha tarehe ya sehemu ya nusu ya pili ya milenia ya pili KK [miaka ya 1500-1300 B.C.].

Tofauti na hili, watu wenye nguvu wa Minni walitajwa kwenye Yeremia 51:27. Hata hivyo, Waminni walianza karibu mwaka 1200 KK, na Waminni hawajatajwa kwenye Mwanzo, kwa sababu kitabu cha Mwanzo kiliandikwa mapema.

Kwa ufupi, elimukale inaunga mkono kuwepo kwa Wamedi wakati wa Musa.

 

S: Kwenye Mwanzo10:2, Wayavani walikuwa ni watu gani?

J: Ni Wagiriki wa Ioni. Kwenye Kiebrania hii ni yawan ambayo ni sawa na iaones au iawones ya Kigiriki kwenye Illiad ya Homer 8.685, na yamanu kwenye maandishi ya Sargon II na Darius I. Waioni wameelezwa Misri kuanzia wakati wa Rameses II (karibu mwaka 1300 KK.). Isaya 66:19 na Ezekiel wamewaeleza, na tasfiri ya Kigiriki ya Agano la Kale (Septuagint) inatafsiri jina hili kama "Hellas".

 

S: Kwenye Mwanzo 10:2, Watubali walikuwa ni watu gani?

J: Waliitwa Tabal (au Tabali) na Waashuri na waliishi Uturuki ya leo katika ukanda wa Kapadokia. Mwana historia wa Kigiriki Herodotus aliwajua kama Tibarenoi. Wametajwa katika Ezekiel 27:13, 28:2-3; 39:1, na Isaya 66:19.

Mfalme wa Ashuru Shalmaneser III (mwaka 859-824 KK) alipokea kodi kutoka wafalme 24 wa Tubali. Waashuri walimpindua mfalme wa Tubali mwaka 732 KK. Sargon alisema vyombo vya thamani vya chuma vya kuwekea vitu vilitoka Tubali. Sargon pia aliwaangamiza uasi wa Tubali, Mushki (Mesheki) na Ararati.

 

S: Kwenye Mwanzo 10:2, Wamesheki walikuwa ni watu gani?

J: Waashuri kwanza walitajwa kama "Mus-ka-a-ia" waliokuwa na jeshi la watu 20,000 wakati wa Tiglath-pileseri I(karibu mwaka 1100 KK). Walitajwa pia wakati wa Shalmaneser III (mwaka 859-824 KK). Wycliffe Bible Dictionary uk.1105-1106 pia inasema awali waliishi kati ya Bahari ya Kilikia na Bahari ya Kaspi, lakini wakati wa Sargon II (mwaka 722-705 KK) waliishi katika eneo la Frigia katika Uturuki ya leo. Herodotus 3:94 anawaorodhesha kama "Moschoi", ambao walikuwa miongoni mwa maakida 19 wa Dario.

The New Bible Dictionary (Eerdman's 1962) uk.811 pia inasema wamefananishwa na Wafirgia.

 

S: Kwenye Mwanzo 10:2, Watira walikuwa ni watu gani?

J: Hatujui mengi kuhusu Watira. Wakati Josephus anadai kuwa Wathrakia walitokana nao, siku hizi watu wanadhani walikuwa Waturseniki / Watirsenia, ambao walikuwa maharamia. Wamisri wanawataja "Wathrusa" (Tw-rw-s3) kuwa waliivamia Misri mwaka 1250 KK. Kitabu Apocrypha cha Yubile kinasema Tirasi aliishi kwenye visiwa nne.

 

S: Kwenye Mwanzo 10:3, Togama ilikuwa wapi?

J: Togama ilikuwa karibu maili 70 (km 113) magharibi mwa mji wa Malatya. Wahiti waliiita Tegarama. Waashuri waliita Tilgarimanu, na waliiteka mwaka 695 KK. Wagiriki waliita Gauraena. Waamenia walidai kuwa walitoka kwa Haik, mtoto wa Torgom, kwa hiyo wanaweza kuwa wazao wa Togama.

 

S: Kwenye Mwanzo 10:5, 20, 31, kwa kuwa kulikuwa na ndimi tofauti, kwa nini dunia nzima ina lugha moja tu kwenye Mwanzo 11:1?

J: Mwanzo 10 ni maelezo ya jumla, na Mwanzo 11 inazungumzia tukio moja ndani ya Mwanzo 10. Mwanzo 10:5 inasema, "kwa hao", 10:18 "baadaye ..." Vitu hivi vinaashiria kuwa Mwanzo 10 inasema jinsi ambavyo wazao walienea baadaye. Mwanzo 11:1 inaongelea kuhusu tukio la Mnara wa Babeli, lililotokea kabla ya kusambaa kwa watu.

Kibao cha udongo chenye maandishi huko Babeli kinaelezea hekalu moja lililoichukiza miungu. Waliliharibu katika usiku moja na kuwatawanya watu kwa lugha ya ajabu.

 

S: Kwenye Mwanzo 10:6, 13 na 1 Nya 1:8, 11, kwa nini Misri haitajwi miongoni mwa mataifa haya? (Mkristo mmoja alishangazwa na jambo hili)

J: Misri imetajwa. Neno la Kiebrania la Misri ni Mizraim.

 

S: Kwenye Mwanzo 10:8-12, je matedno ya Nimrod yalikuwa ni mkusanyiko wa sikukuu za Lugal-Zaggasi, Sargon wa Agade, Hammurabi, na Shalmaneser I?

J: Hapana. Wakati hatujui mengi juu ya wafalme wa zamani Sumeria ila kwa makumi ya maelfu ya vibao vyenye maandishi vya ambavyo vimepatikana, kufanana kwa mashujaa hawa na Nimrod ni kudogo sana. Biblia inasema tu kwamba Nimrodi alikuwa muwindaji hodari mbele ya Bwana, kwamba kazi ya Nimrodi ilianza katika miji nne ya Shinari (Sumeri), na baadaye alikwenda Ashuru na ambako alijenga miji minne iliyokuwa karibu karibu sana, ambayo baadaye ilikuja kuwa na ushawishi mkubwa sana. Biblia haisemi kitu kingine chochote kuhusu Nimrod, hivyo ni vigumu kulinganisha. Nimrod hawezi kuwa Hammurabi, kwa sababu Hammurabi (mwaka 1803/1793-1760/1750 KK) aliishi miaka mingi baada ya Abrahamu. Nimrod anaweza kuwa rejeo la kibiblia la Sargon, isipokuwa tunajua kiasi kidogo sana kuhusu Sargon na Nimrod cha kuweza kusema.

 

S: Kwenye Mwanzo 10:9, je Nimrod alikuwa muwindaji mzuri "mbele ya Bwana", au mnyang'anyi asiye mcha Mungu "akipingana na Bwana"?

J: Labda tafsiri nzuri ya neno la Kiebrania paniym ni "kabla". Kama neno la Kiingereza "kabla", paniym imetumiwa katika muktadha nyingi. Kwa mfano, kiongozi anaweza kuwa mbele ya kusanyiko kwenye Yoshua 20:6, 9, Israel alishindwa mbele ya Wafilisti kwenye 1 Samweli 4:2, na Israel alikimbia mbele ya Wafilisti kwenye 1 Samweli 4:17.

Katika kifungu hiki, paniym inaweza ikawa inamaanisha maelezo yasiyokuwa ya kiungu, kama kwenye "kupigana mbele ya." Jina hili linahusiana na neno la Kiebrania marad lenye kumaanisha "kupinga" (The Bible Knowledge Commentary : Old Testament uk.42) au "tutapinga" kwa mujibu wa New Geneva Study Bible uk.25. Baada ya Mnara wa Babeli, Nimrod alijenga mji wa Babeli kwenye uasi dhidi ya Bwana.

Nimrod akiwa "muwindaji mwenye nguvu mbele ya Bwana" ni maelezo hasi na yasiyo ya kiungu kuhusu Nimrod kwa mujibu wa Believer's Bible Commentary uk.45-46, Unger's Bible Dictionary uk.794.

 

S: Kwenye Mwanzo 10:9, je Nimrod/Nimrud alikuwa mtu wa mbari gani?

J: Kuna vitu vitatu vinavyowezekana.

Ashuru inaitwa nchi ya Nimrud kwenye Mika 5:6, mji wa Kala, pia hujulikana kama Nimrud, na mji wa Babeli wa Borsippa pia uliitwa Birs Nimrud.

Wazao wa Kasi wa Kishi, walioishi Mesopotamia na kutawala Babeli karibu mwaka 3200 KK, na Mwanzo 10:8 inasema kuwa Kushi alikuwa baba wa Nimrod. Nin-Maradda ni jina lisilokuwa la Kisemiti la mji ulio kusin magharibi mwa Kishi, kwa mujibu wa Unger's Bible Dictionary uk.794. Wazo hili linaendana pia na wazo la kwanza.

Waubaidi walikuwa ni wakazi wa Sumeria wa mapema zaidi (karibu mwaka 3800-3500 KK) na Mesopotamia kabla Wasumeria ambao walitokea kusini. Mwanzo 10:8-10 inaonesha kuwa Nimrod alikuwa Babeli kwanza kisha akaelekea kaskazinihadi Ashuru. Tunajua vitu vichache sana kuhusu Waubaidia, lakini kwa ajili ya kuhusiana na Hamu wanaweza kuwa na uhusiano na Waharapa watu wenye ngozi nyeusi wa India. Tazama Wycliffe Bible Dictionary uk.1207-1208 kwa habari zaidi kuhusu maoni haya.

 

S: Kwenye Mwanzo 10:22 na 22:21, je Aram anadhaniwa kuzaliwa mara mbili?

J: Hapana, lakini kuna majibu mawili yanayowezekana:

Watu wengi: Hapakuwa na watu wawili tu, lakini watatu katika Biblia walioitwa Aramu.

1. Mwanzo 10:22 inasema Syria Aramu alikuwa mzao wa Shemu. (Neno la Kiebrania ni moja kwa baba na mhenga).

2. Mwanzo 22:21 inamtaja Aramu, ambaye alitokana na Kemueli (mpwa wa Ibrahimu), ambaye mtoto wa Nahori, aliyetoka Tera, aliyeshuka kutoka Shemu.

3. Baadaye sana kwenye 1 Nyakati 7:34 kulikuwa na Aramu mwana wa Shamer wa kabila la Asheri. Wycliffe Bible Dictionary uk.122 na New International Dictionary of the Bible uk.74 pia zinawataja watu watatu.

Mtu mmoja: Kumbuka kuwa Waramu wawili kwenye Mwanzo 10:22 na 22:21 wote ni wazao wa Shemu. Kwa hiyo wanaweza kuwa mtu mmoja, ambaye orodha ya mataifa inamtaja Shemu kuwa mhenga wa Aramu.

 

S: Kwenye Mwanzo 11, je watu walikuwa na maoni "dhaifu" sana kuhusu mbinguni hata wakajaribu kujenga Mnara wa Babeli hadi kuifikia?

J: Haya hayakuwa maoni ya Musa, bali ya watu waliokuwa wanajenga mnara. Mwanzo 11 inarekodi bila kuunga mkono, baadhi ya mawazo ya kipumbavu ya watu. Bila shaka, wazo la kipumbavu kwa halaiki ya watu linaweza kuwa la busara kwa makuhani kuhakikisha watu wanawahofu.

Zifuatazo ni baadhi ya piramidi/ziggurats nyingine ambazo wataalam wa elimukale wamegundua vichwa vya maelezo vyenye madai kama hayo.

Larsa: Nyumba ya Kiunganisho cha Mbingu na Dunia

Borshippa: Nyumba ya Waongozaji Saba wa Mbingu na Dunia

Asshur: Nyumba ya Mlima wa Ulimwengu

Babylon: Nyumba ya Msingi-Jukwaa la Mbingu na Dunia

Bible Knowledge Commentary : Old Testament (uk.44) inaelezea Enuma Elish VI, mistari ya 55-64 na kusema Babeli ilijengwa na miungu ya mbinguni kama mji angani. Babili maana yake ni "lango la Mungu."

 

S: Kwenye Mwanzo 11, dhambi ilikuwa ni ipi katika kujenga Mnara wa Babeli?

J: Haikuwa ujenzi wa jengo, lakini motisha wa kiburi wa (ujinga) kufikiri kuwa wanaweza kupaa mbinguni juu kwa uwezo wao wenyewe. Katika kiini cha ibada ya sanamu kuna imani kuwa watu wanapaswa kuwa washika dini kwa namna yoyote wanayotaka kwa "njia yao wenyewe", badala ya kumtafuta Mungu Mmoja wa Kweli. Itikio la Mungu halionekani kuwa la adhabu lakini la kuwaepusha kufanya maovu zaidi. Wazazi wenye hekima hawapendi watoto wao wapuuzie kabisa sheria na amri zao wenyewe, na Mungu naye hataki watu aliowaumba wafanye hivyo pia.

 

S: Kwenye Mwanzo 11, tunafahamu nini kuhusu Kisumeria?

J: Kisumeria kilandikwa kikabari, na si lugha ya Ulaya. Inafanana kiasi na lugha ya Kituruki, Kihangari, na baadhi ya lugha za milima ya Caucasus. Wasomi wanaweza kusoma Kisumeria leo, na wanajua jinsi maneno yalivyokuwa yanatamkwa. Kisumeria hakikuwa na sauti f, i, j, th, ch laini, v, w, au sauti za umlaut. Walikuwa na "ng" (kama Cantonese na Kivietinamu), na hawakuwa na unyambulisho kwenye miisho ya maneno kama nyingi za lugha za Ulaya. Pia kulikuwa na lahaja kadhaa za Kisumeria. Kama kulivyokuwa na aina za zamani za Kiingereza na Kichina, Encyclopedia Britannica inasema palikuwa na vipindi vinne vya Kisumeria: cha zamani, cha kiwango juu zaidi, na kilichofuata Usumeria. Ibrahimu aliishi wakati ambapo walikuwa wanasema "Kisumeria Kipya."

Kiebrania kilikuja kwa sehemu, kutoka kwenye Kisumeria. Kama Kisumeria, Kiebrania hakikuwa na sauti "j."

 

S: Je Mwanzo 11 haikufuata mfuatano?

J: Hapana, hakuna kitu kinachoonyesha kuwa haikufuata mfuatano. Fikiri kuhusu jambo hili. Kama watu wote waliangamizwa isipokuwa watu 8 waliokuwa na uhusiano wa damu au ndoa, kuna uwezokano mkubwa kuwa wote waliongea lugha moja. Hata hivyo, baada ya muda fulani, watu walianza kuzungumza lugha tofauti, na jambo hilo lilianza wakati walipokwa wametengana na kwenda sehemu mbalimbali. Kama nyongeza ya kufurahisha, wataalamu wa lugha wasio na mwelekeo wa kidini wanafikiri wanaweza kufuatilia chanzo cha lugha zote za Ulaya (kutoka lugha za Celtic hadi Ujerumani, hadi Kigiriki na hata Sanskrit) kwenye lugha moja, ambayo wanafikiri ilizungumzwa Ukraine karibu mwaka 4000 KK.

 

S: Kwenye Mwanzo 11:1-9, kwa nini kulikuwa na lugha moja kabla ya Babeli , kwa kuwa Mwanzo 10:5, 20, 31 inasema kulikuwa na lugha nyingi zilizoanza baada ya gharika?

J: Yote ni kweli, kwa sababu Mwanzo 10 inaelezea jinsi makabila yalivyokua kabla na baada ya Babeli.

Mambo matatu ya kuzingatia katika kujibu swali hili.

Mwanzo 10:5 inasema jinsi watu wa baharini walivyogawanyikana "kuwa nchi zao." Kuenea huku kulitokea baada ya Babel.

Mwanzo 10:20 pia inasema ikiongelea maeneo ya wana wa Hamu, na Wahamu kuhamia kwenye maeneo yao kutakuwa kulitokea baada ya Mnara wa Babeli.

Mwanzo 10:31 ni karibu sawa na Mwanzo 10:20, isipokuwa inahusu watoto wa Shemu.

S: Kwenye Mwanzo 11:5 na 18:21, kwa kuwa Mungu yupo kila mahali, je Bwana alishukaje "ili auone mji na mnara"?

J: Huu ni usemi unaoonyesha kuwa Mungu aliuangalia mji kwa umakini.

 

S: Kwenye Mwanzo 11:7, kwa kadri tunavyojua, je imani za awali zilikuwa za miungu wengi huku imani kwa Mungu mmoja ikiwa ni kitu kilichotoks baadaye?

J: Hapana. Kwa kadri tunavyojua kutoka kwenye historia, dini ya kale ya Kichina ilikuwa ya Mungu mmoja, pamoja na jamii nyingine za Asia ya kusini. Jina la awali la Kichina la Mungu mmoja lilikuwa Shang-di, ambalo hutumiwa kwa Mungu kwenye Biblia ya Kichina leo.

 

S: Kwenye Mwanzo 11:7-9, je mchanganyikano wa lugha kwenye Mnara wa Babeli ulinukuliwa kutoka kwenye hadith ya Kigiriki ya Aloadae?

J: Origen (mwaka 230-254 BK) alilichunguza jambo hili kwenye Origen Against Celsus kitab cha 4 sura ya 21, uk.505 na kusema kuwa haiwezekani kuwa kwa sababu:

a) Hakuna mtu wa Kigiriki aliyejulikana kwake (au sisi) kwamba alikuwa amesikia habari hii kabla ya Homer.

b) Homer aliishi karne kadhaa baada ya Musa.

Kwa taarifa zaidi, kuna mgongano wa tarehe kuhusu lini Homer aliishi. Mwana historia wa kale wa Kigiriki Aristarchus anasema mwaka 1044 KK, mamlaka huko Philostratus zinasema mwaka 1159 KK, Herodotus wa uongo The Life of Homer puts it as 1102 B.C.. In contrast to that the historian Theopompus anaiweka mwaka 1102 KK. Tofauti na hiyo, mwana historia Theopompus alisema Homer aliishi hadi mwaka 685 KK. Herodotus anasema haikuwa mapema zaidi ya mwaka 730 KK. Kutoka kwa Waisrael katika utumwa wa Misri kulikuwa karibu mwaka 1447 KK.

Hitimisho: Ama Wagiriki waliichukua hadithi toka kwa Waebrania wa kale, Wagiriki waliichukua hadithi toka mahala pengine nje ya Ugiriki, au maelezo ya Biblia na ya Wagiriki yanatokana na tukio moja.

 

S: Kwenye Mwanzo 11:9, je kutoa jina "Babel" toka kwenye neno la Kiebrani balal kulimaanisha "iliyochanganywa, iliyochanganyikiwa, au iliyochanganywa na kitu kingine hata inakuwa vigumu kuitambua" si sahihi, kwa sababu kwenye kugha ya Kibabeli neno Bab-ilu linamaanisha "lango la Mungu"?

J: Hapana. Hapana jambo hili linatokana na dhana kuwa Babeli iko kwenye eneo la mji wa Babeli. Biblia haisemi Wababeli au Wasumeri walisema ni kwa sababu lugha zilichanganywa, zulichanganyikiwa au zilichanganywa hata ilikuwa vigumu kuzitambua. Lakini Mwanzo ilisema kuwa popote Babeli ilipokuwa, watu baada ya hapo, (ikiwa ni pamoja na Waebrania waliosoma kitabu cha Mwanzo), waliita Babeli kwa sababu lugha zilichanganywa huko.

 

S: Kwenye Mwanzo 11:11, je Shemu alikuwa na umri gani mafuriko yalipokuja?

J: Yafuatayo ni mambo ambayo mtu anaweza kuyaona kwenye Maandiko, na kisha hitimisho:

Mwanzo 11:11 inasema Shemu alikuwa na umri wa miaka 100 miaka miwili baada ya mafuriko.

Mwanzo 5:32 inasema kwamba Hamu, Shemu na Yafethi walizaliwa wakati Nuhu akiwa na miaka 500.

Mwanzo 7:06 inasema Nuhu alikuwa na umri wa miaka 600 wakati gharika ilipokuja duniani.

   Hakuna kitu chochote kwenye Maandiko kinachoonyesha kuwa Hamu, Shemu na Yafethi walikuwa mapacha (watatu). Mwanzo 7:6 ilikuwa ni idadi ya wastani; watatu hawa walizaliwa, pengine kila mmoja kwa muda wake, Nuhu alipokuwa na karibu miaka 600.

 

S: Kwenye Mwanzo 11:18-24, kuna rekodi yoyote mbali ya Biblia ya Reu, Serug, na Nahori?

J: Hakuna mtu anayeweza kutarajia kuwa tutakuwa na rekodi tofauti ya kila mtu. Hata hivyo, katika suala hili tunaweza kuwa na rekodi nyingine. Kumbukumbu za Ashuru zimerekodi vijiji kwenye Syria ya kisasa viitwavyo Paligg, Reu, na Sarugi, na Nakhur. Kumbukumbu ya Mari pia inaitaja Nakhur.

 

S: Kwenye Mwanzo 11:27 na Gen 17:5, etimolojia (asili) ya majina "Abram" na "Abrahamu" ni nini?

J: Asili ya jina haina uhakika. Ni jina la Semitiki ya magharibi, na linaweza kumaanisha "baba ametukuzwa" au "baba aliyetukuzwa." Jina "Abrahamu" linamaanisha "baba wa umati (uwingi)" au "baba wa umati (umoja)."

 

S: Je Mwanzo 11:27 inafundisha kuwa Abram, Nahori, na Harani walizaliwa kwa mfuatano wowote ule maalum?

J: Wakati baadhi ya watu wanakosea kwa kufikiri kuwa orodha ya kwenye Biblia mara zote hudokeza mtu aliyezaliwa kwanza, jambo hili si kweli. Kwa mfano, kwenye 1 Nyakati 3:15, Zedekia aliorodheshwa kama mtoto wa tatu wa Yosia, na Shalumu / Yehoahazi aliorodheshwa kama wanne. Lakini wakati Yehoahazi alipokuja kuwa mfalme mwaka 609 KK, alikuwa na umri wa miaka 23, na Zedekia alikuwa na umri wa miaka kumi tu. Kwa mfano mwingine, Hamu ametajwa kabla Shemu na Yafethi, lakini Mwanzo 9:24 inaonyesha kuwa Hamu alikuwa mdogo. Kwa hiyo Biblia inapotoa orodha bila kusema kuwa watu hao wameandikwa kwa kufuata mfuatano wao wa kuzaliwa, tusikujaribu kusoma kwenye Biblia jambo ambalo halipo.

   Katika jambo hili hili, kwa kuwa Abramu alikuwa na miaka 75 wakati alipoondoka Harani baada ya Tera kufa (Mwanzo 12:4), na Tera alikufa akiwa na miaka 205 (Mwanzo 11:32), Abramu hakuwa mtoto aliyezaliwa wakati Tera akiwa na miaka 70. Abramu hakuwa amezaliwa mpaka Tera alipokuwa na walau miaka 130.

 

S: Kwenye Mwanzo 11:28, je Abram alitokea mji wa Ur, au alitokea mji wa Harani kwenye Mwanzo 24:4?

J: Hapo awali Abramu alitokea Uru ya Wakaldayo kusini mwa Mesopotamia, lakini kabla ya kwenda Kanaani, Abramu na ndugu zake kwanza waliishi mji wa Harani ulio kwenye Syria ya leo.

 

S: Kwa nini Mwanzo 11:28 inaitaja Ur ya Wakaldayo, kwa kuwa Ur ulikuwa mji wa Kisumeria?

J: Wakaldayo na Wasumeri wa Iraq walikuwa na desturi zinazofanana wakati wa Musa, na Musa aliitaja nchi ya Iraq ya leo kama ilivyojulikana wakati wa Musa. Pia, nyaraka za Ebla zinautaja mji uitwao Uru uliokuwa Padan Aram (Syria ya leo). Hivyo, kuna uhakika kuwa hapakuwa na makosa, badala ya kusema tu "Ur", inasema "Uru ya Wakaldayo."

 

S: Kwenye Mwanzo 11:28, je Abraham anaweza kuwa aliondoka kutoka mji mwingine uitwao Ur?

J: Hapana. Kulikuwa na mji karibu na Harani ulioitwa Ur / Urfa (Edessa ya leo), mji wa Wahiti ulioitwa Ura kaskazini mwa Anatolia / Armenia, na bandari ya Wahiti ambayo pia iliitwa Ura karibu na Tarso. Hata hivyo, miji hii imetajwa kwa mara ya kwanza miaka 500 baada ya Abrahamu.

 

S: Kwenye Mwanzo 11:28, tunajua nini kuhusu mji wa Uru wa Mesopotamian kutoka vyanzo vingine mbali ya Biblia?

J: Tunajua mengi kuhusu Uru, shukrani kwa uvumbuzi wa kina wa vitu vya kale. Yawezekana mji huu ndio uliokuwa mkubwa zaidi ulimwenguni wakati ule, ukiwa na idadi ya watu inayokadiriwa kufikia 180,000 na 200,000 na 300,000. Ulikuwa na umbo la mviringo, na tuta lenye urefu wa futi 3,000 na upana wa futi 800. Ilikuwa na Ziggurat yenye ngazi tatu, futi 70 juu ya uwanda. Kuta zake zilikuwa na kimo cha futi 30. Ulikuwa mji wenye utajiri, wenye kazi nzuri za sanaa. Watu wa Uru watu walikuwa na ufahamu mkubwa, na maandishi ya hisabati yanaonyesha kipeo cha tatu.

Jiografia: Uru ilikuwa na mto Frati upande mmoja, na mifereji ya maji pande nyingine. nchi ilikuwa ya alkali kiasi, lakini ilistawisha sana ngano na shayiri vilivyolimwa kwa umwagiliaji. Kulikuwa na aina 50 ya samaki katika mito ya Tigris na Frati. Hakukuwa na miti maeneo hayo, kwa hiyo waliagiza mbao kutoka umbali wa maili 400.

Ustaarabu: Karibu 40% ya nafaka zote ilitumika kutengeneza pombe. Mmoja wa michezo inaycezew kwenye mbao ulikutwa. Walikuwa na nyumba moja au mbili za ghorofa, na barabara zisizochongwa. Mara nyingi kaburi familia lilikuwa chini ya nyumba.

Uandishi: Maandiko ya kwanza ya Kisumeria yaliandikwa karibu mwaka 3200 KK, miaka 1200 kabla ya Ibrahimu. Vibao 100,000 vyenye maandishi vimegunduliwa Uru, Umma, Lagash, Puzrish-Dagan, na Nippur.

Sayansi: Jedwali la hisabati lenye kipeo cha tatu lilipatikana. Hawakuwa na mfumo desimali, lakini badala yake walitumia 1, 10, 60, 600, 3,600, 36,000 n.k. Imani ya kufanya jambo hili ni kwamba tungawanya miduara kwenye nyuzi 360. Kalenda zao zilkuwa na siku 360, na walifanya unajimu. Mnara mkuu wa Ziggurat ulijengwa vizuri sana.

Mahekalu: Mnara mkuu wa Ziggurat ulikuwa mungu kwa mwezi (si mungu mwanamke) aitwaye Nanna / Nannar kwa Kisuumeria, na Sin kwa Kiakkadia / Kisemiti. Mnara mkuu wa Ziggurat ulikuwa na dari tatu. Dari ya chini kabisa, futi 210 kwa 140 kwa 20, ulijengwa na Ur-Nammu na Dungi. Ur-Nammu aliishi karibu na wakati wa Abrahamu. Nabonido (karibu mwaka 560 KK), alijenga dari la pili, na jengo dogo lilikuwa dari la tatu. Kulikuwa na mahekalu ya E-num-Mah, Nirgal / Ningal (mke wa Nanna), na madhabahu ya Nannar.

Historia: Nasaba ya kwanza ya kifalme ya Uru (mwaka 2600-2500 KK) ilikuwa na wafalme walioitwa Mesanepada na Aanepada. Wagutia walitawala Uru kutoka mwaka 2150-2070 KK mpaka Ur-Nammu alipowapindua na kuanza nasaba ya tatu ya kifalme ya Uru. Watu wa Uru waliiteka Shushani, mji mkuu wa Waelami karibu miaka 50 baadaye. Ibrahimu aliondoka Uru kabla ya mwaka 2000. Mwaka 2004 KK (Wengine wanasema 1950 KK) Waelami waliiteka Uru, na haikuweza tena kuuresha umaarufu wake wa awali. Hivyo kama Abrahamu angeacha kumtii Mungu na kukaa Uru, ama yeye mwenyewe au watoto wake wangeweza kuwa watumwa.

 

S: Kwenye Mwanzo 11:31, je Abram alitoka Uru na kwenda Kanaani, au alitoka Harani kama Mwanzo 12:5 inavyosema?

J: Mwanzo 12 haisemi Abramu alikuwa Harani Mungu alipomwita. Haijaelezwa kuwa Mwanzo 11:31 ilitokea kabla ya Mwanzo 12. Vingi vya vitabu vya kisasa vyenye kuelezea maisha ya watu vinasimulia matukio kwa kufuata muda yaliyotokea, lakini hakuna ualazima wa kuwa hivyo, na mara nyingi hayakusimuliwa kwa kufuata muda yaliyotokea kwenye Agano la Kale na Injili. Tunaweza kuwa na uhakika kuwa masimulizi yalikusudiwa kufuata muda wa matukio kutokea pale tu mwandishi anaposema kuwa yanafuata muda yaliyotokea. Mwanzo 24:4 haisemi "nchi ya kuzaliwa kwangu" kwenye Kiebrania, bali ""nchi yangu", ikimaanisha mahali ambapo Abramu aliishi kwa muda na ambapo ndugu zake wa karibu walikuwa bado wanaishi.

 

S: Kwenye Mwanzo 12:1; 28:10-15 na 32:22-32, kwa nini Mungu aliwachagua Wayahudi badala ya Wachina ou watu wengine?

J: Awali ya yote, Mungu ana haki ya kuchagua yeyote anayemtaka. Hapa Mungu hakuchagua watu, bali mtu mmoja: Ibrahimu. Baadaye agano na uzao vilitambiliwa kupitia Isaka kwenye Mwanzo 17:21 na 21:12. Baadaye Yakobo alichaguliwa kwenye Mwanzo 26:23-24. Ibrahimu alikuwa tayari kuiacha jamii yake na mji wake (Uru), ambao huenda ulikuwa ndio mji mkubwa zaidi (watu 100,000 hadi 180,000) na mji uliostaarabika zaidi duniani kwa wakati ule. Watu wengi wana nia ya kufanya mambo sahihi, lakini watu wachache matajiri watakuwa tayari kukosa mahusiano yao na jamii zao na dini na kumfuata Mungu juu ya yote, hata mahali ambapo hawapajui (Waebrania 11:8).

Leo, Warumi 10:12 na Wagalatia 3:24 zinafundisha kuwa hakuna tofauti kwa Mungu kati ya Wayahudi na wasio Wayahudi.

 

S: Kwenye Mwanzo 12:1, je kuna ushahidi wowote, mbali ya Biblia, wa Mungu wa kweli anayejifunua kwa mtu yoyote mbali ya wakati wa Abraham au kabla ya hapo?

J: Ndio. Kwanza mambao mawili yanayohusu muktadha wa jambo hili na kisha jibu.

B1. Kwenye Mwanzo 14:18-20, Melkizedeki alikuwa mfalme wa Salemu na kuhani wa Mungu Mkuu, aliyemwita "El Elyon." Hata hivyo, hatutamhesabu Melkizedeki kwa sababu ametajwa kwenye Biblia tu, na Melkizedeki anaweza kuwa ni sura ya Kristo kabla ya kufanyika mwili.

B2. Kwenye Mwanzo 24:50, ndugu wa Abramu huko Syria (miongoni mwa Waaramea) walimwamini Bwana.

The answer:

A1. Maandishi ya Ugaritic (kutoka kwenye jamii iliyokuwa kwenye Syria na Lebanon ya leo, pia yanataja, Mungu mwenye nafsi aitwaye "El", na yametumia msemo wa "El Elyon" kwa Mungu aliye juu zaidi, kama Melkizedeki alivyofanya. Kwa bahati mbaya, kwa jamii ya Ugaritic, muunganiko wa dini tofauti ulikuwa unaendelea na hatimaye walimwabudu "Eli" kama mmoja wa miungu wengi.

A2. Huko China kabla ya Ubuddha kuja muda mfupi tu baada ya Kristo, na kabla ya Ukonfyushasi na Utao miaka mia kidogo kabla ya Kristo, waliabudu sanamu kadhaa. Lakini kabla ya hapo, walimwabudu Mungu Mkuu, waliyemwita Shang-di. Nukuu za kale zaidi zilizoandikwa za Shang-di huko China zinatoka mwaka 2600 KK, ambayo ni ya miaka 400-500 kabla ya Ibrahim! Kwa bahati mbaya, wakati wa nasaba ya kifalme ya Zhou, 1000 KK, waliamua kuwa hakuna mtu aliyekuwa mzuri wa kutosha kumwabudu Shang-di ila mfalme, na kumwabudu Shang-di miongoni mwa watu wa kawaida kulikufa. Karne chache zilizopita, Wakristo nchini China hawakukubaliana kiasi kikubwa kwamba ama Biblia ya Kichina itumie neno la jumla la mungu sheng, au pia watumie neno la kale Shang-di. Kundi la pili lilishinda, na Biblia za Kichina zinatumia Shang-di pamoja na Sheng.

Mfalme China alimwabudu Shang-di kwa kutoa sadaka ya ng'ombe dume kwenye madhabahu nyeupe ya marumaru wakati wa "Border Sacrifice" iliyorekodiwa na Wakonfyushasi kwenye Shu Jing (Kitabu cha Historia), ambapo alisema Mfalme Shun (mwaka 2256-2205 KK) alifanya. Ibada hii ilisimama mwaka 1911. Yafuatayo ni baadhi ya maneno yaliyosemwa wakati wa kutoa sadaka.

"Zamani hapo mwanzo, kulikuwa na vurugu kubwa, giza na bila umbo. Vitu vitano [sayari] zilikuwa bado kuanza kuzunguka, wala jua na mwezi kuangaza. Wewe, oh Mtawala wa Kiroho, kwanza uligawanywa sehemu zisizokuwa nzuri toka kwenye sehemu safi. Uliiumba mbingu. Uliumba dunia. Ulimuumba binadamu. Vitu vyote vyenye uwezo wa kujizalisha vilipata maisha yao." Kwa habari zaidi kuhusu Shang-di, tazama makala ya Ethel Nelson kwenye Creation ex Nihilo juzuu ya 20 na.3 June-August 1998 uk.50-53. Tazama pia The Notions of the Chinese Concerning God and Spirits uk.24-25 ya James Legge (Hong Kong Register Office 1852), na God's Promise to the Chinese (Read Books, 1997).

Wakorea wana mapokeo ya kale ya Shang-di, wanayemwita Hananim. Tan-gun kale Kikorea Mapokeo ya Tan-gun ya Korea yanasema kuwa Hananim alikuwa na mtoto aliyetaka kuishi miongoni mwa watu. Unaweza kusoma zaidi kuhusu Shang-di, Hananim, na mafunuo mengine ya kale yaliyotokea kuwa ya Mungu wa kweli kwenye kitabu kiitwacho Eternity in Their Hearts.

 

S: Kwenye Mwanzo 12:1-3,7, je Munug alitimizaje ahadi zake kwa Abraham?

J: Mungu alizitimiza bila masharti, bila kujali Abrahamu amefanya nini.

Mungu alimfanya Ibrahimu kuwa taifa kubwa. Abrahamu alikuwa mhenga wa Waisraeli na wenig wa Waarabu (Mwanzo 12:02)

Mungu alimbariki Ibrahimu. Abrahamu aliishi na kufa akiwa tajiri sana, na mwenye wazao wengi (Mwanzo 12:02)

Mungu alilifanya jina la Ibrahimu kuwa kubwa. Jina lake linaheshimiwa sana mahali popote Wakristo, Wayahudi na Waislamu wanapokuwepo (Mwanzo 12:02)

Mungu atawabariki wote wanaombariki Ibrahimu, na kuwalaani wote wanaomlaani Ibrahimu. Nchi ambazo zimewakaribishwa Wayahudi zimeona baraka kubwa, na zile ambazo zimewalaani, kama vile Ujermani ya Manaazi zimeteseka sana (Mwanzo 12:03)

Uzao wa Ibrahimu umepata nchi ya Palestina (Mwanzo 12:07)

 

S: Kwenye Mwanzo 12:1-5, je Mungu anazungumza kwa Abram hapa, au haya ni marudio ya wakati Mungu alipoongea na Abram kwenye Mwanzo 12:4b-9? (Mkristo mwenye kupinga mtazamo wa mapekeo ya kanisa alisema jambo hili kama ushahidi kuwa kitabu cha Mwanzo kimeandikwa na watu zaidi ya mmoja)

J: This is not a doublet. In Genesis 12:1-4a God commanded Abram to do something without saying whether or not Abram did it. Genesis 12:4b-9 tells us that Abram did what God said, except that Abram took Lot also.

 

S: Kwenye Mwanzo 12, je Abraham aliandika kitabu ambacho Wamormoni wanakiona kuwa ni sehemu ya Maandiko kinachoitwa Kitabu cha Abraham (The Book of Abraham)?

J: Hapana. Kwanza mambo yanayohusu muktadha wa "Kitabu cha Abraham" cha Wawamormoni na umuhimu wa udanganyifu, na kisha uthibitisho kwamba ni udanganyifu. Taarifa hii ilichukuliwa kutoka taarifa za awali kuhusu Umormoni.

Muktadha:

Kitabu cha Wamormoni cha Abrahamu ni sehemu ya Maandiko ya Umormoni "The Pearl of Great Price" (Lulu ya Thamani Kubwa). Ni msingi wa mafundisho ya Umormoni dhidi ya watu weusi, yaliyowazuia Waafrika kupata ukuhani wa Kimormoni. Mafundisho hayo dhidi ya Waafrika yalibadilishwa (na mungu wa Kimormoni?) mwaka 1978.

   Kitabu cha Ibrahimu cha Wamormoni kiliandikwa kutoka kwenye hati za kukunja za Misri ambazo Joseph Smith alizipata Julai 1835, ambazo alisema zilikuwa na maandishi ya Ibrahimu na Yusuf. Hakuijua lugha ya Misri ya kale, ambayo wachache waliweza kuisoma wakati ule. Alidai kuwa Mungu alimvuvia kutafsiri baadhi ya hati hizo kwa Kiingereza, na hivi ndivyo jinsi kitabu cha Ibrahimu kilipatikana.

   Hati hizi za Kimisri ziliwahi kudhaniwa kuwa zimepotea na kuharibiwa, lakini kumi na mmoja kati ya hizo zilipatikana kwenye makumbusho ya jiji la New York na kutolewa kwa kanisa Mormoni mwaka 1868.

Umuhimu wa udanganyifu:

Kitabu cha Mormoni kinasemekana kuwa kimetafsiriwa kutoka kwenye lugha sawa na Kitabu cha Ibrahimu. Kama Joseph Smith hakuweza kutafsiri kimoja basi hakutafsiri kingine, na hakuna maandiko yake yanayoweza kuaminiwa. Isitoshe, kama hati ni maandiko ya kipagani kwa mungu sanamu, Joseph Smith atakuwa Mtume, Nabii, na mwenye kufunua maongozi yake, sanamu ya hati.

Haya ndio maneno Joseph Smith aliyosema juu ya kutafsiri: "Tafsiri ya Kumbukumbu aa zamani, zilizofiaka mikononi mwetu kutoka kwenye makaburi ya chini ya ardhi ya Misri. - Maandiko ya Ibrahimu yaliyoandikwa kwa mkono wake mwenyewe, juu ya karatasi la mafunjo." Pearl of Great Price uk.29.

Ushahidi wa Udanganyifu:

Kuna njia tatu zinazotujulisha kuwa hizi ni hati za Misri ambazo Joseph Smith alijaribu kuzitafsiri.

1. Maandishi matatu kati ya manne ya awali yaliyoandikwa kwa mkono ya Book of Abraham yana picha zinazowakilisha maneno au silabi za Kimisri (hieroglifu) pembeni. Kati ya hieroglifu themanini zisizo za kawaida kwenye hati, 20, 13, na 10 ziliandikwa kwenye maandishi namba 1, 2, na 3 kwa mfuatano. Palipokuwa na pengo kwenye hati ya 7, 6 na 6 hieoglifu zilizotengenezwa ziliongezwa kwenye maandishi matatu. Kutokana na hili tunaweza kuwa na uhakika kuwa hati hii ya Misri ndiyo ambayo Joseph aliitumia.

2. Joseph alibuni lugha ya Kimisri. Kitabu kilichojalidi chenye kurasa thelathini na nne, kiitwacho Egyptian Alphabet and Grammar, bado kinamilikiwa na kanisa hili. Kitabu hiki cha lugha kinaelezea nyingi ya hieroglifu za Misri za kwenye hati. "Tasfiri" inayofanana sana ya Kiingereza imo kwenye Egyptian Alphabet and Grammar kama kwenye Book of Abraham. Baadhi ya watu wanaona hili kuwa moja ya mambo yanayoharibu zaidi kuvuviwa ambako Joseph alidai kuwa nako.

3. Picha mwanzoni mwa hati zote na kitabu cha Smith, Book of Abraham, ni zile zile. Tofauti pekee ni sehemu moja iliyoandikwa kwa karamu ya risasi kwenye picha ya Misri iliyosilibwa kwenye picha Mormoni. Si tu kwamba picha zimenakiliwa sawasawa, lakini maelezo ya picha namba 2 na 3 yanayongelea sanamu za Kimisri pia zimenakiliwa kwenye picha ya maandiko Mormoni.

Tafsiri halisi:

Smith alidhani kuwa anatafsiri hizi hieroglifu. Soma tafsiri halisi iliyofanywa na Dk. Klaus Baer ukurasa unaofuata. (Dialogue: A Journal of Mormon Thought: Autumn 1968 uk.119-120).

"Osiris atapelekwa kwenye Bwawa Kuu la Khons - na vile vile Osiris Hor, alizaliwa na Tikhebyt - baada ya mikono yake kuwekwa juu ya moyo wake na ‘Breathing Permit' (ambayo [Isis] aliitengeneza na aliifanya indikwe upande wa ndani na nje) ilifunikwa kitani ya kifalme na kuwekwa chini ya mkono wake wa kushoto karibu na moyo wake; sanda zake zilizobaki zinapaswa kufunikwa juu yake. Mtu ambaye kitabu hii kimeandikwa kwa ajili yake atapumua milele kama bas za miungu zinavyofanya. (Bas ni nafsi). Kwenye uk.111 Dk Baer anasema, "Joseph Smith alidhani kuwa karatasi lake la mafunjo lilikuwa na "Kitabu cha Ibrahimu."

Smith alitafsiri maelfu ya maneno ya Kiingereza kutoka kwenye hizi hieroglifu. Joseph alisema haya yalikuwa maandishi ya Ibrahimu na neno la Mungu wake. Yalikuwa ni aina nyingine ya Kitabu cha Wafu, kitabu cha miujiza cha wapagani wa Misri kilichojaa miungu wa mataifa na miungu wanawake ambao mara nyingi walizikwa na mabaki ya maiti zilizohifadhiwa.

Dr Richard Parker wa Chuo Kikuu cha Brown kwenye barua binafsi kwa Marvin Cowen ya tarehe 9 Januari 1968, alisema, "5. Nimeona herufi na sarufi za Misri za Joseph Smith. Tafsiri ya ishara zinazodaiwa kuwa za Kimisri haifanani na maana iliyopwa na wataalamu wa mambo ya Misri (Egyptologists)."

Miaka hamsini iliyopita Dk A.B. Mercer alisema, "Kila mwanafunzi wangu atakayeonyesha ujinga mkubwa namna hii wa Misri kama Smith anavyofanya, asitegemee kupata zaidi ya sifuri kwenye mtihani wa mambo ya MIsri." (Improvement Era, juzuu ya 16, uk.615). Jambo hili lingali kweli hata leo.

Dk John A. Wilson alisema, "... kwa upande wangu, naona vipande viwili au pengine vitatu tofauti vya makaratasi ya mafunjo na kila kimojawapo kinaonekana kama Kitabu cha Wafu cha kwenye mapokeo." (barua, Januari 5, 1968).

Maelezo ya kina ya picha

Baada ya hapo hebu sasa tuangalie picha tatu kwenye Kitabu cha Ibrahimu na maelezo yake yanayoendana nazo toka kwenye moja ya hati za kukunja na Times and Seasons juzuu ya 3.

Maandishi na hizi picha ni mandhari ya kawaida kabisa ya mazishi ya sanamu za Kimisri. Joseph alifundisha kuwa sura hizi zinamwakilisha Ibrahimu na Mungu halisi.

Nakala halisi 1:

Hori alimhalalisha mtoto wa mtu mwenye vyeo hivyo hivyo.

Nakala halisi 2:

Ruhusu kuwa nafsi ya Osiris Sheshonk iishi. Mimi (Min) ni ng'ombe dume lifanyalo tendo la ndo bila uliinganifu.

Kaburi hili na lisichafuliwe tena.

Nakala halisi 3:

O miungu ya. . ., miungu ya mapango, miungu ya kusini, kaskazini, magharibi, na mashariki, mruzuku ustawi Osiris Hori aliyehesabiwa haki

Hitimisho:

Mungu wa Smith alimdanganya. Tafsiri ya Joseph Smith haina thamani. Kama unamtafuta Bwana, mpendwa mfuasi wa Mormoni, tafadhali ondoka kwenye Kanisa la Mormoni, ukatae uongo wa Joseph Smith, na toa maisha yako kwa Mungu aliye juu sana kwa njia ya Yesu Kristo Mwana wake.

 

S: Kwenye Mwanzo 12:4, Abram aliwezaje kuwa na miaka 75 alipoondoka mji wa Harani baada ya Terah kufa? Kwenye Mwanzo 11:26, kwa kuwa Terah alikuwa na miaka 70 alipokuwa na watoto wake watatu, Matendo 7:4 inasema Abram aliondoka Harani baada ya Terah kufa, na Terah alikufa akiwa na miaka 205 (Mwanzo 11:32), basi watoto wake watatu wangekuwa na miaka 135.

J: Isipokuwa Abrah, Nahori, na Harani walikuwa mapacha watatu (kitu ambacho hakielekei kuwa kilikuwa hivyo), Mwanzo 11:26 inaongelea Terah kuwa na miaka 70 alipoanza kupata watoto. Abram hakuzaliwa hadi Terah alipokuwa na miaka isiyopngua 130.

 

S: Kwenye Mwanzo 12:8, je wataalamu wa elimikale wameuchimbua mji wa Ai?

J: Hapana. Hawajapata mabaki ya mji mdogo unaosemekana kuwa uliharibiwa kabisa.

 

S: Kwenye Mwanzo 12:10-19, kuna ushahidi wowote toka sehemu nyingine mbali ya Biblia wa watu kutoka Kanaani au sehemu nyingine za Mashariki ya Kati kwenda Misri?

J: Ndiyo upo. Mchoro wa kwenye kaburi kule Beni Hasan Misri unaonyesha "Waasia." Kaburi la 3, la Khnumhotep, linaonyesha Wasemiti 37 wakija Misri kwa ajili ya biashara. Walikuwa na nywele nyeusi, ndevu zilizochongwa, mavazi marefu, pinde, na vijiti vya kutupa. Wycliffe Dictionary of Biblical Archaeology uk.139 inasema mchoro huu ni wa mwaka 1892 KK.

Herufi zilifahamika kwanza kutumiwa na Wasemiti huko Misri mwaka 1800 KK, au mapema zaidi kaskazini mwa Luxor. (Angalia BAR Jan / Feb 2000, uk.12).

   Ngamia kwenye michoro ya ukutani kwenye hekalu la Hatsheput karibu na Thebe pia ilianzi wakati wa Ibrahimu.

 

S: Kwenye Mwanzo 12:10-19 je Abraham alisema mke wake alikuwa dada yake huko Misri, au Isaka alifanya hivyo huko Gerar kwenye Mwanzo 26:2-11? (Mkristo mwenye kutilia shaka maoni ya kimapokea alilieleza suala hili kama jozi inayofanana, yenye kuonyesha kuwa Kitabu cha Mwanzo kimetungwa na mtu zaidi ya mmoja).

J: Hapa siyo swala la kurudia; haya ni matukio mawili tofauti. Isaka huenda alipata mawazo haya mabaya kutoka kwene mfano wa baba yake.

 

S: Kwenye Mwanzo 12:10-20 na 20:1-18, je Mungu alimuunga mkono Abraham alipodanganya?

J: Hapana. Biblia ilirekodo kwa uaminifu, lakini kamwe haikuunga mkono uongo wa Abramu kwa sababu ya ukosefu wake wa imani kwa ulinzi wa Mungu. Hata watu wakubwa wa Mungu bado wanafanya dhambi, kwa hiyo tusivunje moyo tunapofanya dhambi.

   Mungu alimbariki Abrahamu kwa sababu ya imani yake, si kwa sababu hakuwa na dhambi, lakini alimbariki licha ya dhambi yake.

   Mungu tu ndiye mkamilifu. Lengo letu ni kujitahidi kuufikia ukamilifu, ambao tutaufikia mbinguni tu. Angalia maelezo ya Mwanzo 19:30-36.

 

S: Kwenye Mwanzo 13, je Lutu alichagua mahali ambapo Abraham ataishi, au Mungu alimpa Abraham nchi ya ahadi ili aiishi?

J: Vyote. "Kutendeka pamoja " (Concurrency) ni mafundisho ya Mungu kutumia matukio na watu, hata wapotofu na wabaya, kufanya mapenzi yake na kutimiza ahadi zake. Abramu (Ibrahim) alimruhusu Lutu kuchagua upande wa mashariki au magharibi ya Yordani, na Lutu alichagua upande wa mashariki. Ingawa Mungu aliruhusu Abramu ahamie kwenye eneo la jumla, Mungu alipanga pia kuwa Abramu apate upande wa magharibi wa Mto Jordan. Mungu alitumia uchaguzi wa Loti kutimiza mapenzi yake.

 

S: Kwenye Mwanzo 13:8, 29:15, watu hawa walikuwa ndugu ki vipii?

J: Kwenye Mwanzo 13:8 Abramu anamwita Lutu kaka yake, wakati katika Mwanzo 29:15, Labani anamwita Yakobo kaka yake. Biblia inarekodi kuwa Abramu na Labani walikuwa wanaonyesha hisia zao wa karibu na undugu wao wa damu, lakini hawakuwa mtu na kaka yake kweli.

 

S: Kwenye Mwanzo 13:12, je Lutu alipiga hema lake karibu na Sodoma, au Lutu aliishi Sodoma kwenye Mwanzo 14:12?

J: Maswali yote yanaweza kuwa kweli, kwa nyakati tofauti. Kwa sababu ya kuwa wafugaji wenye kuhamahama kunamaanisha kuwa waliweza kuzunguka maeneo mbalimbali kwa urahisi. Lutu alikuwa na hema yake mbali na Sodoma kabla ya kujitenga na kundi Abramu. Kisha alikuwa nalo karibu Sodoma, na katika eneo jirani lililodhibitiwa na Sodoma (Sodoma kubwa) baadaye. Kisha aliishi Sodoma (ama kwenye hema ama nyumba). Baadaye kwenye Mwanzo 19:3, Lutu alikuwa na nyumba Sodoma.

 

S: Kwenye Mwanzo 14:1-2, wafalme hawa ni kina nani?

J: Hii ilitokea karibu mwaka 2000 KK, hivyo si ajabu hatuwezi kuwapata baadhi ya watawala hawa. Hata hivyo, Elamu ilikuwa himaya yenye nguvuzaidi, ikiwa imeushinda mji wa Abramu wa Uru karibu mwaka 2004 KK. Shinari ni neno ambalo Agano la Kale na Wamisri walilitumia kwa Babeli. Chederlaomer inafanana na kudur (mtumishi kwa Kielami) na Lagamar (mungu mwanamke kwa Kielami). Cheder (= Kudur) ilikuwa ni sehemu ya kwanza ya jina la wafalme wengi wa Kielami. Tidali inaonekana inahusiana na jina la Kihiti, Tudhaliya na kulikuwa na angalau wafalme watano wa Kihiti baadaye walioitwa Tudhaliya. Miji ya Si-da-mu (Sodoma) na I-ma-ar (Gomora) imetajwa kwenye vibao vya Ebla vyenye maandishi viliyoandikwa mwaka 2400-2250 KK. Hatuna rekodi ya Arioko ya Ellasar, lakini kuna ushahidi huru wa kihistoria wa mfalme Ariochu wa Larsa, mji mkuu wa Sumeria. Pia, History of Israel uk.61 inasema kuwa Arriyuk(ki) au Arriwuk(ki) inafahamika Mari na Nuzi kuwa ni jina la Kihurria.

Kulingana na Yohana Warwick Montgomery kwenye Evidence for Faith uk.157, watu hapo awali walimtambua Amraphel kuwa Hammurabi, lakini hii si sahihi. Pia anasema kuwa jina Arioko linapendelewa kuliko Ariochu, kwa sababu Arioko lilikuwa jina la kawaida la wakati ule. Lilikuwa ni jina la Kihurria, pia jina la mfalme wa Mari (karibu mwaka 1750 KK), na kwenye vibao katika mji wa Nuzi (mwaka 1500 KK). Kwa kuwa lilikuwa jina la kawaida, idadi yoyote ya wafalme kutoka kwenye idadi yoyote ya majimbo madogo madogo ambayo hayajulikani katika dunia ya sasa.

Kwa muhtasari, majina haya ni ya ajabu sana; kwa ujumla majina haya hayakutumika kabisa, - isipokuwa kipindi hiki cha muda mfupi. Kuna uwezekano mdogo sana kuwa mtu yoyote angeweza kuyapata majina haya, isipokuwa walikuwa na ufahamu sahihi wa historia ya wakati huo.

 

S: Kwenye Mwanzo 14:1-2, ingewezekanaje kuwa na "umoja" wa wafalme ukishiriki vita?

J: Yaelekea palikuwa na jumuiya kadhaa za ushirikiano wa wafalme kabla ya kuanguka kwa dola ya mji wa Uru mwaka 2004 KK. Yaelekea kulikuwa na jumuiya chache sana za ushirikiano wa wafalme baada ya kuinuka kwa Hammurabi wa Babeli ya Kale karibu mwaka 1700 KK. Hata hivyo, kati ya muda ambao Waelami waliiharibu Uru mwaka BC 2004 KK, na Waelami kuivamia Babeli mwaka 1725 KK, Montgomery anaonyesha kuwa jumuiya za ushirikiano wa waflme zilikuwa jambo la kawaida.

Hakuna mtu katika wakati wa Musa ambaye angejaribu kufanya historia ya kuaminika ya jumuiya za ushirikiano wa wafalme, kwa sababu milki zenye umoja imara zilitawala. Kwa mtu kutaja jumuiya za ushirikiano wa wafalme kama hii inaonyesha kuwa alikuwa na ufahamu sahihi wa kipindi cha muda huo. Kwa mujibu wa Evidence for Faith uk.157-164, barua iliyokutwa Mari inaeleza umoja wa wafalme kumi, kumi na tano, na ishirini. Pia, jumuiya nyingine tano zinafahamika.

 

S: Kwenye Mwanzo 14:1-17, je kuna ushahidi wowote mbali ya Biblia wa Sodoma, Gomorrah, na miji mingine?

J: Ndiyo. Awali hapakuwa na ushahidi wowote hadi wataalamu wa elimukale walipokuta vibao vya vyenye maandishi vya Ebla. Vinamtaja si-dam-mu (Sodoma) na sa-ba-i-im (Zeboiim). (Julius Africanus, mwaka 200-245 BK, anaiita hii Seboim. Kwa maelezo ya vibao vyenye maandishi vya Ebla tazama Ready with an Answer : For the Tough Questions About God uk.282-286.

 

S: Kwenye Mwanzo 14:5, Ashteroth-Karnaim ina maanisha nini?

J: Kuna vitu viwili vinavyowezekana hapa kwa mujibu wa Wycliffe Bible Dictionary uk.160 na New Bible Dictionary (Eerdman's 1962) uk.97.

1. Inaweza kumaanisha Ashtarte mwenye pembe mbili, kwa kuwa mungu huyu mwanamke alionyeshwa akivaa pembe mbili huko Gezeri na Beth-Shan.

2. Kuna uwezekano mkubwa zaidi kuwa inamaanisha mji wa Ashteroth ulio karibu na Karnaim, kuutofautisha na miji mingine iliyopewa jina la mungu huyu mwanamke..

 

S: Kwenye Mwanzo 14:5-6, 36:20, na Kumbukumbu 2:12,22, Wahori ni kina nani?

J: Wahori walitokea Armenia ya leo, kwa mujibu wa Archaeological Encyclopedia of the Holy Land uk.176. Walielezwa kwanza wakati wa Sargon wa Akadi kwenye karne ya 24 KK.

 

S: Kwenye Mwanzo 14:14, je Abram na washirika wake waliwezaje 318 tu waliwezaje kulishinda jeshi la ushirikiano wa wafalme wakubwa 4 lililowavamia?

J: inaonyesha kuwa hii haikuwa vita iliyoandaliwa na kupiganwa mahali palipoandaliwa. Yaelekea haya yalikuwa mashambulizi ya kushtukiza ya usiku yaliyofanywa na askari wapanda farasi kwenye jeshi ambalo halijajiandaa. Mungu atakuwa aliwasaidia pia.

 

S: Kwenye Mwanzo 14:14, je mashambulizi ya Abram yanafananaje na mashambulizi mengine ya kushtukiza katika historia?

J: Jeshi linaonekana Kurudi kutoka Dan kwenda Dameski, karibu umbali wa maili 40 (64 km), hivyo jeshi la Abramu lilishinda "uwanja wa mapambano." Hebu tuangalie mashambulizi ya kushtukiza, mashambulizi dhidi ya majeshi kubwa, na kisha tuangalie jambo hili kwa mtazamo wa maadui. Baadhi ya namba hizi zinatoka Encyclopedia Britannica.

Kwanza tutaangalia mashambulizi ya kushtukiza.

Kwenye Mapambano ya San Jacinto mwaka 1836, Sam Houston na askari 743 wasio na uzoefu alifanya uvamizi wa mchana kwa kwa askari 1800 wa Mexico na alishinda.

Kwenye Mapambano ya Trenton, Washington alivuka mto Delaware usiku akiwashangza askari wa kukodiwa wa Hessia na kuwateka 1,000 miongoni mwao.

Huko Teutoberg Wald, Arminius Mjerumanai aliwaua askari 14,000 wenye uzoefu wa Kirumi kwenye mapigano ya kushtukiza.

Sasa hebu na tuangalia ushindi dhidi ya watu wenye ubora mkubwa sana.

Kwenye Mapigano ya Marathon mwaka 490 KK, Wagiriki 10,000 waliwashinda Waajemo 20,000.

Canae, mwaka 216 KK, Wacharthagini 56,000 (wakiwa na askari wapanda farasi) waliwashinda Warumi 86,000.

al-Qadissiyat, mwaka 636/7 BK, Waislam 30,000 waliwashinda Waajemi 120,000.

Pharsalus, mwaka 48 KK, Julius Caesar na askari 20,000 alimshinda Pompey na askari 45,000.

Dorylaeum, mwaka 1091, 70,000 wapiganaji wa Vita vya Msalaba (Crusaders) waliwashinda Waislam 250,000, wakiwaua karibu watu 30,000 miongoni mwao. (Crusaders walikuwa na silaha, lakini askari wa Abramu wanaweza kuwa walikuwa na silaha wakati jeshi la wavamizi lilitupa silaha zao).

Alexander Mkuu dhidi ya Waajemi, Julius Caesar dhidi Wagauli na Helvetians, Belisarius, Napoleon, na wengine pia walishindwa majeshi makubwa sana, ingawa kwa kiwango kikubwa. Hatuna idadi ya majeshi haya, isipokuwa kuwa Julius alikuwa na watu 10,000 alipoivamia Uingereza.

Mtazamo wa maadui: Fikiri kuwa uaskari wa Kielami, umechaguliwa kuwa sehemu ya kundi la watu maarufu kwenda kwenye misheni mbali sana kuiadhibu Sodoma. Unajua kuna idadi kubwa ya adui nje tu ya hema lako, lakini ni mateka; wasiokuwa na silaha na wanalindwa vizuri sana. Katikati ya usiku unaamshwa na askari wanaopanda farasi kutoka kwa adui mpya asiyejulikana anayepita kwa haraka sana na kuua washirika wako. Si tu kwamba wanafanya hivyo, lakini kama wakiwafukuza wanyama wako, au wakiwaachia huru na kuwapa silaha mateka, basi hali yako itakuwa mbaya. Unafanya jambo la busara na kukimbia uelekeo tofauti wa mashambulizi, unajikusanya upya na washirika wako baadaye.

Bila shaka, mbali na sababu hizo zote, yawezekana kuwa Mungu aliwasaidia askari wa Abram ili alete hofu na kuwakimbiza maadui. Kwa mfano mkuu zaidi wa Mungu kusaidia kufanikisha mashambulizi ya kushtkiza angalia vita ya Gideoni na Wamidiani kwenye Waamuzi 7:6-25.

 

S: Kwenye Mwanzo 14:18-19, Melkizedeki, anayedhaniwa kuwa Mkanaani aliyelaaniwa, aliweza kumbariki Ibrahim?

J: Melkizedeki ni mtu wa kushangaza kwenye Biblia. Baadhi ya watu wanafikiri Melkizedeki alikuwa ni muonekano wa Kristo kabla ya kufanyika mwili. Wengine wanasema Melkizedeki alikuwa ni mcha Mungu (labda Mkanaani au si Makanaani) ambaye alikuwa ni mfano wa Kristo. Hata kama Melkizedeki alikuwa Mkanaani, Mungu hajazuiliwa kuwafundisha na kuwatakasa watu mataifa yoyote.

Kama nyongeza, dhehebu la Kiyahudi kuea Qumran liliweka umuhimu mkubwa kwa Melkizedeki kama mkombozi toka mbinguni ambaye atatangaza wokovu wa Mungu.

 

S: Kwenye Mwanzo 14:18, mji wa Yerusalemu una miaka mingapi?

J: Tunadhani ulianzishwa mwaka 3000 KK. Kumbukumbu za kale za Misri zinauita mji huu "Urusalim", kitu ambacho kinamaanisha kuwa sehemu ya "salem" ya Yerusalemu ni ya muda mrefu angalau kama sehemu ya "Jebus."

 

S: Je Mwanzo 14:18 inafundisha "ukuhani wa Melkizedeki" kwa watu kama Wamormoni wanavyofundisha?

J: Hapana. Mwanzo 14 inamsema tu mtu mmoja aitwaye Melkizedeki. Waebrania 7:23-24 inasema huyu Melkizedeki alikuwa mfano wa Yesu. Hakuna sehemu kwenye Biblia inayosema kuwa tunahitaji makuhani wowote zaidi mbali ya Yesu.

 

S: Kwenye Mwanzo 15, agano ni nini hasa, na ni kwa namna gani agano la Mungu na Abraham halikuwa la kawaida?

J: Agano ni makubaliano ya pamoja kati ya pande mbili; pande hizi zinaweza kuwa sawa, kama makubaliano ya biashara, au zinaweza kuwa kati ya mfalme mwenye nguvu zaidi na kibaraka. Pamoja na kuwa agano kati ya Mungu na mwanadamu, agano hili halikuwa la kawaida kwa sababu ilikuwa ni ahadi ya upande mmoja tu wa Mungu; Ibrahimu hakuhitaji kufanya kitu chochote.

 

S: Kwenye Mwanzo 15, je Mungu alifanya agano na Abram hapa, au kwenye Mwanzo 17 baada ya Ishmael kuzaliwa? (Mkriso mwenye kutilia shaka mapokea alileta jambo hili kama ushahidi wa watunzi zaidi ya mmoja wa Kitabu cha Mwanzo)

J: Yote agano la awali kwenye Mwanzo 15 na uthibitisho wake baadaye kwenye Mwanzo 17 ni ya kweli. Kwenye Mwanzo 15, Mungu alifanya agano rasmi na Abramu na kulikamilisha kwa dhabihu na kisha alimuahidi mtoto. Kwenye Mwanzo 17:2, baada ya Ismail kuzaliwa, Mungu alithibitisha agano lake na Abramu, na ishara yake ilikuwa ni tohara. Uthibitisho wa ahadi hiyo muhimu ulifanyika hapa kimsingi, kwa sababu Mungu alihitaji kusahihisha mawazo ya Abramu. Abramu alifikira kwa makosa kwamba ahadi za agano zitatimia kwa njia ya Ishmaeli.

Kwa mfano ya pili wa kuthibitisha agano, baada ya Mungu kuruhusu Waisraeli washindwe huko Ai, walithibitisha agano alilofanya katika mlima Ebali kwenye Yoshua 8:30-35.

Wakati mwingine Mkristo, ambaye tayari amefanya agano na Mungu, anapaswa apate muda wa kuthibitisha agano lake pia.

 

S: Kwenye Mwanzo 15:2, kuna jambo gani lisilokuwa la kawaida kwenye jina la Eliezar?

J: Huenda hakuna, lakini Expositor's Bible Commentary juzuu ya 2, uk.131-132 inasema "si rahisi kuwa bahati tu" kuwa thamani ya herufi za jina la Elieza kwa Kiyahudi ni 318, idadi hiyo hiyo ya askari ambao Ibrahimu alikuwa katika Mwanzo 14 : 14.

 

S: Kwenye Mwanzo 15:12, je Abraham alikosea kwa kutokuwakata ndege vipande viwili, kama Mch. Moon anavyofundisha kwenye Divine Principle toleo la 5, 1977, uk.269, 507?

J: Hapana. Makuhani hawakutakiwa kukata ndige vipande viwili kwenye Walawi 1:17 na 5:9.

 

S: Kwenye Mwanzo 15:13, je Waisraeli walikuwa Misri miaka 430, au waliteswa kwa muda wa miaka 400?

J: Yote ni sawa. Tazama maelezo ya Matendo 7:6 juu ya jinsi Waisraeli waliivyoishi Misri miaka 30 kabla hawajawa watumwa kwa miaka 400.

 

S: Kwenye Mwanzo 15:16, je Waisraeli waliwezaje kuwa watumwa kwa vizazi vinne tu, kwa kuwa walitumikishwa kwa muda wa miaka 400 kwenye Mwanzo 15:13?

J: Kwenye Mwanzo 15:13,16, Ibrahimu, ambae anaweza kuwa alielewa kizazi kuwa kama miaka 100, aliambiwa: miaka 400, vizazi 4. Musa kwa mfano, aliishi miaka 120.

 

S: Kwenye Mwanzo 15:16, je Kutoka kwa Waisraeli Misri kulitokea kwenye kizazi cha nne, au sita kama 1 Nya 2:1-9 na Mt 1:3-4 zinavyodokeza?

J: Kuna mambo mawili ya kuyazingatia kwenye jibu la swali hili.

1. Hii yote inategemea na urefu wa muda unaofikiri kizazi kinao. Ibrahimu na Sara walimpata Isaka wakati walipokuwa na miaka 101 na 91. Mungu alikuwa akizungumza na Ibrahimu hapa.

2. Kwa kubuni, hakutakuwa na makosa hata kama Biblia ilisema ingekuwa namba yoyote, ilimradi kifungu hicho hicho kinafafanua kizazi kiusahihi. "Vizazi vinne" kwenye Mwanzo 15:16 vinaelezwa kutumikishwa kwa "miaka 400" kwenye Mwanzo 15:13.

 

S: Kwenye Mwanzo 15:17 na 19:23, kwa nini Biblia inasema kuwa jua "linaenda chini" na "linaenda juu"?

J: Nitawaambieni baada ya jua kuzama. Kama ambavyo tunatumia nahau za kawaida na lugha ya mtaani kujieleza, Biblia hutumia nahau za Kiebrania na Kigiriki, pia.

S: Kwenye Mwanzo 15:18, je Mto wa Misri n upi?

J: Huu si Mto Nile, bali kijito kidogo kinachoitwa Wadi el-Arish, ambacho kiko upande wa mashariki wa Rasi ya Sinai. The New Geneva Study Bible uk.35 na The Nelson Study Bible uk.33 zinasema kinaweza kuwa ama Wadi el-Arish ama tawi la mashariki la Mto Nile.

 

S: Kwenye Mwanzo 15:18, kwa kuwa Mungu aliwapa uzao wa Abram nchi yote hadi Mto Frati, kwa nini hawakuipokea nchi hiyo?

J: Falme za Daudi na Suleimani zilipanuka hadi Mto Frati. Pia zinaweza kuja kuwa na nchi kwenye Utawala ujao wa Yesu hapa duniani wa miaka Elfu moja.

 

S: Kwenye Mwanzo 16:1, kwa kuwa Abraham na Sarai hawakuwa na watoto, Abraham aliwezaje kupata watoto zaidi baada ya Isaka? (Muislam mmoja aliuliza swali hili)

J: Mwanzo 16:1 inaonyesha kuwa ilikuwa Sarai, sio Abraham, aliyekuwa tasa. Abraham alikuwa na watoto zaido, lakini Sarai hakuwa nao.

 

S: Kwenye Mwanzo 16:1-4, je Abraham alizini na Hajiri?

J: Hapana, Ishmael hakuwa matokeo ya zinaa; hakuwa mtoto haramu. Mambo manne ya kuyazingatia katika jibu la swali hili.

Masuria waliruhusiwa: mitala iliruhusiwa katika Agano la Kale, na Sarah alimtoa Hajiri kuwa suria wa Abrahamu. Kwa hiyo jambo ambalo Abrahamu alilifanya lilikuwa "halalo" kulingana na jinsi Mungu alivyomfunulia na baadaye Sheria ya Musa, na hata sheria ya Mesopotamia ya wakati ule.

Mifano inyofanana na huo: Zaidi ya hapo jambo hili si la ajabu sana kama linavyoweza kuonekana kuwa kwa baadhi ya wasomaji wa leo. Mifano kama hiyo ya mjakazi kuchukua nafasi ya mke mwenye matatizo ya uzazi inapatikana kwenye sheria za Hammurabi, vibao vyenye maandishi vya Nuzi, vibao vya Alalakh, na vibao vya Mari. Hata hivyo, kama jambo lina kawaida ya kufanywa na "limeruhusiwa kisheria", haimaanishi kuwa linampendeza Mungu. Mwanzo 16:4-5 inaonyesha kuwa Sarah alijutia kitendo chake muda si mrefu.

Hajiri aliringia hadhi yake mpya: Zaidi ya hayo, Hajiri alipokuja kuwa mke wa Abramu, hakukataa. Hajiri aliringia ujauzito wake na kumdharau Sarai (Mwanzo 16:4, 5). Katika Agano la Kale, ingawa kuoa mateka kuliruhusiwa, hakuna sehemu ngono nje ya ndoa ilihalalishwa bali lilichukuliwa kuwa uovu wa uasherati.

Kwa upande mwingine, Waislam wameruhusiwa kuwalazimisha mateka wao kufanya nao ngono hata kama hawajawaoa. Angalia Bukhari juzuu ya 3 na.113, 432; juzuu ya 9 kitabu cha 93 sura ya 18 na.506, uk.372; Sahih Muslim juzuu ya 2 na.3371-3374; Abu Dawud juzuu ya 2 na.2150, 2167 kwa habari zaidi.

Hitimisho, Mungu ni mtakatifu, Abraham hakuwa mzinzi, na Wakristo wana viwango vikubwa vya utakatifu kuliko alivyokuwa navyo Muhammad kwa washiriki wake kwenye Hadithi.

 

S: Kwenye Mwanzo 16:1-8, kwa kuwa Hajiri alikuwa mjakazi, je tendo la ndoa la Abraham na yeye lilikuwa ubakaji, kama baadhi ya Waislam walivyoruhusiwa kufanya kwenye dini yao? (Tazama Bukhari Hadiths juzuu ya 3 na.113, 432)

J: Mwanzo 16:4 inasema Hajiri alikuja kuwa mke wa Abramu, na hakukataa. Hajiri aliringia ujauzito wake na alimdharau Sarai (Mwanzo 16:4, 5). Katika Agano la Kale, ingawa kumoa mateka kuliruhusiwa, hakuna mahali paliporuhusu ngono nje ya ndoa bali kuiona kuwa uasherati mkuu.

 

S: Kwenye Mwanzo 16:3; 17:20 na 21:13, kwa kuwa Hajiri alikuwa mama wa Ishmael, je jambo hili linamaanisha alikuwa mama wa Muhammad?

J: Hajiri suria wa Ibrahimu na mwanawe Ishmaili wametajwa kwenye Biblia. Hata hivyo kuna utata kuhusu ‘Adnan (mhenga wa Muhammad) kuwa mzao wa Ishmaili. Mwana historia wa Kiislam aliyatajwa hapo awali al-Tabari juzuu ya 6, uk.37 inasema, "nasaba hazihitalifiani kuhusu uzao wa Nabii wetu Muhammad kwa mujibu wa Ma'add b. ‘Adnan, ... wanatofautiana kuhusu kitu kinachofuata baada ya hapo." Hata hivyo, mwishoni hili ni jambo linalokusudia kupotosha watu, kwa sababu kuwepo kwa Ishmaeli kwenye Biblia hakuthibitisho kuwa Muhammad anatoka kwa Mungu.

 

S: Kwenye Mwanzo 17:1; 28:3; 35:11; 43:14; 48:3 na Kutoka 6:3, jina El Shaddai linamaanisha nini hasa?

J: El-Shaddai ni jina la Mungu ambalo maana yake halisi ni El "Mungu" Shaddai "Mwenyezi." Jina hili ni moja ya majina makubwa ambayo Abrahamu, Isaka na Yakobo waliyajua. Ingawa walikuwa wamefunzwa jina "halisi" kuwa ni Yahwe (ambalo huenda wakawa hawakufunzwa), Mungu mwenyewe hakujifunus kwao na kama Yahwe kama alivyofanya kwa Musa kwa kujibu wa Kutoka 6:2, 3.

Majina ya Mungu yanatumika kwa Yesu kama mmoja wa Utatu Mtakatifu, lakini hakuna swali kuwa El Shaddai inatumika kwa Yesu zaidi ya kwa Baba au Roho Mtakatifu.

Neno la Kiebrania el lilitumika ssawa na jinsi neno la Kiingereza "Mungu / mungu" linavyotumika leo. Tunamwita Mungu Mmoja Mwenyezi na Muumba kuwa Mungu, tunaziita sanamu kuwa "mungu", n.k. Neno Shaddai (Mwenyezi) bila el linatumika kwenye Mwanzo 49:25 na Hesabu 24:4, 16; Ruth 1: 20, 21 mara 31 kwenye Ayubu 5:17-40:2 na Zaburi 68:14 na 91:1. Baadhi ya wakosoaji wenye kuutilia shaka msimamo wa kimapokea wanadai kuwa El-Shaddai lilitokana na neno la kipagani linalotumika kwa "mungu wa mlima", lakini hakuna ushahidi kuwa Biblia inamaanisha hivi.

El Shaddai inatumika kwenye kitabu cha Mwanzo kwa Ibrahimu kwenye 17:1, na Yakobo kwenye 28:3, 35:11, 43:14, 48:3; na Musa kwenye kitabu cha Kutoka 6:3.

Majina ya Mungu sawa na hili ni El Elyon "Mungu Mkuu Zaidi" lililotumiwa na Melkizedeki kwenye Mwanzo 14:18 na Hesabu 24:16, Kumbukumbu 32:8, 2 Samweli 22:14, Zaburi 9:2, Isaya 14:14; Maombolezo 3: 35, 38), El Hai "Mungu aliye Hai" Yoshua 3:10, au tu El "Mungu" kwenye sehemu nyingi.

 

S: Kwenye Mwanzo 17:5 kubadilisha jina toka Abram kuwa Abraham kuna umuhimu gani?

J: Jambo hili linaweza kuchukuliwa kuwa "Utani unaokuwa kweli." Wakati Abramu inamaanisha "baba", jina la kejeli kwa mtu asiyekuwa na mtoto, Ibrahimu inamaanishaa ya "baba wa umati wa watu." Kama 735 Baffling Bible Questions Answers uk.39 inavyosema, "Tunaweza kuwasikia watu wenye kucheka kwa kujificha wakati Abramu asiye na mtoto akitangaza kwa wachungaji wake wengi na familia zao kwamba kuanzia sasa atakuwa anaitwa Ibrahimu." Kuwa na watoto lilikuwa jambo la muhimu sana katika jamii ya kale, lakini unaweza kuona jinsi imani ya Abrahamu kwa Mungu inavyoweza kumfanya achekwe kirahisi. Hata hivyo, Mungu alitimiza ahadi yake, na Ibrahimu mbinguni aliweza kuutabasamia "utani ambao Mungu alimfanyia kutimiza haja ya moyo wa Ibrahimu."

 

S: Kwenye Mwanzo 17:12, kwa nini Mungu aliamuru kutairiwa kufanyike siku ya nane barabara?

J: Maandiko hayasemi. Hata hivyo, watoto waliotoka kuzaliwa hawawi na damu inayoweza kuganda sawa na watu wazima. Baada ya kula na kutumia vitamini K, damu yao ina prothrombin zaidi, ambayo hutumiwa kufanya damu igande. Kwa watoto ambao hawajachomwa sindano za vitamini K, viwango vya prothrombin huongezeka siku ya nane.

Kama nyongeza, Wycliffe Bible Dictionary uk.354 inarekodi kuwa Wamisri walifanya tohara ya wanaume; picha moja inaonyesha tohara ikiwa inafanywa kwa mvulana mwenye miaka 13. Inasema kwamba watu wengi wa Kisemitiki walifanya tohara, isipokuwa wa Wafilisti, Wababeli, Waashuri, na Waedomi baadaye. Waarabu, ambao asili yao hutoka kwa Ismail, pia walifanya tohara kabla ya Uislamu.

 

S: Kwenye Mwanzo 17:12, watu gani wengine walifanya tohara?

J: Mwana historia wa Kigiriki Herodotus kwenye kitabu chake History kitabu cha 2 sura ya 104, uk.69 anasema kuwa ni Wamisri, Warthiopia, na Wakolkia (Colchians) tu waliofanya tohara. Anadai kuwa Wakolkia walihama kutoka Misri. Pia alisema baadhi Wafoeniki na Washami walifanya jambo hili hili, wakidai kuwa wamejifunza kutoka kwa Wamisri.

   Mwandishi wa zamani Bardesan (mwaka 154-224-232 BK) alisema kuwa watu wa jimbo la Kirumi la Arabia walifanya tohara, lakini Warumi waliwalazimisha kuacha wakati walipoliteka jimbo hilo. Habari hii imo kwenye Book of the Laws of Diverse Countries uk.730.

 

S: Kwenye Mwanzo 17:17 na 18:12, je Abraham na Sara walicheka kwa kutokuamini, au Sara alicheka kwa furahia kwenye Mwanzo 21:6?

J: Aya zote hizi zinakamilishana. Abraham na Sara walicheka kwa kutokuamini kabla Isaka hajatungwa tumboni. Wakati mwingine mtu anapotaka kitu fulani sana, na mtu mwingine anajitolea kumpa, asili ya binadamu inaweza kumfanya asiamini na kucheka ili kujilinda dhidi ya kukatishwa tamaa.

Hata hivyo, Sara alicheka tena kwa furaha Isaka alipzaliwa.

S: Kwenye Mwanzo 17:17 na 18:12-15, kwa nini Mungu alimkaripia Sara kwa kucheka na si Abraham?

J: Kucheka kwa mshangao mara unapojifunza kitu fulani ni tofauti na kucheka kwa kutia mashaka mara nyingine zifuatazo baada ya kuwa tayari umeambiwa. Neno la Kiebrania la kucheka, sahaq, linamaanisha vitu vyote hivi viwili.

S: Kwenye Mwanzo 17:19, je mtoto wa ahadi wa Abram aliitwa Isaka hapa, au kwenye Mwanzo 21:3?

J: Kabla ya kuzaliwa kwa Isaka, Mungu alisema aitwe Isaka kwenye Mwanzo 17:19. Biblia haisemi kama walimwita hivyo au la. Kwenye Mwanzo 21:3, baada ya Isaka kuzaliwa, walimwita Isaka. Ni kama vile malaika Gabriel alivyomwambia Maria kumpa mwanae jina la Yesu, na baada ya kuzaliwa, walitii maagizo ambayo malaika aliwapa.

 

S: Kwenye Mwanzo 17:27, kwa nini Abraham aliwatahiri wanaume wote waliozaliwa kwenye nyumba yake, ikiwa ni watumwa au watu huru?

J: Ibrahim hakujali watoto wake tu kuwa sehemu ya familia ya agano la Mungu duniani, bali watu wote walio nyumbani mwake. Hii inaonyesha kuwa watoto wao pia watakuwa sehemu ya washiriki wa agano la Mungu.

   Philo Myahudi (mwaka 15/20 KK hadi 50 BK) alitoa jibu hilohilo kimsingi kwenye Questions and Answers on Genesis, III (62) uk.863.

 

S: Kwenye Mwanzo 18, je kujifunua kwa Kristo (Christophanies) na kujifunua kwa Mungu (Theophanies) kwenye Agano la Kale kulikuwa ni nini?

J: Kujifunua kwa Kristo ni neno lenye kuelezea kutokea kwa Kristo hapa duniani, kabla ya kuzaliwa kwake na Maria. Kujifunua kwa Mungu ni kuonekana kwa Mungu, iwe ni Baba, Mwana, Roho, au Utatu Mtakatifu. Kwa kuwa baadhi ya watu hawakubaliani kujifunua kwa Kristo dhidi ya kujifunua kwa Mungu, na wakati mwingine haieleweki vizuri endapo malaika ni muonekano wa Kristo au malaika tu, ifuatayo ni orodha ya kujifunua kwa Mungu kwenye Agano la Kale.

Katika Bustani ya Edeni kabla ya anguko (Mwa 1:29-3:24)

Melkizedeki anaweza kuwa ni kujifunua kwa Mungu (Mwa 14:18-20)

Wageni watatu wa Ibrahimu (Mwa 18:1-33)

Kutokea kwa Mungu kwa Abramu (Mwa 17:1-2)

Ngazi ya Yakobo huenda isiwe kujifunua kwa Mungu kwani hii ilikuwa ndoto tu (Mwa 28:12-15)

Mapambano ya Yakobo na malaika huenda yasiwe kujifunua kwa Mungu (Mwa 32:30)

Kutokea kwa Mungu kwa Yakobo huko Betheli (Mwa 35:9-15)

Musa na kichaka kinachoteketea kwa moto (Kut 3:2-22)

Wingu nene (Kut 19:9)

Katika Mlima Sinai (Kut 19:11-12; 24:10)

Musa kuona upande wa nyuma wa Mungu (Kut 33:19-20)

Yoshua na Kamanda wa jeshi la Bwana (Yos 5:13-15)

Gideon kumwona malaika (Amu 6:11-24)

Kutokea kwa malaika kwa mama wa Samsoni (Amu 13:3-5)

Wingu juu ya sanduku la Agano (1 Fal 8:11-13)

Eliya kwenye ufa wa mwamba (1 Fal 19:9-18)

Kuondoka hekaluni (Ezekieli 10:3-18), na Isaya 6 pengine havihusiki kwa sababu haya yalikuwa ni maono.

 

S: Kwenye Mwanzo 18:2, kwa kuwa Abraham aliinama mbele ya wafalme, je jambo hili linaunga mkono desturi ya Wakatoliki na Waothodoksi ya kuinama mbele ya sanamu?

J: Hapana, kuheshimu sanamu hakuungwi mkono na Biblia kwa sababu hatutakiwi kuchonga sanamu kwa ajili ya kuziabudu kwa mujibu wa amri ya pili. Hata hivyo, bila kujali imani ya mtu kuhusu kuheshimu sanamu, aya hii haiwezi kutumiwa kuunga mkono kuziinamia sanamu. Tofauti na picha,

1. Ibrahimu aliinama ili kuonyesha heshima kwa mtu halisi.

2. Ibrahimu alikuwa anaonyesha heshima kwa mfalme wa kipagani, hapakuwa na namna yoyote ya kutukuza au kutoa heshima ya kidini.

3. Abrahamu hakuomba kwa hawa wafalme. Pia hakuomba kwa Mungu kupitia kwa wafalme hao, kama Waorthodoksi wanavyodai kuomba kwa Mungu kupitia sanamu.

   Msomaji mmoja alidai kuwa kutukuza hakuna tofauti na kutoa heshima kwenye Uorthodoksi. Hata hivyo, jambo hili si kweli, kwa sababu Waorthodoksi huomba sanamu (au kwa usahihi zaidi kupitia) kwa Mungu, na watakatifu mbalimbali. Lakini pamoja na hayo hawachukui wake zao, mtoto, wazazi au mtu mwingine wanaye muheshimu, au kumweka mbele yao, na kumwomba.

 

S: Kwenye Mwanzo 18:10, 14 na 21:1,2, je aya hizi zinafundisha kuwa Mungu alimpa Sarah ujauzito, kama Born Again Skeptic's uk.217 inavyodai?

J: Hapana. Mtu huyu asiyeamini uwepo wa Mungu alishindwa kufahamu kuwa Mungu hakuwa anarudi kumpa Sarah ujauzito, bali Mungu alirudi baada ya mtoto kuzaliwa. Mungu alisema vitu vitatu tu kuhusu mtoto wa Sara.

1. Mungu angewatembelea tena mwakani kama ambavyo Mwanzo 18:10, 14 inasema

2. Mungu angetimiza ahadi yake ya Sarah kuwa na mtoto kama ambavyo Mwanzo 21:1 inasema.

3. Jambo la muhimu zaidi, mtoto atatoka kwa Ibrahimu (Mwanzo 17:15,17). Kwa usahihi zaidi, mtoto alitoka kwenye mwili wa Ibrahimu mwenyewe kama ambavyo Mwanzo 15:4 inasema.

 

S: Kwenye Mwanzo 19, je dhambi halisi ya Sodoma na Gomorrah ilikuwa kukosa ukarimu kama Ezekiel 16:49 inavyosema?

J: Mashoga wengi hunukuu Ezekiel 16:49 lakini wanapuuzia Ezekiel 16:50, ambayo inataja "kufanya machukizo." Mwanzo 19:5-7 inasisitiza ushoga. Yuda 7 pia anaongelea uasherati na mambo yasiyo ya asili. Mwanzo 13:13 inaonyesha kuwa maovu ya Sodoma yalitokea kabla ya Loti kuwasili.

 

S: Kwenye Mwanzo 19:8, kwa nini Lutu aliwatoa mabinti wake mabikira kwa umati wa watu? (Mtu asiye amini uwepo wa Mungu aliuliza swali hili)

J: Maandiko hayatuambii nia ya Lutu ya kufanya kitendo hiki kiovu, lakini tunaweza kuona mambo matatu.

1. Lutu alikuwa katika hali ya kukata tamaa, na pengine alishikwa na hofu.

2. Watu wa Sodoma hawakuwataka mabinti wake

3. Lutu aliishi Sodoma kwa muda mrefu, na Lutu huenda alijua kuwa watu hawa hawakuwataka mabinti wake. Lutu huenda alikuwa anajaribu kuwazuia.

Biblia haiungi mkono kitendo cha Lutu hapa; inakisimulia tu. Kama Biblia ingekuwa "propaganda" tu, basi ungetarajia isimulie mambo yote chanya na kutokutaja kitu chochote hasi. Hata hivyo, Biblia si propaganda bali ni neno la kweli la Mungu, na inasema kwa uaminifu kuhusu maisha ya watu, ikiwa pamoja na mambo yasiyofurahisha.

 

S: Kwenye Mwanzo 19:24-26, Sodom na Gomorrah ziliangamizwaje hasa?

J: Biblia inasema tu kuwa Bwana alinyesha moto wa kiberiti, na mke wa Lutu aliyebaki nyuma aligeuka na kuwa nguzo ya chumvi. Ingawa hatuna maelezo zaidi, tunajua kwamba eneo hili lina utajiri wa madini (petroli) na lami karibu na uso wa nchi. Fikiria dhoruba, upepo, na umeme ambavyo vinaweza kusababisha moto kwenye madini. Moto utakaotokea unaweza kuleta upepo wake wenyewe, na eneo lote litakuwa sehemu ambayo hautapenda uwepo.

 

S: Kwenye Mwanzo 19:26, je tunajua kitu chochote kuhusu watu wengine toka wakati huo zaidi ya mke wa Lutu aliyefanyika "nguzo ya chumvi"?

J: Kimwili, watu (na mbwa) wamekuwa wakiuawa mara moja na kufunikwa na majivu huko Pompeii Mlima Vesuvius ulipokuwa unalipuka. Bila shaka jambo hili lilitokea pia kwenye milipuko mingine mikubwa.

Kwa kuongea kwa mfano, mke wa Lutu alifanywa kuwa mgumu hata kushindwa kufikiri vitu vingine kwa ajili ya upendo wake wa maisha (ya Sodoma) aliyokuwa anayaacha. Watu wengi toka wakati ule , wamekuwa wakifanywa wagumu kwa upendo wao wa dunia pia. Kama mifano dhahiri, watu waliolemazwa na matumizi ya madawa ya kulevya wanapotafuta kulewa, walevi wa pombe wapotafuta kunywa, huwa hawafahamu furaha rahisi ya maisha iliyo pamoja nao. Dhambi kwa ujumla, au kutamani kitu chochote zaidi ya Mungu, inaweza kusahaulisha mambo ambayo Mungu ametupa. Clement wa Alexandria (aliyeandika mwaka 193-217/220 BK), alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kuona matumizi haya kwenye Exhortation to the Heathen sura ya 10, uk.201.

 

S: Kwenye Mwanzo 19:30-36, kwa nini Biblia inafundisha kuwa Lutu alifanya tendo la ndoa na mabinti wake? Siwezi kuamini kuwa jambo hili liliweza kuwa sahihi.

J: Vema. Biblia haisemi kuwa jambo hili lilikuwa zuri. Kufanya tendo la ndoa na ndugu wa karibu na zinaa ni vibaya, na Biblia ilikuwa inasimulia kwa uaminifu kitu ambacho Lutu alifanya.

Katika kumtetea Loti, Irenaeus, kwenye Against Heresies sura ya 31 (alindika mwaka 182-188 BK), anasema Biblia inaonyesha kuwa Lutu hakushiriki kwa sababu ya tamaa, lakini alilazimishwa baada ya kulewa sana.

Origen (mwaka 225-254 BK) alisema kuwa habari kama ya Lutu na binti zake zimo kwenye Maandiko Matakatifu ya Biblia ili kuonyesha jinsi waandishi wa Biblia walivyoupenda ukweli, hata hawakuficha kitu chochote hata kile kilichowaaibisha (Origen in Against Celsus kitabu cha 4 sura ya 45, uk.518).

 

S: Kwenye Mwanzo 20 na Kutoka 23:31, ilikuwaje Wafilisti waliweza kuwa Israel wakati wa Abraham karibu mwaka 2000 KK?

J: Ingawa kulikuwa na uhamiaji mkubwa sana mwaka 1200 KK, kimo cha kwanza cha Ashdodi kilikaliwa na watu kuanzia karne ya 17 (H.F. Vos, Archaeology in Bible Lands). Kuna mtu aliyeishi katika nchi ile yenye rutuba wakti ule, na hakuna ushahidi wa kihistoria unaosema kuwa hawakuwa Wafilisti. Baada ya Wamisri kuwashinda Wafilisti mwaka 1190 KK, walikwenda Palestina wakiwa wenye nguvu, na inaeleweka kuwa walijitoa na kuelekea kwenye maeneo ambayo tayari walimiliki miji.

 

S: Kwenye Mwanzo 20:3, 6 kwa nini Mungu alijipinga kwa kusema kuwa Abimeleki alikuwa amekufa wakati alikuwa hai?

J: Mungu haibadiliki (Malaki 3:6, Yakobo 1:17, Waebrania 13:8). Lakini Ezekiel 33:12-20 inaonyesha kuwa mapenzi ya Mungu yaliyofunuliwa kwa watu yanaweza kubadilika watu wanapobadilika.

   Angalia maelezo kwenye Kutoka 33:5-6; Kumbu 20:17, Yer 15:6; Yoh 3-4, 10 na 4:1-2 kwa maelezo zaidi.

 

S: Kwenye Mwanzo 20:3,8-10; 26:1; Amu 8:31 na 9:1, jina Abimeleki linamaanisha nini?

J: "Ab" maana yake baba, na "meleki" maana yake mfalme au mtawala. Jina hili linamaanisha ama baba wa mfalme au baba ni mafalme. Mbali na kuwa jina la waflme wawili wa Gerar, na mtoto wa Gideoni, Cyril Aldred kwenye Akhenaten King of Egypt uk.186 anasema kuwa Abimilki alikuwa mtawala wa Tiro aliyeelezwa kwenye barua za Amarna. Picha za vibao vya barua kadhaa za Amarna zimo kwenye New International Dictionary of the Bible uk.80 na Wycliffe Bible Dictionary uk.1828.

 

S: Kwenye Mwanzo 20:12, kwa nini Abram alimwoa Sara ambaye alikuwa ni binamu yake?

J: Tendo la ndoa kwa ndugu wa karibu halikuwa limezuliwa kiwazi kabisa wakati ule. Pia, Abram hakuwa muumini wa Mungu alipokuwa anaoa.

 

S: Kwenye Mwanzo 21:14, je Abraham alifanya sawa kumfukuza Hajiri nyumbani?

J: Katika hali ya kawaida, ni makosa kumfukuza Hajiri na mtoto wake wa miak kumi na kitu bila ulinzi na wakiwa na maji kidogotu, na hii ndiyo sababu ombi la Sara lilimfadhaisha sana Ibrahimu kwenye Mwanzo 21:11. Lakini, katika tukio hili, Mungu alimwambia Ibrahimu aendelee kufanya hivyo na kila kitu itakuwa sawa. Mungu mwenyewe aliwapa Hajiri na Ishmaili maji (Mwanzo 12:17-19), na Mungu alikuwa na Ishmaili alipokuwa anakua (Mwanzo 21:20).

   Kama nyongeza, Hajiri lilikuwa ni jina la Kisemiti kwa mujibu wa Expositor's Bible Commentary juzuu ya 2 rejeo la 15 chini ya uk.307. Palikuwa na Wasemiti wengi walioishi kaskazini mwa Misri.

 

S: Kwenye Mwanzo 21:14, ukisoma Agano la Kale, ni dhahiri kuwa katika kitabu cha Mwanzo mtoto wa kiume wa kwanza (yaani aliyechaguliwa na Mungu, mrithi wa baba yake), ni ISHMAIL na uongo ulioongezwa na Wayahudi kwenye Agano la Kale kumfanya asiwe mrithi (kwa nini? Kwa sababu hawakuweza kumkubali mtu asiyekuwa wa kabila lao) unaonekana kuwa wazi kabisa walipoandika kuwa ISHMAIL pamoja na mama yake HAJIRI walitoweka kutoka kwenye kabila la ABRAHAM milele? Lakini tunaposoma Mwanzo zaidi tunakuta kuwa habari ya kweli ni kuwa "ISHMAIL alikufa machoni pa ndugu zake" (familia) na zaidi "ISAKA" alikufa machoni pa ndugu zake wote." Maelezo haya kutoka kwenye Biblia yanaonyesha wazi nyongeza zaidi ya Kiyahudi ambayo iliwasababisha watunge tukio la kufukuzwa milele kwa HAJIRI na ISHMAIL ili kwamba wamtoe ISHMAIL aliyekuwa "mtoto pekee wa ABRAHAM" hapo awali wakati ABRAHAM alipokuwa tayari kutoa kitu chochote kafara tokana na upendo na utiifu wa mapenzi ya Mungu, pia inaonyesha kuwa ahadi ya mwokozi wa wanadamu ilifanywa kupitia ISHMAIL (mzaliwa wa kwanza mwanaume) na si ISAKA (mzaliwa wa pili mwanaume). (Muisla aliuliza swali hili).

J: Kwanza kabisa, baadhi ya Waislamu wanaweza kuwa hawafahamu kuwa Kurani haiko bayana endapo mtoto wa kiume aliyetolewa kuwa kafara alikuwa ni Ishmail au Isaka.

Madai yako kuwa Ishmaili alikufa mbele "ya familia yake" hayamaanishi kuwa hakuwa amefukuzwa. Kitu pekee ambacho Biblia inasema kuhusiana na hili ni Mwanzo 25:17b ambapo inasema "Akakata roho, akafa, akakusanyika kwa watu wake." Hii ilikuwa tasifida ya kawaida kwa kusema alikufa. Hii haiwezi kuthibitisha kuwa alizikwa na mahenga wake, kwa sababu Abrahamu pia alikuwa "alikusanyika kwa watu wake" katika Mwanzo 25:8, na hiyo haimaanishi alizikwa Uru ya Wakaldayo.

Kinyume na swali lako, haisemi kuwa Abrahamu alitakiwa kumtoa kafara mzaliwa wake wa kwanza wa kiume. Badala yake, Abrahamu alitakiwa kutoa kafara ya mtoto wake wa pekee, kwa sababu Ishmaeli alikuwa tayari amefukuzwa na Isaka alikuwa ndie mtoto pekee wa ahadi.

Hata hivyo nina swali kwako, je Kurani yaweza kuwa imekosea?

1. Sura 32:23 "Tulitoa kitabu kwa Musa Kitabu kabla. Basi usiwe na shaka kikikufikia: na tumekifanya kuwa muongozo kwa wana wa Israeli." Kwa hiyo unakubali kuwa Torati, kama ilivyotolewa awali, ilikuwa sahihi na kutoka kwa Mungu wa kweli?

2. Sura 5:46 "Na katika hatua zao [manabii] tumemtuma Yesu mwana wa Maria, kuthibitisha Torati kuwa imetoka kwake; tumempa Injili; ambayo ndani mwake kuna muongozo na mwanga. Na uthibitisho wa Torati kuwa ilikuja kabla yake; muongozo wa na mawaidha kwa watu wanao mcha Allah." Kwa hiyo je, unakubali kuwa Torati wakati wa Yesu, kama alivyoithibitisha, ilikuwa ni neno ya kweli la Allah?

3. Hati toka Bahari ya Chumvi (Dead Sea Scrolls) zina nakala nyingi za maandiko ya Agano la Kale yaliyoandikwa wakati wa Kristo na kabla ya hapo. Mambo matatu yanayofanya ufikiri kuwa Biblia imekosewa ni:

3.1. Isaka alikuwa ni mtoto wa ahadi, agano (Mwanzo 17:19, 21)

3.2. Ismail na Hajiri walifukuzwa (Mwanzo 21:8-19)

3.3. Ibrahimu alimtoa Isaka kuwa sadaka dhidi ya Ishmaeli (Mwanzo 22:1-18)

Hati toka Bahari ya Chumvi zinasema kuwa Isaka ni mtoto wa ahadi. Philo alikuwa mwanazuoni wa Kiyahudi aliyeishi Alexandrina Misri, alikufa mwaka 50 BK. Aliandika maoni ya Kitabu cha Mwanzo, na maoni yake yanaonyesha kitu hicho hicho kama tulicho nacho leo.

Clement wa Rumi alikuwa askofu wa awali wa kikristo, anaweza kuwa Clement aliyeongelewa na Paul, aliyeandika barua kwa Wakorintho mwaka 96-98 BK. Anasema kwa mtoto ambaye Abraham alimtoa kafara alikuwa mtoto wa uzeeni. [Hata hivyo, hasemi moja kwa moja kuwa alikuwa Isaka].

4. Huwezi kuwalaumu Wakristo kwa kushutumu madai yako dhidi ya Injili ya wakati wa Yesu na wakati wa Muhammad kwa sababu ya Sura 5:47. Inasema, "Na wahukumu Watu wa Injili kwa yale ambayo Allah aliyowafunulia ndani yake...."? Hivyo unakubali kuwa Wakristo wanapaswa kuhukumu kwa kadri ya Injili, ambayo tuna nakala zake tokea muda mrefu kabla ya wakati wa Muhammad? Kama siyo, basi je Kurani imekosea?

Sura 5:48 iansema, "Kwako (Watu wa Kitabu) tulituma Maandiko kwa ukweli, kuthibitisha Maandiko yaliyotangulia, na kuyalinda katika usalama: kwa hiyo hukumu baina yao kwa mambo ambayo Allah ameyafunua, na usifuate matakwa yao yasiyo na maana yoyote, yakiuacha ukweli ambao umekujia ....." Kama wewe ni Muislam ambaye hakubaliani na maneno haya, basi ni jinsi gani Allah anatofautisha kati ya maneno yake haya, ambayo amewaruhusu wacha Mungu wanaomwabudu kujifunza kwa namna ya upotofu tu, na maneno yake ambayo yangali hayajapotoshwa?

Waislamu wengi wanaziamini Hadith, ambazo ni mkusanyiko wa maneno na matendo ya Muhammad, kama mamlaka ya juu zaidi ya Kurani. Kati ya mikusanyikoo sita inayotambuliwa zaidi ya Hadithi, Bukhari ndio mkubwa. Nadhani utapenda kusoma kitu ambacho inasema kuhusu Hajiri [Hagari] na Ishmaili.

Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 55 sura ya 9 na.583, uk.373 "Ibrahimu alimleta [Hajiri] na mwanawe Ishmaili alipokuwa anamnyonyesha, mahali fulani Ka'ba chini ya mti kwenye Zam-zam, mahali pa juu kabisa katika msikiti. Katika siku hizo hapakuwa na mtu yoyote Maka, wala hapakuwa na maji. Kwa hivyo aliwafanya wakae hapo na kuwawekea karibu yao mfuko wa ngozi uliokuwa na tende, na kiriba cha maji, na kurudi nyumbani. Mama yake Ishmaili alimfuata na kumwambia, "Ewe Ibrahim! Unakwenda wapi, unatuacha kwenye bonde hili ambako hakuna mtu ambaye ushirika wake tunaweza kuufurahia, wala hakuna kitu chochote (cha kufurahia)?" Alirudia maneno haya kwake mara kadhaa, lakini hakugeuka nyuma kwake. Kisha akamwuliza, "Je, Allah amekuamuru kufanya hivi?" Alisema (Abraham), "Ndiyo." ... (uk.374 Hadithi hiyohiyo) "Nabii alisema, "Hiki ni chanzo cha mapokeo kutembea kwa watu kati yao (yaani Safa na Marwa). Alipofika Marwa (kwa mara ya mwisho), aliisikia sauti na akajiambia kukaa kimya na kusikiliza kwa makini. ... Akamwona malaika sehemu ya Zam-zam akifukua ardhi kwa kisigino (au bawa lake), hadi maji yakatoka kutoka mahali hapo."

Mwana historia maarufu wa Kiislam al-Tabari (mwaka 839-923 BK), alichunguza endapo ilikuwa Ishmaili au Isaka aliyekaribia kutolewa kafara, na alisema kuwa ni Isaka, si Ishmaili (al-Tabari juzuu ya 2, uk.68). Alikuwa na maelezo ya kurasa kumi ya mamlaka za Kiislamu ambao walisema kuwa alikuwa Isaka na kwamba waliosema kuwa ni Ishmaili (al-Tabari juzuu ya 2 uk.82-92), ingawa walihitimisha kwa kusema kuwa alikuwa Isaka.

Hata hivyo, nadhani kuwa suala hili, la kuwa mtoto yupi wa Ibrahimu alikuwa ndiye yupi, ni kitukidogo kulinganisha na kuweza kujibu swali la Mithali 30:4: "Ni nani aliyefanya imara ncha zote za nchi? Jina lake ni nani? Na ni nani jina la mwanawe? Kama wajua!"

 

S: Kwenye Mwanzo 22, kwa nini Mungu alitia moyo kafara ya binadamu kwa Abraham na Isaka?

J: Mambo manne ya kuangalia katika kujibu swali hili.

1. Ibrahimu tayari aliisha onyesha kuwa anampenda Mungu kuliko watu wake na utamaduni wake, lakini Mungu alimjaribu Ibrahimu ili kuona kama alimpenda Mungu kuliko mtoto wake mpendwa.

2. Hata suala hili pekee la Mungu kuagiza kafara mwanzoni, Mungu alizuia isitolewe. Hakuna mtu aliyekufa.

3. Mungu Baba hakumtaka Ibrahimu afanye kitu chochote ambacho yeye mwenyewe hakukifanya, katika kumtoa Yesu kuwa kafara kwa ajili yetu.

4. Amri kumi (usiue, n.k.) hazikutolewa hadi wakati wa Musa kwenye Mlima Sinai.

 

S: Kwenye Mwanzo 22:1-18, je mvulana ambaye Abraham alikaribia kumtoa kafara anaweza kuwa Ishmaili, siyo Isaka, kama Waislam wanavyodai? Vinginevyo, Isaka anawezaje kuwa "mwana wa pekee" wa Abram?

J: Ilikuwa ni Isaka aliye tolewa kafara na sio Ishmaili kwa sababu angalau nne:

Hata Kurani haisemi kuwa alikuwa Ishmaili: Mwanzo 22:2 inasema alikuwa Isaka. Kwa Waislam, ingawa Kurani ya Kiislam inaongelea jambo hili kwenye Sura 37:99-111, hakuna sehemu yoyote kwenye Kurani nzima inaposema kuwa ama alikuwa ni Ishmaili au Isaka.

Mvulana pekee ambaye Abram alikuwa naye wakati ule: Ismail alikuwa na miaka 14 wakati Isaka anazaliwa, kulingana na Mwanzo 17:25 na 18:10. Hajiri na Ishmaeli walikuwa wamepelekwa sehemu nyingine ya mbali siku Isaka alipoachishwa kunyonya kwenye Mwanzo 21:8-10. Ibrahimu ilijaribiwa "muda mrefu" baada ya hii kwenye Mwanzo 21:34, na "kijana" ilikuwa juu ya madhabahu kwenye Mwanzo 22:12.

Mtoto pekee machoni pa Mungu: Mungu alisema kuwa ni kupitia Isaka na si Ishmaili ambapo uzao wa Ibrahimu utatambuliwa kwenye Mwanzo 21:12. Ibrahimu hakuwa na Ishmaili kwa sababu Ishmaili na mama yake walikuwa "wameondolewa" na kupelekwa sehemu ya mbali kulingana na Mwanzo 21:10-12.

Mrithi tu hapa duniani: Isaka alikuwa mrithi pekee, na mtoto pekee inamaanisha "mtoto mpendwa." Ingawa utamaduni wa wakati ule uliruhusu kuwa na masuria kwa ajili ya kuendeleza kizazi, urithi na haki ya mzaliwa wa kwanza ilikwenda kwa watoto wa wake halisi, si watoto wa masuria.

Mtoto wa ahadi tu: Mwanzo 21:12 inasema, "katika Isaka uzao wako utaitwa." Abrahamu alikuwa na watoto wengine pia, lakini walizaliwa baada ya ahadi hii.

 

S: Kwenye Mwanzo 22:2, ilikuwaje Isaka alikuwa mtoto pekee wa Abram"?

J: Ingawa Ishmaili alizaliwa kwanza, alipelekwa mbali kwa wakati huu, na Isaka alikuwa ndiye mtoto wa pekee Abramu aliyekuwa naye. Isaka alikuwa mrithi wa pekee, na mwana wa pekee inaweza pia kumaanisha kuwa mwana mpendwa. Mwanzo 21:12 inasema, "katika Isaka uzao wako utaitwa." Abrahamu alikuwa na watoto wengine pia, lakini wamezaliwa baada ya ahadi hii. Ingawa utamaduni wa wakati ule uliruhusu kuwa na masuria kwa ajili ya kuendeleza kizazi, urithi na haki ya mzaliwa wa kwanza vilikwenda kwa watoto wa wake halisi, si watoto wa masuria.

 

S: Kwenye Mwanzo 22:2, je Roho Mtakatifu anaweza kuwaongoza watu kutokutii jambo ambalo limefunuliwa kwenye Biblia?

J: Hapana. Mambo matatu ya kuzingatia katika jibu la swali hili.

1. Bila shaka, Mungu hakumwongoza Ibrahimu kufanya kitu chochote dhidi ya Maandiko yaliyofunuliwa, kwa sababu hakuna Maandiko yaliyokuwa yameandikwa wakati wa Abrahamu.

2. Tangu Maandiko yalipofunuliwa, Mungu hamwagizi mtu yeyote kufanya mambo kinyume na amri zake zilizofunuliwa. Hata wakati Roho Mtakatifu alipomwongoza Yesu kwenda nyikani, ambako Yesu alijaribiwa na Shetani, Roho Mtakatifu hakumjaribu Yesu au kumwambia Yesu kufanya jambo lolote lisilo sahihi.

3. Mungu hapendi mtu yeyote kufanya vitendo vilivyo kinyume na matakwa yake. Hata wakati Mungu alipomwamuru Ibrahimu amtoe Isaka kama kafara, Mungu hakumruhusu Ibrahimu kumuua Isaka.

 

S: Kwenye Mwanzo 22:12, kwa kuwa Mungu alisema "Sasa ninajua ya kuwa unamcha Mungu", je Mungu hakujua kitu ambacho Abram atafanya?

J: Bila shaka Mungu alijua, lakini maelezo haya yanamaanisha kuwa ilikuwa ni wakati huu ambapo Ibrahimu alithibitisha kitu ambacho atakifanya.

 

S: Kwenye Mwanzo 23, je Wahiti walikuwepo kweli duniani?

J: Wataalam wa elimukale wa kisasa walitambua Wahiti mapema mwaka 1892. Hata hivyo, baadhi ya wasomi bado walitilia shaka uwepo wao miaka kumi baadaye (1902, E. A. W. Budge). Leo vitabu vizima vimeandikwa kuhusu Wahiti. Kitabu kimoja kizuri na chenye kusomeka kirahisi ni The Secret of the Hittites by C.W. Ceram (Dorset Press 1955).

S: Kwenye Mwanzo 23, Wahiti wanawezaje kuwa Palestina?

J: Wahiti walikuwa watu waliotapakaa sana, kundi moja liliishi kwenye milima ya Palestina. Wahiti wa Ulaya waliiteka Babeli mwaka 1590 KK. Wengine wanaamini kuwa hii inaongelea Wahati, watu wasiotoka Ulaya walioshindwa kabla ya mwaka 2000 KK. Maneno Hatti na Hitti yanaandikwa sawasawa kwenye Kiebrania.

 

S: Kwenye Mwanzo 23:2, kwa nini inaelezwa kuwa Kiriath-Arba inaitwa Hebron pia?

J: Kuna sababu mbili za ziada zinazoweze kuwa chanzo cha Hebroni kutajwa hapa.

Kumbuka kuwa wakati Ibrahimu aliishi karibu mwaka 2000 KK, kitabu cha Mwanzo kiliandikwa wakati wa Musa, mwaka 1447-1407 KK, kwa hiyo mji ule unaweza kuwa uliitwa Hebroni na Waisraeli na/au Wakanaani wakati wa uhai wa Musa. Wapelelezi wa Kiisraeli waliijua jiografia ya Kanaani na labda walitumia jina kwa mji wa wakati wa Musa.

Hata hivyo, Waisraeli waliuita mji ule Hebroni, si Kiriath Arba, muda mfupi baada ya kutekwa na Yoshua. Maelezo haya rahisi kuwa Kiriath Arba sasa ni Hebroni, yanaweza kuwa yaliongezwa muda mfupi baada ya hapo.

 

S: Kwenye Mwanzo 23:5, kwa nini Wahiti walimwona Ibrahim kuwa mfalme mwenye nguvu miongoni mwao?

J: Ibrahim alikuwa tajiri sana. Ibrahimu pia alionekana kujenga uhusiano wa karibu nao, na walimwona kuwa si rafiki tu, bali mmoja wao.

 

S: Kwenye Mwanzo 23:15-16, kwa nini Ibrahim alihitaji kupima fedha?

J: Shekeli ilikuwa kiwango cha uzito, na baadaye tu ndipo kilipokuwa kiwango cha fedha pia. Ibrahimu alitakiwa "kupima" fedha kwa sababu sarafu hazikuwa zinatumika mpaka karibu mwaka 800 KK, kwa mujibu wa Can Archaeology Prove the Old Testament? uk.27. Kadhalika Akani aliiba dhahabu na fedha, iliyokuwa na "uzito" wa shekeli 50 na 200. Wycliffe Bible Dictionary uk.1798 inasema sarafu za kwanza kufahamika zilitoka Lydia karibu mwaka 700 KK. Pia inasema kuwa neno la Kilatini pecunia (kutoka na hilo Kiingereza kimepata neno pecuniary lenye kumaanisha fedha) lilitokana na neno la pecus Kilatini ambalo linamaanisha ng'ombe.

 

S: Kwenye Mwanzo 24:1, kwa nini Mungu aliruhusu baadhi ya watoto wake wasumbuke na uzee?

J: Hatusumbuki na uzee mbinguni., na furaha ya milele ya mbinguni, itaufanya muda wetu mfupi wa mahangaiko hapa duniani uonekane mdogo. Angalia maelezo ya Yoshua 13:1 kwa jibu.

 

S: Kwenye Mwanzo 24:15, je Isaka na Rebeka walikuwa na uhusiano gani?

J: Rebeka alikuwa binti wa ndugu wa Ibrahimu, kitu ambacho kinamfanya kuwa binti wa binamu wa Isaka.

   Isaka na Rebeka hawakuwa wamevunja amri ya Walawi 18, kwa sababu ilikuwa bado kuandikwa. Hata hivyo, imekuja kuwa kwamba ndoa yao ilikuwa kwenye miongozo ya amri za baadaye kwenye Mambo ya Walawi.

 

S: Kwenye Mwanzo 25:1, je Ketura alikuwa mke au suria?

J: Suria anahesabiwa kuwa aina ya mke. Mwanzo 25:1 inaweza kumaanisha ama mke ama suria.

 

S: Kwenye 25:2, kulitokea nini kwa watoto wa Ketura?

J: Ibrahimu na Ketura walikuwa na wana sita wanaojulikana.

Zimran anaweza kuwa mhenga wa kabila la Arabia, Zimri kwenye Yeremia 25:25. Leo hii kuna mji wa Zambran kwenye Bahari ya Shamu magharibi ya mji wa Maka.

Yokshan, hajawahi kusikika tena, ila kwamba alikuwa mhenga wa Sheba na Dedani. Sheba ni taifa lililokuwa kwenye kona ya kusini magharibi ya rasi ya Arabia. Wadedanim wa Isaya 21:13 walikuwa Waarabu ambao huenda ni uzao wa Yokshani na Hamu kupitia Kushi (Mwanzo 10:7, 1 Nyakati 1:9). Mji wa Dedani ulikuwa maili 100 (160 km) kusini magharibi mwa Tema kwenye oasisi ya el-‘Ula, umbali wa maili 175 (280 km) upande wa kaskazini wa Madina. Dedani pia imetajwa kwenye maandishi ya Sabea kabla ya kuingia kwa Uarabu na Minaea.

Medan huenda ikawa imetajwa nje ya Biblia. Wycliffe Bible Dictionary uk.1093 inasema kuwa konsonanti "m" na "b" huwa zinabadilishana mara nyingi kwenye lugha ya Kiarabu, hivyo hawa wanaweza kuwa kabila la Bedana, ambalo Mwaashuri Tiglath-pileseri III (mwaka 858-824 KK) aliwashinda.

Midiani lilikuwa ni kabila lililofahamika sana lililpwatesa Waisraeli kwenye Waamuzi 8.

Ishbaki alianzisha kabila lililoishi kaskazini mwa Syria na lilitajwa kwenye kumbukumbu za Kiashuri za Shalmanase III (mwaka 858-824 KK).

Shuah lilikuwa ni kabila alilotokea Mshuhi Bildadi kwenye Ayubu 2:11.

 

S: Kwenye Mwanzo 25:6, je Abraham alikuwa na wake na masuria wangapi?

J: Ingawa jambo hili halina umuhimu mkubwa, hatujui idadi halisi. Baada ya Sara kufariki, Ibrahimu alimuoa Ketura kwenye Mwanzo 25:1. Hajiri alikuwa mmoja wa masuria wake, lakini Mwanzo 25:6 inaonyesha kwamba Abrahamu alikuwa na masuria zaidi ya moja.

 

S: Kwenye Mwanzo 25:8, 17 na 49:33, je mababa wa familia ya Israeli "waliacha kufanya kazi"?

J: Hii ni tafsiri isiyokuwa makini sana ya neno la Kiebrania gâva', ambalo maana yake halisi ni kupumua nje au kumaliza muda wake. Tafsiri sahihi zaidi ni "kupumua kwa mara ya mwisho" yaani, "kukata roho."

 

S: Kwenye Mwanzo 25:8, 17 na 49:33, Abraham na Yakobo "walikusanyika kwa watu wao", hivyo basi kunawezaje kuwa na maisha baada ya kifo?

J: Msemo huu unamaanisha kuwa mtu anayeelezewa alifariki, na unaonekana kuwa mzuri kuliko "kicked the bucket", ambao pia unaomaanisha kufariki.

 

S: Kwenye Mwanzo 25:13, je maelezo kuhusu Kedar yanahusiana na Muhammad?

J: Mwanzo 25:13 inamtaja Kedari, mwana wa Ishmaeli, lakini kuna shaka kuhusu undugu wa Muhammad na Ishmaeli na Kedari. Vyovyote itakavyokuwa, Mwanzo 25:13 inapowataja wana kumi na mbili wa Ishmaeli, ikiwa ni pamoja na Kedari, haisemi chochote kizuri au kibaya juu yao. al-Tabari juzuu ya 6, uk.6, inasimulia mambo matatu:

1) Kuna tofauti kati ya orodha ya vizazi vya Muhammad baada ya ‘Adnan, (uk.37)

2) Nyingi ya orodha hizo (lakini si zote) zinamhusisha Muhammad ... ‘Adnan ... Nabt b. Qaydhar [Kedari?], b. Ismail [Ishmael]

3) Tofauti hizi hutokea kwa sababu ni sayansi ya zamani, zilizochukuliwa kutoka kwa watu wa Kitabu cha kwanza (Agano la Kale).

Kwa hiyo kama al-Tabari inakubali kuwa walichukua majina ya vizazi kutoka kwa Wayahudi na Agano la Kale, huu hauwi ushahidi unaojitegemea.

 

S: Kwenye Mwanzo 25:22-23, swali la Rebeka kuhusu hali ya sasa na ya baadaye, lakini jibu la Mungu linazungumzia miaka mingi sana ya baadaye. Kwa nini Mungu anafanya hivyo?

J: Mambo matano ya kuzingatia kwenye jibu la swali hili.

1. Mungu alkuwa anataka kuufunua ukweli huu wa kinabii kuhusu Yakobo na Esau.

2. Kama walimu wazuri wa kibinadamu, Mungu anajua kuwa jambo litaweza kukumbukwa vema endapo litakuwa jibu kwa swali la mwanafunzi.

3. Bila kujali kama Mungu alisababisha watoto kushindana ili kumchochea Rebeka kuuliza swali, mashindano hayo yalichochea kuulizwa kwa swali.

4. Rebeka anaweza kuwa hakuwa anafikiri kwa mtazamo wa muda mrefu wakati huu, lakini swali hapa halikuwa na jibu moja kiasi kwamba ufunuo wa Mungu bado ulilijibu.

5. Tunapoulizia mambo ya Mungu, tunapaswa kuuliza kwa namna "iliyo wazi" na si tu kama tunavyotaka sisi. Tunapaswa kuwa tayari kumruhusu Mungu kutuonyesha ukweli ambao hatukuutarajia na ambao hatukuuulizia moja kwa moja.

 

S: Kwenye Mwanzo 25:31-33, je haki ya uzaliwa wa kwanza ya Yakobo ilipatikana kwa kununua au kwa kudanganya?

J: Vyote.

1. Yakobo "alinunua" haki hii toka kwa Esau kwa bei ya bakuli la dengu (Mwanzo 25:29-34).

2. Yakobo baadaye alimdanganya Isaka kupata haki ya uzaliwa wa kwanza ambayo Esau aliishachagua kui, haki ya uzaliwa wa kwanza alikuwa tayari kuitoa (Mwanzo 27:19).

Haley's Alleged Discrepancies of the Bible uk.345 inaonyesha kuwa Yakobo alinunua tu haki ya uzaliwa wa kwanza, lakini alisema uongo ili kupata baraka.

Mbali na kununua na kudanganya, Mungu alichagua kwamba watu wake, Wayahudi, waje kupitia Yakobo (Mwanzo 26:24-24).

 

S: Kwenye Mwanzo 26:2, je Waisraeli walitakiwa kwenda Misri au la?

J: Isaka aliambiwa asiende Misri kwenye Mwanzo 26:2. Yakobo, siyo Isaka, aliambiwa aende kwenye Mwanzo 46:3. Kwa njia hiyohioy, kwenye 2 Samweli 7:5, 12-13, Daudi aliambiwa kuwa si yeye, bali mtoto wake ambaye atajenga hekalu la Yerusalemu. Somo la kujifunza hapa si kwamba kwenda Misri ni kuzuri au kubaya, bali kwamba tunapaswa kwenda mahali ambako Mungu anataka twende, wakati ambao Mungu anataka twende.

 

S: Kwenye Mwanzo 26:3-5; 12:1; 17:1, 9-14 na 22:16, je Mungu alimbariki Abraham kwa sababu ya kazi?

J: Hapana. Kwa Abraham au watu kwa ujumla, kuna vitu viwili tofauti hapa: wokovu na baraka.

Wokovu: Kazi za Ibrahimu hazikuwa muhimu, kwa maana ya kwamba hazikumfanaya aende mbinguni. Kazi zake zilikuwa muhimu sana kama kielelezo kinachoonekana cha imani yake kwa Mungu, na kitu kisichoweza kutengwa na imani yake kwa Mungu.

Baraka: Kwa sababu ya kazi, Ibrahimu na sisi mara nyingi tunapokea baraka kwenye maisha haya na thawabu kwenye maisha yajayo.

Agano la Mungu lilikuwa na vipengele visivyobadilika na vile vinayotegemea mambo maengine. Walawi 26:44-45 inaonyesha kuwa hata kama watu wa Mungu watashindwa kwenye vipengele vinavyotegemea mambo mengine, vipengele visivyobadilika vitaendelea kuwepo.

 

S: Kwenye Mwanzo 26:6-7, kwa nini Isaka, kama mfano wa kuiga kwetu, kwa kuwa alidanganya hapa?

J: Hapana. Tazama jibu la Mwanzo 12:10-20.

 

S: Kwenye Mwanzo 26:8-9, je huyu ni Abimeleki yule yule wa Gerar kama kwenye Mwanzo 20:2-3?

J: Kulingana na jina, pengine siye. Abimeleki inamaanisha "Baba ni mfalme", na hili hunda lilikuwa ni jina la cheo. Kwa upande mmoja kuna matukio mengi ya baba na mtoto au mzao wa ukoo husika kuwa na jina moja, hapa pengine ni jina la cheo.

 

S: Kwenye Mwanzo 26:33, je ni Abraham aliyetoa jina kwa mji wa Beersheba au Isaka?

J: Kwenye Mwanzo 21:31, ilikuwa inaitwa Beersheba wakati wa Ibrahimu kwa sababu ya kiapo kati ya Ibrahimu na Abimeleki. Bila shaka Isaka alijua jambo hili tokana na kuishi Beersheba na baba yake kwenye Mwanzo 22:19. Ili kumkumbusha Abimeleki, ambaye yaelekea alikuwa mtoto wa Abimeleki wa wakati wa Abrahamu kuhusu agano lililopita, alikipa kisima kipya jina hilohilo, "Shibah."

 

S: Kwenye Mwanzo 26:34 na 36:2-3, wake wanne wa Esau ni kina nani?

J: Wake 1-2: Akiwa na miaka 40, Esau alioa Wahitiwawili, Judith na Basemathi, binti wa Eloni (Mwanzo 26:34-35).

Ada, binti wa Eloni, Mhiti (Mwanzo 36:2), huenda ni jina lingine la Basemathi.

Mke wa 3: Baada ya Yakobo kuondoka, shoto, Esau ndoa Mahalathi Mwishmaeli, dada Nabaioth (Mwanzo 28:8-9)

Basemathi, binti wa Ishmaili na dada ya Nabaioth (Mwanzo 36:3), pengine ni jina lingine la Mahalathi.

Mke wa 4: Esau alimuoa Oholibama, binti wa Ana (Mwanzo 36:3).

Judith huenda hakutajwa kwenye orodha ya vizazi ya Mwanzo 36, kwa sababu hakuzaa watoto.

 

S: Kwenye Mwanzo 27, kwa nini Mungu anadaiwa kuridhia Yakobo kumdanganya Isaka na Labani kwenye Mwanzo 31:20?

J: Mungu hakuridhia uongo wa Yakobo. Kwanza, Biblia hurekodi kwa usahihi na uaminifu mambo mema na mabaya yaliyofanywa na watu. Pili, hata watu wa Mungu kwenye Biblia wamefanya makosa.

 

S: Kwenye Mwanzo 27, kwa nini kubariki ni muhimu?

J: Kwa kawaida, mzaliwa wa kwanza alipata baraka, ambayo ilimaanisha sehemu maradufu ya urithi, pamoja na kuwa na kiongozi wa familia. Vibao vyenye maandishi vya karne ya 15 KK kutoka Nuzi vinaelezea kesi kati ya ndugu watatu, kuhusiana yupi kati yao amuoe mwanamke aliyeitwa Zululishtar. Ndugu mmoja alishinda kwa sababu aliweza kuonyesha kuwa baba yake aliridhia ndoa hiyo akiwa anakaribia kufa.

 

S: Kwenye Mwanzo 27:29, je neno la Kiebrania "Bwana" linamaanisha nini hasa?

J: Neno la Kiebrania hapa, gebiyr (linatamkwa gheb-EER) linaweza kutafsiriwa kwa njia mbili: bwana au shujaa. Katika suala la Esau na wazao wake ilikuwa ni bwana [asiyehitajika]. Katika maisha yetu, kama Mungu amemweka mtu juu yetu ambaye humpendi, unaweza kuchagua kuwachukulia kama bwana asiyehitajika au shujaa.

 

S: Kwenye Mwanzo 27:39-40, kwa nini Isaka hakumbariki Esau kama alivyombariki Yakobo?

J: Biblia haisemi kwa nini Isaka alikuwa na imani (sahihi au isiyo sahihi) kuwa hakuweza kuwabariki wote wawili. Hata hivyo, Evidence That Demands a Verdict juzuu ya 2, uk.328-329 inasema kuwa kwa mujibu wa vibao vyenye maandishi vya wakati ule vilivyopatikana kwenye mji wa Nuzi, wosia uliotolewa muda mfupi kabla ya mtu kufa ulichukuliwa kuwa halali na usioweza kutanguliwa. Angalia pia jibu la swali linalofuata.

S: Kwenye Mwanzo 27:39-40, kwa nini Mungu hakumbariki Esau kama alivyombariki Yakobo?

J: Kuna sababu tatu zenye kuongezeana uzito.

1. Warumi 9:10-15 inaonyesha kwamba Mungu anaweza kufanya kama atakavyo bila kutuambia sababu zake.

2. Esau alikuwa mmataifa, yaani mtu asiyemcha Mungu (Waebrania 12:16), na Yakobo alikuwa mdanganyifu; Mungu angekuwa ametenda haki kama angewalaani wote wawili. Badala yake kila mmoja alipokea baraka (Waebrania 11:20).

3. Mungu ana haki ya kuchagua kutoa huruma na upendo maalum kwa baadhi ya watu tu kama anavyoona inafaa — unaweza kumuuliza Paulo.

 

S: Kwenye Mwanzo 27:42-44, je Yakobo alikwenda kwenye mji wa Harani ili kumkimbia Esau, au kupata mke?

J: Vyote. Wakati mwingine kuna kuwa na sababu nyingi ya kufanya jambo fulani. Rebeka alimwambia Yakobo aondoke ili amkimbie Esau kwenye Mwanzo 27:42-46, lakini alimwambia Isaka kuwa sababu ni kutafuta mke kwenye Mwanzo 27:46. Sababu ya Isaka ya kumtuma Yakobo ilikuwa kutafuta mke katika Mwanzo 28:1-6.

 

S: Kwenye Mwanzo 27:45, je neno "nyote" linamaanisha Yakobo na Isaka au Yakobo na Esau?

J: Inaweza kuwa namna yoyote kati ya hizo mbili. Hata hivyo, kuna uwezekano mkubwa zaidi wa kuwa Isaka na Esau si kwa sababu Isaka alikuwa karibu ya kufa, Esau angemuua Yakobo mara baada ya hapo, na hapakuwa na tishio kwa Esau.

 

S: Kwenye Mwanzo 27:46, je wake wa Esau walikuwa Wahiti au Wakanaani?

J: Je mtu anaweza kuwa wa Texas na Marekani? Wahiti kule Kanaani walkuwa ni moja ya jamii za watu wa Kanaani.

 

S: Kwenye Mwanzo 28, je Rebeka na Yakobo walfanikiwa kupata kitu walichotaka?

J: Kwa kuangalia kijuu juu ndiyo, lakini katika uhalisia wa jambo hapana. Walitaka Yakobo apate haki mzaliwa wa kwanza, na kwa njia isiyokuwa sahihi ya kudanganya na waliipata, kwa hiyo walifanikiwa.

Hata hivyo, mtoto mwenye haki ya mzaliwa wa kwanza huwa anakuwa na mahali pa heshima katika familia baadaye; lakini, Yakobo alilazimika kukimbia ili kunusuru maisha yake. Rebeka alifanikiwa katika kumsaidia mtoto wake aliyempenda zaidi; lakini, hakuweza kumwona Yakobo tena hapa duniani. Kama Women in the Bible inavyosema, Rebeka alilazimika kuishi na mtoto aliyemdhulumu maisha yake yote.

 

S: Kwenye Mwanzo 29:15-25, kwa nini tuvutiwe na Labani kwenye Biblia, kwa sababu alimdanganya Yakobo?

J: Yoyote aliyesema tuvutiwe na Labani? Swali hili linabeba dhana ya kwamba Biblia inaweza kuongelea watu wa Mungu kweney ombwe, na haiwezi kuwataja watu wengine waliohusika nao. Biblia inazungumza juu ya watu waovu na watu wema. Isitoshe, Biblia inatuonyesha kuwa hata watu wema hawakuwa wazuri wakati wote.

Mlinganisho unaweza kusaidia hapa. Mtu anaweza kusema, "huwezi kuvutiwa na mashujaa wa Marekani. Angalia kwa mfano Yohana Wilkes Booth, ambaye alimpiga risasi Abraham Lincoln." Naam, tunaweza kusoma jinsi John Wilkes Booth alivyokuwa na jukumu muhimu katika historia ya Marekani, lakini hakuwa shujaa wa Marekani.

Labani alikuwa na jukumu katika historia ya Israeli, lakini hakuwa shujaa. Ulinganisho wa Booth unaweza kuonekana wa kijinga kidogo, kwa kuwa hakuna mtu anayemwona Booth kama shujaa, lakini kumtumia Labani kukosoa watu ambao tunapaswa kuiga mfano wao kwenye Biblia, (kama mtu mmoja asiyemwamini Mungu alivyofanya), hakutakuwa na maana pia.

 

S: Kwenye Mwanzo 29:21-30, Raheli alitolewa lini awe mke wa Yakobo?

J: Yakobo alifanya kazi miaka saba, akapewa Lea, alisubiri kwa juma moja, kisha akapewa Raheli wakati huo kwa malipo ya ahadi ya kufanya kazi kwa miaka mingine saba.

 

S: Kwenye Mwanzo 29:28, kwa nini Yakobo alioa mtu na dada yake, kwa sababu Mambo ya Walawi 18:18 inakataza kuoa mtu na dada yake wakati wote wangali wanaishi?

J: Mambo ya Walawi 18:18 ilikuwa sehemu ya Sheria ya Musa, ambayo ilitolewa zaidi ya miaka 400 baada ya Yakobo kuoa wake zake. Hakuna mtu atakayemtaka Yakobo aitii sheria ambayo bado hajaisikia, na Mungu bado hajaiamuru.

 

S: Kwenye Mwanzo 29:31, kwa nini Munguhakumwambia Yakobo ampende Lea pia, badala ya umfanya Raheli tasa?

J: Wakati mwingine watu wanaweza kuelewa somo kwa njia ngumu tu. Je, sisi tuko tofauti?

 

S: Kwenye Mwanzo 30:14-15, je kutumia tunguja hakuonekani kama ushirikina?

J: Mengi ya madawa ya kiasili haifanyi kazi. Muda mrefu ambao Raheli alikuwa hana watoto baada ya kuzitumia unaonyesha wazi kuwa tunguja hazihusiki katika kumfanya Mungu afungue tumbo la Raheli. Kifungu hiki kinaonyesha kuwa hata waamini wanaweza kufanya makosa na kuamini tiba za kijinga.

 

S: Kwenye Mwanzo 30:27, Labani angewezaje kutumia uaguzi kumwelewa Yakobo?

J: Hebu tufikiri kuwa Labani alikuwa anasema ukweli hapa, wakati mwingine watu hupata majibu sahihi kwa njia ya uaguzi. Hata hivyo, hata kama uaguzi ungetoa ukweli wote badala ya mchanganyiko wa ukweli na makosa, waumini hawapaswi kufuata mfano wa Labani kwa sababu Mungu amezuia kufanya uaguzi kwenye Kumbukumbu 18:10,14. Isitoshe, uaguzi wa Labani haukumpa mambo aliyoyakusudia kwenye Mwanzo 31:1-2, 9.

 

S: Kwenye Mwanzo 30:37-43, je kitendo cha Yakobo cha kuwafanya "kondoo" wawe na madoadoa hakionekani kuwa kama ushirikina?

J: Hakuna kidokezo cha ushirikina, ni mawazo yasiyo sahihi tu jenetiki za wanyama. Mungu alimbariki Yakobo bila kujali jambo hili, kama Yakobo mwenyewe alivyojua kwenye Mwanzo 31:7-13.

S: Kwenye Mwanzo 31:23 na 37:25, je Gileadi wazo ambalo limekosewa muda wake, kwa kuwa Hesabu 26:26 inasema kuwa Manase alikuwa babu wa Gilead?

J: Hapana kabisa. Nitaanza na wazo lisilohusika na jibu, na kisha jibu.

Si sehemu ya jibu: Gileadi lilikuwa jina la kawaida kwa kiasi fulani. Gileadi hakuwa si tu mzao wa Manase (Hesabu 26:29-30 na Yoshua 17:1), lakini Gileadi mwingine alikuwa baba wa Yeftha (Waamuzi 11:1), na Gileadi wa tatu alikuwa anatoka Gadi (1 Nyakati 5:14).

Jibu lenyewe ni kwamba neno "Gileadi" linaonyesha wakati (kitabu) kilipoandikwa. Yakobo na Yusufu wasingeweza kuuita ukanda huo Gileadi, lakini hakuna mtu anayedai kitabu cha Mwanzo kiliandikwa wakati wa Yakobo na Yusufu. Badala yake, Mwanzo iliandikwa wakati wa Musa. Makabila mawili na nusu ya ng'ambo ya mto Yordani yalikuwa tayari kwenda kupokea nchi yao kabla ya Musa kufa.

Wazo lililokosewa muda ni wakati hati yenye kudai kuandikwa wakati fulani inapotumia maneno ambayo yangetumika katika muda baadaye tu. Kutumia maneno wakati wa kuandika kuelezea wakati uliopita siyo kukosea muda. Kwa mfano, siyo kukosea wakati endapo mtu katika karne ya ishirini anasema mkoa wa Gileadi ulikuwa kwenye nchi ya Yordani. Yakobo, Yusufu na Musa hawakuijua nchi ya kisasa ya Yordani, lakini basi, hakuna mtu anayeadai kuwa walifanya hivyo.

 

S: Kwenye Mwanzo 31:32, 34, je Biblia [inadaiwa] ingewezaje kuridhia Raheli kuiba sanamu toka kwa baba yake?

J: Miungu ya familia haikuwa si tu na maana za kidini, kuimiliki kulimaanisha haki ya urithi kulingana na vibao vyenye maandishi, vilivyoandikwa karibu na wakati wa uhai wa Musa na kupatikana katika mji wa Nuzi.

Kufangamanishwa kidin kwa Raheli na sanamu hizi kunaweza kuwa ni moja ya sababu.

Ingawa baadhi ya watu wanaweza kukubaliana na mtazamo wa chuki wa Raheli, Biblia haiungi mkon jambo hili, inalirekodi tu. Rachel alikufa wakati wa kujifungua mtoto miaka michache tu baada ya kuchukua miungu kwenye Mwanzo 35:17-19, hivyo hiyo miungu ya familia haikufanya jema lolote kwake. Biblia si kitabu cha mashujaa walivuka viwango vya wanadamu, bali watu halisi kabisa walio na mapungufu mengi — kama tuliyonayo.

 

S: Kwenye Mwanzo 31:47, kwa kuwa Mwanzo iliandikwa mapema sana, kwa nini kuna maneno mawili ya Kiaramu kwenye mstari huu?

J: Jambo hili linaonyesha kuwa Kiaramu kilikuwepo pamoja na Kiebrania mapema sana. Kumbuka, Washami walikuwa wakiishi Syria ambako Labani aliishi. Wake wa Yakobo walitoka huko. Jambo lingine, haya yanaweza kuwa maneno ya kawaida kwenye Kiebrania cha kale.

 

S: Kwenye Mwanzo 32:22-32, je Yakobo alibadilishwa jina kuwa Israel hapa, au Yakobo alibadilishwa jina kuwa Israel kwenye Mwanzo 35:9-10? (Mkristo mwenye kutilia shaka mtazamo wa kimapokeo alisema jambo hili kama ushahidi kuwa Mwanzo iliandikwa na watunzi zaidi ya mmoja).

J: Mwanzo 32:22-32 ina maelezo mengi sana, na inasema jinsi ambavyo Yakobo alishindana na Mungu, na alivyopewa jina la Israeli. Mwanzo 35 inatoa muhtasari wa maisha ya Yakobo, na aya mbili, 35:9-10 zinaongelea kuhusu kubadilishwa jina kwa Yakobo hivyo tunaweza kujua mahali ambapo tukio la Mwanzo 32 ilitokea. Ndiyo, aya hizi mbili ni marudio, lakini jambo hili linasaidia masimulizi, si matokeo ya mpango wa makusudi wa kuweka habari hii mara mbili. Leo, watu wanapoandika, mara nyingi huwa wanarudia kwenye hitimisho kitu ambacho wamesema kwenye sehemu kuu ya insha, lakini hii haimaanishi kuwa sehemu mbalimbali za insha ziliandikwa na waandishi tofauti.

 

S: Kwenye Mwanzo 32:27-28, kwa nini Yakobo alibadilishwa jina na kuwa Israel?

J: Ingawa Biblia haisemi kuna vitu viwili vinavyowezekana, na vyote vinaweza kuwa kweli.

Kitendo cha kubadilisha jina kilionyesha kuwa Mungu anadhibiti maisha yote, hata maisha yao, na kwamba walikuwa watu tofauti, wenye hatima tofauti, kwa sababu ya Mungu. Nadhani kuwa tutkapofika mbinguni tunaweza kumuuliza Abraham, Petro, na Sauli owa Tarso kuhusu jambo hili.

Majina na maana kubwa nyakati hizo, na Israel inaonekana kumaanisha "Mungu anahifadhi" au "Anavumiliana na Mungu", na inahusiana na "umeshindana na Mungu."

 

S: Kwenye Mwanzo 32:24, 27, kwa kuwa Yakobo alishindana na mtu, ambaye alitokea kuwa malaika au Mungu, je Mungu ni malaika au mwanadamu?

J: Mungu anaweza kuonekana hata kuwa kama kichaka kinachowaka moto, lakini jambo hilo halimfanyi Mungu kuwa mmea. Ingawa Mungu yupo kila mahali, anaweza pia kuonyesha uwepo wake kwenye eneo lolote kupitia kitu chochote anachokitaka. Angalia pia jibu la Mwanzo 3:8 kwa maelezo zaidi.

 

S: Kwenye Mwanzo 32:24-32, je Yakobo alikuwa anapambana na malaika halisi, au alikuwa anapambana ni kitu kingine chochote?

J: Hakuna kitu kinachoonyesha kuwa tunaweza kuongeza kwenye Maandiko kuwa huyu hakuwa malaika halisi.

Tazama Now That's A Good Question uk.571-572 kwa maelezo zaidi kuhusu mambo haya matatu yafuatayo:

1. Kuichukua maana iliyowazi ya Biblia ndio njia pekee ya kuitafsiri kwa uaminifu

2. Kuchukua maana iliyowazi ya Biblia haimaanishi kuiwekea maana kavu kama mbao au saruji

3. Kuchukua maana iliyowazi ya Biblia maana yake ni kukitafsiri kitabu kama kilivyoandikwa.

Ingawa Wayahudi Josephus na Philo walitafsiri mapambano ya Yakobo kama ndoto, ndoto hazitegui uvungu wa mapaja..

 

S: Kwenye Mwanzo 32:24-30, je Allah [Mungu] wa Ukristo ni mnyonge sana hata anachukua usiku mzima kupambana na Yakobo, kama Muislam mmoja alivyosem?

J: Awali ya yote alikuwa ni malaika wa Mungu (ambaye Yakobo alimwita mtu), sio Mungu mwenyewe aliyepambana naye. Yakobo alisema kuwa alimwona Mungu uso kwa uso, lakini Yakobo alikutana na Mungu kupitia kwa malaika tu. Bila kujali kuwa Mungu alimtuma malaika huyu, aliyekuwa na nguvu za kumpiga Yakobo.

Kama baba anapambana na mtoto wake wa miaka miwili mwenye msimamo wa nguvu, na hata hata kama ikitokea kuwa mtoto wa miaka miwili akashinda nyakati zingine, jambo hili halimfanyi baba huyu kuwa dhaifu. Kadhalika, nia ya Mungu ilikuwa kushindana na ukaidi wa Yakobo, na si kumharibu Yakobo na mshikamano wake. Mungu alitaka Yakobo aelewe kuwa Yeye ni nani, si kumuua.

Fikiri ingeweza kuwa vema kiasi gani endapo mwili wako ungekuwa vilevile isipokuwa uwe na nguvu nyingi mara 100. Unaweza kufanikiwa kwenye riadha, kuvunja kuta, na kukimbia haraka sana. Lakini, kila wakati unapojaribu kuchukua ua unalivunja, kila wakati unaposhika mkono wa mtoto mdogo unauvunja, na kila wakati unapomshika mke au mume wako analazimika kwenda hospitali. Huenda kuwa na misuli yenye nguvu mara 100 si kitu chema kabisa.

Mungu ni mwenye nguvu zote, lakini Mungu pia ana upole na maarifa. Mungu ni mwenye nguvu nyingi kuliko sisi mara nyingi zisizohesabika, lakini Mungu ana udhibiti mkubwa wa nguvu zake mwenyewe kuliko jinsi tunavyofanya na nguvu zetu. Sefania 3:17 inatoa mfano wa jinsi Mwenyezi Mungu alivyo mpole: "Bwana, Mungu wako, yu katikati yako shujaa awezaye kuokoa; Atakushangilia kwa furaha kuu, atakutuliza katika upendo wake, atakufurahia kwa kuimba."

Kwenye 1 Wafalme 19:11-13, Mungu anamwambia Eliya ataushuhudia uwepo wa Bwana. Haikuwa kwa kuleta upepo mkali, tetemeko la ardhi, au moto, bali kwa sauti ndogo ya utulivu.

Hiyoo kwa muhtasari, Wakristo wanamwabudu Mungu ambaye ni mpole bila kupunguka kuwa Mwenye enzi yote.

 

S: Kwenye Mwanzo 32:30, je kuna mtu yoyote anayeweza kuuona uso wa Mungu, kwa sababu Kutoka 33:20 inasema hakuna mtu atakayemwona na kuishi?

J: Yakobo aliona umbo la malaika; mara ya kwanza alidhani alikuwa mtu, na kwa hakika hakuwa amemuona Mungu uso kwa uso katika utukufu wake.

 

S: Kwenye Mwanzo 33 na 36:7, je Esau na Yakobo walitengana kwa sababu mali zao zilikuwa nyingi sana, au kwa sababu ya hofu ya Yakobo kwa Esau?

J: Vyote.

 

S: Kwenye Mwanzo 33:18-19 na Yoshua 24:32, je Yakobo alinunua ardhi Shekemu, au Abraham ndiye aliyeinunua kama Matendo 7:15-16 na Mwanzo 23:16-20 zinavyosema?

J: Ibrahimu alinunua ardhi Mamre karibu na Hebroni kwa ajili ya Sara kwenye Mwanzo 23:16-20, lakini hiyo si mahali pale pale. Kuhusu ardhi iliyonunuliwa Shekemu, kuna majibu mawili yanayowezekana.

Yakobo na Abraham waliinunua: Yoshua 24:32 na Mwanzo 33:18-19 zinasema Yakobo, mjukuu wa Ibrahimu, ndiye aliyenunua ardhi karibu na Shekemu. Bila kujali endapo Ibrahimu alikuja kushuhudia ununuzi wa ardhi akiwa na fedha aliyompa Isaka au la, inawezekana kusema kuwa ukoo wa Ibrahimu uliinunua ardhi. Hata leo, kijana, kwa ridhaa ya baba yake, anaweza kununua gari kwa kutumia jina la baba yake.

Stefano aweza kuwa amekosea: Kwa kuwa Yakobo alinunua ardhi watoto wake walizikwa hapo, ingawa Yakobo mwenyewe alizikwa Mamre pamoja na Ibrahimu, Stefano anaweza kuwa alichanganya matukio haya mawili kwa bahati mbaya. Hata kama Stefano alkosea, Biblia bado ingekuwa sahihi. Biblia ilirekodi tu kitu ambacho Stefano alichokisema kwa makosa.

Angalia maelezo ya Mwanzo 50:13 kwa maelezo zaidi.

 

S: Kwenye Mwanzo 33:18-19, ni kitu gani zaidi tunachokijua kuhusu mji wa Shekemu?

J: Ingawa mji huu ulikuwa umeharibiwa wakati wa Abrahamu, mahali mji ulipowepo palijulikana, kama Can Archaeology prove the Old Testament? uk.26 inavyosema. Abrahamu hakuununua mji bali ardhi iliyokuwa karibu na Shekemu.

The Wycliffe Dictionary of Biblical Archaeology uk.518-522 inatoa maelezo mengi ya kina juu ya Shekemu. Mji huu ulikuwa unajengwa upya mara kwa mara kwa sababu ulijengwa kwenye mlima ulioweza kuimarishwa kiulinzi na ulikuwa na kijito kizuri. Shekemu ilijengwa upya karibu mwaka 1900 KK, lakini Farao Senusert III (karibu mwaka1880-1840 KK) aliuteka. Shekemu ilibomolewa tena karibu mwaka 1750 KK. Ilijengwa upya, lakini ilibomolewa tena na Wamisri karibu mwaka 1550 KK. Ilijengwa upya, wakti wa barua za Amarna (mwaka 1500-1200 KK) ambayo imeutaja kama kituo cha Mfalme Lab'ayu ambaye alikuwa mshirika wa wavamizi wa "Habiru." Ilijengwa upya, lakini iliharibiwa na Waashuri, Waaremi, Mfalme Menaham wa Israeli, na Waashuri mwaka 723KK.

 

S: Kwenye Mwanzo 34:13-17, Munugu [inadaiwa] angewezaje kuunga mkono majibu ya uongo ya watoto wa Yakobo kuhusu Dinah?

J: Mungu hakuyaunga mkono, na watoto wawili wa Yakobo waliowaua watu wa Shekemu walilaaniwa kwa ajili ya jambo hilo.

 

S: Kwenye Mwanzo 34:25-30, je Simeoni na Lawi waliwezaje kuuangamiza mji wote peke yao?

J: Waliongoza uvamizi, lakini walikuwa na watumishi wengine, askari wa kuajiriwa, na/au ndugu chini ya uongozi wao.

 

S: Kwenye Mwanzo 35:1-5, je mfuatano wa matukio ukoje hapa?

J: Huu hapo ndio mfuatano.

1. Yakobo anaonekana kutokuwa mwangalifu sana kuhusu kuruhusu sanamu za kigeni kati ya kundi lake la wafugaji wanaohamahama.

2. Mungu alimwambia Yakobo kuwa alitaka Yakobo aishi Betheli na kumjengea madhabahu.

3. Yakobo aliona kiusahihi kuona kuwa kama watakwenda kujenga madhabahu kwa ajili ya Mungu, haitafaa kuwa na sanamu yoyote kati yao.

4. Mara walipojitoa kikamilifu kwa Bwana, hawakuwa na kiti chochote cha kuwahofia watu wanao wazunguka.

S: Kwenye Mwanzo 35:21, je watoto wote wa Yakobo walizaliwa Migdal Eber, au walizaliwa kabla kama sehemu nyingine za kitabu cha Mwanzo zinavyosema? (Mkristo mwenye kutilia shaka msimamo wa kimapokeo alilitaja jambo hili kama utata).

J: Mwanzo 35:21-26 haisemi kila mmoja wa watoto wa Yakobo walizaliwa Migdal Eberi, hasa kwa vile kwenye Mwanzo 35:19-20, Rachel alikuwa ametoka kufariki kabla ya wao kuhamia huko. Mwanzo 35:21-26 inaoorodhesha tu watoto, ikifuatia maelezo ya Israeli (= Yakobo) kupiga kambi ng'ambo ya Migdal Eberi.

 

S: Kwenye Mwanzo 36, kuna sababu gani ya watu kujishughulisha na nasaba ya uzao wa Esau?

J: Kwa kusema ukweli hii si sura muhimu zaidi katika Biblia. Hata hivyo, sura hii inaonyesha hoja ya usahihi wa kihistoria na maelezo ya kina ya kihistoria.

 

S: Kwenye Mwanzo 36:2, je Zibeon ulikuwa mji wa Wahivi au Wahori kama Mwanzo 36:20 inavyosema?

J: Kuna mambo mawili yanayowezekana:

Makosa ya kuandika: Wasomi wengi wanadhani haya ni makosa ya kuandika kwenye maandishi ya Massoretiki, kwani kwenye Kiebrania Mhivi ni h[i]wwt, na Mhori ni h[o]rrt. Tafsiri ya Kigiriki ya Agano la Kale (Septuagint) inawataja Wahori kwenye Mwanzo 34:2 na Yoshua 9:7.

Majina mawili ya kundi moja au makundi mawili yaliyoungana: Wahori (Hurrians) pia waliishi Palestina kwenye maeneo ambayo Wahivi waliishi, kama ilivyoshuhudiwa na majina ya watu ya Kihuria. Hata mkuu wa Yerusalemu katika karne ya 14 KK alikuwa na jina la Kihuria la Abdi-Hepa.

 

S: Kwenye Mwanzo 36:31, je msemo "kabla ya kumiliki mfalme yeyeto juu ya wana wa Israel" unaonyesha kuwa wakati wa kuandikwa kitabu cha Mwanzo ni wakati wa Sauli au baadaye?

J: Hapana. Musa aliweza kufahamu si tu kwamba kutakuwa na mfalme juu ya Israeli (Kumbukumbu 17:14-15), bali Waisraeli wote hadi wakati wa Yakobo walifahamu kuwa Israeli atakuwa na mfalme toka kabila la Yuda, kwa sababu unabii wa Yakobo kwenye Mwanzo 49:10.

 

S: Kwenye Mwanzo 37:3, 23, 32, je kuna ushahidi wowote mbali ya Biblia wa koti lenye rangi nying?

J: Ndio, ingawa si vazi halisi la kweli la Yusufu. Wataalamu wa elimukale wamegundua "Waasia", wenye makoti yenye rangi nyingi, waliochorwa kwenye kuta za kaburi la mtu mashuhuri wa Mmisri aitwaye Khnumhotep. Tazama Pharaohs and Kings : A Biblical Quest uk.332, 360 kwa picha na maelezo zaidi.

 

S: Kwenye Mwanzo 37:17, je kuna ushahidi mbali ya Biblia wa kufanya watu "watoweke" kwa kuwatupa kwenye visima?

J: Ndiyo. Kaka za Yusufu walikuwa karibu na Dothani, na Can Archaeology Prove the Old Testament? uk.29 inasema kisima kilichopo Dothani kilikutwa kikiwa na mifupa mingi ndani yake.

 

S: Kwenye Mwanzo 37:17, je kaka zake Yusufu walikuwa wanapanga kumuua, au waliamua kumuuza Yusufu kwa wafanya biashara wa Midiani kama Mwanzo 37:28-29 inavyosema?

J: Yote ni kweli, kwa sababu watu wanaweza kubadili mipango yao. Awali walipanga kumuua Yusufu, isipokuwa Reubeni alipanga kumwokoa. Lakini walipoona wafanyabiashara wa Midiani, walifikiri wanaweza kutengeneza hela tokana na Yusufu na kubadili mipango yao. Kwa mtazamo wa kaawaida mtu anaweza kufikiri kuwa Yusufu alikuwa na "haki" ya kuwa na uchungu kuhusiana na jambo hili. Lakini, Yusufu alimfuata Mungu, nyakati ngumu hazikumfanya awe na uchungu, bali zilimfanya kuwa mtu bora.

 

S: Kwenye Mwanzo 37:25, je wafanya biashara hawa walikuwa Waishmaili, au Wamidiani kama Mwanzo 37:28 inavyosema?

J: Kaka za Yusufu hawakuweza kujua ni watu gani waliokuwa wanakuja, au endapo walkuwa mchanganyiko wa Waishmaili na Wamidiani. Hata hivyo, haijalishi kwa hawa ndugu, wao walitaka hela tu. Huenda neno Waishmaili au Wamidiani likawa kosa la kunakili. Au, kaka zake walidhani kuwa walikuwa Waishmaili wakati walikuwa Wamidiani.

 

S: Kwenye Mwanzo 37:28, je shekeli 20 za fedha zilikuwa bei sahihi ya mtumwa kama Yusufu?

J: Ndiyo. Kwa mujibu wa K.A. Kitchen kwenye Ancient Orient and Old Testament Introduction uk.52-53, hii ni bei sahihi karibu mwka 1800 KK. Karne zilizotangulia bei ilikuwa shekelo 10 hadi 15 za fedha, na ilikuwa shekeli 30 za fedha karibu na wakati wa Musa, na baadaye watumwa walikuwa ghali zaidi. Kwenye Hosea 3:2, mtumwa alikuwa na thamani ya karibu shekeli 30. Tazama Biblical Archaeology Review juzuu ya 21 na.2, uk.53 kuona grafu ya bei ya mtumwa na muda.

 

S: Kwenye Mwanzo 38:1-21, kwa nini habari hii ya Yuda na Tamari imo kwenye Biblia?

J: Kwa kipimo kuanzia cha chini (si kiwango kibaya kama) cha 1 na cha juu (kibaya zaidi) cha 10, zinaa ikwa 10, utaitaje kutokukusudia kutimiza ahadi ambayo mtu mwingine alikuwa anaitegemea muda wote uliobaki wa maisha yake? - Kwa hakika ni zaidi ya 1. Kuna angalau mambo matatu tunaweza kujifunza kutokana na hili.

1. Tusije kufikiri kuwa Yuda na mababa wengine wa taifa la Israeli walikuwa na haki kuliko kila mtu mwingine yoyote, habari hii na nyingine zote zinaturudisha kwenye ukweli kwamba hakuwa na haki kabisa.

2. Biblia inatupa habari wazi na sahihi ya jinsi watu walivyoishi wakati ule. Biblia "haipaki sukari" historia yao kwa namna yoyote ile. Tunaweza kujifunza tokana na mambo waliyoyafanya kimakosa pamoja na yale waliyofanya kwa usahihi.

3. Jambo hili linaonyesha aina ya dhambi iliyopo leo lakini haiongelewi mara nyingi: kupungua kwa uwajibikaji. Hii inachukuliwa kuwa dhambi mbaya sana machoni pa Mungu, kwani Onani aliuawa kwa sababu hiyohiyo. Yuda pia hatukutimiza wajibu wake kwa mkwe wake (mke wa mtoto wake), na hakufanya maneno aliyosema yeye mwenyewe. Yuda hakuruhusu mtoto wake amrithi Tamari, kwa sababu aliogopa kuwa mwanawe atakufa kwani hakuamini wema wa Mungu. Ni dhahiri, Yakobo hakudhani kuwa kitendo cha Onani kukataa kutimiza wajibu wake kilstahili kifo.

 

S: Kwenye Mwanzo 38:29-30, je Zerah/Zarah na Perez/Pharez zinamaanisha nini?

J: Kwanza nini maana zake, na kisha matumizi yake mawili. Strong's, kamusi za Biblia, na maoni (commentaries) zote zinakubaliana kuwa Perez/Pharez ina maana penya, tengua, shinda, songa mbele licha ya ushindani au vunja (amani, mkataba). Alivunja au kufungua tumbo tumbo. Hata hivyo, kuna tofauti ndogo ya maoni kuhusu Zera/Zarah.

Rangi nyekundu: Kwa sababu ya uzi mwekundu uliofungwa mkononii mwake, "Zera" hivyo basi inaweza kumaanisha "rangi nyekundu" kwa mujibu wa Wycliffe Bible Dictionary uk.1844.

Inamaanisha mwangaza au wekundu kwa mujibu wa New International Bible Commentary uk.139.

Inamaanisha ‘nyekundu' kwa mujibu wa Bible Knowledge Commentary : Old Testament uk.89.

Kuinuka: Zerah inatokana na neno la Kiebrania Zerah, ‘kuinuka' kwa mujibu wa New International Dictionary of the Bible uk.1085.

Sababu ya tofauti ya maoni inaweza kupatikana kwenye Strong's Exhaustive Concordance (neno la 2226). Inasema ni sawa na neno la 2225 "zerach, zeh'-rakh kutoka 2224; kuinika kwa mwanga:- kuinuka." 2224 inasema "zarach, zaw-rakh'; makini/nadhifu. Mzizi; chanzo, kuangazia (au kutoa miale), yaani, kuinuka (kama jua); kiubayana kutokea (kama dalili ya ukoma): - inuka, simama (juu), mara itakapouwa juu. Kwa hiyo neno Zerah limetokana na kuchomoza kwa jua, na linaweza kumaanisha kuchomoza halisi kwa jua, au inaweza kumaanisha rangi nyekundu ya wakati wa kuzama kwa jua.

Ukoo wa Masihi kwenye Mathayo 1:3 inaeleza kwa ufupi uzazi wote huu. Katika kuja kwake mara ya kwanza, Yesu alisema kuwa ataleta mafarakano kwenye Luka 12:51. Paulo anazungumzia ung'aavu wa kuja kwa Yesu kwa mara ya pili kwenye 2 Thesalonika 2:8. Kwa hiyo mapacha yamekuja kufuata ujio wa Yesu mara mbili. Hata hivyo, kwa upande mwingine, Yohana 1:5, 9 inasema kuwa Yesu alikuwa nuru ya kweli inayowapa nuru watu wote, na kwamba alikuja ulimwenguni.

Akani, ambaye aliuawa kwenye Yoshua 7 alikuwa mzao wa Zera. Hivyo mtu mwenye asili maalum au ya kiungu hainamaanishi kuwa ni lazima awe mwenye haki, au anaweza kuepuka hukumu.

 

S: Kwenye Mwanzo 39:7-10, kwa kuwa Amri Kumi zilikuwa bado hazijaandikwa, palikuwa na ubaya gani kwa Yusufu kulala na mke wa mwajiri wake?

J: Yusufu hakuhitaji Amri Kumi kujua kwamba kufanya hivyo kungevunja imani ya bwana wake kwake. Yusufu pia alisema kuwa jambo hili lingekuwa dhambi kwa Mungu.

Watu wengine wanaishi kwa kufuata sheria kama zilivyoandikwa tu. Lakini, hivyo sivyo Yusufu alivyotenda, na hivyo sivyo Wakristo wanavyopaswa kutenda. Badala ya kuuliza "ninaweza kuepukana na jambo hili" au "je kunza kizuizi cha wazi kabisa cha jambo hili", inatunapasa tuwe tunauliza "jambo gani litakuwa linampendeza Mungu."

Kuna hadithi ya kuvutia ya Kiarabu inayoonyesha fikra za utiifu wa sheria kama ilivyoandikwa tu. Mtu mmoja alibalina na jini mwovu. Wote wawili walisaini karatasi, ambapo jini lilitakiwa kumpa mwanamke mzuri zaidi ambaye lingeweza kumfikiria kuwa mke wake na kwamba jini lisinge mdhuru. Jini lilitoweka, na baadaye mwanamke mzuri akatokea na alitaka kuwa mke wake. Yule mwanaume hakujua kuwa mwanamke huyo alikuwa jini aliyejigeuza sura. Usiku mmoja "mwanamke" alimwomba mwanaume aangalie makubaliano. Mtu huyo alipochukua mkataba, jini lilisababisha nta kutoka kwenye mshumaa kufunika neno "hakuna" kwenye "hakuna kumdhuru mtu", na jini lilimuua yule mtu.

Inavutia kwamba, kwa baadhi ya watu, nta kidogo tu ya mshumaa ilikuwa ndiyo kitu kilichotakiwa kuhalalisha kubatilisha ahadi ya watu hao wawili. Leo kuna watu wanaodhani sahihi kuvunja makubaliano kwa sababu zisizokuwa na msingi. Kwa waamini wa kweli wa Mungu, si tu kwamba tunatimiza ahadi zetu kama maneno ya makubaliano yetu yalivyoandikwa, lakini pia tunatimiza kusudi la maneno yetu, na kutoruhusu sababu zisizokuwa za msingi kuwa visingizio vya kutokuwa waaminifu.

 

S: Kwenye Mwanzo 40:15, je Yusufu alichukuliwaje kutoka nchi ya Waebrania?

J: Tunafikiri kuwa Ebrania ni sawa na Israeli, lakini haikuwa hivyo wakati ule. Muebrania, au ‘Apiru, pia ilimaanisha mfugaji mwenye kuhamahama, na Abramu aliitwa Muebrania. Hivyo, Yusufu ama alimaanisha asili yake toka kwa Ibrahimu na kuishi kwake kwenye nchi mpya ya Ibrahimu, au kwamba alitoka kwenye nchi ya wafugaji wanaohamahama, au vyote viwili.

 

S: Kwenye Mwa 40:20-22, Mt 14:6, na Mk 6:21, je ni vibaya kusherehekea siku za kuzaliwa kwani sherehe pekee za siku za [inadaiwa] kwenye Biblia ni wakati ambapo Farao alipomuua mwoka mikate wake na Herode alipomuua Yohana Mbatizaji?

J: Hapana. Mashahidi wa Yehova hujaribu kutumia hoja jambo ambalo halijaongelwa kupinga maadhimisho ya siku ya kuzaliwa. Wote Farao na Herode walikuwa watu makatili, wakandamizaji na watawala wasio na kiasi ambao waliwaua watu hata katika siku zisizokuwa za kuzaliwa, lakini kuna sababu mbili zenye nguvu zenye kuonyesha kuwa kuadhimisha siku maalum ya mtu kuzaliwa ni sawa.

Ayubu alikuwa mcha Mungu, na kila mmoja wa watoto wake alisherehekea karamu nyumbani kwao "kila mmoja wao kwa siku yake" (Ayubu 1:4). Msemo "siku yake" unamaanisha siku zao za kuzaliwa kama ilivyoonyeshwa na Ayubu kuilaani "siku yake", ambayo ilikuwa ni siku ya kuzaliwa kwenye Ayubu 3:1-3.

Pia, malaika Gabrieli alitangaza kuwa watu wengi watashangilia kuzaliwa kwa Yohana Mbatizaji (Luka 1:14) na kama malaika waliweza kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu (Lk 2:14), ni sahihi kwetu kusherehekea kuzaliwa kwake pia.

Tazama Jehovah's Witnesses Answered Verse by Verse uk.24-26 kwa maelezo mapana zaidi.

 

S: Kwenye Mwanzo 41:32, kwa nini Farao alimfanya mtu asiyekuwa Mmisri kuwa wa pili kuwa msaidizi wake?

J: Ingawa wafalme waliweza kufanya mambo ya ajabu wakati mwingine, kwenye tukio hili ilieleweka vizuri sana. Kama Yusufu angejaribu kuasi, Wamisri wasingemfuata. IKumbukumbu zinaonyesha kuwa Wakanaani, kama vile Meri-Ra, Ben-Mat-Ana, na Msemiti Yanhamu, naibu wa Amenhotep III, alikuwa na nafasi ya juu katika Mahakama ya Misri. (Amenhotep III alikuja kuwa Farao baada ya Waisraeli kuondoka Misri).

 

S: Kwenye Mwanzo 41:45, je jina la Kimisri la Yusufu, Zaphenath-Paneah, lilikuwa ni cheo au jina la mtu?

J: Huenda lilimaanisha "anayeitwa maisha" au kitu kama hicho. Hakuna ushahidi wowote wa Wamisri kuwa cheo kama hiki, hivyo huenda lilikuwa ni jina. Farao huenda alitaka Yusufu aweze kuonekana kuwa Mmisri zaidi kwa wengi wa viongozi wake. Hata hivyo, hii haimaanishi kuwa Yusufu aliliacha jina lake la asili. Jambo hili linafanana kiasi na wakati watu wanatoka China kwenda nchi za Magharibi, mara nyingi huwa wanajipa majina ya magharibi, na wakati watu wanatoka Magharibi kwenda China, mara nyingi nao pia wanajipa majina ya Kichina.

 

S: Kwenye Mwanzo 41:45, je kuna ushahidi wowote mbali ya Biblia wa jina la Kimisri la Yusufu, Zaphenath-Paneah?

J: Ndiyo. Ingawa wasomi hawajui majina yoyote ya majina ya viongozi wa juu Misri kwenye karne za karibu na muda wa Yusufu, wataalamu wa elimukale wamegundua uhusiano.

Zaphenath: Jina la Yusufu la Kimisri kwenye Mwanzo 41:45 huenda lilifikishwa kwentu likiwa limegeuzwa herufi ‘t' na ‘p.' Zat-en-aph linamaanisha "anayeitwa" ambao ulikuwa ni masemo wa kawaida. Papyrus Brooklyn 35.1446 inaonyesha mifano mingi ya Waasia waliopewa majina ya Kimisri. Mengi ya majina haya yana "yeye" (mwanaume/mke) anayeitwa kama sehemu ya kwanza.

Paneah: "Pa" au "Pe" huwakilisha Ipi au Ipu. "Anea" ni sawa na ankh ya Kimisri, inayomaanisha "maisha" au ankhu inayomaanisha "ni hai." Pharaohs and Kings : A Biblical Quest uk.350 inahitimisha kwa kusema Ipiankhu na majina mengine tofauti yalikuwa ya kawaida wakati wa Yusufu lakini hayakuwa ya kawaida sana kabla na baada ya hapo.

 

S: Kwenye Mwanzo 41:57, kwa kuwa njaa ilikuwa kali duniani kote, kwa nini sehemu nyingine hazikupatwa na njaa hiyo?

J: Msemo huu umeeleza kuwa njaa ilikuwa kali hata sehemu nyingine zaidi ya Misri.

 

S: Kwenye Mwanzo 42:6-20, kwa nini Yusufu aliwafanyia hivi kaka zake waliokuwa wamemsahau?

J: Ingawa Biblia haiuridhii wala kuukosoa mkakati huu, jambo hili lilionekana kuwa busara kwa upande wa Yusufu. Yusufu alitaka kujua mtazamo wao ukoje kuhusu mtoto wa pili wa upande wa mama yake, na kitu ambacho wamejifunza miaka yotr toka kuondoka kwake. Alitaka kuona yaliyomo ndani ya mioy yao kabla ya kufungua moyo wake kwao.

Ingawa hakuna mtu leo atakayeweza kuwa katika hali kama hii, kanuni ya jumla bado ni kweli na yenye kufaa kuwa ni vema kujaribu kujua kitu kilichomo kwenye moyo wa mtu kabla ya kumwamini. Katika muktadha tofauti, Yesu alikataza kuwatupia lulu nguruwe kwenye Mathayo 7:6.

 

S: Kwenye Mwanzo 44:5, je Yusufu, mcha Munugu, aliwezaje kudai kutumia uaguzi?

J: Aya hii haisemi Yusufu aliwahi kutumia kile kikombe, isipokuwa tu aliwaambia kaka zake kuwa alitumia kile kikombe kufanya uaguzi. Kwa mujibu wa Mwanzo 44:15, Yusufu anaonekana kutokujali sana kuhusu kikombe. Tunapaswa kuepuka hata ishara za uovu (2 Wakorintho 8:22; 1 Wathesalonike 5:22), na hata Yusufu hakuwa mtu mkamilifu.

 

S: Kwenye Mwanzo 45:6 na 47:28, je Waisraeli walikuwa watumwa wakati Yusufu yuko hai?

J: Ndiyo. Kwa kuangalia Mwanzo 37:2; 41:1, 29-39; 45:6 na 47:28, Yusufu alikuwepo Misri miaka 71 kati ya 110 ya maisha yake, hivyo Waebrania walikuwa watumwa tena wakati Yusufu akiwa bado yuko hai, kwa sababu walikuwa watumwa Misri kwa miaka 400, na waliishi Misri kwa jumla ya miaka 430.

 

S: Kwenye Mwanzo 45:8 na 50:19, je Mungu huwafanya watumwa watu wanaomcha? Je Mungu alimfanya Yusufu, au kaka zake watumwa?

J: Huu ni mfano wa dhana ya kiteolojia inayoitwa ‘Concurrence.' Mungu si tu kuwa alijua maovu ambayo wangeamua kuyafanya kwa uhuru na kwa hiari iwapo wangekuwa kwenye mazingira yale na kutekeleza matakwa ya moyo wao. Pamoja na hayo, Mungu alipanga na kutumia uovu wao kuleta mema. Kama Warumi 8:28 inavyosema, "... katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema...." Mambo yote ni pamoja na maovu.

 

S: Kwenye Mwanzo 46:3-4, je Mungu anazungumza na Yusufu kama mtu mmoja, au wazao wake?

J: Vyote. Mungu anawaunganisha hawa wawili wakati anamwambia Yakobo kuwa "utafanywa" kuwa taifa kubwa. Ingawa Yakobo, alifia Misri, mwili wake ulirudishwa Palestina kwa ajili ya mazishi. Hii ilikuwa ni ishara kuwa "nyinyi" mtatoka Misri miaka 430 baadaye.

 

S: Kwenye Mwanzo 46:4, kwa nini Yakobo alikufa Misri, kwa sababu Munug aliahidi kuwa atamtoa kutoka huko?

J: Watu walijiona kama wazao wao na kama wao wenyewe. Uzao wa Yakobo ulitolewa kutoka Misri. Pamoja na hayo, mwili Yakobo ulichukuliwa kutoka Misri kwenye Mwanzo 50:13-14.

 

S: Kwenye Mwanzo 46:8-27, je kuna makabila 12, 13, au 14?

J: Kulikuwa na watoto 12 wa Israeli (10 + Lawi + Joseph)

Kulikuwa na makundi 12 ya wapiganaji na makabila yenye ardhi (10 + watoto wawili wa Yusufu, Manase na Efraimu na si Lawi).

 

S: Kwenye Mwanzo 46:33, je kuna ushahidi mbali ya Biblia kuwa wachungaji walikuwa chukizo kwa Wamisri?

J: Hatuna ushahidi wowote wa moja kwa moja, lakini tuna vipande kadhaa vya habari.

1. Wakati Wahiksosi wageni walitawala nchi ya Misri, baadaye Wamisri waliwaita watawala wa kigeni waliodharauliwa "wafalme wachungaji."

2. Wakati wa Yusufu, wataalamu wa elimukale wanasema kundi kubwa la Waasia liliishi kwenye bonde la mto Nile. According to Pharaohs and Kings: A Biblical Quest uk.354 uchambuzi wa mabaki ya mifupa ya kondoo unaonyesha kuwa muda karibu na huu walowezi wa Kiasia walileta kwa mara ya kwanza kondoo wenye nywele ndefu kwenye bonde la mto Nile Misri.

 

S: Kwenye Mwanzo 47:20-21, Mungu angewezaje kuridhia kitendo cha Yusufu cha kuwafanya watu wa Misri watumwa wa Farao?

J: Mungu hakutoa maoni kuhusiana na jambo hili, bali aliruhusu kodi hii ya 20% kwenye Mwanzo 47:23-26.

 

S: Kwenye Mwanzo 47:31, je Yakobo alikufa kwenye kichwa cha kitanda chake, au akiwa ameinama kwenye fimbo yake kama Waebrania 11:21 inavyosema?

J: Ingawa mtu anaweza kuwa kwenye kitanda akiinamia fimbo ili asimame kuongea, kuna maelezo rahisi zaidi. Konsonanti za maneno "kitanda" na "fimbo" zinafanana kwenye Kiebrania, na Agano la Kale awali liliandikwa kwa konsonanti tu. Maandishi ya Masoretiki yanaweka vokali ili kulifanya hili neno kuwa "kitanda", wakati Septuagint inalitafsiriwa kama "fimbo." Kama Waebrania 11:21 kwa Kigiriki inasema fimbo, na Wakristo wanaamini kuwa kitabu cha Waebrania kimevuviwa, basi itakuwa fimbo.

 

S: Kwenye Mwanzo 48:5, kulikuwa na umuhimu gani Yakobo kusema kuwa Manase na Efraimu ni watoto wake?

J: Inaonekana kuwa katika mgawanyo wa ardhi wa siku zilizofuata, Manase na Efraimu walichukuliwa kuwa sawa na watoto halisi wa Yakobo. Hivyo, wazao wa Yusufu walipokea mafungu mawili ya mgao wa ardhi, si moja. Mara nyingi mzaliwa wa kwanza alipata mafungu mawili. Ingawa Yusufu hakuwa mzaliwa wa kwanza, alikuwa na haki ya mzaliwa wa kwanza.

 

S: Kwenye Mwanzo 49 na Kumbukumbu 33, unabii huu ulitimizwaje?

A: Kwa kila mtoto, muhtasari wa unabii umetolewa, na kisha kutimia kwake. Kwa ujumla, Mwanzo 49 imetoa unabii mwingi, na Kumbukumbu ina vidokezo vichache tu vya hali ya baadaye kwenye maombi ya Musa.

Reubeni, ingawa ndiye aliyekuwa mzaliwa wa kwanza, hatafanikiwa tena. Kabila la Reubeni lilifanya makazi upande wa mashariki wa Mto Jordan, na halikuwahi kuwa kabila kubwa. Kwa mujibu wa Encyclopedia of Bible Difficulties uk.103, Wamoabu walilishinda kabila la Reubeni katika karne ya tisa, kwa mujibu wa maandiko ya kwenye jiwe la Moabu (mwaka 850 KK).

Simeoni atatawanywa katika Israeli. Kabila la Simeoni lilifanya makazi katikati ya Yuda (Waamuzi 1:3), na lilipoteza vingi ya vitambulisho vya kikabila lao kwani walitawanyika miongoni mwa Yuda.

Lawi pia atasambazwa Israeli. Walawi hawakupewa ardhi, isipokuwa miji tu ya kuishi sehemu zote za Israeli. Walitakiwa kuwa walimu wa Israeli. Wakati wa siku za ufalme uliogawanyika, wengi wao walihamia kusini hadi Yuda.

Yuda atasifiwa na ndugu zake, mkono wake utakuwa shingoni mwa adui zake, na watoto wengine watapiga magoti mbele yake. Yuda atakuwa kama simba. Fimbo ya enzi haitaondoka hadi hapo Shilo atakapokuja. Daudi na viongozi wengine wote waliofuata wa ufalme wa kusini walitoka kwenye kabila la Yuda. Yesu alikuwa mzao wa Daudi, kibaiolojia kupitia Mariamu, na "kisheria" kwa baba yake wa kuasiliwa, Yusufu. Mwanzo 49:10-12 ni aya zinazomwongelea Masihi.

Zabuloni ataishi kando ya bahari na mpaka wake ulikwenda hadi Sidoni ya Foinike. Utabiri huu kuhusu mahali watakapoishi ulitimia.

Issakari atakuwa katika sehemu nzuri ya kupumzikia yenye kufurahisha, na atafanya kazi za kulazimishwa. Isakari alitawaliwa na wageni pamoja na makabila meingine ya kaskazini wakti wa utawala wa Waashuru mwaka 732 KK.

Dani atatoa haki, kama nyoka hatari. Kama mwana simba, atainuka kutoka Bashani. Dan alirithi sehemu ya kati (mbali kutoka Bashani), lakini washambuliwa kikatili na Laishi kwenye Waamuzi 18, walikwenda upande wa kaskazini karibu Bashani.

Gadi atshambuliwa, lakini atalipiza mashambulizi. Wamebarikiwa hao wanaopanua milki ya Gadi. Maneno haya yanaweza kuwa yanaongelea kiunabii kuhusu Naftali Mgadi, aliyewashinda Waamoni.

Asheri atakuwa na chakula kingi na maridadi sana. Asheri atakuwa na nguvu siku zake zote. Asheri alikuwa na matatizo kadhaa vitani, lakini yalikuwa yanafanana na utamaduni wa Kifonisia.

Naftali atakuwa kama ayala mwanamke anayezaa watoto wazuri. Naftali atairithi upande wa kusini hadi kwenye ziwa. Naftali hakuwa na jukumu kubwa katika vita vingi, na walifanya makazi pembeni mwa Bahari ya Galilaya.

Yusufu atakuwa mzabibu wenye kuzaa matunda mengi, ambao matawi yake hupanda juu ya ukuta. Wapiga mishale watampiga, lakini upinde wake utakuwa imara. Kama mtoto wa mfalme miongoni mwa kaka zake. Yusufu atakuwa na vitu vingi kwa ziada. Nusu ya makabila mawili ya Yusufu, yani, Efraimu na Manase, yalikuwa na idadi kubwa zaidi ya watu baada ya Yuda. Baadaye Ephraim amekuja kuwa sawa na ufalme wa kaskazini, kama Yuda alivyokuja kuwa sawa na ufalme wa kusini.

Benjamini atakuwa mbwa mwitu mkali sana. Ehud Mbenyamini alikuwa ni hakimu aliyemuua Egloni wa Moabu. Benjamin, ingawa kabila dogo, alipigana kwa ukali dhidi ya makabila mengine katika kwenye Waamuzi 20.

 

S: Kwenye Mwanzo 49:5-7, Yakobo aliwezaje kumlaani Lawi, kwa sababu Musa alimbariki Lawi baadaye kwenye Kumb 33:8-11?

J: Wazao wa Lawi walisambaa Israeli yote kwa sababu ya kitendo hiki cha kikatili. Wazao wa Lawi walibarikiwa kwa sababu ya kupewa heshima ya kufundisha Israeli. Kuna somo la kujifunza hapa. Laana, tunapoivumilia na kumfuata Mungu, inaweza kubadilika kuwa baraka.

 

S: Kwa kuwa Mwanzo Gen 49:10 inasema fimbo ya enzi haitaondoka hadi "Shiloh" atakapokuja, huyu anawezaje kuwa Masihi?

J: Tafsiri za Kigiriki na Kilatini zinasema "yeye ambaye ni yake." Usemi huu ulijulikana kuwa unamwongelea Masihi na watafsiri wa kihistoria wa Kiyahudi, kama Targumi ya Kiaramu inavyoutafsiri usemu huu "Masihi." Usemi huu pia unamwongelea Masihi kwa mujibu wa Targumi ya Yonathani na Targumi ya Pseudo-Jonathan (= Targumi Yerushalmi I, = Targumi Ezez). Wayahudi walipoteza haki ya adhabu ya kifo katika mwaka wa 11, BK kama Talmud ya Babeli inavyosema kwenye Sanhedrin sura ya 4 kufuatia 51b; sura ya 4 kufuatia 37; recto. Ezekiel 21:27 ina maelezo sambamba kama Mwanzo 49:10.

Wengine wanaweza kumwona kuwa kama kiongozi rasmi wa Palestina. Chini ya utawala wa Warumi, mfalme wa Wayahudi Archelaus aliondolewa madarakani na wakili anayewakilisha utawala wa Kirumi Coponius alichukua nafasi yake.

Kama nyongeza, Expositor's Bible Commentary juzuu ya 1, uk.224 inasema Talmudi ya Babeli inaeleza kuwa Trgumi ya Yonathani iliandikwa na Jonathan bin Uzziel, aliyeishi karne ya kwanza BK, na alikuwa mwanafunzi mashuhuru zaidi wa Hillell.

Kwenye Dead Sea Scroll Commentary on Genesis (4Q252 [=4QpGena), kipande cha 2 ikijadili Mwanzo 49:10, inasema "Wakati wowote Israeli ilipotawala, [hapata]kosa kuwa mzao wa Daudi kwenye kiti cha enzi. Kwa sababu fimbo ya mtawala agano la ufalme, [na koo] za Israeli ni makundi, hadi Masihi wa Haki atakapokuja, Tawi la Daudi. The Dead Sea Scrolls in English 4th ed. uk.300-302 pia inasema kuwa maoni haya yanawachukulia wafalme wa Kiyahudi wa Hasmonea kuwa watawala wasiokuwa halali, kwa kuwa si wa ukoo wa Yuda.

Josephus kwenye kitabu chako, Wars of the Jews (mwaka 93-94 BK) kitabu cha 2 sura ya 8 inasema, "Na sasa sehemu Archelaus ya Yuda ilipunguzwa hadhi kuwa mkoa, na Caponius, moja ya utaratibu wa Equestrian wa Warumi, alitumwa kama wakili, akiwa amepewa na Kaisari mikononi mwake mamlaka ya kuua na kuacha hai " Josephus pia anasema kuwa Baraza la Wayahudi (Sanhedrin) lilipoteza mamlaka ya kesi za mauaji kwenye Antiquities of the Jews 20.9 (iliandikawa karibu mwaka 93-94 BK).

Wayahudi wenyewe waliuelewa usemi huu kama unabii unaomhusu Masihi. Kwenye Babylonian Talmud, Sanhedrin, sura ya 4 ifuatayo 37, recto. Rabi Rachman alisema, "Wajumbe wa Baraza walipojikuta wamenyimwa mamlaka yao ya kuua na kuacha hai, mashaka yaliwashika; walipaka vichwa vyao majivu, na miili yao nguo za magunia, huku wakisema kwa mhangao: ‘Ole wetu, kwa sababu fimbo ya enzi imetoweka Yuda, na Masihi hajaja!" Jambo hili lilitokea mwaka 7 BK (Imetolewa kwenye kitabu cha Josh McDowell, Evidence That Demands a Verdict juzuu ya 1, uk.169, na Jesus Before the Sanhedrin cha Augustin Lemann, 1886 kilichotafsiriwa na Julius Magath, NL#0239683, Library of Congress # 15-24973. Tazama pia Pugio Fidei cha Martini, Raymundus, kilichochapishwa na De Vosin mwaka 1651 (uk.148).

Babylonian Talmud, Sanhedrin 98b, Rabi Johanan aliandika, "dunia iliumbwa kwa ajili ya Masihi, jina la huyu Masihi ni nini?" Shule ya Rabi Shila ilisema ‘jina lake ni Shilo, kwa maana imeandikwa; hadi Shilo atakapokuja" (uk.147).

Talmud "miaka zaidi kidogo ya arobaini kabla ya kubomolewa kwa Hekalu, mamlaka ya kutoa hukumu ya kifo ilichukuliwa toka kwa Wayahudi." Talmud ya Yerusalemu, Sanhedrin folio 24 (uk.147).

Targum Onkelos inasema, "upitishaji wa mamlaka hawatakoma kwenye nyumba ya Yuda, wala mwandishi toka kwa watoto wa watoto wake, milele, hadi Masihi atakapokuja." (The Messiah: An Aramaic Interpretation; The Messianic Exegesis of the Targum, Samson H. Levy (Cincinnati: Hebrew Union College Jewish Institute of Religion 1974) uk.2 (uk.146).

Targum Pseudo-Jonathan kuhusu Mwanzo 49:11a, "Wafalme na watawala hawatakoma kutoka kwenye nyumba Yuda ... hadi Masihi Mfalme atakapokuja" (uk.7).

Chanzo cha ziada cha Kiyahudi kinaonyesha kuwa Wayahudi waliouelewa kuwa huu ulikuwa unabii unaomhusu Masihi ni Targumi ya Jonathan ya Mwanzo 49:10, 11a. Justin Martyr (aliyeandika mwaka 138-165 BK) aliyesema kuwa unamwelezea Kristo kwenye kitabu chake, First Apology sura ya 32.

 

S: Kwenye Mwanzo 49:10 inaongelea fimbo ya enzi ya ufalme hadi "Shiloh" atakapokuja. Je unabii huu wenye sura ya vita unawezaje kumwongelea Yesu?

J: Kiroho, Yesu alikuwa na sura ya vita katika kumshinda Shetani wakati wa kuja kwake kwa mara ya kwanza. Pamoja na hayo, Yesu atakuwa na sura ya vita na kuwaua wengi wakati wa kuja kwake mara ya pili kwenye Ufunuo 19:11-16.

 

S: Kwenye Mwanzo 49:10, kwa kuwa fimbo ya enzi haitaondoka kutoka Yuda hadi Masihi atakapokuja, kwa nini hapakuwa na wafalme toka Yuda baaada ya uhamisho isipokuwa watawala wa Maccabees?

J: Mwanzo 49:10 haiahidi kuwa kutakuwa na wafalme huru. Inasema tu kuwa kutakuwa na mtawala, na Gedalia, na wengine wengi walifanya hivyo kama maliwali chini ya Babeli, Uajemi, na serikali nyingine.

 

S: Kwenye Mwanzo 49:10, kwa kuwa Yuda alipaswa kutawala hadi Masihi atakapokuja, kwa nini Sauli alikuwa anatoka kwenye kabila la Benjamini?

J: Hapakuwa na mfalme wakati unabii huu unatolewa. Sauli alikuwa amekataliwa kuwa mfalme, lakini mara Daudi (kutoka Yuda) alipokuwa mfalme, ilitambulika kuwa Yuda alikuwa mstari wa kifalme hadi Masihi atakapokuja. Yesu alikuwa wa ukoo wa Yuda "kisheria" kama Yusufu alivyokuwa baba yake ya kisheria, na kibailojia, kama Mariamu alikuwa anatokea ukoo wa Yuda.

 

S: Kwenye Mwanzo 49:14-15, kwa nini Yakobo alitabiri utumwa kwa Isakari, lakini Kumb 33:18-19 ilitabiri baraka?

J: Sehemu zote zilitimizwa. Isakari alikuwa na baraka kubwa katika nchi yao yenye rutuba. Hata hivyo, wakati wa Waashuri, walikuwa watumwa na kabila lao lilibakia kuwa hivyo. Tunapozichukulia baraka za Mungu kiurahisi, zinaweza kutufanya kuwa wavivu na wepesi wa kuingia kwenye dhambi. Tazama Waamuzi 8:27, 33 kwa mfano mwingine wa kusikitisha wa Gideon.

 

S: Kwenye Mwanzo 50:3, kwa nini ilichukua siku 40 kuupaka dawa mwili wa Yakobo, na si zaidi au pungufu?

J: Hakuna haja ya kujaribu kutafuta maana ya kiistiari hapa, wakati Biblia inatoa sababu. Mwanzo 50:3 inasema kuwa huo ulikuwa muda unaotakiwa kuipaka dawa maiti. KMT Magazine: A Modern Journal of Ancient Egypt juzuu ya 3 na.3 Fall 1993 uk.7, inasema kuwa majaribio ya kutia mumiani panya yanaonyesha kuwa siku arobaini ni muda unaohitajika kukamilisha kukauka mwili kwa kutumia chumvi za natron. Pia inasema kuwa siku arobaini bado ni kipindi cha maombolezo cha Misri ya leo.

 

S: Kwenye Mwanzo 50:13, je Yakobo alizikwa kwenye pango ambalo Abraham alilinunua karibu na Mamre, au baadhi ya mababa wa taifa la Israeli walizikwa karibu na Shekemu kama Matendo 7:15-16 inavyodokeza?

J: Kwanza mambo matatu yanayohusiana na jibu, kisha majibu mawili yanayowezekana.

Kwanza, sehemu hizi mbili zilikuwa tofauti, kwani umbali kati ya Mamre na Shekemu ulikuwa karibu maili 45 (kilomita 72).

Kabla ya Kutoka, Mwanzo 50:13 inasema kuwa Yakobo alizikwa karibu na Mamre. Mwanzo 50:24-26, inasema mwili wa Yusufu ulipakwa dawa na kuhifadhiwa kwenye sanduku, huko Misri, kwa matarajio kuwa siku za usoni utakwenda kuzikwa kwenye nchi ya ahadi.

Baada ya Kutoka, zaidi ya miaka 477 baadaye, watoto wa Yakobo walizikwa karibu na Shekemu kama Matendo 7:15-16 inavyosema. Yoshua 24:32 pia inaongezea kuwa mifupa ya Yusufu ilizikwa kwenye eneo lililo karibu na Shekemu.

Yafuatayo ni majibu mawili tofauti.

"wakachukuliwa . . . wakazikwa": Matendo 7:15 inasema "akafa yeye [Yakobo] na baba zetu." "Wakachukuliwa . . . wakazikwa" kwenye Matendo 7:16 inaongelea watoto kumi na mbili wa Yakobo (baba zetu) waliozikwa baada ya Waisraeli kutoka Misri, na si Yakobo, aliyezikwa miaka 477 iliyotangulia.

Makosa ya Stefano: Kama Stephen angekuwa "ameyaunganisha" kimakosa matukio haya mawili kuwa moja wakati aliposema, basi Matendo 7:15-16 bado haina makosa. Matendo 7:15-16 inarekodi bila kukosea makosa yasiyo na maana aaliyoyafanya Stefano. Hakuna kitu kinachoonyesha kuwa Stefano hakutakiwa kukosea katika maneno yote aliyosema. Hata hivyo, kulingana na kumbukumbu za utendaji wa Stefano wa mambo mengine kwenye Matendo 7, mtu anaweza kupendelea jibu la kwanza.

Hata hivyo, hata kama jibu la pili ni sahihi, kuna somo kwa ajili yetu. Wakati waumini leo hii wapo katikati ya mapenzi ya Mungu, na wanasema kwa watu wengine kama Mungu anataka tufanye, Mungu hajaahidi kuwa maneno na mafundisho yetu yote hayatakuwa na makosa. Lakini jambo hilo ni sawa. Mungu hufanya kazi kupitia kwentu licha ya makosa yetu, na hata kupitia makosa yetu ili kuudhihirisha ukweli wake.

Bila kujali kama Stefano hakutumia pronomino kwa usahihi wa kisasa au Stefano alikosea kwenye sehemu ndogo ya historia, ujumbe wa Mungu si kama Yakobo alihusishwa kwenye maelezo "wakazikwa" Shekemu au la. Ujumbe wa Mungu ni kwamba Mungu aliwaongoza Waisraeli kwenye uhusiano wa agano na yeye, na Mungu aliwatumia Waisraeli kwa maelfu ya miaka kuweka muktadha wa tukio kubwa zaidi la wakati wote, kuja kwa Mwana wake Mungu, Yesu Kristo.

Angalia pia maelezo ya Mwanzo 33:18-19 kwa habari zaidi.

 

S: Kwenye Mwanzo 50:16, je kaka za Yusufu walidanganya waliposema kuwa Yakobo alimwamuru Yusufu kutokuwadhuru?

J: Biblia haisemi endapo Yakobo aliwahi kuagiza waziwazi jambo hili hivyo kaka hawa wanaweza kuwa wanasema kweli. Kwa upande mwingine, bila ya shaka Yakobo alidokeza kuwa alitaka Yusufu kutolipiza kisasi kwa ndugu zake. Leo, tunasikia mambo mengi kutoka kwa watu bila kujua kwa uhakika kama mtu huyo anasema ukweli kabisa au la. Bado tunahitaji kuitikia kwa busara, na njia ambayo Mungu anataka tuitikie, hata kama hatuwezi kuthibitisha au kukanusha ukweli wa jambo linalosemwa.

 

S: Kwenye Mwanzo 50:19-20, tunawezaje kufanya uchaguzi wetu wenyewe, kwa kuwa Mungu "anakusudia" kuwa tufanye maamuzi tunayoyafanya?

J: Mambo rahisi matatu yanayoelezea kulingana huku.

Mungu halazimishi watu kufanya dhambi au kuwafanya wachague uovu huu. Mungu hamjaribu mtu yeyote, kwa mujibu wa Yakobo 1:13.

Mungu aliishajua uchaguzi wao na aliwaruhusu kufanya maamuzi hayo. Charles Hodge refers to this concept as "permissive decrees".

Mungu alitumia maamuzi yao maovu kama sehemu ya mpango wake. Hakika, kila kitu kimo kwenye mpango wa Mungu, kwa mujibu wa Waefeso 1:11 na Mithali 16:4. Louis Berkhof alibuni neno "concurrence" (kulingana) kwa dhana hii.

 

S: Kwenye Mwanzo, kwa nini neno "Elohim" linatumika mara 33 kwenye mistari 34 ya kwanza, likifuatiwa na "Yahweh-Elohim" mara 20 kwenye mistari 45, likifuatiwa na "Yahweh" mara 10 kwenye mistari 25 (Evidence That Demands a Verdict volume 2 uk.121). Je jambo hili linaonyesha watunzi zaidi ya mmoja wa kitabu cha Mwanzo?

J: Jambo hili si bahati mbaya, bali lilitumiwa kwa makusudi kabisa kwanza kumueleza Mungu kuwa juu zaidi ya mipaka ya wanadamu wote, likifuatiwa na mambo yake binafsi zaidi. Kuna hali inayofanana sana na hii kwenye Kurani. Neno "Allah" linatumiwa zaidi kwenye Kurani, Sura za baadaye za Madina, wakati "Bwana", si "Allah" inatumiwa zaidi kwenye sura za awali, Sura za Maka. Ifuatayo ni idadi niliyoipata kwenye Sura za Madina. 4 (~211), 9 (~152), 24 (75), 33, 48, 49, 57 (33), 58 (37), 59 (29), 60-66. Ifuatayo ni idadi niliyoipata ya neno ‘Bwana' kwenye Sura za Maka, ikifuatiwa na namba ya karibu ya matumisi ya neno ‘Allah'. 15 (3), 32 (1), 50-53, 54-55 (0), 56 (2), 67 (4), 68 (0), 75 (x), 78 (x), 85-96 (9), 100-109 (1), 110-112 (6), 113-114 (x).

Jambo hili halionyeshi kuwa Kurani ilikuwa na watunzi wengi, kama vila ambavyo ushahidi usiojitosheleza wa kitabu cha Mwanzo kuwa kilikuwa na watunzi wengi. Badala yake, jambo hili linaonyesha kuwa matumizi yasiyokuwa pacha ya majina hayakuwa mageni kwenye maandiko ya Mashariki ya Kati.

 

S: Kwenye Mwanzo, lini kitabu hiki kiliandikwa?

J: Maandiko ya kale ya Kiyahudi na Kikristo yanasema kwa kauli moja kuwa kiliandikwa na Musa. Endapo Musa ndiye aliyeandika hasa, au mwandishi mwingine chini ya usimamizi wake, bado ilikuwa ni wakati wa Musa.

Julius Wellhausen, mtu mwenye kutilia shaka msimamo wa kimapokeo, mwaka 1885 alisema kiliandikwa ama wakati au baada ya uhamisho wa Babeli (mwaka 598-539 KK). Hata hivyo, hakuna mtu, hata wenye kutilia shaka msimamo wa kimapokea, anayeamini jambo hili kwa sasa.

 

S: Kwenye Mwanzo, tunajuaje kuwa mambo yaliyomo ndiyo yale yaliyoandikwa awali?

J: Kama Wakristo tunaamini kuwa Agano la Kale ambalo Kristo alilithibitisha ndiyo Agano la Kale tulilonalo. Kwa ajili hiyo, kwa Waislamu Kurani yao inasema kuwa Yesu alipewa Torati kwenye Sura 5:46. Tunayo maandiko ya kale kutoka wakati wa Kristo, ambayo swali linalofuata linayaongelea. Hata hivyo, kuna ushahidi mwingine pia. Philo wa Alexandria alikuwa mwanazuoni wa Kiyahudi aliyeishi mwaka 15/20 KK hadi 50 BK. Aliandika maoni ya kitabu cha Mwanzo, na kajibu maswali kuhusu Agano la Kale. Aliandika kwa Kigiriki, lakini inafurahisha kuwa nukuu zake za Kigiriki za Agano la Kale zinakubaliana kwa karibu zaidi na maandishi ya Kimasoretiki (Kiebrania) ya Agano la Kale (yaani Massoretic text) badala ya maandisi ya tafsiri ya Kigiriki (yaani Septuagint). Aliandika kwa kina kikubwa maana za aya mbalimbali. Zifuatazo ni aya alizoziongelea kwenye kitabu cha Mwanzo.

1:1-2, 4, 26, 27, 31

2:1-10, 13-25

3:1-24

4:1-12, 14,25-26

5:1,3, 23-24, 29,32

6:1-12, 14-17

7:1-2, 4-5, 10-11, 16-17, 19, 21-24

8:1-18, 20-22

9:1,3-8, 10-11, 13, 18, 20-28

10:1, 6, 8

11:1-2, 4, 6-8, 10, 29

12:1-4, 6-7

13:1, 9

14:1, 3, 7, 17, 18, 20-24

15:1-3, 5, 20

16:1-9, 11-16

17:16, 8, 10-22, 24, 26, 27, 32

18:1, 3, 6, 7, 9-11, 15-17, 22, 23, 27, 32, 33

19:4, 11, 20, 20, 32, 33, 35

20:7, 12

21:1-2, 5-7, 11-12, 14, 19-20, 33

22:1-2, 4, 6, 7, 9, 16, 22, 62-63, 67

25:5, 8, 11, 17, 21, 23-25, 27, 29, 33

26:2, 3, 5, 9, 12, 32-33

27:1, 20, 28, 30, 33, 36, 40-43, 45

28:1-2, 7, 11-17, 21-22

29:4, 13, 26, 31, 35

30:1, 2, 13, 16, 18, 24, 30, 36, 37, 42

31:3-5, 10-14, 20, 27-28, 33, 35, 43

32:10, 25, 28-29, 31

33:5, 11

34:1, 3

35:2, 4, 16, 18, 25

36:12

37:2-3, 7-9, 12-13, 15, 33, 36

38:7, 9, 11, 20, 25

39:1, 3, 7, 21

40:8-10, 15-17, 20

41:17, 28, 45 ,49

42:1, 11, 16, 18, 36

43:9

45:5, 11, 16,18, 22, 26, 28

46:1, 4, 2733-34

47:3, 9, 24

48:1, 5, 13, 15-16, 22

49:2, 15-18, 22, 33

50:7-8, 19, 24

Hata hivyo, kuna tofauti kubwa nne kwenye maelezo yake ya aya hizi, zote zikiwa kwenye kitabu cha Mwanzo.

Aya

Kiebrania cha Masoretiki

Kigiriki cha Philo

Mwa. 4:13

Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukulik

Kosa langu ni kubwa mno hata halisameheki (mara 3)

Mwa. 5:22

Henoko aliishi miaka 65 kabla ya kumzaa Methusale, alienda pamoja na Mungu miaka 300 iliyofuata

Henoko aliishi miaka 165 kabla ya toba, na miaka 200 baada ya hapo

Mwa. 6:6

Bwana alighairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani

Mungu alifikiria kwa wasiwasi, kwa sababu amemfanya mwanadamu duniani; na alilitatua jambo hili mawazoni mwake mwenyewe

Mwa. 10:9

Alikuwa hodari kuwinda wanyama mbele za Bwana

Alianza kuwa jitu kubwa sana duniani

 

 

Kama unaweza kuona kwenye orodha iliyotangulia, (Philo) alitoa maoni mengi sana kwenye sura za awali za Mwanzo na machache kwenye sura za baadaye. Kwa Muislam yeyote atakayeweza kuwa anasoma, kwenye Mwanzo 22 Philo anasema alikuwa Isaka, si Ishmaili alitolewa kafara, kama vile nakala za Mwanzo miongoni mwa Hati toka Bahari ya Chumvi (Dead Sea Scrolls) na Agano la Kale tulizonazo leo.

 

S: Kwenye Mwanzo, ni maandishi gani ya kale zaidi ambay bado yapo leo?

J: D Hati toka Bahari ya Chumvi: (kabla ya Kristo) nakala 20 au vipande (The Dead Sea Scrolls Translated : The Qumran Texts in English 2nd ed.), zimekadiriwa nakala 15 tofauti (The Dead Sea Scrolls Today uk.30) au nakala 18; The Dead Sea Scrolls in English 4th ed.. The Wycliffe Bible Dictionary uk.436-438 inasema nakala 15. Maandishi haya yametajwa:

1Q1 - vipande vya Mwanzo

2Q1 Mwanzo

4Q1 Mwanzo + Kutoka

4Q2 Mwanzo, sawa na Maandishi ya Kimasoretiki

4Q3 Mwanzo 40-41

4Q4 Mwanzo 1

4Q5 Mwnzo, sawa na Maandishi ya Kimasoretiki na Maandishi ya Kisamaria

4Q6 - Sehemu ya Mwanzo 48

4Q7 vipande vya Mwanzo 1 na 2

4Q8a Mwanzo 2:17-18

4Q8b Maelezo ya Mwanzo 12:4-5

4Q8c Jina la maandishi ya Mwanzo

(4Q8a, b, na c inatoka kwenye maandishi tofauti)

4Q9 Mwanzo, sawa na Maandishi ya Kisamaria

4Q10 Mwnzo 1-3

4Q11 Mwnzo 50:26 hadi Kutoka 36

4Q12 Mwnzo 26 kwenye herufi za Kiebrania cha zamani

6Q1 kipande cha Mwnzo 5

8Q1 Vipande viwili vya Mwnzo 17:12-19 na 18:20-25.

Hati toka Bahari ya Chumvi zina aya hizi zifuatazo kutoka kwenye kitabu cha Mwanzo.

1:1-28; 2:1-3, 6-7, 14-19; 3:1-2, 11-14; 4:2-11; 5:13/14; 6:13-21; 8:21; 10:6; 12:4-5; 17:12-19; 18:20-25; 19:27-28; 22:13-15; 23:17-19; 24:22-24; 26:21-28; 27:38-39, 42-43; 32:4-5 30, 33; 33:1, 18-20; 34:1-3, 5-10, 17-21, 30-31; 35:1, 4-10, 25-29; 36:1-17, 19-27;35-37, 43; 37:1-2, 5-6, 22-30; 39:11-23; 40:1, 12-13, 18-23; 41:1-11, 15-18, 23-27, 29-44; 42:15-22, 38; 43:1-2, 5-14; 45:14-22, 26-28; 46:7-11?; 47:13-14; 48:1-11, 15-17, 18-22; 49:1-8; 50:3, 26?

Maoni ya Hati toka Bahari ya Chumvi kuhusu kitabu cha Mwanzo kwenye pango la 4.

Septuagint ni tafsiri ya Kigitiki ya Agano la Kale na Apocrypha. Greek Manuscripts of the Bible uk.62-63 picha ya kipande, Mwanzo 14:12-15, kutoka karibu nusu ya pili ya karne ya pili BK. Unaweza kuiona picha ya kipande cha Mwanzo 42:7-19 ya Chester Beatty Papyrus V, kwenye Greek Manuscripts of the Bible uk.72-73.

The Complete Text of the Earliest New Testament Manuscripts uk.369 inasema kuwa nakala ya Kigiriki ya Mwanzo, iitwayo inv. 319 iliandikwa kabla ya mwaka 100 BK. Haifahamiki endapo maandishi haya ni yaleyale yaliyotajwa hapo kabla au la.

Kwenye uk.7.2, inasema kuwa Mwanzo 1:1-5 kwenye Septuagint iliandikwa kwenye uk.12 (Papyrus Amherst 3b). Hii iliandikwa mwaka 264-282 BK.

Maandishi ya Vienna yaliandikwa karne ya tano au sita BK na kurasa 24 za Mwanzo zimepatikana. Unaweza kuangalia ukurasa mmoja, Mwanzo 39:9-18, kwenye Greek Manuscripts of the Bible uk.92-93.

Maandishi mengine ya Kigiriki ni pamoja na

Papyrus Oxyrynchus 656 ni maandiko ya karne ya pili BK yaliyo na kitabu cha Mwanzo kwenye Kigiriki. Yameelezwa kwenye Complete Text of the Earliest Manuscripts of the Greek Bible uk.73.

Papyrus Oxyrynchus 1007 ni kipande kilichoandikwa karne ya tatu BK. Mwandishi alikuwa na tabis isiyokuwa ya kawaida ya kuandika ‘yod' ya kwanza mara mbili kwenye Tetragrammaton kwa mujibu wa Manuscripts of the Greek Bible uk.34. Haifahamiki endapo hii ni nakala ya Septuagint au la.

Chester Beatty Papyrus 5 ina Mwanzo 42:7-19. Iliandikwa mwaka 350-400 BK.

Vaticanus (mwaka 325-350 BK) ina Mwanzo 46:29-50:26. Vaticanus ina Agano la Kale lote.

Alexandrinus (karibu mwaka 450 BK) ina Mwanzo yote isipokuwa 14:14-17; 15:1-5, 16-19; 16:6-9, ambazo zimeondoka.

Sinaiticus (mwaka 340-350 BK) Mwanzo 23:19-24:26 (ikiwa na mapengo kadhaa)

Wasamaria waliandika nakala yao wenyewe ya Torato kwenye karne ya pili KK, ingawa nakala za kale zaidi zilizopo ziliandikea kwenye Enzi za Kati. Picha ya hati ya kukunja ya Kisamaria ipo kwenye Bible Almanac uk.390.

Maandishi ya Kale ya Kikristo: Kwa mujibu wa Encyclopedia of Religious Knowledge uk.746, Chester Beatty Papyrii (karne ya 2-4 BK) ina kitabu cha Mwanzo.

Peshitta ya Kisiria afsiri ya Mwanzo iliyoandikwa karne ya tano BK (New Bible Dictionary 1978, uk.1262).

Tafsiri ya Kisiria ya Septuagint ilfanywa na Askofu Paul of Tella (mwaka 616-617 BK), ambayo bado tunayo leo, kwa mujibu wa Manuscripts of the Greek Bible uk.35 (rejeo chini ya ukurasa).

Philo Myahudi (mwaka 15/20 KK hadi 50 BK) ananukuu sana Mwanzo kwenye Allegorial Interpretation, I.

Waandishi wa kanisa la kale walikitambua kitabu cha Mwanzo kuwa sehemu ya Biblia.

1 Clement (mwaka 96-98 BK) ananukuu au kuelezea yaliyomo kwenye Mwanzo 1:26-28; 2:23; 4:3-8 (Septuagint); 5:24; 9:6; 12:1-3; 13:14-16; 15:5,6; 18:27; 19:24; 21:22; 22:17; 27:41; 37:6.

Justin Martyr (aliyeandika mwaka 138-165 BK) ananukuu au kuelezea Mwanzo 1:26,28; 2:3; 3:15; 3:22; 6:16; 8:10,12; 9:24-27; 11:5,4; 15:6; 18:1, 2, 10, 13f, 14, 16, 17, 20-23, 23; 19:1, 10, 16-25, 27, 28; 21:9-12; 226:4; 18:10-19; 31:10-13; 32:22-30; 35:6-10; 49:5, 8-12, 18,24.

Irenaeus (aliyeandika mwaka 182-188 BK) ananukuu kutoka kwenye vifungu vingi vya Mwanzo.

Cyprian (mwaka 248-258 BK). Ananukuu kitabu cha Mwanzo, akitaja kuwa maneno hayo yanatoka Mwanzo kwenye Treatise 12 The Third Book 20, 32 baadhi ya sehemu nyingine.

Waandishi wengine wa kanisa kabla ya kipindi cha Nikea (pre-Nicene church writers) walionukuu kitabu cha Mwanzo ni paoja na Barua ya Barnaba, Meleto wa Sardis, Athenagoras, Tertullian, Clement wa Alexandria, Hippolytus, Origen, Novatian, Archelaus, Alexander wa Alexandria na Methodius.

 

S: Kwenye Mwanzo, je nukuu za Philo zilikuwa sahihi kiasi gani?

J: Zifuatazo ni nukuu ambazo Philo anazitumia kwa mfuatano kwenye On the Creation:

"Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na nchi" ... "giza lilikuwa juu ya uso wa lindi kuu." ... "aliiita ‘siku'". ... "Natumfanye mtu kwa sura yetu, kwa mfano wetu." ... "waliumbwa mwanaume na mwanamke" ... "hiki ni kitabu cha uumbaji wa mbingu na nchi, ulipotokea katika siku ambayo Mungu aliziumba mbingu na nchi, na mimea yote ya kijani kabla haijatokea juu ya nchi, na majani yote ya shamba kabla haijachipua." ... "Na chemchemi hazijaenda juu toka kwenye nchi na kumwagiliwa uso wote wa nchi." ... "Mungu alimuumba mtu, akichukua udongo wa ardhi, na kumpulizia usoni mwake pumzi ya uhai." ... "Mungu aliwaleta wanyama wote kwa mtu, akitaka kuona ni majina gani atatoa kwa kila mmoja." ...

Hizi ni nukuu anazozitumia bili kufuata mfuatano kwenye Allegorical Interpretation, I na sehemu ndogo ya II.

"Na mbingu na nchi, na ulimwengu wao wote ulikamilika." ... "Na siku ya sita Mungu alimaliza kazi yake aliyoifanya." ... "Mungu alikamilisha kazi zake siku ya sita." ... "Alivifanya kupumzika vitu vyote alivyokuwa ameanza." ... "Kwa hiyo, siku ya saba, Mungu alipumzika kutoka kwenye kazi zake zote alizozifanya." ... "Na Mungu aliibariki siku ya saba, na kuitakasa." ... Hiki ni kitabu cha vizaza vya mbingu na nchi, wakati vilipoumbwa." ... "Siku Mungu alipoumba mbingu na nchi, na kila mmea wa kijani wa kondeni, kabla haujatokea juu ya nchi, na majani yote ya shambani kabla hayajachipua. Kwa maana Mungu haikunyesha mvua juu ya nchi, na binadamu hakuwepo kuilima ardhi." ... "Lakini chemchemi ilipanda juu ya ardhi na kuumwagia maji uso wote wa nchi." ... "Mungu akamuumba mtu, akichukua donge la udongo kutoka ardhini, na kumpulizia usoni mwake pumzi ya uhai: na mtu akawa nafsi hai." ... Na Mungu aliipanda Paradiso huko Edeni, upande wa mashariki: na huko alimwekwa mtu aliyemfanya." ... "Na mtu aliyemfanya," ... "Mungu alimweka paradiso." ... "Na Mungu alifanya umee kwenye nchi kila mti unaotamanika kwa macho na mzuri kwa chakula, na mti wa uzima aliuotesha katikati ya Paradiso, na pia mti wa ujuzi wa mema na mabaya." ... "Na mto hutoka Edeni kumwagilia Paradiso. Kutoka hapo unagawanyika sehemu nne: jina la mmoja ni Pheison. Huu ndio unaoizunguka nchi yote ya Evilat. Kuna nchi ambayo kuna dhahabu, na dhahabu ya nchi ile ni njema. Pia kuna kito chekundu na yakuti (ya samawi). Na jina la mto wa pili ni Gihon; huu ndi ule unaoizunguka nchi yote ya Ethiopia. Na mto wa tatu ni Tigris. Huu ni mto unaopita mbele ya Waashuri. Na mto wa nne ni Frati."

... "Bwana Mungu akamtwaa mtu aliyemuumba na kumweka Paradiso, ili ailime na na kuilinda." "Bwana Mungu alimwamuru Adamu, akisema, mti wowote uliomo Paradiso unaweza kuula; lakini mti wa ujuzi wa mema na mabaya hamtakula; lakini siku mtakayokula mtakufa hakika." (II) "Na Bwana Mungu akasema, "Si vema mtu awe peke yake: basi natumfanyie msaidizi wa kufanana naye." ... "Mungu akasema, Nchi na izae viumbe hai kwa aina zao, wanyama wenye miguu minne, na wadudu watambaao, na wanyama wa porini." (Anaendelea hadi kufika kwa Ibrahimu).

Kwa kulinganisha sehemu hizi mbili inaonyesha kuwa Philo hakuwa ametumia maneno yale yale alipokuwa akinukuu kifungu.

 

S: Kwenye Mwanzo, tofauti za kutafsiri kati ya Kiebrania na Septuagint ya Kigiriki ni zipi?

J: kwa kuzingatia sura ya 1, zifuatazo ni baadhi ya tofauti kwenye aya 1,533 za kitabu cha Mwanzo.

Mwa 1:1 "mbingu" (uwingi) na "mbingu" (umoja)

Mwa 1:2 "ukiwa, tena utupu" na "isiyovutia na isiyokamilika" (Septuagint) na "tupu na isiyo na kitu" (Aquila) na "iliyolimwa na kuacha kupandwa mbegu na isiyo dhahiri" (Symmachus) na "iliyoachwa ukiwa bila binadamu au wanyama na isiyo na mimea au miti yoyote iliyopandwa" (ufafanuzi wa Neophyti I) na "tupu na isiyo na kitu" (Vulgate)

Mwa 1:2 "uso wa vilindi" na "vilindi"

Mwa 1:2 "uso wa maji" na "maji"

Mwa 1:5 "siku" (Massoretic, Septuagint) na "mchana" (Hati toka Bahari ya Chumvi 4QGeng)

Mwa 1:6 "maji" (uwingi) na "maji" (umoja), mara tatu

Mwa 1:7 "ikawa hivyo" na (msemo huu haupo), maneno 2 ya Kiebrania, maneno 3 ya Kigiriki

Mwa 1:8 "mbingu" (uwingi) na "mbingu" (umoja)

Mwa 1:9 "ikawa hivyo" na "Ikawa hivyo. Na maji yaliyokuwa chini ya mbingu yalikusanywa kwenye sehemu zake, na nchi kavu ikatokea." (maneno 17 ya Kigiriki)

Mwa 1:11-12 "machipukizi mapya" na "mimea" (mara mbili)

Mwa 1:14 "mbingu, kutenganisha" na "mbingu, kutoa mwanga duniani, kutenganisha"

Mwa 1:16 "utawale" vs. "usimamie" (mara mbili)

Mwa 1:16 "utawale usiku; akafanya na nyota pia" na "kusimamia [kutawala] usiku, nyota pia"

Mwa 1:20 "kitu kiendacho chenye uhai" na "mijusi" (reptilia kwa Kigiriki)

(Kumbuka kuwa kwenye Mwanzo 1:20, 21 Green's Literal Translation inasema ‘ndege‘ kwa makosa, wakati ambapo ilitakiwa iwe viumbe wenye kuruka kwa sababu neno hilo hilo la Kiebrania linamaanisha popo na wadudu wenye mabawa kwenye Walawi 11:19-22 na Kumbukumbu 14:18-20).

Mwa 1:21 "and all that creeps" vs. "and every living reptile"

Mwa 1:21-25 "kitu" na "vitu" (mara nyingi), hili ni jambo lenye kudodosa sana kisarufi.

Mwa 1:22 "mkaongezeke" na "ongezekeni"

Mwa 1:24 "wanyama wa kufugwa nacho kitambaacho" na "wanyama wenye miguu minne na mijusi"

Mwa 1:26 "kwa mfano wetu, kwa sura yetu" na "kwa namna ya sura na mfano wetu"

Mwa 1:26 "wanyama, na nchi yote pia" (Massoretic, Septuagint) na "wanyama wa nchi" (Kisiria)

Mwa 1:26 "chenye kutambaa kitambaacho" na "kitambaacho mijusi"

Mwa 1:27 "kwa mfano wake; kwa mfano wa Mungu" na "kulingana na sura ya Mungu"

Mwa 1:28 "Mungu akawabarikia, Mungu akaswaambia" na "Na Mungu akawabariki akisema"

Mwa 1:30 "majani yote ya miche" na "wanyama wote wa mwituni"

Mwa 2:1 "jeshi lake lote" na "ulimwengu wao wote"

Mwa 4:8 "Abel" na "Abel, twende zetu nyikani" (Samaritan Pentateuch, Septuagint, Neophyti I Targum, Syriac, linganisha na Vulgate)

Mwa 4:15 "Kwa sababu hiyo" (Maandishi ya Kimasoretiki, Targumi) na "Si hivyo. Kwa hiyo" (Septuagint, Syriac, Vulgate), hakuna mabasiliko ya maana

Orodha la vizazi kwenye Mwanzo 5na 11:10-26 ni tofauti kidogo kwenye Samaritan Pentateuch (The Anchor Bible Dictionary juzuu ya 5)

Mwa 6:5 "Bwana" (Massoretic Text, Targumi) na "Bwana Mungu" (Septuagint) na "Mungu" (Vulgate)

Mwa 7:22 "pumzi ya roho ya uhai" na "pumzi ya uhai" (Septuagint, Vulgate)

Mwa 9:25 Baadhi ya maandiko ya Septuagint na Agano la Kale la Kiarabu yanasema laana haikuwa kwa "Kanaani" lakini kwa "Hamu, baba wa Kanaani"

Mwa 10:4 "Dodanimu" na "Rodanimu" (Baadhi ya maandiko ya Kiebrania, Samaritan Pentateuch, Septuagint)

Mwa 10:23 "Mashi" (Massoretic Text) na "Meshech" (Septuagint na 1 Nyakati 1:27 Massoretic text)

Mwa 11:12 ina Kanaan ikiwa imewekwa kati ya Arphaxad na Shelah kwenye Septuagint na Luka 3:36.

Mwa 14:1, 9 "Arioko mfalme wa Elasari" (maandiko ya Kiebrania) na "mfalme Arioko, mfalme Elasari" ufafanuzu kwenye Theophilus to Autolycus Kitabu cha 2 sura ya 31, uk.107. Elimukale ya Sumeria imegundua "Mfalme Arioku wa Larsa."

Mwa 18:22 "Ibrahimu alikuwa akali akisimama mbele za Bwana" na "Bwana alikuwa akisimama mbele ya Ibrahimu" (mapokeo ya kale ya waandishi wa Kiebrania)

Mwa 19:17 "mmoja alisema" na "walisema" (Septuagint, Syriac, Vulgate)

Mwa 20:13; 31:53; 35:7 "Elohim" na "El" (Samaritan Pentateuch) (The Anchor Bible Dictionary juzuu ya 5). Pia kwenye Kutoka 22:8.

Mwa 21:10 "pamoja na mwanangu, Isaka" na "pamoja na mtoto wake Isaka" (Septuagint, Vulgate)

Mwa 22:2 "mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaya" na "mwanao, mpendwa, umpendaye, Isaka"

Mwa 22:13 "Kondoo mume yuko nyuma yake" (mengi ya Massoretic Texts) na "Kondoo mwanaume" (baadhi ya Massoretic Text, Samaritan Pentateuch, Septuagint, Syriac)

Mwa 23:1 "umri wake Sara" na "miaka" (Septuagint, Vulgate)

Mwa 24:62 "alikuwa amekuja kwa njia ya" na "kutoka" (Syriac Targums)

Mwa 30:36 haipo na "malaika alitokea kwa Yakobo kwenye ndoto akimfunulia sehemu yake kwenye kundi la Labani" (Samaritan Pentateuch)

Mwa 30:11 "Bahati njema" (Massoretic Text, Kethib, Septuagint, Vulgate) na "Kundi" (Qere. Syriac, Targums) (Qere ni maneno fulani ya Kiarami yanayosomwa kwa sauti, hutofautiana na maneno yaliyoandikwa kwenye Massoretic text. Kethib (iliyoandikwa Kiarami) ni maneno yaliyoandikea ya Agano la Kale la Kiebrania)

Mwa 31:49 "Mizpah" na "shahidi nguzo" (Septuagint) na "nguzo ya Mizpah" (Samaritan Pentateuch)

Mwa 33:4 "akambusu" (ipo ila iwekewa alama za nukta kwenye Massoretic Text) na haipo (Septuagint)

Mwa 36:2, 14 "binti za" na "mtoto (wa kiume) wa" [Zibeon/Sebegon] (Pentateuch, Syriac)

Mwa 36:3 "Basemathi" (Massoretic Texts, Septuagint) na "Mahalath" (Samaritan Pentateuch) (The Expositor's Bible Commentary uk.195)

Mwa 36:16 "Kora/Core" (Massoretic Texts na Septuagint) na (haipo) (Samaritan Pentateuch, 1 Nyakati 1:36)

Mwa 36:24 "maji" (Massoretic Texts, Vulgate) na "chemchemi za moto" (Septuagint)

Mwa 36:39 "Hadadi" (nyingi za Massoretic Texts) na "Baradi" (Septuagint) na "Hadad" (baadhi Massoretic Texts, Samaritan Pentateuch, Syriac)

Mwa 37:36 "Wamidiani" na "Wamidiani" (Septuagint, Samaritan Pentateuch, Vulgate, Syriac)

Mwa 41:22 "kisha nikaona" na "nililala kwa mara ya pili na nikaona" (Septuagint, Syriac, Vulgate)

Mwa 41:48 "chakula chote cha miaka ile saba katika nchi ya Misri" na "chakula cha miaka saba, ambayo kulikuwa na neema katika nchi" (Septuagint, Samaritan Pentateuch)

Mwa 41:56 "akazifungua ghala zote" na "ghala zote (Septuagint, Vulgate, Syriac)

Mwa 44:4 "mema?" na "mema? Kwa nini mmeiba kikombe changu cha fedha?" (Septuagint, Vulgate)

Mwa 46:13 "Puva" na "Phua" (Septuagint) na "Puvah" (Samaritan Pentateuch, Syriac, 1 Nyakati 7:1)

Mwa 46:13 "Iob" vs. "Jashub" (baadhi ya Septuagint, Samaritan Pentateuch)

Mwa 46:16 "Sefoni" vs. "Zephon" (Septuagint, Samaritan Pentateuch, Hesabu 26:15)

Mwa 46:20 "kwake" vs. "kwake, hata] Manase na Efraim. Na kulikuwa na watoto waliozaliwa kwa Manase, ambao suria wa Kisyria alimzalia, [hata] Makiri. Na Makiri alimzaa Galaadi. Na watoto wa Efraim, kaka wa Manase; Sutalaamu, na Taamu. Na watoto wa Sutalaam: Edomu." (Septuagint, linganisha na Hati toka Bahari ya Chumvi 4QExoda) (The Expositor's Bible Commentary juzuu ya 2, uk.262)

Mwa 46:23 "Hushimu" na "Hashum"

Mwa 46:27 "katika Misri walikuwa nafsi wawili. Nafsi zote za nyumba ya Yakobo walioingia Misri walikuwa sabini." (Massoretic) na "katika nchi ya Misri, walikuwa nafsi tisa; nafsi zote za nyumba ya Yakobo waliokuja Misri na Yusufu, walikuwa nafsi sabini na tano" (Septuagint)

Mwa 47:21 "Akawahamisha hao watu akawaweka katika miji" na "aliwafanya kuwa watumwa" (Septuagint, Samaritan Pentateuch)

Mwa 49:4 "ulikpanda kitand cha baba yako ukakitia unajisi - alikipanda" na "ulikitia unajisi - ulikipanda" (Septuagint, Syriac, Targums)

Mwa 49:5 "Yusufu" na "wao"

Mwa 49:7 "Ghadhabu yao na ilaaniwe" na "ghadhabu yao ni nzuri" (Samaritan Pentateuch) (The Anchor Bible Dictionary juzuu ya 5)

Mwa 49:20 "kutoka Asheri" na "Asheri" (Septuagint, Vulgate, Syriac)

Mwa 50:16 "walimwamuru Yusufu" na "wakapeleka watu kwa Yusufu" (Septuagint, Syriac)

Mwa 50:23 "magotini mwa Yusufu" na "katika siku za Yusufu" (Samaritan Pentateuch) (The Anchor Bible Dictionary juzuu ya 5)

Matumizi ya Elohim na Yehovah yamesambaa kiasi tofauti kwenye Septuagint dhidi ya Massoretic Text. Julius Wellhausen aliona jambo hili kuwa ni hoja dhaifu zaidi ya dhana ya watunzi wengi wa kitabu cha Mwanzo (Documentary Hypothesis Theory).

Bibliografia ya swali hili: tafsiri ya Kiebrania inatoka kitabu cha Jay P. Green, Literal Translation na tafsiri ya Septuagint inatoka kwenye kitabu cha Sir Lancelot C.L. Brenton, tafsiri ya The Septuagint : Greek and English. The Expositor's Bible Commentary, The Anchor Bible Dictionary juzuu ya 5, na rejeo chini ya ukurasa kwenye NASB, NIV, NKJV, na NRSV Bibles pia zilitumika.