Maswali ya Biblia Zekaria



S: Kwenye Zekaria, muhtasari wa kitabu ukoje?

J: Ufuatao ni muhtasari wa kiwango cha juu.
A. Zek 1:1-1:6
Mrudie Bwana na achana na maovu
B. Zek 1:7-6:8
Maono nane ya siku zijazo
1. Wapanda farasi wane miongoni mwa mihadasi (Zek 1:7-17)
2. Pembe nne na wafua vyuma wanne (Zek 1:18-21)
3. Mtu mwenye kamba ya kupimia (Zek 2:1-13)
4. Mavazi safi kwa kuhani mkuu (Zek 3:1-10)
5. Kinara cha taa na mizeituni miwili (Zek 4:1-14)
6. Gombo la chuo lirukalo (Zek 5:1-4)
7. Mwanamke akaaye kwenye efa (Ze 5:5-11)
8. Magari manne ya vita (Zek 6:1-8)
C. Zek 6:9-15
Yoshua atawazwa kuwa kuhani mkuu
D. Zek 7:1—8:23
Kufunga
1. Haki na huruma, siyo kufunga
2. Ahadi ya Mungu mwenye wivu
E. Zek 9:1—11:17
Ujumbe wa Kwanza: Mfalme anakataliwa
1. Mataifa ya kaskazini na magharibi dhidi ya Israeli (Zek 9:1-13)
2. Ahadi ya mvua za majira ya kuchipua (Zek 9:14-10:12)
3. Wachungaji wapumbavu na wachungaji wazuri (Zek 11:1-17)
F. Zek 12:1—14:21
Ujumbe wa pili: Mfalme atawazwa
1. Israeli atamrudia Mungu, ingawa theluthi mbili itaangamia (Zek 12:1—13:0)
2. Bwana atapigana kwa ajili ya Israeli siku zijazo (Zek 14:1-21)

S: Je Kitabu cha Zekaria kinatajwa mara nyingi kwenye vitabu vingine vya Biblia?

J: Kwa kulinganisha na ukubwa wake, Kitabu cha Zekaria kimetajwa mara nyingi kuliko kitabu kingine chochote. Moja ya sababu ni kuwa Kitabu cha Zekaria ni kidogo sana kuliko vitabu vya manabii wakubwa. Hata hivyo, Believer's Bible Commentary, uk.1157 inasema kuwa Agano Jipya linakinukuru kitabu hiki karibu mara arobaini.
Kuna watu wengine kwenye Biblia ambao nao wanaitwa Zekaria. Hata hivyo, Zekaria ambayo ni mwandishi wa kitabu hiki ametajwa kwenye Neh 12:4, 16 na Ezr 5:1; 6:14.

S: Kwenye Zekaria, kuna mambo gani yanayofanana na Kitabu cha Ufunuo?

J: Ingawa Ufunuo ina vitu vingi ambavyo havimo kwenye Zekaria, nabii nyingi za kwenye Zekaria zimerudiwa kwenye Ufunuo. Ifuatayo ni orodha ya mambo hayo:

S: Kwenye Zekaria, kuna mambo gani yanayofanana na Kitabu cha Hagai?

J: Manabii hawa wawili walihudumu wakati mmoja na Ezra, na hakuna shaka kuwa walifahamiana, kwa hiyo kuna uwezekano wa mambo kadhaa kufanana. Wanazuoni wameainisha mambo kumi na nane yanayofanana kati ya Zekaria na Hagai:
1. Msemo "BWANA wa majeshi" ni maarufu sana umetumiwa mara 90 kwenye Hagai, Zekaria na Malaki. Umetumiwa mara 14 kwenye Hagai: Hag 1:2, 5, 7, 9, 14; 2:4, 6, 7, 8, 9 (2x), 11, 23 (2x)
2. Vitabu vyote viwili vinaelezea muda ambao nabii zake zilitolewa. Jambo hili halikufanywa kwenye vitabu vilivyoandikwa kabla ya muda huu, lakini lilitumiwa sana wakati wa Babeli mpya na Himaya ya Uajemi.
3. Vyote vinamwongelea zaidi Zerubabeli gavana, Joshua kuhani mkuu, na watu
4. Zek 3:10 na Hag 2:3 zinasema kuwa hekalu linaweza kuonekana kuwa halina thamani lakini walisilidharau.
Kuna mambo mengine pia yanayofanana:

S: Kwenye Zek 1:1, Kitabu cha Zekaria kiliandikwa lini?

J: Kwa mujibu wa Zek 1:1, huduma yake ilianza karibu mwaka 520 KK.
Zek 1:1 ilitokea mwezi Okt/Nov 520 KK.
Zek 1:7 ilitokea 15 Feb 519 KK.

S: Kwenye Zek 1:1, je Zekaria alikuwa mwana wa Berekia, mwana wa Ido, au mwana wa Ido tu kwenye Ezr 5:1 na 6:14?

J: Zekaria alikuwa mwana wa Berekia na mjukuu wa Ido. Kwenye lugha za Kisemeti neno ‘mwana' linaweza kumaanisha ‘mzao.'

Dhana au msemo Ufunuo Zekaria
Roho saba Ufu 1:4 Zek 3:9; Isa 11:2
Waovu walimchoma Yesu na wataomboleza Ufu 1:7 Zek 12:10-14
Malaika wanne wa uharibifu Ufu 7:1 Zek 6:1-8; ~Yer 49:36
Ukimya mkuu Ufu 8:1 Zek 2:13; Hab 2:20
Mzeituni miwili na vinara viwili vya taa Ufu 11:4 Zek 4:3,11-14
Maovu ya siku zijazo ya Babeli Ufu 17 Zek 5:5-11; 1 Pet 5:13
Gogi na Megido wauawa, vita nje ya Yerusalemu Ufu 20:7-9 Zek 12:7-11; 14:2-8, 12; Eze 38-39
Mto utoao maji nje ya Yerusalemu Rev 22:1-2 Zek 14:8


S: Kwenye Zek 1:3-5 kwa nini watu wanaathirika na dhambi za wazazi wao, kwani watu hawawajibiki na dhambi za baba zao kama Ezekieli 18 inavyosema?

J: Ezekieli 18 inaonyesha kuwa Mungu hawachukulii watu kuwa na hatia kwa sababu ya dhambi za baba zao, na Mungu hawafanyi wafe kwa sababu dhambi za baba zao. Hata hivyo, Mungu hawaruhusu tu kupata matokeo ya dhambi za watu wengine, mara nyingine Mungu hulaani wazao wa mtu.
Mara nyingi haki na usawa havitokei kwenye maisha haya. Mambo haya mawili haytatokea hadi kwenye siku ya hukumu.

S: Kwenye Zek 1:5b, kwa nini Mungu anawauliza manabii endapo wanaishi milele?

J: Watu walkuwa na muda wa kutubu manabii walipowaambia nafasi ambayo Mungu amewapa. Lakini Mungu asingewangojea milele kupokea nafasi hiyo kabla ya hajaleta hukumu. Wakati huu amewapa mwaliko wa neema wa kutubu, na wanaakiwa kutubu wakati nafasi ipo. Kwa bahati nzuri waliitumia fursa hiyo na kutubu.

S: Kwenye Zek 1:5, 12; 4:5, 7, 10, 13; 5:2; 7:5, 6, kwa nini Mungu anauliza maswali mengi sana?

J: Kwa kuwa watu wanauliza maswali mengi sana kuhusu Biblia, ni sahihi kwa Mungu kutuuliza maswali haya.
Kwa kweli, Mungu hana haja ya kuuliza maswali yeyote yale ili ajifunze kitu kipya. Badala yake, katika kifungu hiki, Mungu alitumia kitu tunachoweza kukiita njia ya Kisokrate ya kumfundisha (inayotumia mjadala) Zekaria na wasomaji wa kitabu hiki. Mungu anaweza kuwa aliamsha udadisi wa Zekaria, au aliyasema maswali ambayo Zekaria alikuwa anajiuliza, au aliyatarajia maswali ambayo wasomaji wangeyadadisi. Wakati mwingine tunajifunza ukweli kwa kujiuliza maswali, na si kukariri mambo.

S: Kwenye Zek 1:6, ni jambo gani linastahili kusifiwa katika haya yaliyosemwa hapa?

J: Wote wawili walikubali kuwajibika kwa ajili ya mambo waliyoyatenda na walitubu kwa ajili ya matendo yao maovu. Lakini kila kizazi kinawajibika kutii mambo yanayokihusu. Hekalu lilibomolewa kwa sababu ya dhambi za mababu wao. Lakini kujengwa upya kwa hekalu kulicheleweshwa kwa sababu ya uchelewaji wao.

S: Kwenye Zek 1:7, mwezi wa Sabati au Shebati ulikuwa lini?

J: Huu ulikuwa ni mwezi wa kumi na moja, na miezi ilianza wakati wa kutokea mwezi mpya. Hii ilikuwa Februari 15, 519 KK.

S: Kwenye Zek 1:8, je maono haya nane yalitokea usiku mmoja au tofauti?

J: Tarehe iliyoonyeshwa ni ya maono ya kwanza, kisha neno "naliona" kati ya maono, inaonyesha kuwa mambo yote haya yalitokea usiku mmoja. Hausemi "ndoto" lakini maono, na Zekaria aliingilia maongezi na kujibu wakati wa maono, hivyo Zekaria yaelekea alikuwa macho akiyaona maono haya. Zekaria atakuwa alikosa usingizi usuku huu.

S: Kwenye Zek 1:8, kwa nini mihadasi? Kwa nini haisemi aina nyingine ya miti, au "miti" tu kwa jumla?

J: Kwanza, natuangalie mihadasi, na kisha tujibu swali. Mhadasi unaweza kukua ama kama mti ama kichaka, na neno la Kiebrania halisemi "miti ya mihadasi", ila "mihadasi" tu. Midarasi ni mizuri sana, lakini haikuonekana kama vichaka vikubwa kulinganisha na mierezi ya Lebanoni, hata miti ya mihadasi yenye urefu wa mita 1.8 hadi 2.4 (futi 6 hadi 8). Mihadasi ilitoa matunda madogo yanayoliwa ya mduara kama forosadi, kunazi au fuu, yaliyokuwa yanatumika kutengeneza kinywaji kinachofanana na mvinyo. Matunda haya hayakuwa muhimu kiuchumi kama miti ya mizeituni. Matunda haya yana harufu nzuri, ingawa si kama mbao zitokanazo na mishubiri. Inawezekana kuwa mihadasi ilikuwa ishara ya amani na ustawi, na baraka za Mungu. Mbao hizi zilitumika kutengenezea samani, magongo ya kutembelea, na mishikio ya zana mbalimbali. Majani yake yalikuwa na harufu na yalitumika kutengenezea viungo vya chakula, manukato, na mashada ya maua ya kwa ajili ya wasichana mabikira. Wababeli walitumia mihadasi kama alama ya mabibi harusi. Mihadasi ya kijani ilikuwa inakuwa kwenye miti, mwaka mzima, na matawi ya mihadasi yalikuwa yanatumika kwenye Sikukuu ya Vibanda, wakati ambapo watu walitakiwa kutengeneza vibanda vyao wenyewe.
Miti ya mihadasi haijasemwa sana kwenye Biblia. Ni moja ya aina saba za miti iliyotajwa kwenye Isa 41:19. Mihadasi, pamoja na misonobari, imetajwa kwenye Isa 55:13 badala ya miiba na mawaridi mwitu. Baada ya kipindi cha Zekaria kilifuatia cha Esta, ambaye jina lake la Kiebrania, Hadasseh, linamaanisha mhadasi. Mahali pekee pengine ambapo mihadasi imetajwa kwenye Biblia ni Neh 8:15. Kulikuwa na mihadasi mingi kwenye korongo chini ya Mlima wa Mizeituni.
Kwa muhtasari, mihadasi ilikuwa miti ya kawaida kabisa ambayo wenyeji wa Yerusalemu waliiona chini ya Mlima wa Mizeituni, ambao una umuhimu kwenye nyakati za mwisho za ulimwengu. Baada ya muda huu, Waebrania wataokolewa kutoka kwenye hatari ya kuangamizwa kabisa, na "mhadasi" tunaoutambua kama Esta.

S: Kwenye Zek 1:8-11, nini maana ya farasi mwekundu na farasi wengine wekundu, na wa rangi ya kijivujivu, na weupe?

J: Farasi hawa walisafiri dunia nzima kuangalia hali ya watu wengine. Walikuta kuwa mataifa mengine yalikuwa yamekaa katika hali ya raha, wakati ambapo Wayahudi hawakuwa hivyo. Mambo haya yanaelekea kufanana na wapanda farasi wane waliokwenda wakati kila mmoja wa mihuri minne ulifunguliwa kwenye Ufu 6:1-8, isipokuwa waliiangalia dunia tu, na hawa walikuwa farasi, si wapanda farasi. Kuna watu wanaowachukulia wapanda farasi hawa kuwa sawa, kistiari, na magari ya farasi manne kwenye Zek 6:1-8.

S: Kwenye Zek 1:9, 19, 21; 2:1; 4:4, 11; 5:6; 6:4, kwa nini Zekaria aliuliza maswali mengi sana, na kwa nini hakuna maswali zaidi baada ya sura ya 6?

J: Malaki na Habakuki nao pia waliuliza maswali mengi. Maswali ni njia nzuri ya kujifunza, na ni vema kwetu kumuuliza Mungu maswali kwa njia ya staha.
Kuhusiana na kutokuwepo maswali zaidi, inawezekana kuwa, kama kwenye Habakuki, sehemu ya mwisho ya kitabu inahusisha kimsingi Mungu kumpa Zekaria "mzigo" wa unabii, wakati sehemu ya kwanza ihusisha zaidi "majadiliano" na kila maono.
Kwa kuwa tunaweza kukisoma kitabu chote cha Zekaria kwa siku moja au mbili, kuna uwezekano wa kudhania kimakosa kuwa kitabu kizima kiliandikwa katika kipindi cha siku chache. Kitabu hiki kilichuka muda wa maisha yote ya utu uzima wa Zekaria, na siyo tu kwamba maono mengine yalipishana kwa miaka kadhaa, lakini pia Zekaria au mwandishi wake anaweza kuwa aliandika sehemu tofauti za Kitabu cha Zekaria katika vipindi vilivyotofautiana kwa miaka mingi sana.

S: Kwenye Zek 1:10, je kwenda huko na huko duniani kunamaanisha nini?

J: Msemo huu unamaanisha kuwa waliitawala dunia. Toleo la Kigiriki la Agano la Kale (Septuajinti) linasema, "aliowatuma kwenda huko na huko duniani." Hapa, neno hili linadokeza kufanya doria au kupeleleza.

S: Kwenye Zek 1:11, je inawezekanaje kuwa na amani kila mahali, wakati Hag 2:6-9, 20-23 inasema kuwa Mungu ataitikisa dunia na kung'oa falme?

J: Zek 1:11 inaongelea kipindi cha maisha ya Zekaria, wakati Hag 2:6-9, 20-23 inalinganisha muda wa sasa na ule ujao baada ya "Yeye aliyesuburiwa kwa hamu na mataifa (yaani Masihi) kuja, na nyumba ya Mungu kujaa utukufu wake. Jambo hilo halitatokea hadi watu waliohamishwa watakapoijenga upya nyumba ya Mungu.

S: Kwenye Zek 1:11-15, kwa nini Mungu hakufurahishwa kuwa mataifa mengine yamekaa katika hali ya raha?

J: Sehemu ya mwisho ya mstari wa 15 inatoa jibu la swali hili. Mataifa haya, These nations, "yalisaidia uovu" (kwenye toleo la Kiebrania) au "waliungana kupambana na uovu" (kwenye toleo la Kigiriki, Septuajinti). Jambo linaloongelewa ni kwamba mataifa yaliyoishambulia Yerusalemu yalikuwa yanafanikiwa sana, na yalikuwa bado hayajahukumiwa kwa ajili ya kuishambulia Yuda. Jambo hili linakwenda kubadilika.
Palikuwa na watawala wengi wa Kiajemi walioitwa Dario, lakini huyu alikuwa ndiye wa kwanza, aliitwa Dario Hystapes (mwaka 522-486 KK). Alianza kutawala miaka miwili kabla ya maono haya, na mara baada ya kuishinda Babeli aliwaruhusu Wayahudi waliokuwa uhamishoni warejee makwao.

S: Kwenye Zek 1:11-15, je kipindi hiki cha utulivu kilianza lini, na kitaisha lini?

J: Kwa kuangalia vita tunazozijua, kulikuwa na amani kiasi wakati huu baada ya Waajemi kuishinda Babeli. Miaka ambayo inawezekana ilikuwa ya amani ni 538-536, 532, 530-529, 527-526, 523, 520, 518-514 KK. Katika kulinganisha, kipindi kilichopita kilichokuwa na amani kiasi kilikuwa karibu mwaka 592, 590 KK. Baada ya muda huu, muda mwingine wa amani kiasi ulikuwa karibu mwaka 117-116 KK. Mwaka wa mwisho kabisa ambao pana uwezekano wa kutokuwa na vita ulikuwa 149 BK.

S: Kwenye Zek 1:11-15, ni vita zipi na maafa gani vilivyokuwa vinaendelea ulimwenguni wakati huu?

J: Ifuatayo ni miaka inayoelekea kuwa bila vita vinavyojulikana, ikifuatiwa na vita. Kisha orodha ya majanga na njaa.
Miaka inayoelekea kutokuwa na vita kutoka mwaka 859 hadi kuja kwa Kristo (miaka 45 kwa jumla)

637-634, 629, 628, 618-617, 602, 592, 590, 573-571, 569, 566-561, 544, 542-541, 538-536, 532, 530-529, 527-526, 523, 520, 518-514, 117-116, 98-97, 95, 28,
Kwenye miaka ya 528, 525, 522, 521, 519, na 513-512 KK, vita pekee zilizojulikana zilikuwa wakati Waajemi walihusika.
Vita za wakati huu

Karibu mwaka 650 KK Uasi wa Wamesenia (walioishi eneo la kale kusini magharibi mwa Ugiriki) dhidi ya Wasparta.
Mwaka 650 KK Wasinthia (walioishi ukanda wa zamani wa kusini mashariki mwa Ulaya na Asia)/Wasimeria (wafugaji wa kale wanaohamahama waliotawala Asia Ndogo kwenye karne 7 KK) waivamia Uyahudi
Mwaka 648 KK Waashuri wauteka nyara mji wa Babeli
Mwaka 646 KK Waashuri wawapeleka Waelami (wakazi wa Elamu, jimbo la kale lililokuwa kusini magharibi mwa Irani) uhamishoni.
Mwaka 642-639 KK Waashuri wauteka mji wa Shushani ulio Elamu, na wamkata kichwa Mfalme Teumman.
Mwaka 638 KK Kwenye Mto Hong, watu wa Chu (jimbo kubwa wakati wa ufalme wa Zhou wa China ya kale, karibu mwaka 1030-223 KK) waishinda Song (Song, ufalme uliotawala China mwaka 960-1279 BK).
Mwaka 633 KK Waashuri wauteka mji wa Thebes wa Misri.
Mwaka 632 KK Kylon anajaribu kuuteka mji wa Athene.
Karibu mwaka 631/627 KK Kyaxares Mmedi auteka mji wa Ninawi.
Mwaka 630 KK Watu wa Di waivamia China kaskazini.
Mwaka 628-571 KK Waludi wapigana na Wasimeria.
Mwaka 626/625 KK Wababeli wanapata uhuru.
Mwaka 625 KK Cyaxares Mmedi awaasi Wasinthia.
Mwaka 623 KK Watu wa Di waipiga China ya kaskazini tena.
Mwaka 620 KK Watu wa Di wapiga kaskazini mwa China tena.
Mwaka 615 KK Mji wa Ashuri wa Arrapkha watekwa.
Mwaka 614 KK Mji wa Ashuri wa uitwao Asshur watekwa.
Mwaka 614 KK Wamedi wajaribu kuiteka Ninawi.
Karibu mwaka 613-7-8/612 KK Wamedi waiteka nyara Ninawi (Wababeli walichelewa kufika).
Mwaka 612 KK Wamedi waitwaa Armenia
Mwaka 612-609 KK Waashuri waliosalia waangamizwa.
Mwaka 611-604 KK Luda yapambana na Miletus huko Asia Ndogo.
Mwaka 609 KK Wamedi waiteka Tuspa, mji mkuu wa Urartia.
Mwaka 609-606 KK Wababeli washambulia kaskazini mwa Isreali.
Mwaka 609/608 KK Wamisri waiangamiza Megido na kuishambulia Gaza huko Yuda.
Mwaka 606-605 KK Watu wa Di washambulia kaskazini mwa China tena.
Mwaka 604 KK Huko Carchemish, Wababeli wawashinda Wamisri.
Mwaka 11-12/605/604 KK Wababeli waiteka nyara Ashkelon huko Uyahudi.
Mwaka 603 KK Wababeli waiteka nyara Ekron huko Uyahudi.
Mwaka 601 KK Wababeli na Wamisri wapigana na hakuna anayeshinda; palikuwa na hasara kubwa.
Mwaka 599-598 KK Wababeli wapigana na Waarabu.
Mwaka 3/16/597 KK Wababeli waiteka Yerusalemu.
Mwaka 596 KK Wababeli wapigana na Waelamu.
Mwaka 595-594 KK Nebukadreza II azimisha uasi.
Mwaka 593 KK Mmisri Psamtik II pamoja na askari wa kukodiwa wa Kigiriki, Kifoenike na Kiyahudi waushinda ufalme wa Kushi huko Sudani.
Mwaka 591 KK Misri yaivamia Nubia.
Mwaka 589-587 KK Wayahudi wawaasi Wababeli.
Mwaka 586/5-573/2 KK Wababeli waizingira Tiro.
Mwaka 585 KK Vita yaisha kati ya Wamedi na Alyattes mfalme wa Luda 5/28/585.
Mwaka 586-573 KK Nebukadreza II aizingira Tiro.
Mwaka 581 KK Wababeli wawapeleka uhamishoni Wayahudi zaidi.
Mwaka 570 KK Wagiriki huko Kirene wamshinda Apries wa Misri.
Mwaka 568-567 KK Apries na Wababeli waivamia Misri.
Mwaka 560 KK Croesus aishinda miji ya Ioni.
Mwaka 560-547/546 KK Waajemi wamdhibiti Mfalme Croesus wa Luda.
Mwaka 559 KK Wamedi na Wababeli waungani dhidi ya Waajemi.
Mwaka 554 KK Mashariki mwa Mto Hyrminus, Camarina ajaribu kuiasi Syracuse.
Mwaka 554 KK Mtawala wa mabavu Phalais wa Acragas, Sicily apinduliwa.
Mwaka 553 KK Camarina, Sicily yajaribu kuiasi Syracuse.
Mwaka 550 KK Koreshi Muajemi amshinda Mmedi Astyages.
Mwaka 549 KK Waajemi waishambulia Ashuru.
Karibu miaka ya 550 KK Babeli yajaribu kuasi Uajemi, watu 3,000 wauawa.
Mwaka 545 KK Koreshi na Waajemi waishinda Bactria.
Wagiriki milioni 2.1 waliwahamasisha Waajemi milioni 5 (kwa mujibu wa Herodotus).
Mwaka 543 KK Sinhalese amshinda Veddahs huko Sri Lanka.
Mwaka 540 KK Polycrates aongoza maasi huko Samos.
Mwaka 540-10/16/539 KK Waajemi waishinda Himaya ya Babeli.
Mwaka 539 KK Wagiriki wawashinda watu wa Carthage.
Mwaka 535 KK Huko Alalia, watu 120 toka Etruria na Carthage dhidi ya meli 60 za Phocis na kuua watu 2,000.
Mwaka 534-533 KK Tarquinis Superbus, mfalme wa mwisho wa Roma, awaua maseneta/wananchi wengi.
Mwaka 528 KK Waajemi wapigana na Wamisri.
Mwaka 525 KK Waajemi wamshinda Koreshi.
Mwaka 525 KK Huko Pelusium, Cambyses II, Waajemi na Waarabu waishinda Misri (Psamtik II).
Wayahudi chini ya Waajemi (Esta 9:12-16) watu 76,000 wauawa.
Mwaka 524 KK Aristodemus wa Cumae awashinda Wartruria huko Italia.
Mwaka 522 KK Bardiya wa uongo na vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Uajemi.
Mwaka 522 KK Waajemi wazimisha maasi ya Wababeli; Waajemi waiteka Samos.
Mwaka 521 KK Waajemi wayazimisha maasi ya Wababeli.
Mwaka 519 KK Waajemi waishinda Gandhara, India.
Mwaka 516 KK Dario wa Uajemi afanya mapambano yakijenshi.
Mwaka 513 KK Msinthia Idanthyrsus amzuia Dario wa Uajemi.
Mwaka 512 KK Dario I apigana na Wasinthia huko Thrace.
Mwaka 512-510 KK Waseltiki waivamia Etruria. Muetruria Lars Porsens anaishambulia Roma.
Mwaka 510 KK Tarquinius Superbus, mfalme wa mwisho wa Roma, apinduliwa.
Mwaka 510 KK Kroton na miji mingine yateketeza kwa moto mji wa Wagiriki wa Sybaris huko Italia.
Mwaka 510 KK Dario aivamia Urusi ya kusini.
Mwaka 510-474/473 KK Gou Chian wa Yueh amshinda Fu Chai wa Wu huko China.
Mwaka 508 KK MueEtruria Lars Porsena aishambulia Roma.
Mwaka 507 KK Athene yaishinda Thebes.
Mwaka 507 KK Spartans ajaribu kuurejesha utawala wa kikabaila huko Athene.
Mwaka 506 KK Wathene wiatwaa Chalcis huko Ugiriki.
Mwaka 504 KK Vijaya, kutoko kaskazini mashariki mwa India, aishinda Sri Lanka.
Mwaka 501 KK Watu wa Carthage waiteka Cadiz, Hispania.
Mwaka 500/499-478 KK Vita vya Wagiriki na Waajemi.
Mwaka 500/499-496/493 KK Ionia yawaasi Waajemi.
Mwaka 500 KK Wasemiti wavamia Eritrea, Afrika.
Mwaka 500 KK Wabantu waenea Afrika.
Mwaka 500 KK Waajemi waizingira Naxos huko Ugiriki.
Mwaka 499 KK Waajemi waiteka Efeso.
Mwaka 498 KK Wagiriki wa Ionia waiasi Uajemi.
Karibu mwaka 498-415 KK Watu wa Selinus na Segesta wapigana huko Sicily (Italia).
Mwaka 494 KK Kujiondoa kwa Waroma wasiokuwa kwenye tabaka la watawala wakabaila (Waplebu, Plebeians) kwa ajili ya sheria za madeni za Claudius.
Mwaka 494 KK Waajemi waiteka nyara Miletus na kumaliza maasi ya Wagiriki wa Ionia.
Mwaka 494 KK Huko Ner Lade, vita ya majini ya Wagiriki yenye kuhusisha meli 100 dhidi ya meli 210.
Mwaka 494 KK Huko Sepeis, Sparta amshinda Argives Ugiriki.
Mwaka 492 KK Mardonius ashindwa katika kuongoza kundi la manowari za Uajemi dhidi ya Athene.
Mwaka 490 KK Waajemi wauangamiza mji wa Eretia huko Ugiriki.
Tarehe 8/12/490 KK Kwenye Huko Marathon Wagiriki 10,000 wawashinda Waajemi 20,000. Wagiriki 192 na Waajemi 6,400 wapoteza maisha.
Majanga:

Kuna habari kidogo kuhusiana na majanga, lakini habari zifuatazo hapa ndizo tulizo nazo.
Mwaka 765 KK Janga la Ashuru kabla ya Yona.
Mwaka 759 KK Janga la Ashuru kabla ya Yona.
Mwaka 701 KK Janga la jeshi la Ashuru kuizingira Yerusalemu, watu 185,000 wafa.
Mwaka 700 KK Kaswende yajulikana miongoni mwa Wagiriki huko Italia.
Mwaka 430 KK Janga huko Athene, Ugiriki.

S: Kwenye Zek 1:18-21, pembe nne na mafundi seremala wanne ni nini?

J: Kwa ujumla, pembe huwakilisha mamlaka za kisiasa na kijeshi kwenye maandiko ya Mashariki ya Kati. Upinde ulitengenezwa kwa kutumia pembe. Zaidi ya haya, kuna maoni matatu:
Himaya nne zilizowatawala Wayahudi:
Wababeli, Wamedi wa Kiajemi, Wagiriki, na Waroma. Mungu anasema himaya hizo zitaangushwa. Kuna nabii zinazofanana na huu kwenye Kitabu cha Danieli.
Himaya nne zilizo wasambaza Wayahudi:
Wamisri, Waashuru, Wababeli, na Wamde wa Kiajemi.
Misukosuko minne:
Pembe nne zinawakilisha vita, majanga, na magonjwa.

S: Kwenye Zek 2:1-7, nini maana ya mtu mwenye kamba ya kupimia?

J: Jambo hili linawakilisha mafanikio, idadi kubwa ya watu, na usalama. Hili linaonyesha kuwa Mungu alikuwa anaiongeza na kuilinda Yerusalemu.

S: Kwenye Zek 2:1-7, je kamba ya kupimia hapa ina maana sawa na kwenye 2 Fal 21:13?

J: Hapana. Hapa inamaanisha kujenga, wakati kwenye 2 Fal 21:13 inamaanisha kubomoa. Picha ambayo ni stiari haiwi na maana hiyo hiyo kila wakati inapotumika.

S: Kwenye Zek 2:2-4, je kijana aliyetajwa hapa ni Zekaria au mpimaji?

J: Inaelekea kuwa ni mpimaji, na Zekaria alikuwa anasikiliza maongezi kwa mbali kwenye maona yake.

S: Kwenye Zek 2:3-5, kuna tofauti gani kati ya kutegemea kitu kama ukuta wa ulinzii, na kumtegemea Mungu?

J: Kuna hali tatu z muumini.
1) Muumini anaweza kutegemea kwenye ulinzi wa kawada, kama vile ukuta, lakini akatumaini kuwa Mungu anaweza kumsaidia kwa kiasi kidogo pia.
2) Muumini anaweza kumtegemea Mungu kwa ulinzi, lakini akajenga ukuta pia. Ukuta unaweza kuwa halisi, kama ule ambao Nehemia alitarajiwa kuujenga, au ulinzi wa aina nyingine, kama vile makufuri kwenye milango yako, kufunga gari lako, bima ya maisha, au bima ya afya.
3) Muumini anaweza kumtegemea Mungu, na asichukue hatua zozote zile za ziada za kujilinda.
Hapa Zekaria anasema kuwa hapo baadaye Mungu aishi miongoni mwao, na hapatakuwa na haja ya ukuta. Hata hivyo, kwa wakati huu, kuna haja ya ukuta ambao Nehemia aliujenga. Leo hii ni jambo jema tu kuwa na makufuli, na bima. Lakini, bima inaweza kushawishiwa na mambo matatu: ulafi wa kutaka kujipatia hela nyingi zaidi wakati wa majanga, uoga uliozidi kiasi wa majanga, na ulinzi. Ni sababu ya tatu tu ya bima ndiyo iliyo sahihi.

S: Kwenye Zek 2:3-5, ni wakati gani tunapaswa kumtumaini Mungu na "kujenga ukuta" kama alivyofanya Nehemia, dhidi ya kumtumaini Mungu na kutokujenga ukuta?

J: Mungu akikuambia moja kwa moja au kupitia Maandiko kuwa "usijenge ukuta", kama kwenye Yos 6:26 (1 Fal 16:34), usijenge ukuta. Mungu akikuambia, ama moja kwa moja ama kupitia Maandiko, kuwa ujenge ukuta, basi ujenge. Wakati Mungu hajasema kitu chochote, ama kujenga ukuta ama kutojenga, basi omba, tafuta ushauri wa waumini wengine, na jiulize maswali kama haya hapa:
1) Je ninajenga ukuta huu ili kuutegemea kwa ajili ya ulinzi wangu badala ya Mungu?
2) Ikiwa msingi wa tumaini langu ni Mungu, je ni busara kujenga ukuta huu?
3) Jambo lipi litampa Mungu utukufu zaidi?

S: Kwenye Zek 2:8; Kum 32:10; Zab 17:8; Mit 7:2, je msemo "mboni ya jicho lake" unamaanisha nini?

J: Msemo wa Kiingereza kisicho rasmi cha kisasa unaelekea kutoka kwenye mstari huu wa Biblia. Leo hii, msemo huu unamaanisha mtu anayependwa sana. Lakini, maana ya awali ni kuwa sehemu ya jicho iliyo na rangi nyeusi ilichukuliwa kuwa ni "tufaha." Mungu alikuwa mwangalifu kuwalinda Wayahudi wakati wa Agano la Kale kama ambavyo mtu alivyo mwangalifu kutoruhusu mtu yeyote yule aguse jicho lake.

S: Kwenye Zek 2:11, ni lini mataifa wataungana na Bwana?

J: Wakristo wanaamini kuwa jambo hili lilitokea baada ya Yesu kuja duniani. Sifahamu ni jinsi gani mfuasu wa dini ya Kiyahudi anaweza kulijibu swali hili; hili ni swali zuri kuwauliza.

S: Kwenye Zek 2:13, ni kwa nini dunia nzima iliamriwa kuwa kimya?

J: Maandiko hayasemi endapo jambo hili lilikuwa heshima, mshangao, hofu, utiifu, amri ya kufanya hivyo, au mchanganyiko wa mambo haya. Hata hivyo, tunaweza kuona mambo matatu kuhusiana na tukio hili la siku zijazo.
1.
Haikuwa kuwa kimya tu, lakini kuwa kimya mbele za Bwana.
2.
Mungu aliinuka kutoka mahali pake patakatifu.
3.
Ukimya mkuu duniani kote, yaelekea ndio huo huo uliotajwa pia kwenye Hab 2:20 na Ufu 8:1.

S: Kwenye Zek 3:1, je jambo hili lilikuwa ni ushahidi kuwa dhana ya Kiajemi kuwa uhalisi una vitu viwili vinavytofautiana imeiathiri dini ya Kiyahudi, kama Asimov's Guide to the Bible, uk.665 inavyodai?

J: Si hivyo kabisa. Uzoroastria wa Kiajemi uliamini kuwa kuna mungu wawili: mungu mzuri wa moto na mungu mwovu, pepo. Pia waliamini kuwa kuna mapepo mengi madogo maovu, na mengi ya mapepo haya maovu yana majina sawa na miungu ya dini ya Kihindu. Imani kuwa kuna muungu mwema muubaji, na mjaribu mdogo imetokea kwenye Mwanzo 3.

S: Kwenye Zek 3:1-3, nini maana ya Yoshua na shetani hapa?

J: Kwenye Kiebrania, Yoshua inamaanisha "Yehova anaokoa", na ni jina hilo hilo alilopewa Yesu. Shetani inamaanisha adui. Kuhani mkuu halisi hapa, anayeitwa Yoshua, alisamehewa dhambi zake, kama ilivyoonyeshwa na kuvuliwa kwa mavazi yake machafu. Yesu Kristo, ingawa hakuwahi kufanya dhambi (Ebr 4:15), alifunikwa na dhambi zetu. "Yeye asiyejua dhambi alimfanya dhambi kwa ajili yetu . . ." (2 Kor 5:21).

S: Kwenye Zek 3:3, nguo chafu sana zinawakilisha nini? Kwenye Ufu 3:5; 6:11; 19:8, mavazi meupe yametajwa mbinguni kama kiwakilishi cha matendo ya haki wa watakatifu.

J: Mavazi hayakilishi dhambi za kuhani mkuu, kwa sababu kuhani mkuu ni kielelezi cha Yesu. Lakini mavazi macahfu sana yanawakilisha dhambi, kama vile Yesu alivyofunikwa na dhambi zetu msalabani. Lakini kama kuhani mkuu, ambae naye anaitwa Yoshua/Yesu, alivyovikwa upya mavazi masafi, mavazi yanayofaa, ndivyo hivyo Yesu atakavikwa tena haki.

S: Kwenye Zek 3:8; 6:12; Isa 4:2; 11:1; Jer 23:5 na 33:15, tawi ni nani?

J: Huyu ni Masihi, aliyetokea kwenye ukoo wa Daudi, ambaye leo hii tunamfahamu kuwa Yesu Kristo.

S: Kwenye Zek 3:9 na 4:10b, nini maana ya jiwe lenye macho saba?

J: Inaelekea hawa ni wale wale roho saba wa Mungu waliotajwa kwenye Isa 11:2 na Ufu 1:4.

S: Kwenye Zek 3:9, je uovu wa nchi utaondolewaje kwa siku moja?

J: Dhambi zetu ziliondolewa siku Yesu alipokufa msalabani kwa ajili yetu. Hili ni swali zuri la kuwauliza Wayahudi: je unadhani Mungu angeondoa uovu wa nchi kwa siku moja?

S: Je Zek 3:9 na 3:10 zinaongea kuhusu Masihi?

J: Kwa njia isiyokuwa ya moja kwa moja, ndiyo. Kuna aina nne za nabii zinazomhusu Masihi: za moja kwa moja, zisizokuwa za moja kwa moja, taipolojia (dhana na njia ya kutafsiri aina au alama zenye kuelezea mambo kabla ya kutukia kwenye vitabu vya Biblia), na taipolojia-unabii. Huu ni unabii usiokuwa wa moja kwa moja kuhusu Masihi. Haumtaji Masihi moja kwa moja, lakini jambo hili haliwezi kutokea hadi wakati Masihi atakapotokea.

S: Kwenye Zek 3:10, je usemi kuwa kila mtu atakaa chini ya mzabibu na mzeituni wake?

J: Hiki kitakuwa ni kipindi cha amani kwa jumla, hasa wakati wa milenia. Inachukua muda kwa mizabibu na mizeituni kukua, hivyo amani hii itadumu muda mrefu.

S: Kwenye Zek 4:2-7, je mizeituni miwili na kinara cha taa ni vitu gani?

J: Kwenye hekalu la Sulemani, makerubi yalitengenezwa kwa kutumia miti ya mizeituni iliyofunikwa na dhahabu. Milango ya ndani ya madhabahu nayo pia ilitengenezwa kwa kutumia miti ya mizeituni iliyorembezwa na makerubi. Mizeituni miwili inaelekea kuwa mashahidi wawili waliotajwa kwenye Ufu 11:4. Tazama maelezo kuhusu Ufu 11:4 ili kujua watu hawa wawili ni kina nani.

S: Kwenye Zek 4:2-7, kuna uhusiano gani kati ya mizeituni miwili na kinara cha taa?

J: Ingawa kinara cha taa kiliweza kuchoma mafuta ya mzeituni, hapa pana uhusiano ulio mkubwa zaidi. Mizeituni miwili inapeleka mafuta kwenye kinara cha taa bila kukoma ili kukifanya kiwake.

S: Kwenye Zek 4:6b, je maneno, "si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu" yanamaanisha nini?

J: Mungu anasema atatimiza mapenzi yake katika mambo haya, kinara cha taa cha dhahabu, mizeituni miwili, na kujengwa upya kwa Yerusalemu, bila kutumia jeshi, siasi, au nguvu nyingine za kibinadamu.

S: Kwenye Zek 4:7, "mlima mkubwa" unabadilikaje kuwa "nchi tambarare?"

J: Kwenye mandhari hii, mlima mkubwa ni kizuizi kinachoonekana kutokushindwa kukamilisha maneno ambayo Mungu anasema. Inaonekana Mungu anapenda siyo tu kuonyesha kuwa anaweza kutimiza mapenzi yake, lakini pia kuwa anaweza kutimiza mapenzi yake kwa kuvishinda hata vizuizi vikubwa zaidi vitakavyo jitokeza.

S: Kwenye Zek 4:7, je unaona vizuizi vya kumtumikia Mungu? Unapomwomba Mungu aviondoe, kwa nini mara nyingi huwa haviondoi mara moja?

J: Vizuizi vinaweza kuwa vya kimwili (afya, fedha, umbali, n.k.), vya ndani (kuvunjika moyo, majaribu, uvivu, n.k.), au watu wengine au watu wengine (familia, upinzani, n.k.). Wakati mwingine Mungu huondoa vizuizi mara moja, na wakati mwingine haondoi. Wakati mwingine Mungu hutumia vizuizi hivi kujenga tabia yetu, hasa uvumilivu. Mara nyingine tunafikiri kuwa Mungu ni mvumilivu na anangoja kwa muda mrefu, lakini si kwamba tu anangoja, bali pia anatumia muda huo kutujenga, na uvumilivu.

S: Kwenye Zek 4:10, timazi inawakilisha nini?

J: Timazi yenyewe haiwakilishi kitu chochote kile. Lakini timazi kwenye mikono ya Zerubabeli ni ishara yenye kuthibitisha unabii kuwa hekalu litajengwa. Kiolezo kiliisha kamilika tarehe 13 Machi, 515 KK.

S: Kwenye Zek 4:10, "mambo madogo" yaliyoongelewa hapa ni yapi?

J: Aya hii inaongelea hekalu, ambali litaonekana dogo na bapa kulinganisha na hekalu lililokuwepo kabla ya uhamisho. Inaweza pia kumaanisha Yerusalemu kwenye mlima wa Sayuni. Kwa ujumla, ingawa tunaweza kuvunjika moyo kwa kuangalia matokeo madogo ya hatua zetu za mwanzo za utiifu, Mungu anapendezwa na hatua ndogo, zinapokua na kuwa vitu vikubwa na hatua kubwa. Kumbuka kuwa Mungu haangalii mambo kama wanadamu wanavyoyaangalia, na tunapaswa kuangalia mambo kupitia macho ya Mungu.

S: Kwenye Zek 4:11, kwa nini Mungu na wanadamu wana mitazamo tofauti namna hii kuhusu mambo yaliyo madogo na makubwa?

J: Kwanza, hebu tuangalie vitu vitatu: mali, muda, na uhakika.
Mali:
Kama watoto waliodekezwa, mara nyingi huwa tunatilia mkazo vitu tusivyokuwa navyo, na kupenda kuwa navyo, badala ya vitu tulivyo navyo. Kama Hudson Taylor alivyosema, "Kazi ya Mungu iliyofanywa kwa njia ya Mungu haitakosa rasilimali za Mungu." Bado hatujamwomba Mungu na watu wengine kutupa rasilimali tunazozitaka, lakini tunapaswa kufahamu kuwa vita ni ya Bwana, si yetu.
Muda:
Tunafikiri kuwa hatuna muda tunaouhitaji. Mungu hajatupa muda wa kutosha kufanya kila kitu tunachoweza kutaka kukifanya, lakini ametupa muda wa kutosha kufanya mambo ambayo anataka tufanye. Tunatakiwa kuwa waangalifu kutokutapanya muda ambao Mungu ametupa, lakini Mungu ametupa muda unaotosheleza mambo anayoyataka, ikiwa ni pamoja na muda wa kupumzika na kujiburudisha.
Uhakika:
Kama mtoto mwoga, tunaogopa vitu tusivyovijua, na tunapenda kupunguza uwezekano wa hasara. Tunasahau kuwa Mungu anafahamu kikamilifu hali ya baadaye, na ana uhakika zaidi kuliko tunavyojua mambo yaliyopita. Mungu hataki tuwe majasiri pasibusara na kufanya mambo yenye uwezekano mkubwa wa kuleta hasara, lakini Mungu anataka tuache hali au mambo ambayo tunaiona tuko salama na kufanya mambo kwa ajili yake.
Hata hivyo, hakuna jambo lolote kati ya haya yaliyotangulia yaliyo chanzo cha msingi cha watu kuona vitu kwa mtazamo tofauti na wa Mungu. Mara nyingine tunakuwa na mtazamo tofauti na Mungu kwa sababu hatuujui mtazamo wa Mungu. Lakini mara nyingi, huwa tunakuwa na ufahamu kiasi kuhusu mtazamo wa Mungu, na tunachagua kusistiza matatizo tunayoyaona ya rasilimali, muda, na uhakika badala ya Mungu na watu wengine.

S: Kwenye Zek 4:11-12, je maisha ya Mkristo, aliyejazwa na watu wengine, yanatofautiana na maisha ya Mkristo aliyewapa watu wengine mafuta?

J: Mkristo anaweza kuishi maisha ya uadilifu, kwenda kanisani na kujifunza, na bado akawa "mchukuaji" badala ya "mtoaji." Wanaweza kujifunza kutoka kwa Wakristo wengine, kitu ambacho ni kizuri, lakini pia wanahitaji kujifunza kutoka kwa Mungu mwenyewe, kupitia maombi na kusoma neno lake. Sote tunapaswa kutumikiana, na ni vema Wakristo wengine wakakusaidia. Lakini je watu wengine wanatumia muda mwingi zaidi kukusaidia wewe, au unatumia muda mwingi zaidi kusaidia watu wengine? Kuna wakati katika maisha ya kiroho ya Mkristo ambapo inakuwa sahihi na inafaa kujifunza kutoka kwa watu wengine, na kusaidiwa zaidi na watu wengine; wakati huu unaitwa kuwa mchanga katika Kristo. Lakini polepole tunapaswa kukua na kuwa wanaume na wanawake wenye nguvu, na kisa washauri wenye hekima, tunapoenda kwa imani.

S: Kwenye Zek 4:11-12, ingawa tunatakiwa kuwapa watu wengine mafuta, mwisho wa siku, waumini wanatakiwa kujifunza kupata "mafuta" kutoka kwa Mungu. Je tunapataje "mafuta" kutoka kwa Mungu?

J: Tunapata ujazo kwa kuwa na muda na Mungu, tukisali na kusoma Biblia. Pia tunaupata uwepo wa Mungu siku nzima kwa kumuishia Yeye.

S: Kwenye Zek 5:1-4, nini maana ya gombo la chuo lirukalo?

J: Hivi ni vipimo vile vile vya hema la kukutania, na kuwa gombo la chuo lirukalo litaleta hukumu kwa haraka. Ukubwa wa gombo utaleta kivuli kwenye eneo kubwa la nchi.

S: Kwenye Zek 5:5-11, mwanamke akaaye katikati ya efa, na Babeli ni nani?

J: Mwanamke anawakilisha uovu, na upepo unampeleka nyumbani kwake, huko Babeli. Kuabudu sanamu katika nchi kutakwenda Babeli bila hiari, na kutabakia huko kwa muda. Kwa upande mmoja, unajimu wa kimagharibi umetokea Babeli. Lakini jambo lilichukua uzito zaidi ni jukumu kuu ambalo mwanamke huyu atalitimiza kwenye nyakati za mwisho, makao ya uovu na mahali pa kukimbilia waumini. Babeli imetajwa kwenye Ufunuo 17-19, Isa 21:9; 48:20, na Yer 50:2-8.

S: Kwenye Zek 6:1-8, magari manne ya vita yanawakilisha nini?

J: Hizi ni roho nne kutoka mbinguni ambazo zinafanya doria duniani, kwa kuwa madhumuni na athari zao vinatofautiana na vile vya wapanda farasi wanne kwenye Ufu 6:1-4.

S: Kwenye Zek 6:5, je hizi ni "roho" nne, au "pepo" nne?

J: Neno la Kiebrania ruah linawema kumaanisha vitu vyote hivyo viwili, lakini vitendo vyao vinaonyesha kuwa maana iliyokusudiwa hapa ni roho. Hata hivyo, Zekaria anaweza kuwa alitumia neno hili kwa makusudi kuonyesha maana zote mbili.

S: Kwenye Zek 6:8, je Roho ya Mungu ilitulizwaje kwenye nchi ya kaskazini?

J: Unabii huu unasema kuwa watu wa Mungu watapumzika kaskazini. Kuna namna nne ambazo unabii huu unaweza kutimizwa.
Uajemi
ulichukuliwa kuwa kaskazini (Isa 41:25; Yer 50:3; 51:48). Kwa uhalisi wa mambo, Uajemi ilikuwa kaskazini mashariki, lakini ili kwenda Uajemi kutoka Israeli, unaelekea kaskazini kwanza.
Khazars:
Baada ya karibu mwaka 700 BK, kabila la Kituruki lililoitwa Khazars liliteka sehemu kubwa ya mashariki mwa Ukraine. Badala ya kubadilika na kuwa Waislamu, na kujitenga na Wabezantini, au kuwa Wakristo na kujitenga na Waislamu, waliamua kubadilika na kuwa Wayahudi. Hata hivyo, kuna watu wanaoweza kufikiri kuwa jambo hili haliwakilishi utimilifu wa Zek 6:8, kama ambavyo baadhi ya Wakristo wanavyoamini kuwa kuanzia wakati wa kusulubiwa kwa Yesu Wayahudi si wateule wa Mungu tena.
Baadaye kwenye historia:
Kwa upande mwingine, baada ya ushindi wa Waislamu, Wakristo waliweza kuhamia Ulaya na kuwa salama zaidi. Hata hivyo, katika kipindi chote cha Enzi ya Kati, na hata sasa, kwenye nchi nyingi za Kiislamu Wakristo walikuwa salama kiasi, almradi wanalipa kodi ya ziada (jizyah) iliyotozwa kwa Wayahudi na Wakristo.
Wakati ujao:
Jambo hili linaweza pia kutimia siku za mwisho. Yoe 2:20 pia inawataja wavamizi kutoka kaskazini.

S: Kwenye Zek 6:9-15, je kuna jambo gani lisilo kuwa la kawaida kwenye muundo wa kifungu hiki?

J: Hii ni mtindo wa uandishi unaoitwa ‘kiazim' wenye mtiririko wa mawazo, na kisha kinyume chake, na kufanya kama umbo la herufi ‘X').
Neno la Bwana likanijia
..Pokea kutoka kwa hao waliohamishwa
....nyumba ya Yosia
......fedha na dhahabu ukafanye taji
........ukamvike kuhani mkuu
..........Chipukizi atalijenga hekalu na Bwana
........milki na ukuhani katika kiti hiki cha enzi
......hizo taji
....ukumbusho katika hekalu la Bwana
..nao walio mbali watakuja na kujenga
Utii sauti ya Bwana
Tazama An Exegetical Commentary: Haggai, Zechariah, Malachi, uk.199, Zekaria 11b-13c kwa maelezo zaidi.

S: Kwenye Zek 6:10, Tobia ni nani?

J: Huyu anaelekea kuwa mtu yule yule aliyerudi na Zerubabeli na Yoshua kwenye Ezr 2:60.

S: Kwenye Zek 6:11, kwa nini mataji mawili yalitengenezwa hapa?

J: Haya yanatenganisha aina mbili za mamlaka duniani: ya kidini na isiyo ya kidini (ya kidunia). Mamlaka hizi hazitaunganishwa hadi kuja kwa Yesu kwa mara ya pili.

S: Kwenye Zek 6:12-13, Chipukizi ndilo lililokuwa lilijenge hekalu la Bwana, lakini Chipukizi ni nani?

J: Chipukizi ni Yesu Kristo. Kupitia kifo chake, tumefanywa kuwa sehemu ya hekalu la Mungu. Ili kupata maelezo zaidi kuhusu jambo hili, soma Ebr 3:1-6; 1 Kor 6:19; 1 Pet 2:5-6 na Zek 6:15.

S: Kwenye Zek 6:13, je mstari huu ulisema "mataji" (wingi) hapo awali, na baadaye ulibadilishwa wakati unabii huu ulipobainika kuwa siyo sahihi, kama Asimov's Guide to the Bible, uk.666 inavyodai?

J: Hapana. Maandishi ya Kiebrania bado yanasema "mataji", wakati matoleo ya Kigiriki la Agano la Kale (Septuajinti) na Kishamu yanasema "taji." Hati za Kale toka Bahari ya Chumvi hazina mstari huu.

S: Kwenye Zek 7:1-2, kwa nini watu walifunga mwezi wa tano na wa saba?

J: Jambo hili halikuagizwa sehemu yeyote ile kwenye Agano la Kale; watu waliamua kufanya hivi kwa hiari yao wenyewe, ili kuombolezea hasara ya kutokuwa na hekalu na nchi. Mungu hakusema kuwa kufunga ni kubaya kwa ujumla, lakini hakufurahishwa kuwa waliangalia zaidi kukosa hekalu badala ya kujiweka sawa na Mungu. Wakati mwingine tunaweza kuangalia zaidi ama kazi ya Mungu, ama vitu tulivyopoteza, kuliko kumsogelea Mungu zaidi. Mungu hakusema kuwa matendo yao yalikuwa mabaya, lakini vipaumbele vyao havikuwa sawa.

S: Kwenye Zek 7:3-6, ni wakati gani Mungu anapokea kulia na kufunga, na lini havipokei?

J: Wakati wote Mungu hupokea kulia na kufunga kwa kweli kwa ajili ya dhambi zetu. Hata kama mtu hafanyi hivyo kwa kweli hasa, anaweza kufunga, lakini awe wazi kwa Mungu kuwa hajawa mkweli kikamilifu.
1. Hata hivyo, Mungu hapkei kulia na kufunga ambavyo havitokani na toba ya kweli.
2. Hapokei kulia na kufunga kama kigezo cha kumlazimisha afanye kitu fulani.
3. Mungu hapokei kulia na kufunga kwa miungu mingine kama kulia na kufunga kwake.

S: Kwenye Zek 7:4-6, watu walikuwa wanafunga vipi kwa ajili yao wenyewe?

J: Walikuwa wanajishughulisha sana na kuomboleza kwa ajili ya hekalu, lakini Mungu alitaka wamsogelee karibu zaidi, na walijenge upya hekalu lao. Huu haukuwa wakati wa kuomboleza, lakini wakati wa kujenga upya, na wao walikuwa wanafanya jambo hilo pole pole sana.

S: Kwenye Zek 7:8-10, ni kwa jinsi gani haki, rehema na huruma ni bora kuliko kufunga?

J: Yesu alisema kuwa amri ya pili kwa ukubwa ni kumpenda jirani yako kama nafsi yako. Kufunga kunaweza kukusaidia kuelekeza kujitoa kwako kwa Mungu. Lakini kufungu kunakuhusu wewe mwenyewe. Haki, rehema, na huruma yanakazia kumtumikia Mungu kwa kuwasaidia watu wengine.

S: Kwenye Zek 8:1; Kut 20:5; 34:14; Kum 4:24; 5:9; 6:15; Yosh 24:19; Nah 1:2, na 1 Kor 10:22, kwa nini Mungu anakuwa na wivu, kwani 1 Kor 13:4 inasema upendo hauhusudu?

J: Mungu anaweza kuwa jinsi yeyote anayotaka kuwa. Mungu ni upendo, lakini Mungu ni vitu vingine pia. Tunapaswa kuwa na tabia hizi za Mungu, kwa kiasi kidogo kuliko yeye: upendo, huruma, upole, ukweli, hekima, utakatifu, n.k. Lakini tabia nyingine za Mungu hatutakiwe kuwa nazo, kama vile kulipiza kisasi, kuabudiwa, na wivu. Na tunapaswa kujenga tabia mbili ambazo Mungu wa mbinguni hana: imani na tumaini.

S: Kwenye Zek 8:3, Yerusalemu uliwahi kuwa mji ambapo hekalu la Sulemani lilikuwepo, lakini kuanzia wakati ule, tokana na kuabudu miungu mingine na kubomolewa kwa hekalu hilo na Wababeli, Yerusalemu haukuonekana mahali patakatifu tena. Lakini Zek 8:3 inasema Mungu aufanya kuwa mtakatifu tena. Je Mungu anawezaje ‘kuyafanya maisha ya mtu kuwa matakatifu tena?"

J: Vitu ni vitakatifu tu, au si vitakatifu, kwa sababu Mungu ameviita hivyo, na si kwa sababu nyingine. Lakini Mungu amesema tutakuwa ukuhani na taifa takatifu kwenye 1 Pet 2:5, 9, na Mungu ametupa wajibu wa kuifanya miili yetu hekalu takatifu kwa Bwana kwenye 2 Kor 6:16-17, 2 Pet 3:11, na Ebr 12:14.

S: Kwenye Zek 8:4-5, Yerusalemu ilikuwa na kumbukumbu nyingi mbaya, kwanza ya kumuasi Mungu, kisha huzuni ya kuzingirwa, kubomolewa, na uhamisho. Lakini Mungu anaahidi patakuwa mahali pa amani tena. Wakati mtu anatanga kwenda mbali Mungu anataka warudi, je Mungu anaweza kuwafanya wawe mahali pa furaha tena?

J: Ni kweli. Mtu anapotubu na kujinyenyekeza kwa Mungu, hata kama wameadhibiwa, Mungu anaweza kuwapa tena. Mungu anaweza "kurejesha miaka ambayo nzige walikula" na bila kujali kuwa mateso yalikuwa adhabu au sababu nyingine, kama Ayubu Mungu anaweza kuwafanikisha watu tena. Kuna watu ambao hawaoni kurejeshwa huku katika maisha haya; lakini kutatokea mbinguni.

S: Kwenye Zek 8:9-13, kwa nini ujumbe huu umeongezewa maneno "mikono yenu iwe hodari?"

J: Mbali ya maudhui ya ujumbe huu kuwa kutia watu moyo, Mungu alikuwa anawaambia watu moja kwa moja wawe hodari, wenye bidii, na furaha kwa ajili ya kazi yao. Kujua kuwa kazi si bure, na kujua kuwa ni mapenzi ya Mungu kutatoa motisha wa kuifanya. Hata hivyo, tunapaswa kutumia motisha huo kufanya mambo ambayo Mungu anataka tuyafanye.

S: Kwenye Zek 8:10, ni kwa jinsi gani Mungu anawaacha watu wagombane na jirani zao?

J: Jambo hili linaweza kuwa ni kufanywa moyo mgumu kama hukumu kwa jinsi Farao alivyofanyiwa na Mungu baada ya Farao mwenyewe kuufanya moyo wake kuwa mgumu. Kama mtu alikuwa anajaribu kupata vitu vingi sana kutoka kwa watu wengine, itafaa tu endapo watu wengine wanajaribu kupata vitu vingi kutoka kwa mtu huyo. Adhabu mojawapo ya kuwa na tamaa ya mali na kujinufaisha na watu wengine ni juhudi inayotokea wakati watu wengine wanapoona jinsi mtu huyo alivyo.

S: Kwenye Zek 8:13, laana inawezaje, hata laana kutoka kwa Mungu, ikabadilika kuwa baraka?

J: Wakati mtu mmoja au taifa linatubu na kumgeukia Mungu, hata baada ya kuadhibiwa, au kuharibiwa, Mungu ana njia ya ajabu ya kubadilisha hata laana kuwa baraka. Rum 8:28 inasema kuwa mambo yote hufanyika vema kwa watu wanaompenda Mungu. Mambo haya yanaweza kuhusisha adhabu, uharibifu, na laana.

S: Kwenye Zek 8:14, kwa nini Mungu haonyeshi huruma nyakati zingine, na kwa nini Mungu alionyesha huruma hapa?

J: Je kila mtu anastahili nafasi nyingine? Vipi kama hawastahili kitu chochote kutoka kwa Mungu, si hata rehema au huruma. Kama mtu haombi kupewa nafasi nyingine, hataki nafasi nyingine, kama watapata nafasi nyingine watafanya jambo lile lile walilolifanya kabla, hivyo kwa nini tunadhani wanastahili nafasi ya pili, ama kutoka kwa Mungu ama kutoka kwetu. Lakini watu hawa wa Mungu kwenye Zekaria 8 walitubu, na Mungu amependezwa kuwapa nafasi nyingine, na kuwaonyesha neema, huruma na rehema.

S: Kwenye Zek 8:14, kwa nini Mungu aziwaadhibu nyumba za Israeli na Yuda kwa makosa ya baba zao, kwani Ezekieli 18 inasema kuwa Mungu hawaangamizi watoto kwa ajili ya maovu ya baba zao?

J: Hakuna kitu kwenye Maandiko kinachosema kuwa Mungu ataliadhibu taifa au atalihesabia kuwa lina hatia kama litatubu na kutokuenenda kwenye njia za baba zao. Hata hivyo, ikiwa wataishi kwa njia fulani, kama wazazi wao walivyofanya, watapata adhabu hiyo hiyo. Kama wazazi wa mtu wanamfundisha vitu vibaya, na yeye anavifuata vitu vibaya ambavyo wazazi wake wamemfundisha, Mungu atamhesabia kuwa ana hatia, si wazazi wake tu.

S: Kwenye Zek 8:21-23, ni wakati gani mataifa wengi wataomba fadhili za Mungu Yerusalemu?

J: Inaelekea kuwa jambo hili litatokea wakati wa milenia.

S: Kwenye Zek 8:23, je jina "Myahudi" linamaanisha mtu kutoka ufalme wa kusini tu, au falme zote za kaskazini na kusini?

J: "Myahudi" inamaanisha mtu kutoka ufalme wa kusini, hata wakati wa uhamisho. Lakini baada ya uhamisho, kwa kuwa karibu ni watu wa ufalme wa kusini tu ndio waliorudi, jina hili lilikuja kumaanisha Waisraeli wote waliotunza utambulisho wa taifa lao.
Ufalme wa kusini:
Msemo kwenye 2 Fal 16:6 unamaanisha "Wayahudi." Kwenye 2 Fal 25:25, inamaanisha Wayahudi. Kifungu hiki kinaongelea muda mara baada ya uhamisho wa Babeli, na linamaanisha watu wa kwenye ufalme wa kusini.
Kwenye 2 Fal 18:26, 28; 2 Nya 32:18, na Isa 8:1 wakati wa Nabii Isaya, na Hezekia, during the time of Isaiah, and Hezekiah, wakati Senakaribu na Waashuru walikuwa wanaizingira Yerusalemu, walimaanisha lugha ya Kiyahudi.
Benjamini
ilikuwa kwenye ufalme wa kusini. Wakati wa uhamisho, Mordekai alikuwa mtu wa kabila la Benjamini aliyeitwa Myahudi mara nane kwenye Kitabu cha Esta. Mtume Paulo pia alikuwa mtu wa kabila la Benjamini kwenye Fil 3:5.

S: Kwenye Zekaria 9-14, kuna ushahidi gani kuwa kifungu hiki kiliandikwa na mwandishi tofauti na yule aliyeandika sura za 1 hadi 8?

J: Hakuna. Kuna waandishi wamakinifu na wenye mawazo huru walidai hivi wakisimamia kwenye maelezo mawili ambayo ni kubadilisha mkazo na mambo yaliyomo.
Kazi ya mwandishi mwenye kushuku, Asimov's Guide to the Bible, uk.668-669, inasema kuwa Zekaria 9-14 iliandikwa wakati wa Waseleusidi (watawala wa kinasaba wa dola ya Kigiriki walioitawala sehemu mojawapo ya himaya iliyogawanyika ya Rumi baada ya kifo cha Alexander Mkuu mwaka 323 KK). Hata hivyo, mwandishi huyu hatoi ushahidi wowote ule kwa madai haya. Inaelekea ameyarudia tu maoni ya waandishi wamakinifu wenye mawazo huru.

S: Kwenye Zek 9:1, je nchi ya Hedraki ipo wapi?

J: Nchi hii pia iliitwa Hatarika. Ipo sehemu ya kaskazini magharibi ya Shamu (Syria) ya sasa, kaskazini mwa Hamathi kwenye Mto Orontes.

S: Kwenye Zek 9:1-9, kwa nini hasa Mungu alikasirishwa na nchi hizi mbili, Shamu/Lebanoni, na Ufilisti, pia Babeli kwenye Zek 2:7-10?

J: Zifuatazo ni sababu zilizotolewa kwenye Kitabu cha Zekaria.
Tiro (pwani) ilijenga ngome na kujilimbikizia shaba na dhahabu kama vumbi na udongo kwenye Zek 9:3-4.
Wafilisti walikuwa watu wenye maringo na wauaji wakatili kwenye Zek 9:6.
Babeli walipora vitu kutoka Sayuni kwenye Zek 3:7.
Babeli ilikuwa makazi ya mwanamke mwovu kwenye Zek 5:7-11.
Kwa ujumla, laana ya Mungu ilikuwa juu ya wakandamizaji waliowasambaza watu wa Mungu kwenye Zek 9:8b.
Leo hii Mungu anapokuwa amekasirishwa na nchi sababu inaweza kuwa hizo hizo.

S: Kwenye Zek 9:5, ni lini Ashkeloni itaacha kukaliwa na watu?

J: Wakati Wababeli walipoivamia Yuda. Ashkeloni ilijengwa upya baadaye, kwa sababu Yudas Maccabeus aliiteka kwenye 1 Maccabees 10:86; 11:60. Zek 9:5 haikusema kuwa Ashkeloni itatelekezwa daima.

S: Kwenye Zek 9:5-7; Amo 1:6-8; Sef 2:4-5, kwa nini kuna miji mikubwa mine au mitano ya Wafilisti iliyotajwa, na Gathi haumo?

J: Hatufahamu kama mji wa Gathi ulikuwepo wakati huu. Kumbukumbu za Waashuru zinataja "Gimti kwenye nchi ya Ashdodi", lakini hakuna maelezo yeyote yale ya kihistoria baada ya wakati huo. Makaburi ya Waislamu kwenye eneo hili yanazuia ufukuaji zaidi.

S: Kwenye Zek 9:13, je Wayahudi na Wagiriki watapigana lini?

J: Jambo hili lilitokea wakati wa Alexander Mkuu, muda ambapo Wamakabia walipowaasi Waseleusidi mwaka 175-163 KK.

S: Kwenye Zek 10:1-2, mara nyingine watu hufanya dhambi kwa kutokutafuta vitu kwa ajili ya Mungu, lakini kwenye habari hii Mungu anapingana na watu wanaoziliza sanamu mambo ambayo Mungu anayatoa. Je ni mambo gani ambayo Mungu anayatoa, ambayo watu wa leo wanayaafuta kutoka sehemu nyingine?

J: Kwa kiwango cha nje, vitu mbalimbali vilivyopo, fedha, afya, furaha, na anasa. Kwa kiwango cha kina, upendo, heshima, usalama, na umuhimu. Wakati mwingine watu wanafanya mambo yanayoonekana kuwa ya kijinga, kwa sababu ya juhudi zao zisizokuwa nyoofu za kuyafikia mambo haya kutoka kwa watu wengine.

S: Kwenye Zek 10:2b-3, ni wachungaji gani hasa ambao Mungu amekasirishwa nao hapa?

J: Si waalimu wa uongo tu, kwa sababu inasema kuwa watu hawana mchungaji. Lakini, ni wachungaji wanao waangusha kuhusu kazi ya kuongoza watu. Kuna uwezekano kuwa baadhi yao walikuwa wanato mafundisho ya uongo, lakini wengine hawakuwa wanafanya kitu?

S: Kwenye Zek 10:3, kwa nini Mungu anasema kuwa aliwaadhibu mbuzi?

J: Hawa wanaweza kuwa ni wachungaji wa mbuzi, kwa maneno mengine viongozi wa watu ambao hawakuwa kondoo wa Mungu. Vinginevyo, inaweza kumaanisha miungu mbuzi na watu wote wanao iabudu.

S: Kwenye Zek 10:4; Isa 22:23-25; Ezek 15:3, je msumari unawakilisha kitu gani?

J: Kwenye vifungu vyote hivi msumari unataka usiwe unaondoshwa, na vitu mbalimbali vinawza kuning'ing'izwa kwenye msumari. Hata hivyo, msumari utaishia kukatwa. Eze 15:3 inasema msumari unatakiwa utengenezwe kwa kutumia mbao ngumu, siyo mzabibu.

S: Kwenye Zek 10:4, je uimara wa jiwe kuu la pembeni, msumari, na upinde unatofautianaje? Ni uimara wa aina gani unaoelezea vizuri zaidi uimara wako kiroho?

J: Jiwe kuu la pembeni ni lazima liwe imara, kwa sababu jengo linajengwa juu yake, ni lazima liwe na vipimo sahihi, kwa sababu vitu vingine vinapimwa kutokana na hili. Msumari, endapo unatakiwa kushikilia hema, au kushikilia vitu vingine ukutani, hauhamishwi, haubadilishwi, na utaweza kutumaini kuwa kitu kinachokushikilia hakitaondoka mahali palipo. Kitu chochote cha kukazia kigingi ili kisiondoke. Kinyume cha hapo, upinde huzunguka sana, lakini kwenye pande fulani tu. Tunatakiwa tuwe kama mwamba ili watu watutegemee wakitambua kuwa jiwe letu kuu la pembeni ni Kristo. Tunatakiwa kuwa kigingi ambacho watu wanaweza kukitegemea kupata mafundisho sahihi na mashauri ya hekima, na siyo mashauri yanayobadilika kulingana na jinsi upepo wa kisiasa unavyovuma. Lakini hatutakiwi kuwa waangalifu tu, bali pia watu wenye kujishughulisha kwenye kulilinda kundi la Bwana lisishambuliwe.

S: Kwenye Zek 10:6, Mungu anatoa ahadi nzuri sana kuwa atawajibu. Ni njia zipi ambazo Mungu hatatujibu, kwa sababu hatujaomba?

J: Mara nyingine tunashindwa kuomba, kwa sababu tumesahau, tunajaribu kujibidisha kwa nguvu zetu wenyewe. Mara nyingine tunashindwa kuomba kwa sababu tunafikiri kuwa jambo linalotukabili ni dogo sana hivyo Mungu hatajishughulisha nalo. Mara nyingine hatudhani kuwa Mungu anatujali hata atusaidie. Lakini bado tunapaswa kuomba na kuona jinsi ambavyo Mungu anafanya.

S: Kwenye Zek 10:6-10, ni sababu gani unazoziona za Mungu kuwatia nguvu na kuwarejesha watu wake?

J: Zifuatazo ni baadhi ya sababu ambazo zimewahi kutolewa.
Mungu aliwahurumia (Zek 10:6).
Mioyo yao itafurahi kwa Bwana (Zek10:7b).
Mungu anawakomboa (Zek 10:8b).
Watamkumbuka Mungu, hata kama ni kwenye nchi za mbali (Zek 10:9a).
Mungu anataka kuwakusanya ili wawe wengi zaidi (Zek 10:10).

S: Kwenye Zek 10:6-10, wewe kama kiongozi au mtu anayetia watu moyo, unamsaidiaje mtu anayejiona ameangushwa na mchungaji wake, au na Mungu? Je tunaweza kuwapa ahadi gani watu kama hawa?

J: Shida ya makanisa yote ni kuwa yanaongozwa na viongozi wenye wenye dhambi ambao wana uwezo wa kufanya makosa. Ikiwa mtu atawaangalia viongozi badala ya kumwangalia Mungu, ni dhahiri kuwa mtu huyo atakuja kuvunjika moyo siku moja, kwa sababu sisi sote huwa tunafanya makosa ama katika mafundisho, matendo, au hata fikara tu. Lakini tunaweza kutiwa moyo na mambo tunayoyafanya yaliyo mazuri, lakini tumwngalie kama kielelezo chetu, ndipo tutaweza kuitii vema Rum 15:7, kuwa tumpokee kila mmoja, kama Yesu alivyotupokea. Tunatakiwa kuwaondosha nje ya kanisa walimu wa uongo na wasiokuwa na moyo wa toba, lakini pia tunapaswa kutambua kuwa hakuna mtu aliye mkamilifu. Kuna ushauri wa utani unaoendana na wazo hili kuwa ukitokea kulikuta kanisa ambalo ni kamilifu usijiunge nalo; kwa sababu mara ukijiunga utaliharibu.

S: Kwenye Zek 10:8 na Isa 5:26, je ni jambo lisilofaa kuwa Mungu anadaiwa "kuzomea", kama Muislamu Ahmad Deedat anavyosema?

J: Zek 10:8 inasema, "Nitawapigia kelele, na kuwakusanya pamoja." Vivyo hivyo, Isa 5:26 inasema, "Naye [Mungu] atawapigia miunzi tokea mwisho wa nchi." Pia si jambo baya kwa Mungu kuwaita watu na waende kufanya kile atakachowataka wafanye.

S: Kwenye Zek 10:11, ni lini kiburi cha siku zijazo cha Ashuru kitaondolewa?

J: Kwanza tuangalie kitu ambacho siyo jibu kisha jibu lenyewe.
Kitu ambacho siyo jibu:
Baada ya Waturuki kuitwaa Mashariki ya kati, waliwatesa Wakristo wenye asili ya Amenia na Ashuru. Hata hivyo, hapakuwa na Waashuru wengi waliokuwa wamebaki, na hawakuwa wengi kiasi cha kuweza kujivuna. Neno hili linaweza kuwa ni makosa ya kunukuru ya jina Shamu (Syria).
Jibu lenyewe:
Baada ya Alexander, himaya kubwa mbili zilikuwa Watolemi (watawala wa kinasaba wenye asili ya Kimasedonia) wa Misri na Waseleusidi (watawala wa kinasaba wa dola ya Kigiriki walioitawala sehemu mojawapo ya iliyokuwa himaya ya Rumi baada ya kifo cha Alexander Mkuu mwaka 323 KK) wa Shamu. Kwa kuwa Misri na Ashuru (Assyria) zimetajwa, jambo hili huenda lilikuwa makosa ya kunukuru ya jina Shamu (Syria).
Kwa vyovyote vile, nchi ya Waashuru ilikuwa sehemu ya Himaya ya Waseleusidi.

S: Kwenye Zek 10:11, fimbo ya enzi ya Misri itaondoka lini?

J: Kuanzia wakati wa Wababeli na kuendelea, hapatakuwa na Farao mwingine tena. Misri haitakuwa nchi huru tena, isipokuwa kwenye kipindi kifupi cha uasi dhidi ya Waajemi, na chini ya Watolemi wa Kigiriki, na baadaye sana chini ya Waislamu Wafitimidi (ufalme uliotawala sehemu za Afrika Kaskazini, Misri, na Shamu kuanzia mwaka 909 hadi 1171), na siku za sasa.

S: Kwenye Zek 10:12, je Mungu anawezaje kumuimarisha mtu katika Bwana?

J: Hata kama tumekwisha okolewa wakati tulipompokea Kristo kwa mara ya kwanza, tuna wajibu wa kuwa imara katika Bwana. Na hatuwezi kuutimiza wajibu huu sisi wenyewe. Bali tungali tuna wajibu wa kujinyenyekeza kwa Roho Mtakatifu, kuwa tunahitaji sio tu kumruhusu bali pia kumtaka atubadilishe. Kubadilika kunamaanisha tunaacha kufanya na kufikiri mambo kwa namna ya zamani, na tunaanza kufanya na kufikiri kwa njia ya Mungu, njia ambayo anataka tuifuate. Je unapata muda wa kutosha kusali, kusoma neno la Mungu, kushiriki pamoja na waumini wengine kwa ajili ya kuimarishwa na kuwaimarisha, na kufanya mambo ambayo tunajua Mungu anataka tufanye?
Kama ukiangalia nyuma katika maisha yako miaka mitano iliyopita, na kulinganisha na sasa, natumaini mambo yamebadilika. Natumaini upo karibu zaidi na Mungu, unamtii zaidi, una hekima zaidi katika maneno yake, na umejengeka zaidi kwenye upendo wa kusaidia na kushirikiana na watu wengine. Natumaini kuwa unapanga kuwa miaka mitano ijayo, kama Bwana atakuwa bado kurudi, unategemea kuwa utakuwa karibu zaidi na Mungu kuliko sasa.

S: Kwenye Zek 10:13, ni lini kiburi cha siku zijazo cha Ashuru kitaondolewa?

J: Baada ya Alexander, himaya kubwa mbili zilikuwa Watolemi wa Misri na Waseleusidi wa Shamu. Kwa kuwa Msri na Ashuru (Assyria) zimetajwa, inaelekea neno hili lilikuwa ni kosa la kunukuru la neno Shamu (Syria).
Kwa vyovyote vile, nchi ya Waashuru ilikuwa sehemu ya Himaya ya Seleusidi.

S: Kwenye Zek 10:13, fimbo ya enzi ya Misri itaondoka lini?

J: Kuanzia wakati wa Wababeli na kuendelea, hapatakuwa na Farao mwingine tena. Misri haitakuwa nchi huru tena, isipokuwa kwenye kipindi kifupi cha uasi dhidi ya Waajemi, na chini ya Watolemi wa Kigiriki, na baadaye sana chini ya Waislamu Wafitimidi (ufalme uliotawala sehemu za Afrika Kaskazini, Misri, na Shamu kuanzia mwaka 909 hadi 1171), na siku za sasa.

S: Kwenye Zek 11:1-3, kwa nini aya hii inasema moto utaimeza mierezi yenye nguvu ya Lebanoni na kuiangamiza miti?

J: Miti ni sitiari (lugha ya picha) ya nguvu na uzuri wa Lebanoni, na hii inamaanisha kuwa nguvu na uzuri wa Lebanoni utaangamizwa. Leo hii, Lebanoni ni nchi ambayo bado ni nzuri, lakini ina mauaji ya watu wengi wasiokuwa na hatia, yanayofanywa na Waislamu pamoja na watu wanaojiita Wakristo.

S: Kwenye Zek 11:5, ni tabia zipi za wachungaji waliokuwa wanawatunza kondoo wao, dhidi ya wachungaji ambao hawawatunzi kondoo?

J: Zek 11:5-6 inaonyesha kuwa waliwatunza kondoo kwa ajili ya manufaa ya kifedha ambayo wangeyapata. Walikuwa wakiwagandamiza watu. Mchungaji hakutakiwa kuuza kondoo bila kumtaarifu bwana wake. Alikuwa ameajiriwa kuwatunza kondoo, kuwalinda dhidi ya mbwa mwitu, kuanguka kwenye miteremko ya ghafla, baridi ya msimu wa baridi kali, na kuwatembeza sehemu mbalimbali kupata chakula na maji vya kutosha.

S: Kwenye Zek 11:7, fimbo hizi mbili ni nini?

J: Ufalme wa Daudi ulikuwa na sifa mbili: umoja wa kaskazini na kusini, na upendeleo wa Mungu. Mamba haya yote mawili yaliondoka. Inaelekea kuwa kuna uhusiano kati ya tabia za ndani za kuwa na upendeleo wa Mungu, na ishara za nje zenye kuonekana za umoja.
Kimsingi, upendeleo hapa unamaanisha ulinzi dhidi ya maadui wa Israeli. Ni dhahiri kuwa upendeleo kwa maana ya kuwa mwenye kufurahisha machoni pa Mungu haukuwepo tayari. Kwa sababu hivi ndivyo ilivyokuwa, kugawanyika kati ya Israeli na Yuda hakukuwa tu kumetabiriwa na Mungu, bali pia kuliamriwa naye kwenye 1 Fal 11:29-33; 12:22-24.

S: Kwenye Zek 11:7, je fimbo hizi mbili zinahusiana na zile mbili za kwenye Eze 37:15-23?

J: Hapana. Nabii Ezekieli anatuambia kuwa zile fimbo mbili za kwenye Ezekieli 37 zinaziwakilisha Israeli and Yuda. Zekaria anatueleza kuwa hizi ni "upendeleo" na "umoja."
Si lazima kuwa neno ‘fimbo' linapotumika kwenye Biblia ni lazima liwakilishe kitu kile kile. Kwa ajili hiyo, mfano wa tatu ni "mwanzi" kwenye Eze 29:6, ambalo limeelezwa bayana kuwa ni Misri. Kama sitiari ya mwanzi wa Misri, kwenye sura nyingine ya Biblia haimaanishi fimbo mbili, sitiari ya fimbo mbili haimaanishi fimbo mbili za kwenye Zek 11:7.

S: Kwenye Zek 11:8, je kufukuzwa kwa wachungaji watatu katika mwezi mmoja kuna umuhimu gani?

J: Hawa wanaweza kuwa ni
1.
Watu watatu
2.
Huduma za mfalme, kuhani, na nabii
3.
Makuhani, waalimu, na mahakimu
Kwenye Yer 25:34-38, Mungu pia aliwakemea viongozi wa watu kama wachungaji.

S: In Zech 11:8-9, when a leader is good, why do followers still grow weary or detest him or her?

J: Mara nyingi ni kwa sababu wafuasi wanafikiri wanacheleweshwa kupata kitu au mtu bora zaidi. Wakati mwingine kiongozi huongoza watu wake kwenye uelekeo wanaotakiwa kuufuata, lakini unaweza kuwa ni uelekeo wanaotaka kwenda, hasa kama unahusisha usumbufu au gharama vya namna fulani. Kiongozi wa kikristo anaweza kuwa anapenda watu wawe karibu zaidi na Mungu, lakini watu hawataki kufanya hivyo. Wakati mwingine kiongozi anakuwa na mawazo ya kuwaongoza watu anaowasimamia, lakini watu wana mawazo tofauti ya namna ambavyo kiongozi anatakiwa afanye.

S: Kwenye Zek 11:10, ni lini Mungu alivunja maagano?

J: Mungu hajawahi kuvunja ahadi yake. Lakini, wakati Mungu anaweka ahadi yenye kuwa na masharti ya mwenendo unaotakiwa kwa watu, na watu wanazidi kutotimiza masharti, wakati utafika ambapo Mungu atasema kuwa ahadi hii yenye masharti haitaweza kutimizwa. Moja ya ahadi zinazofahamika sana zenye masharti, ambayo haijawahi kutimizwa, inapatikana kwenye 2 Nya 7:14.

S: Kwenye Zek 11:12-13, vipande thelathini vya fedha vina umuhimu gani?

J: Zekaria ameliweka jambo hili kuwa kama fumbo, walau hadi wakati wa baadaye kwake. Kut 21:32 imeweka vipande thelathini kuwa ni kiasi cha kulipa kwa kumuumiza mtumwa. Ni kweli, miaka mingi baadaye Yuda alimsaliti Yesu kwa vipande thelathini vya fedha.

S: Kwenye Zek 11:13, je ni kweli kuwa neno "mfinyanzi" linatakiwa kuwa "hazina?"

J: Wazo hili halina uhakika. Toleo la Kishamu linasema "hazina" hapa. Toleo la Kiebrania linasema "mfinyanzi", na toleo la Kigiriki (Septuajinti) linasema "tanuru."

S: Kwenye Zek 11:14; 1 Fal 11:11-13, 12:22-24, ni nani aliyevunja umoja wa Yuda na Israeli, na kwa nini?

J: Mungu alifanya hivyo, lakini kuna majibu matatu ya nyongeza. Mungu aliahidi kufanya hivyo, Mungu aliwatumia watu kama mawakala wake, na Mungu aliwazuia kurudiana tena. Kwenye 1 Fal 11:11-13, baada ya Sulemani kutotii, Mungu alimwambia kuwa atachukua sehemu kubwa ya Israeli kutoka kwenye nyumba yake. Hat hivyo, kwa ajili ya Daudi baba yake, Mungu hatafanya hivyo wakati wa uhai wa Sulemani bali wakati wa watoto wake. Wakala hasa wa jambo hili ni usumbufu wa Rehoboamu mtoto wa Sulemani, na watu ambao hawakupenda kufanyishwa kazi kwa lazima. Rehoboamu alitaka "kutatua" tatizo hili kwa kulikusanya jeshi ili kuyashinda makabila ya kaskazini, lakini Mungu alimtuma nabii wake Shemaya kumwambia Rehoboamu na watu wote kutokuungana tena, kwa sababu "jambo hili limetoka kwangu." Kundi lililojiita ‘the local church' linasema kuwa migawanyiko miongoni mwa waumini ni moja ya dhambi mbaya zaidi, na wanatoa mfano wa ufalme uligawanyika wa taifa la Israeli. Uadui na mashindano miongoni mwa Wakristo ni dhambi kubwa, lakini kugeuka na kwenda mbali na Mungu ni kubaya zaidi, na Mungu hakutaka umoja wa falme hizi mbili wakati wakiwa hawamfuati kwa mioyo yao yote.

S: Kwenye Zek 11:16-17, je mchungaji huyu asiyefaa ni yupi?

J: Kuna maoni mawili kuhusu mstari huu.
Mpinga Kristo:
Mstari huu unaweza kuwa unamwongelea mpinga Kristo.
Viongozi wasiofaa
, kama wale wa mwaka 66 BK, wakati wa maasi ya Wayahudi kwa Rumi.

S: Kwenye Zek 12:1, ni kwa namna gani hasa Mungu hutengeneza roho ya mwanadamu ndani yake (mwanadamu)?

J: Maandiko hayasemi namna gani. Kuna maoni mawili miongoni mwa Wakristo, na inawezekana kuunganisha maoni haya mawili.
Maoni ya Kitradusia (Traducian view):
Moja ya mambo makubwa ya maoni haya yanahusu namna watu wanavyopatikana. Kama ambavyo miili ya wanadamu inavyotokana na chembe chembe za miili ya wazazi wao, maoni haya yanasema nafsi za watu hutokana na nafsi za wazazi wao pia. Hata hivyo, kama ambavyo miili ya wazazi wa watu haiondoki mtoto anapozaliwa, pia nafsi za wazazi haziondoki mtoto anapozaliwa. Utradusia una baadhi ya mambo ambayo hayafurahishi, kama watoto wadogo kuwa na hatia kwa ajili ya dhambi za wazazi wao na wazazi wa wazazi wao (kinyume na Ezekieli 18), lakini kuna uwezekano wa kushikilia jambo hili la Utradusia bila kuchukua mengine yasiyokuwa mazuri. Katika historia, Augustine, makanisa ya Kilutheri, pamoja na sehemu ndogo ya wafuasi wa Calvin, wamekuwa wakifuata maoni ya Utradusia. Kanisa la Greek Orthodox kwa ujumla linaamini Utradusia kuhusiana na asili ya nafsi, lakini wanakataa nadharia ya kurithi hatia.
Maoni ya Kiuumbaji:
(Hayahusiani na uumbaji kama unavyoelezewa kwenye Kitabu cha Mwanzo) Kama ambavyo Mungu alimuumba Adamu bila kutumia kitu chochote, Mungu huumba roho zetu leo hii "bila kutumia kitu chochote." Miili yetu tu, na akili zetu ndivyo vinavyoweza kurithiwa, lakini vinapitishwa kwenye jeni zetu na siyo kwingineko kokote. Nafsi zetu hazirithishwi kwa mujibu wa maoni haya.
Mchanganyiko wa Maoni:
Ebr 4:12 inasema kuwa neno la Mungu hugawanya hata nafsi na roho, na viungo na mafuta. Kwa mujibu wa daktari Mkristo, ambaye pia ana shahada ya uzamili ya theolojia (Masters of Divinity degree), aliyenifahamisha kuhusu maoni haya ya kitheolojia, ni vigumu sana (tuseme haiwezekani) kibinadamu kutenganisha mfupa na mafuta mwishoni mwa mifupa mirefu. Mfupa ni kama kiunzi cha fito, kilichojazwa mafuta.

S: Kwenye Zek 12:1, kuna kitu gani cha kishairi kuhusiana na mbingu na nchi?

J: Tunapaswa kufurahi kuwa Mungu hajakitaja kila kitu alichokiumba, vinginevyo tusingeweza kumaliza hata sura moja. Mungu anaposema kuwa alizitandaza mbingu na nchi, anamaanisha vitu vingine vyote pia. Mtindo huu wa uandishi wa kutumia sehemu au miisho miwili kuwakilisha vitu vingine vyote kati yao unaitwa "merisimu." Merisimu ni aina ya sindoche, yaani aina ya lugha ya picha ambayo sehemu ya kitu inatumiwa kuwakilisha kitu chote, au kinyume chake.

S: Kwenye Zek 12:1-4, ni kwa kiasi gani, kizuri au kibaya, tunaathiriwa au kuthibitiwa na jenitiki zetu, jinsi tulivyolelewa na wazazi wetu, mazingira/jamii, na utashi wetu wenyewe?

J: Ingawa hatujui jibu kamili, haya hapa ni baadhi ya mambo ya jumla tunayoweza kuyatambua yatakayotusaidia kupata jibu.
1. Jenitiki, jinsi tulivyolelewa na wazazi wetu, mazingira/jamii, n.k. vyote vinahusika, lakini havihusiki kila kimoja peke yake; vinahusiana kwa pamoja.
2. Huwezi kupata ufumbuzi bila kuangalia vitu ambavyo mtu mwenyewe amechagua kufanya. Vinginevyo huwezi kuelezea watu mapacha wanaofanana (identical twins), waliokulia nyumba moja, ambao mmoja anakuja kuwa mhadhiri wa chuo kikuu, na mwingine anatiwa jela mara mbilimbili kwa sababu ya madawa ya kulevya. Wote walikuwa na mazingira yaliyokuwa na uwezo sawa wa kuwaathiri na madawa ya kulevya, lakini mmoja aliathirika nayo lakini mwingine alijiepusha nayo.
3. Mahali palipo na hali mbaya sana, jambo hilo linaathirije tabia ya mtu anayehusika nayo? Jibu la swali hili kwa kiasi kikubwa linategemea uamuzi wa mtu mwenyewe. Je mtu huyu atatawaliwa na tamaa kutokana na hasara au tukio husika muda wote wa maisha yake, au ataweka kando jambo hilo, na kujipanga upya, na kuendelea na maisha. Wakati watu wawili wanaweka mikono yao juu ya kinanda, na kukipiga kwa kutumia nguvu sawa, je sauti itakuwa na ukubwa sawa? Jibu ni kwamba inategemea: je mmoja wao anakanyaga pedali ya valvu (damper pedal), au kifuniko cha kinanda hakijainuliwa, hivyo hawezi hata kupiga? Kwa kuamua kushikilia jambo fulani, au kulipuuzia, kimahesabu utashi unaweza kuwa kama aina ya mzunguko wa miitikio (feedback loop).

S: Kwenye Zek 12:2, ni mahali gani pengine Mungu alifanya "kikombe" kinachowafanya watu wayumbeyumbe, na kwa nini?

J: Tunapaswa kufahamu maana ya lugha ya picha ya kikombe.
Bwana alisema ana kikombe mkononi mwake kilichojaa mvinyo iliyochanganyika na viungo kwa ajili ya waovu kunywa (Zab 75:8). Maandiko mara nyingi hutumia kikombe kuwakilisha hasira ya Mungu (Isa 51:17, 22; Yer 25:15-29; 51:7; Omb 4:21; Eze 23:31-33; Hab 2:15-16; Ufu 14:10; 16:19).
Kikombe cha Babeli kipo Ufu 17:4; 18:6.
Kwenye upande chanya,
Daudi alisema Mungu alimpa sehemu yake (Zab 16:5). Daudi alisema kikombe chake kinafurika (Zab 23:5). Kikombe ni lugha ya picha ya wokovu kwenye Zab 116:13.
Kina maana kubwa lakini chanya
kwenye Mat 20:22-23; 26:39-42.
Yesu aliomba
kuwa "kikombe" hiki kimuepuke kwenye Mat 26:39-42; Mak 14:36. Pia aliongelea jambo hili kwenye Yoh 18:11.
Kikombe kinaweza kuwa kwa ajili ya vyote furaha na maumivu ya moyo, na mara nyingine kikombe hicho hicho kinaweza kuwa vitu hivi viwili vyote wakati huo huo, kama kilivyokuwa kikombe kwenye gunia la Benjamini (Mwa 44:2-17).

S: Kwenye Zek 12:3-4, kwa nini watu wengi sana walitaka kuwashambulia Wayahudi?

J: Wayahudi walichaguliwa na Mungu kuwa watu wake; na Shetani anaelekea aliwachukia sana. Jambo hili limedhihirishwa kwa wanadamu kwa njia zisizopungua nne.
Mali:
Sababu mojawapo ni maoni kuwa kiasi kikubwa cha mali kiko mikononi mwa Wayahudi wengi wanaofanya biashara ya upendeleo miongoni mwao. Muda mfupi kabla ya kuanza kwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia, serikali ya Ujerumani ilikopa kiasi kikubwa cha hela kutoka kwa baadhi ya wananchi wake matajiri sana wenye asili ya Kiyahudi kwa ajili ya vita. Mara baada ya vita kuanza, baadhi ya wananchi hawa walishtakiwa kwa uhaini, ili kwamba serikali isiwe na ulazima wa kuwalipa hela zao.
Watu:
Kwa baadhi ya watu, kama Hitler, alitaka kuwatokomeza kabisa Wayahudi. Bila kujali kuwa Wayahudi walikuwa maskini au matajiri, Hitler alitaka kuwaondosha wote kabisa, na mali, ardhi, au hata dini havikuhusika kabisa. Hitler pia alijaribu kuwaondoa wadanganyifu na mabasha na wasenge.
Ardhi:
Kwa watu wengine, sababu ya kuwashanbulia Wayahudi ni nchi ya Uyahudi. Kwa upande mmoja, Wayahudi wanasema kuwa Israeli ni nchi ya mababu zao tokea wakati wa Yoshua, isipokuwa kwa kipindi cha miaka 70 cha uhamisho wa Babeli. Ikiwa mtu atasema kuwa Israeli ni mali ya watu walioimiliki awali, kabla ya mwaka 1948, basi nchi hii inatakiwa iwe chini ya Uingereza. Au kama itakuwa kabla ya hapo, basi hii inatakiwa iwe chini ya Uturuki, ambayo ni sehemu pekee iliyobaki ya Himaya ya Ottoman. Kwa upande mwingine, kuna Wapalestina walio na funguo za nyumba zao Israeli, kabla ya 1948, ingawa wakati wa vita waliondolewa. Kama Israeli inataka nchi yote, ikiwa ni pamoja na Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza, basi Wapalestina wote wawe wananchi wa Israeli wenye haki ya kupiga kura? Kwa upande mwingine, kama Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza viwe nchi moja (au mbili) tofauti, basi ni kwa nini Israeli inajenga makazi ya Wayahudi humo? Waislamu wengine wamesema kuwa nchi yeyote iliyowahi kuchukuliwa na majeshi ya Kiislamu ni mali yao halisi na inapaswa kurudishwa kwa Waislamu, iwe ni Israeli au Hispania.
Mji:
Mwandishi mmoja wa Kiarabu alisema kwa utambuzi mkubwa kuhusu mateso ya kiakili aliyoyaita "wazimu wa Yerusalemu" (Jerusalem madness). Ni kutawaliwa na mawazo ya kuupata mji wa Yerusalemu ambako kumesababisha matatizo mengi sana. Watu wengi sana wanausumbukia mji wa Yerusalemu, hata kuliko wanavyojishughulisha kuhusu Mungu. Kwa ujumla Waislamu wauchukulia mji wa Yerusalemu kwa wa tatu kwa utakatifu katika dini yao. Kwenye Kurani ya Kiislamu, Sura 17 inazungumzia safari ya Muhammad ambapo alichukuliwa kimiujiza kwenda kwenye msikiti wa mbali zaidi, na kutoka hapo alipanda buraq (aina ya punda mwenye mabawa) na kwenda mbinguni. Waislamu (ikiwa ni pamoja na Bukhari juzuu ya 5 kitabu cha 58 sura ya 40 na.228, uk.148-149) mahali hapa palikuwa Yerusalemu. Hata hivyo, hapakuwa na msikiti Yerusalemu wakati huo kama al-Tabari juzuu ya 12, uk.195-196; Ibn-i-Majah juzuu ya 1 kitabu cha 4 sura ya 7 na.753, uk.414. Ni "tanzia-ramsa" kuwa mvutano huu kuhusiana na mji, unatokana na sura ya kwenye Kurani inayozungumzia msikiti ambao haungeweza kuwepo Yerusalemu ya wakati ule.

S: Kwenye Zek 12:7-11; 14:2-8,12, ni lini mataifa yanayoizingira Yerusalemu yataangamizwa?

J: Inaelekea kuwa vifungu hivi vinaongelea vita itakayotokea mwishoni mwa milenia. Vita hii imetajwa kwenye Ufu 20:7-9 na Ezekieli 38-39.

S: Kwenye Zek 12:10, je maandishi ya Kiebrania yamefafanuaje maneno haya?

J: Kuna njia tatu.
Mengi ya maandishi ya Kiebrania yanasema "watanitazama mimi, ambaye walimchoma."
Machache ya maandishi ya Kiebrania yanasema "yeye ambaye walimchoma."
Maandishi mengine ya Kiebrania yanasema "watanitazama mimi ambaye walimchoma" (yaani, mtu mwingine mbali ya Mungu alichomwa).
Hakuna sababu nzuri ya kutokukubaliana na mengi ya maandishi ya Kiebrania.

S: Kwenye Zek 12:8-9, ni njia zipi mbili ambazo Mungu anaweza kuzitumia kuwakinga watu, na Mungu atafanyaje hapa?

J: Mungu anaweza kututoa kwenye jaribu, au kututia nguvu tuweze kulimudu jaribu. Hapa Mungu anawatia nguvu ili walimudu jaribu.

S: Kwenye Zek 12:10, ni nani waliyemchoma kama mtu amliliaye mtoto wake pekee?

J: Ndiyo, imedokezewa. Ingawa baadhi ya Wayahudi walimwamini Kristo mara baada ya siku ya Pentekoste, wengi wao hawakumwamini. Inaelekea kuwa Zek 12:10 inaongelea nyakati za mwisho, ambapo Wayahudi wangi watakuja kumfuata Kristo. Vifungu vingine vyenye kuelezea jambo hili ni Rum 11:25-26 na huenda hata sehemu ya pili utimilifu wenye pande mbili wa Mal 4:5-6. Inaelekea kuwa Amo 8:10 inaongelea tukio hilo hilo nyakati za mwisho.

S: Kwenye Zek 12:10, je aya hii inataoa unabii wa kuja kwa Kristo mara mbili?

J: Hata mtu mwenye kushuku ataafiki kuwa aya hii inaongelea matukio mawili. Tukio la kwanza ni kudharauliwa na kukataliwa, na tukio la pili ni kuomboleza kwa ajili ya kukataliwa kwa awali.
Hard Sayings of the Bible, uk.345-346 inaonyesha kuwa sarufi ya Kiebrania iliyo nyepesi na rahisi kueleweka imefunikwa kwenye tafsiri ya New Jewish Publication Society Tanakh: The Holy Scriptures (1988), inayosema, "Lakini nitaijaza nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu roho ya upole na rehema; na wataomboleza kwangu kuhusu watu waliowaua, wakiwalilia kama kwa ajili ya mtoto apendwae sana . . ." Hata hivyo, Walter Kaiser kwenye Hard Sayings of the Bible, uk.346 anasema tafsiri hii "inakiuka kanuni za sarufi ya Kiebrania ili kuepuka kidokezo kilicho dhahiri cha mstari huu wa Kiebrania." Tafsiri hii,
a)
inapindisha kitenzi "kuchoma" kutoka kuwa kitenda na kukifanya kitendewa
b)
inabadilisha mtendaji mmoja ‘wao' kuwa mtendewa.
Kama Kaiser anavyosema, "Ni juhudi ya kishujaa sana kutokuzingatia kidokezo chenye mantiki kuwa mtu anayeongea hapa ndiye aliyechomwa . . ." Yaelekea Kaiser alikuwa mpole sana kwa Wayahudi walikiuka kanuni za sarufi ya Kiebrania hata kuitafsiri aya hii kwenye Kiingereza kwa makosa ili kuifanya iafikiane na theolojia yao.
Kaiser anaendelea kusema kuwa Wayahudi wengine wanatafsiri aya hii kwa usahihi, lakini baadhi yao wanaitafsiri na kuonyesha kuwa kuna Masihi wawili. Masihi mmoja aliyeteswa, na Masihi mwingine ambaye hateswi, bali anakuja katika utukufu.

S: Kwenye Zek 12:11, ilikuwaje kulikuwa na kilio kikubwa huko Hadadrimoni katika bonde la Megido?

J: Kwanza, tungalie kitu ambacho sio jibu la swali hili, kisha jibu lenyewe.
Kitu ambacho sio jibu:
Wababeli, Wafoenike, na watu wengine walijulikana kwa kuomboleza kwa ajili ya Tamuzi mungu wa Kimesopotamia (Kibabeli), ambaye kwa mujibu wa masimulizi ya kubuniwa, aliuawa na nguvu za ulimwengu ulio chini ya dunia kila majira ya majani kupukutika, na alifufuka kila majira ya kuchipua. Hata hivyo, lingekuwa jambo la ajabu endapo Mungu angetaja kulilia sanamu hapa. Isitoshe, wapagani na Wayahudi wanaotenda maovu walimlilia Tamuzi, mungu wa Babeli na si sanamu Hadadrimoni, ambaye anamaanisha Mungu wa Kisemitiki "Hadad mleta radi."
Jibu:
Hadadrimoni ni jina la mahali kwenye bonde la Megido. Vita itakayotokea baada ya milenia pia inaitwa Har-Magedoni. Kwenye bonde, chini ya Mlima Megido, ndipo mahali ambapo Gideoni aliwashinda Wamidiani kwenye Amu 6:33, Wafilisti walimuua Sauli na Yonathani kwenye 1 Samuel 31, na mfalme mwovu Ahazia alifia kwenye 2 Fal 9:27. Lakini kulia kunaweza kuwa kunaongelea kifo cha mfalme mzuri Yosia alipokuwa anapigana na Wamisri kwenye 2 Fal 23:29-30. Wamisri hawakutaka kupigana na Yosia, na kufa kwa Yosia na kushindwa kwa jeshi la Yuda havikuwa na maana yeyote ile.

S: Kwenye Zek 12:11-13, kuna kitu gani cha pekee kwenye maombolezo haya?

J: Yaligusa hisia na yalipangiliwa vizuri. Kila ukoo ulionekana dhahiri kuwa peke yake; hivyo hakuna ukoo ambao ungesema "hatuhitaji kuomboleza", kwani ililikuwa ni jukumu la ukoo mwingine. Yalikuwa ni maombolezo yaliyofanywa kwa pamoja, hasa kwa lengo la kumwomba Mung msamaha.

S: Kwenye Zek 13:1, chemchemi ya utakaso itafunguliwa lini?

J: Ilifunguliwa Yesu alipokufa kwa ajili ya dhambi zetu. Tazama kuwa aya hii haisemi kuwa watu wote watatakaswa, ila kuwa chemchemi itafunguliwa kwa ajili ya utakaso. Kwa maana nyingine, itafunguliwa kwa ajili ya Wayahudi walioongelewa hapa wakati watakapotambua kuwa Yesu ni Masihi.

S: Kwenye Zek 13:2, ni wakati gani patakapokuwa na sanamu nyingi zaidi nchini?

J: Kwa wakati huu hakuna sanamu miongoni mwa Wayahudi kwenye nchi ya Yuda. Hata hivyo, kwa kuwa neno "nchi" linaweza pia kumaanisha "dunia", unabii huu wa nakati zijazo unaweza kuwa unaongelea wakati wa milenia.

S: Kwenye Zek 13:2, kuna tofauti gani kati ya dhambi na uchafu?

J: Ingawa maneno haya yanafanana sana, kuna tofauti ndog kati yao. Dhambi ina maana mbili: inaweza kuwa inamaanisha matendo ya dhambi, lakini pia inaweza kuwa inamaanisha asili na haja ya dhambi vilivyo ndani mwetu. Uchafu unamaanisha hali ya kutokuwa safi ambayo mwenye dhambi anakuwa nayo tokana na kutenda dhambi.
Exegetical Commentary: Haggai, Zechariah, Malachi
, uk.328 inasema kuwa dhambi "inahusika na kutokuafikiana na mapenzi ya Mungu, na uchafu unahusika na hali ya unajisi unaotokana na kuvunjwa kwa kanuni za utakatifu. Dhambi huonyesha ushiriki wa kutenda uovu, na uchafu unaonyesha matokeo ya kufanya hivyo." Hivyo, mambo haya mawili ni kama pande mbili za sarafu.

S: Kwenye Zek 13:2, ni dhahiri kuwa sanamu wanahusika na kufanya dhambi, lakini kuna uhusiano gani kati ya sanamu na uchafu?

J: Ingawa dhambi ndiyo inayosababisha kuabudu sanamu, uchafu ni matokeo ya kuabudu sanamu. Vitu vichafu, kama mifuniko ya takataka na vyombo vya kuendea haja haviwezi kutumika kwenye mambo mazuri, kama kuhifadhia nguo nzuri au kupikia chakula. Rum 3:12 inasema kuwa mtu anaweza kufanya asiye mwenye thamani, bila kueleza kwa namna gani. Lakini 2 Fal 17:15 na Yer 2:5 inasema kuwa kufuata sanamu zisizokuwa na thamani hufanya mtu akose thamani. Sanamu zinamkasirisha Mungu kwa mujibu wa Kum 32:21; 1 Fal 16:13, 26.
Sanamu zinaweza kuwa dhahiri kama Baali, Astate, Krishna, Budha, n.k. Sanamu zinaweza pia zisiwe dhahiri, kama umaarufu, mali, pombe, ngono, tamaa ya vitu, au usalama. Hata vitu vizuri kama kazi, afya, mwenzi wa maisha, au watoto vinaweza kuwa sanamu kama vitachukuliwa kuwa muhimu kuliko Mungu. Wakati fulani nilikuwa naongoza ibada ya watoto kwenye kanisa la Wachina, ingawa siukumbuki usemi niliutoa, inaelekea nilisema kuwa Mungu ni muhimu kuliko masomo yako ya kinanda. Juma lilifuata mama mmoja alinijia akiwa na kicheka cha chinichini, na alisema kuwa mtoto wake wa kiume aliuliza kama maneno hayo yalikuwa ya kweli. Ingawa alimhakikishia mwanae kuwa maneno hayo ni ya kweli, wazazi kwa ujumla wanatakiwa kuwaeleza watoto wao kwa ufasha mambo yaliyo muhimu maishani. Mfano wako unaweza kusema kwa sauti kubwa kuliko maneno, kwa hiyo unatakiwa uwe na vyote mfano na maneno vyenye kuwakilisha jambo muhimu.

S: Kwenye Zek 13:3-6, je unabii utapita lini?

J: Maandiko hayasemi bayana ni lini utapita, lakini sehemu hii ya Zekaria inaongelea milenia itakayo kuja. Pia 1 Kor 13:8 inaongelea muda ambao unabii na lugha vitapita.
Kwa kiasi kidogo kiasi, manabii na ufunuo vilitoweka kwa kipindi kifupi mara baada ya muda huu na hadi muda wa Kristo na Yohana Mbatizaji. Mik 2:6 pia inaongelea watu ambao hawapendi kusikia tena kuhusu manabii wa Mungu.

S: Je mchungaji mwema kwenye Zek 13:7 ni Kristo, na mchungaji mwema atapigwa lini?

J: Yesu alisema kuwa mchungaji aliyeongelewa hapa ni yeye mwenyewe (Mat 26:31, 56; Mak 14:27). Tazama Believers Bible Commentary, uk.1169 kwa habari zaidi.

S: Kwenye Zek 13:8-9, ni lini unabii wa kufa kwa theluthi mbili utakapotimia?

J: Kitabu cha Zekaria hakisemi kitu. Kuna uwezekano kuwa jambo hili litatokea wakati wa dhiki kuu.

S: Kwenye Zek 14:1-2, ni kwa nini unadhani Mungu huwa anaruhusu matukio kama kutokea?

J: Itakuwa kana kwamba kila kitu kimetoweka wakati Kristo mwenyewe atakapotokuja kuwatetea. Majeshi yalipoizunguka Yerusalemu kwenye Yoeli, Mika, na Ezekieli, mji haukuangamizwa. Lakini mara hii mji ulichukuliwa kimabavu. Tafsiri ya Kigiriki ya neno la Kiebrania sara ni thlipsis, ambalo ndilo neno alilolitumia Yesu kwa dhiki kuu. Luk 21:24 inasema muda ambao nyakati za watu wa mataifa zitakapokuwa zimetimia.
Jambo hili haliwezi kuwa ni kubomolewa kwa mji wa Yerusalemu na Warumi mwaka 70 BK, au mwishoni mwa Maasi ya Barkuba ya mwaka 135/136 BK, kwa sababu katika mara hizo mbili zote, Warumi tu, na si mataifa mengine yote yaliyokuwa yanapingana na Yerusalemu, na waliwaacha nusu tu ya wakazi kubaki kwenye nyumba zao.

S: Kwenye Zek 14:3-5, Mungu anakuja pamoja na watakatifu wake wote sehemu gani nyingine?

J: Yesu na majeshi ya mbinguni yatakuja kwenye Yuda 14-15, na Ufu 19:11-21.

S: Kwenye Zek 14:4-5, ni mahali gani pengine ambapo Mlima wa Mizeituni unaendana na nyakati za mwisho?

J: Mlima wa Mizeituni unakizidi Kilima cha Hekalu (Temple Mount) mita 100 (futi 330). Inashangaza kuwa Mlima wa Mizeituni haujawahi kuitwa hivyo kwenye Agano la Kale isipokuwa hapa na "njia ya kuupandia Mlima wa Mizeituni" kwenye 2 Sam 15:30.
Divai toka milimani (Yoe 3:9-17; Ufu 14:14-20).
Kukimbia kupitia Mlima wa Mizeituni ilikuwa ni njia ambayo Daudi aliitumia alipokuwa anamkimbia mwana wake Absalomu (2 Sam 15:16-30).
Mlima wa Mizeituni /Gethsemane: Mat 26:36-56; Mak 14:32-50; Luk 19:37; 21:37; 22:39-53
Edomu (Yoe 3:19; Mal 1:4-5, na Obadiah.
Vita kuu ya Gogu na Magogu (Ufu 20:7-10).
Wayahudi walijua kuwa jambo hili lilikuwa muhimu. Kutoka karne ya 8 hadi 11 BK, maombi yamekuwa yakifanywa mara nyingi kutokea kwenye Mlima wa Mizeituni.

S: Kwenye Zek 14:6-8, ni vifungu gani vingine vinavyoongelea jambo hili?

J: Ishara za mbinguni zimo Isa 13:9-10; Yoe 2:31; 3:15; Amo 5:18; Mat 24:29-30; Ufu 6:12-14; 8:8-12; 9:1-18; 14:14-20, na 16:4,8-9.

S: Kwenye Zek 14:10, maneno haya yanamaanisha nini kwa kuwa ukanda wa Araba ulikuwa mkavu sana na tambarare?

J: Leo hii Mashariki ya Kati ni pakavu kuliko palivyokuwa nyakati za Biblia. Unabii wa siku zijazo unaweza kuwa unadokezea jambo hili.

S: Kwenye Zek 14:12-15, je pigo hili litatokea lini?

J: Pigo hili litatokea wakati Gogu na Magogo watakapokuwa wamizingira Yerusalemu. Unaweza kusoma zaidi kuhusu jambo hili kwenye Ufu 20:7-9 na Ezekieli 38-39.

S: Kwenye Zek 14:12-21, je nyakati hizi mbaya sana, zitakazofuatwa na mataifa wote kuiadhimisha Sikukuu ya Vibanda, zitatokea lini?

J: Inawezekana kuwa nyakati hizi zitatokea wakati wa milenia.

S: Kwenye Zek 14:14, kwa kuwa Mungu peke yake ndiye anayepigana mwanzoni, kwa nini Yuda anapigana hapa?

J: Ingawa Maandiko hayasemi katika sehemu hii bayana, tunaweza kuongeza swali na kuuliza kwa nini Mungu anatuomba tumfanyie kitu chochote kwani anaweza kufanya mambo yote yeye mwenyewe? Mungu hatuhitaji. Lakini Mungu hutupa upendeleo wa kushiriki kwenye kazi yake, na kukamilisha mambo mazuri kwa ajili yake.

S: Kwenye Zek 14:18, kwa nini Misri imetajwa bayana kuwa inaadhibiwa hapa?

J: Huenda ni unabii kuwa Misri haitakuwa makini kuja Yerusalemu. Inafurahisha kuwa Misri imetajwa kwani mvua hunyesha kwa nadra sana huko. Lakini, Misri inautegemea Mto Naili tu, unaoanzia Ziwa Viktoria lenye kupata maji kutoka mvua nyingi za Afrika ya Kati. Mungu anaweza kupunguza mvua kwenye eneo moja ili ilete madhara kwenye eneo lingine. Tafsiri za Kigiriki (Septuajinti, LXX) na Kiashumu za Agano la Kale zinasema "kutakuwa na pigo", badala ya "mvua haitakuweko."

S: Kwenye Zek 14:20-21, ni kitu gani kisicho cha kawaida kuhusu muundo hapa?

J: Hili ni jambo lisilo la kawaida kwa wasomaji wa kisasa, si wa kale. Huu ni muundo wa kishairi uitwao kiazimu.
Siku hiyo
... katika njuga za farasi yataandikwa maneno haya "WATAKATIFU KWA BWANA"
...... Vyombo vilivyomo ndani ya nyumba ya BWANA vitakuwa kama mabakuli yaliyoko mbele ya madhabahu
......... Kila chombo katika Yerusalemu, na katika Yuda, kitakuwa kitakatifu kwa BWANA wa majeshi,
... nao wote watoao dhabihu watakuja kuvitwaa vile vyombo, na kutokosa nyama ndani yake.
...Hatakuwamo tena Mkanaani [au mfanya biashara] ndani ya nyumba ya BWANA wa majeshi.
Tafsiri hii na maelezo zaidi vimo kwenye Exegetical Commentary: Haggai, Zechariah, Malachi, uk.365.

S: Kwenye Zek 14:21, vyombo vinatumika kwa namna gani kisitiari?

J: Vyombo vilikuwa ni vitu vyenye umuhimu mdogo zaidi hekaluni; vilitumika kuwekea majivu. Jambo hili halisemi tu kuwa vitakuja kuwa vitakatifu, lakini chombo cha kila mmoja kitakuwa kitakatifu.
Ingawa mabakuli matakatifu ya kale yalikuwepo kwenye madhabahu tu, vyombo hivi vitakatifu vitatumika na kila mtu. Wagibeoni walikuwa Wakanaani waliofanya agano na Yoshua na walikuwa watumishi wa hekaluni. Walikuwa ni "maridhiano" ambayo Mungu aliyaruhusu kwenye ibada ya hekaluni. Lakini hapatakuwa na maridhiano kama haya kwenye hekalu la siku zijazo. Watu wote wanaokuja watakuwa watoto wa kike na wa kiume wa Mungu.

S: Kwenye Zek 14:21, Wakanaani walikuwamo lini kwenye nyumba ya Mungu?

J: Wagibeoni walikuwa ni watu walioishi Kanaani na walifanya agano na Waisraeli kwenye Yos 9:23, 27. Baadhi ya watumisho wa hekalu (ambao hawakuwa makuhani wala Walawi) walirudi baada ya uhamisho wa Babeli kwenye Neh 7:26-56 na Ezr 2:43-54. Watumishi wa hekalu watakuwa Wagibeoni.

S: Kwenye Kitabu cha Zekaria, kuna maandishi gani ya kale zaidi ambayo yap oleo hii?

J: Hati toka Bahari ya Chumvi (Dead Sea Scrolls, DSS): (karibu mwaka 1 KK) kuna nakala tatu za Kitabu cha Zekaria miongoni mwa Hati toka Bahari ya Chumvi zinazoitwazo 4Q76 (=4QXIIa), 4Q80 (=4QXIIe), na 4Q82 (=4QXIIg) [Dead Sea Scrolls Translated, uk.478-479].
4Q76
(=4QXIIa) ina Zek 14:18.
4Q80
(=4QXIIe) ina Zek 1:4-6, 9-10, 13-14; 2:10-14; 3:2-10; 4:1-4; 5:8-11; 6:1-5; 8:2-4,6-7; 12:7-12.
4Q82
(=4QXIIg) ina Zek 10:11-12; 11:1-2; 12:1-3.
Nahal Hever
ni pango lililo karibu na Engedi, lenye kipande cha hati yenye vitabu vya manabii wadogo kilichoandikwa kwa Kigiriki (8 Hev XIIgr). Kipande hiki kiliandikwa kati ya mwaka 50 KK na 50 BK. Nahal Hever ilifichwa wakati wa maasi ya Barkuba dhidi ya Warumi. Kipande hiki ni marekebisho ya Septuajinti (LXX), yaliyofanywa Uyahudi, na inafanana zaidi na toleo la Kimasoretiki. Nahal Hever ina Zek 1:1-4, 12-14; 2:2-4, 7-9, 11-12, 16-17 (=LXX 1:19-21; 2:3-5, 7-8, 12-13); 3:1-2,4-7; 8:19-21, 23; 9:1-5.
Hati ya Wadi Murabb'at (Mur XII) iliandikwa mwaka 132 BK. Ina Zek 1:1-4 pamoja na vitabu vya manabii wadogo.
Kwa ujumla, Nahal Hever na wadi Murabb'at kama vilivyo kwenye Hati toka Bahari ya Chumvi, zina mistari ifuatayo ya Zekaria: 1:1-6, 9-10, 12-14; 2:2-4, 7-14, 16-17; 3:1-10; 4:1-4; 5:8-11; 6:1-5; 8:2-4, 6-7, 19-21, 23; 9:1-5; 10:11-12; 11:1-2; 12:1-3,7-12; 14:18. Tazama Meaning of the Dead Sea Scrolls kwa maelezo zaidi.
Tafsiri ya Kishamu
Hati za kale za Biblia ya Kikristo
, zilizoandikwa karibu mwaka 350 BK, zina Agano la Kale, kikiwemo Kitabu cha Zekaria. Hati hizi ni Vaticanus (mwaka 325-250 BK) na Alexandrinus (karibu mwaka 450 BK), ambamo vitabu kumi na mbili vya manabii wadogo viliwekwa kabla ya Kitabu cha Isaya. Kitabu cha Zekaria kimo chote kwenye Vaticanus na Alexandrinus.
Sinaiticus
(mwaka 340-350 BK) pia ina kitabu chote cha Zekaria. Kitabu hiki kinaanzia ukurasa ambao Kitabu cha Hagai kinaisha, na kinaisha ukurasa ambao Kitabu cha Malaki kinaanza.

S: Ni waandishi gani wa awali walioongelea Kitabu cha Zekaria?

J: Waandishi walioandika kabla ya baraza la kanisa la Nikea (Pre-Nicene writers) walioongelea au kudokezea mistari ya Zekaria ni:
Myahudi Philo wa Alexandria (mwaka 15/20 KK-50 BK) anaongelea Zek 6:12, isipokuwa toleo la Kimasoretiki linasema "ambaye jina lake ni chipukizi" wakati Philo anasema "ambaye jina lake ni mashariki."
Barua ya Barnabas
(mwaka 100-150 BK) sura ya 2, uk.138 inanukuru Yer 7:22 na Zek 13:17 kama maneno ya Bwana.
Justin Martyr
(karibu mwaka 138-165 BK) anawataja Ayubu na Zekaria kwenye Dialogue with Trypho the Jew sura ya 103, uk.251.
Justin Martyr inaitaja Zek 3:1 kama kazi ya Zekaria kwenye Dialogue with Trypho the Jew sura ya 79, uk.238.
The Shepherd of Hermas
sura ya 31, uk.53-54 (karibu mwaka 160 BK) inadokezea Yer 13:20 na Zek 11:15-17 kuhusu wachungaji wapotevu.
Melito wa Sardis
(mwaka 170-177/180 BK) alitaja kwa njia isiyokuwa ya moja kwa moja "Agano la Kale" na kuorodhesha vitabu. Havitaji vitabu kumi na mbili vya manabii wadogo kwa majina, bali anaviita vyote ‘Vitabu Kumi na Mbili (Kipande cha 4 kutoka kwenye Book of Extracts juzuu ya 8, uk.759).
Theophilus wa Antiokia
(mwaka 168-181/188 BK) ananukuru kutoka Zek 7:9, 10 kwenye Letter to Autolycus kitabu cha 3 sura ya 7, uk.115.
Irenaeus wa Lyons
(mwaka 182-188 BK) "Zekaria pia, miongoni mwa manabii kumi na mbili, anawaonyesha watu mapenzi ya Mungu, akisema: ‘Mungu mwenye nguvu zote anasema: Fanya hukumu ya kweli, na onyesha rehema na huruma kila mtu kwa ndugu yake. Na usimuonee mjane, na yatima, na mtu aliyebadili dini kuwa Myahudi, na masikini; na mtu yeyote asiwaze maovu moyoni mwake dhidi ya ndugu yako.'" Irenaeus Against Heresies kitabu cha 4 sura ya 17.3, uk.483.
Irenaeus wa Lyons (mwaka 182-188 BK) ananukuru unabii kuhusu Masihi toka Zek 12:10 kwenye Irenaeus Against Heresies kitabu cha 24 sura ya 9, uk.508.
Clement wa Alexandria
(mwaka 193-217/220 BK) ananukuru kutoka Zek 3:2 kwenye Exhortation to the Heathen sura ya 10, uk.197 na Zek 9:9 kwenye Instructor kitabu cha 1 sura ya 5, uk.213.
Clement wa Alexandria (mwaka 193-205 BK) "Katika mwaka wa tano wa utawala wake, Ezekieli alitabiri akiwa Babeli; baadaye Nahumu, kisha Danieli. Baadaye tena Hagai na Zekaria alitabiri katika miaka miwili ya Dario; kisha malaika miongoni mwa kumi na mbili. Baada ya Hagai na Zekaria, Nehemia, mkuu wa wanyweshaji wa Ahasuero, mwana wa Acheli Muisraeli, waliujenga upya mji wa Yerusalemu na kuli. Wakati wa uhamisho kulikuweko Esta na Mordekai, ambao kitabu chao kingali kipo, kama kilivyo kile cha Wamakabia. Wakati wa uhamisho huu Mishaeli, Hanania na Azaria, walikataa kuabudu sanamu hata wakatupwa kwenye tanuru la moto. Lakini waliokolewa na mtu anayeonekana kama malaika. Wakati huo, kwa sababu ya joka, Danieli alitupwa kwenye tundu la simba; lakini kwa sababu alilindwa na Ambacuc kwa majaliwa ya Mungu na akarejeshwa siku ya saba" (Stromata kitabu cha 1 sura ya 21, uk.328).
Tertullian
(mwaka 198-220 BK) ananukuru Zek 14:14 kama kazi ya Zekaria (An Answer to the Jews sura ya 9, uk.162).
Origen
(mwaka 225-254 mwaka) "Na Zekaria anatabirije kuhusu Yesu anaposema" na ananukuu Zek 9:9 (Commentary on John kitabu cha 10 namba 17, uk.395).
Novatian
(mwaka 250/254-256/7 A.D.) alinukuru Zek 7:6 (Septuajinti) kama kazi ya Zekaria (On Jewish Meats sura ya 5, uk.649).
Treatise Against Novatian
sura ya 14, uk.662 (karibu mwaka 248-258 BK) ananukuru Zek 11:16 kama kazi ya Zekaria.
Cyprian wa Carthage
(karibu mwaka 246-258 BK) "Pa kwenye Zekaria Mungu anasema: ‘Na watavuka kupitia kwenye bahari nyembamba, na watayapiga kwa nguvu mawimbi baharini, na watavikausha vina vyote vya mito; na majivuno yote ya Waashuru yataangamizwa, na fimbo ya enzi ya Misri itaondolewa'" (Treatises of Cyprian Mada ya 12 kitabu cha 2 sura ya 6, uk.518).
Cyprian wa Carthage (c.246-258 A.D.) "Kwenye Isaya . . . kwenye Zaburi ya 117 . . . Pia kwenye Kitabu cha Zekaria . . . Pia kwenye Kumbukumbu la Torati . . . Pia kwenye [Yoshua] mwana wa Nave" (Treatises of Cyprian Mada ya 12 sura ya 2.16, uk.522).
Cyprian wa Carthage (karibu mwaka 246-258 BK) ananukuru Maandiko yafuatayo kama unabii wa Wayahudi kumsulubisha Mwokozi msalabani (Isa 65:2; Yer 11:19; Kum 28:66; Zab 22:16-22; 88:9; 119:120; 141:2; Zef 1:7, na Zek 12:10.
Adamantius
(karibu mwaka 300 BK) anafafanua Zek 7:10 na 8:17 kama kazi ya Nabii Zekaria (Dialogue on the True Faith Sehemu ya Kwanza na. 13, uk.56. (Adamantius anaongea).
Adamantius (karibu mwaka 300 BK) ananukuru Zek 9:9 na 8:17 kama kazi ya Nabii Zekaria (Dialogue on the True Faith Sehemu ya Kwanza na.25, uk.69. (Adamantius anaongea). (Hizi ni sehemu pekee ambazo Adamantius anaongelea Kitabu cha Zekaria).
Victorinus wa Petau
(aliyeuawa kama shahidi wa dini mwaka 304 BK) ananukuru Zek 4:14 kama kazi ya Zekaria kwenye Commentary on the Apocalypse sura ya 11 juzuu ya 4, uk.354).
Methodius wa Olympus and Patara
(karibu mwaka 260-312 BK) ananukuru Zek 4:1-3 kama kazi ya Zekaria (Banquet of the Ten Virgins hotuba ya 10, uk.350).
Lactantius
(karibu mwaka 303-karibu mwaka 325 BK) "Pia Zekaria anasema" na ananukuru Zek 12:10 kwenye Epitome of the Divine Institutes sura ya 46, uk.241).
Baada ya Baraza la Nikea

Athanasius wa Alexandria
(mwaka 367 BK) (Alisema kwa njia isiyokuwa ya moja kwa moja kwani anawataja manabii kumi na mbili) "Hivyo, kuhusu Agano la Kale, lina vitabu kumi na mbili; . . . kisha Manabii, wale kumi na mbili wanachukuliwa kuwa ni kitabu kimoja . . ." (Athanasius Easter Letter 39 sura ya 4, uk.552).
Aphrahat Mshamu
(mwaka 337-345 BK) ananukuru Zek 4:2 kama kazi ya Nabii Zekaria (Select Demonstrations Uthibitisho wa 1 sura ya 8, uk.347-348).
Ephraem Syrus
(mwaka 350-378 BK) aanadokedea Zek 2:3 kwenye Hymns on the Nativity wimbo wa 2, uk.227.
Ephraem Syrus (mwaka 350-378 BK) anaweza kuwa anadokezea Zek 2:8 kwenye Seven Hymns on Faith wimbo wa 2, uk.296. Leo hii hakuna kazi nyingine yenye kumwonyesha Ephraem akinukuru Kitabu cha Zekaria.
Basil wa Cappadocia
(mwaka 357-378 BK) ananukuru baadhi ya sehemu za Zek 10:1, 2 kama kazi ya Zekaria (Barua ya 210 sura ya 6, uk.251).
Cyril wa Yerusalemu
(mwaka 349-386 BK) anavitaja vitabu vya Manabii, wote vile kumi na mbili na vinginevyo. Mik 3:8 kama kwenye Kitabu cha Mika, Yoe 2:28 kama kwenye Kitabu cha Yoeli, Hag 2:4 kama kwenye Kitabu cha Hagai, Zek 1:6 kama kwenye Kitabu cha Zekaria (Catechetical Lectures Mahubiri ya 16.29, uk.122).
Ambrose wa Milan
(mwaka 370-390 BK).
Gregory wa Nanzianzus
(mwaka 330-391 BK).
Gregory wa Nyssa
(karibu mwaka 356-397 BK).
Didymus
kipofu (mwaka 398 BK) ana maoni (commentary) kuhusu kitabu chote cha Zekaria.
John Chrysostom
(aliyefariki mwaka 407 BK) anaitaja Zek 5:7, 8 kama kazi ya Zekaria (juzuu ya 10 ya Commentary on Matthew mahubiri ya 38, uk.253).
Orosius/Hosius wa Braga
(mwaka 414-418 BK).
Sozomen
kwenye kazi yake iitwayo Ecclesiastical History (mwaka 370-380/425 BK).
Augustino wa Hippo
anawataja Hagai, Zekaria, na Malaki kwenye City of God kitabu cha 17, sura ya 35, uk.380).
Augustino anawataja Hagai na Zekaria kwenye Commentary on Psalms, Zaburi 148, uk.676.
Mfuasi nusu wa mafundisho ya Pelagius John Cassian (mwaka 419-430 BK).
Theodoret wa Cyrus
(mwaka 423-458 BK).
Kwenye vitabu vya uongo na uzushi

Mwandishi mwenye jina la bandia Hippolytus
(mwaka 225-235/6 BK) ananukuru nusu ya Zek 12:10 kama kifungu chenye kumwongelea Yesu kwenye kipande cha maandiko namba 40, uk.252. Kazi hii imeandikwa kwa mtindo wa Hippolytus, lakini zaidi ya hapo hatujui kuwa imeandikwa na Hippolytus.
Apostolic Constitutions
(karibu mwaka 380 BK) kitabu cha 5 sehemu ya 3 sura ya 20, uk.448 inanukuru Zek 9:9 kama Zekaria inavyosema.
Apostolic Constitutions
(karibu mwaka 380 BK) kitabu cha 5 sehemu ya 3 sura ya 19, uk.447-448 inanukuru sehemu ya Zek 12:10 na kusema kuwa inamwongelea Kristo.
Apostolic Constitutions
(karibu mwaka 380 BK) kitabu cha 5 sehemu ya 3 sura ya 20, uk.448 inanukuru Zek 9:9 kama Zekaria inavyosema.
Mzushi anayefuata mafundisho ya Pelagius Theodore wa Mopsuestia (mwaka 392-423/429 BK) aliandika maoni (commentary) ya Kitabu cha Zekaria.

S: Kwenye Kitabu cha Zekaria, kuna tofauti gani za kutafsiri kati ya matoleo ya Kiebrania na Kigiriki (Septuajinti)?

J: Ifuatayo ni mifano michache ya tofauti za kutafsiri kati ya Toleo la Kimasoretiki na Septuajinti, isipokuwa mahali panapoelezwa tofauti.
Zek 1:3
"unasema" dhidi ya "utasema."
Zek 1:3 "BWANA wa majeshi asema hivi" maneno haya hayamo mara mbili zinazotangulia kwenye baadhi ya matoleo ya Septuajinti. Tazana Exegetical Commentary Haggai, Zechariah, Malachi, uk.97 kwa maelezo zaidi.
Zek 1:6
"Lakini maneno yangu, na amri zangu nilizowaagiza hao manabii, watumishi wangu, je hazikuwapata baba zenu" dhidi ya "Lakini nyinyi mnapokea maneno yangu na maagizo yangu yote niliyoamuru kwa Roho wangu, watumishi wangu manabii, walioishi nyakati za baba zenu."
Zek 1:8
"kati ya mihadasi iliyokuwa kwenye korongo" dhidi ya "kati ya milima yenye kivuli."
Zek 1:8
farasi wa pili ni "mwekundu" dhidi ya "kijivujivu na mwenye madoadoa yaliyoiva" (Septuajinti) dhidi ya "mwenye rangi mbalimbali" (matoleo ya Kishamu cha kale [Peshita] na Kilatini [Vulgeti]) dhidi ya "mweupe mwenye madoamadoa" (toleo la Kiaramu [Targumu]).
Zek 1:10 pia Zek 1:11
"kati ya mihadasi" dhidi ya "kati ya milima."
Zek 1:11
"inatulia nayo inastarehe" dhidi ya "inakaliwa na watu."
Zek 1:12
"utakataa kuurehemu" dhidi ya "utaulaani."
Zek 1:15
"Nami nitawakasirikia sana mataifa" dhidi ya "Nami nimewakasirikia wapagani walioungana kushambulia."
Zek 1:15
"waliyahimiza mateso" dhidi ya "waliungana kushambulia uovu."
Zek 1:16
"Nitaurudia" dhidi ya "nimeurudia."
Zek 1:17
"Na malaika aliyeongea nami aliniambia ‘piga kelele'" dhidi ya "Piga kelele."
Zek 1:17
"wema" dhidi ya "mafanikio."
Zek 1:17
"ataufariji" (toleo la Kimasoretiki) dhidi ya "atauhurumia" (toleo la Kigiriki, Septuajinti). Hapa ni herufi ya kwanza tu iliyotofauti kwenye Kiebrania.
Zech 1:19 maneno "Yerusalemu" na "Israeli" hayamo kwenye baadhi ya matoleo ya Kigiriki (Septuajinti).
Zek 1:21
"zilizowatawanya watu wa Yuda" dhidi ya "zilizowatawanya watu wa Yuda, na kuivunja Israeli vipande vipande."
Zek 1:21
"kuzifukuza, kuziangusha pembe za mataifa" dhidi ya "kuziongezea makali kwa ajili ya mikono yao, hata pembe nne, ambazo ni mataifa"
Zek 1:21
"nchi ya Yuda" dhidi ya "nchi ya Bwana."
Zek 2:6
"nimewatawanya kwenye pepo nne" dhidi ya "nimewatawanya kama pepo nne."
Zek 2:8 "jicho langu" (toleo la Kimasoretiki) dhidi ya "jicho lake" (4Q12[e], na badiliko lilifanywa na wenye kunakiri Kiebrania).
Zek 3:4 "nitamvika" dhidi ya "mvikeni" (toleo la Septuajinti).
Zek 3:8
"chipukizi/tawi" (toleo la Kimasoretiki) dhidi ya "mapambazuko" (Septuajinti, Theodore wa Mopsuestia Commentary on Zechariah sura ya 4, uk.345 na sura ya 6 uk.355, Didymus Commentary on Zechariah sura ya 2, uk.49).
Zek 4:2
"taa zake saba juu yake; tena iko mirija saba" (toleo la Kimasoretiki) dhidi ya "mirija saba" (Septuajinti).
Zek 4:5
"makuhani kwa makuhani" (toleo la Kimasoretiki, Septuajinti ya Kiantiokia, Theodore wa Mopsuestia Commentary on Zephaniah sura ya 1, uk.288) dhidi ya "makuhani" (matoleo mengine ya Septuajinti).
Zek 4:9
"utajua" (toleo la Kimasoretiki) dhidi ya "mtajua" (matoleo ya Kishamu, Targumu, Vulgeti na Hati za Kairo [Misri]).
Zek 5:6
"macho yao" (matoleo ya Kiebrania na Kishamu) dhidi ya "uovu wao" (Septuajinti).
Zek 6:7a "wenye nguvu" (matoleo yote ya Kimasoretiki) dhidi ya "wekundu" (toleo ya Kishamu, Aquila). Tazama kwenye Exegetical Bible Commentary, uk.185.
Zek 6:11 na 14
"mataji" (toleo la Kimasoretiki) dhidi ya "taji" (baadhi ya matoleo ya Septuajinti, Kishamu, na Kiaramu [Targumu]).
Zek 6:10 "Heldai, Tobia, na Yedaya" kama majina (toleo la Kimasoretiki) dhidi ya majina na ujuzi wao wa kazi (Septuajinti iliyoandikwa kabla ya baraza la kanisa la Nikea na imedokezwa na Theodore wa Mopsuestia kwenye Commentary on Zechariah sura ya 6, uk.355) dhidi ya ujuzu wa kazi tu (matoleo mengineyo ya Septuajinti).
Zek 6:13 [haipo] (toleo la Kimasoretiki) dhidi ya ". . . na kuhani atakuwa mkono wake wa kuume" (Septuajinti, ingawa inaweza isiwe hivyo).
Zek 6:14a
"mataji" (toleo la Kimasoretiki) dhidi ya "taji" (matoleo ya Septuajinti na Kishamu).
Zek 6:14b
Jina "Helemu" (matoleo ya Septuajinti, Kiaramu [Targumu] na Kilatini [Vulgeti]) dhidi ya "Heldai" (Toleo la Kishamu).
Zek 8:12
"mbegu ya amani" (toleo la Kimasoretiki) dhidi ya "nitapanda amani" (toleo la Septuajinti) dhidi ya "mbegu yake [itakuwa] amani" (matoleo ya Kishamu na Kiaramu la Manabii).
Zek 9:10
"nitaliondoa" (toleo la Kimasoretiki) dhidi ya "ataliondoa" (Septuajinti).
Zek 9:15
"watakunywa na kufanya kelel kama kwa divai" dhidi ya "atawameza kama divai" (NRSV maelezo chini ya ukurasa yanasema neno la Kiebrania linamaanisha "atakunywa kama divai" na neno la Kigiriki linamaanisha "atakunywa damu yao kama divai").
Zek 10:11
"atapita" dhidi ya "watapita."
Zek 11:7 "kweli/bayana" (matoleo ya Kimasoretiki, Kiaramu [Targumu] na Kilatini [Vulgeti]) dhidi ya "Wakanaani" (Septuajinti).
Zek 11:13
"mfinyanzi . . . ndani ya nyumba ya Bwana" (toleo la Kimasoretiki) dhidi ya "tanuru . . . tanuru kwenye nyumba ya Bwana" (Septuajinti) dhidi ya "hazina" (toleo la Kishamu).
Zek 11:16 "hatawatafuta wadogo" (toleo la Kimasoretiki) dhidi ya "hatawatafuta waliotawanyika" (Septuajinti, Vulgeti). Toleo la Kimasoretiki halieleweki vizuri sana hapa.
Zek 12:10
"nao watamtazama yeye ambaye walimchoma" (toleo la Kimasoretiki, Septuajinti) dhidi ya "walipomtazama yeye ambaye walimchoma" (Theodotion, Yoh 19:37). Ikiwa tutachukua maandishi ya kwanza, Yoh 19:37 itakuwa imebadilisha tu ‘mimi'na kuwa ‘yeye' ili kumuelezea Kristo. Hata hivyo, tafsiri ya Septuajinti iliyoandikwa na Brenton inasema "na watanitazama mimi, kwa kuwa walinidhikahi." Tertullian (mwaka 198-220 BK) aliandika, ". . . yeye waliyemchoma, na watapiga vifua vyao, kabila hata kabila" (Answer to the Jews sura ya 14, uk.172).
Zek 14:2 "watandewa jeuri/watabakwa" (jinsi neno hili lilivyoandikwa [Ketivu] Kiebrania) dhidi ya "walivyokutana kimwili na" (jinsi neno hili lilivyosomwa Kiebrania [Kere]). Kere ililifanya neno liwe zuri kwa mujibu wa Exegetical Commentary: Haggai, Zechariah, Malachi, uk.346.
Zek 14:5
"Mungu" dhidi ya "Mungu wangu" (Exegetical Commentary : Haggai, Zechariah, Malachi, uk.346).
Zek 14:5
"watakatifu wote pamoja nanyi" (toleo la Kimasoretiki) dhidi ya "watakatifu wote pamoja naye" (Septuajinti, Targumu, Vulgeti).
Zek 14:18
"shall not" (Masoretic) vs. "shall" (matoleo ya Septuajinti na Kiashamu). Toleo la Kimasoretiki halieleweki vizuri sana hapa.
Zek 14:18
"hawatapata mvua" (toleo la Kimasoretiki) dhidi ya "watapata pigo" (matoleo ya Septuajinti na Kiashamu). Tazama Exegetical Commentary: Haggai, Zechariah, Malachi, uk.366.